Ifike mahali huu mgao wa umeme angalau uzingatie kuleta Tija

Monasha

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
561
422
Hata kama ni mgao lakini nadhani hii sasa imezidi.

Sijui kama hili shirika linajua kwamba unaounguza uzalishaji na kupunguza ukuaji wa biashara nchini kwa huu mgao.
Hivi Tanesco wameshindwa kukaa chini na kuwaza ni namna gani hata huu mgao wa umeme utakuwa na manufaa kidogo miongoni mwa wananchi?

Unakuta mji mzima hauna umeme kwa masaa yote ya kazi. Unarudisha umeme saa saba au nane za usiku ili huo umeme umnufaishe nani? Bado unakata huo umeme saa kumi na mbili asubuhi. Mgao wa namna hii unalenga nini? Mgao wa namna hii kwa taifa una hasara kubwa sana.

Kama mgao unashindikana kutokomezwa, ifike mahali angalau mgao wa umeme uzingatie masaa ya kazi ili kupunguza madhara katika uzalishaji.

Angalau wananchi tupate umeme katika masaa ya kazi na siyo kukaa siku nzima then uje urudishiwe umeme ukiwa umelala.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom