Tatizo la umeme, bora mgao wa wakati wa ukame kuliko huu wakati wa mafuriko!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,439
Wakuu,

Changamoto ya umeme kama Taifa inahitaji uchunguzi na taarifa tutayoiamini na njia za kutatua tatizo zinazotekelezeka.

Mnakumbuka wakati mgao unaanza tulipewa sababu zinazochangia upungufu wa umeme hasa ukame. Taifa likapewa ratiba ya mgao na shirika likahaidi kufuata hiyo ratiba.

Mungu ametusaidia mvua zimenyesha za kutosha lakini kibaya kinachotokea sasa hali ya mgao ni bora hata mgao ule tukiwa kwenye ukame. Nafikiri kama Taifa ni muda muafaka tufahamu nini kinaendelea.

Waziri wetu Biteko ni jembe na mzalendo mkubwa, kama yupo kwenye hii sector na bado tunapitia hali hii inawezekana tatizo ni kubwa zaidi kuliko tunavyoweza kufikiri.

Nashauri hili swala liwe wazi bila kujali political impact itayotokea ili tuponye Taifa. Ipo hatari bwawa la umeme wa Nyerere likazalisha umeme at full capacity bado zikaja hadithi mpya za upungufu wa umeme.

Tulitegemea hadi muda huu makali yawe yamepungua sana ili tuamini tunaelekea kumaliza mgao lakini sasa inakatisha tamaa kama hili tatizo litaisha hivi karibuni.

Ndugu yangu Biteko kwa uzalendo wako najua swala la mgao halikupi usingizi lakini sisi huku wananchi tunaelekea kukata tamaa kabisa.
 
Back
Top Bottom