Kwa mara ya kwanza ninakwenda kuipigia kura CCM 2020

Magufuli amerudisha imani kwa CCM ya Watanzania wengi sana. Kila mahala habari ya Mujini ni Magufuli
Juzi anasema "Vyama vingine vinapotea kwa sababu watu wanajua mkombozi wao ni Magufuli" mkuu unaona hapo hata yeye mwenyewe hana imani na CCM
 
Watu walitekwa kiakili kwamba wataibiwa kura kwa kauli ya bao la mkono! Haikuwa na maana hiyo. Hivi tuwe wakweli kama kweli CCM ingeamua ishinde kwa kuiba kura au hila nyingine wapinzani mngepata wabunge na madiwani wangapi? Ni woga wenu tu. Kipigo kilikuwa halali maana wapinzani hawakuwa na haja ya kwenda IKULU na wala hawakujiandaa kuchukua dola mwaka 2015 ndio maana waliokoteza hata baadhi ya wagombea dakika za mwisho!!
Pole sana.
 
Kwani unafikiri akili yake bado iko sawa na miaka ya nyuma? Hujui mtu akizeeka na akili inachoka? Zamani alikuwa kijana mwenye ndoto safi ndio maana alikuwa anaikataa ccm, sasa kazeeka akili IMECHOKA ndio maana anafikiri kizembe zembe, mawazo yake hayana tofauti na LYATONGA, Lyatonga huyu wa sasa si yule wa 1995 na sababu ni UZEE, kumbukumbu kwisha kichwani.
Wa2 kama nyie hamjui mnataka nini katika uongozi yaan mpompo2
 
Mmmhhh,watu wengine bana,maisha ya huku mtaani ni magumu sana we unaongea uongo mchana kweupe.
Piga kazi mtoto wa kiume wewe acha kupenda vya dezo
Ulitaka serikali ikuletee chakula mezanii??
Amka
 
Dogo usidanganyike. Hakuna Kiongozi mwenye mipango wala nia ya dhati ya kwenda Ikulu! Mtasubiri sana. Watabaki kuwadanganya kwamba wameibiwa kura!! Zindukeni vijana!
Kwakuwa hiyo ni akili yako unadhani kila mtu yuko hivyo
 
CHADEMA mwaka jana ingemsimamisha Dr. Slaa ingetoa changamoto kuliko wanavyofikiria. Tatizo lao ni kutojiamini tu. Hilo ndilo linafanya Chama chao kipoteze mwelekeo hivi sasa. Hakina mvuto na hata ukiwauliza mtaani kama wanamjua Katibu Mkuu wa CDM watamtaja Dr. Slaa!! Huyo wa sasa sijui anafanya nini!! Na sijui anaitwa nani??
aaah wapi dr asingetikisa lowasa lowasa lowasa lowasaaaaaaaaaaa
 
Pamoja nambwembwe zote hizo kumbukeni juzi ccm imekula zauso huko kilosa na chadema imepeta endelea kujidanganya eti wanaimani namagufuri labda utwambie utafiti umefanyia wapi
 
Juzi anasema "Vyama vingine vinapotea kwa sababu watu wanajua mkombozi wao ni Magufuli" mkuu unaona hapo hata yeye mwenyewe hana imani na CCM
CCM ni kundi la watu linaloongozwa na magufuli
CHADEMA ni kundi la watu linaloongozwa na lowassa na msaidizi wake Mbowe
Na sikuzote kiongozi ndo anaewakilisha waliochini yake yaani waliochini wataiga tabia ya kiongozi ili waendane nae
Ko lowassa angekuwa raisi viongozi wake wa chini wangeiga tabia yake.hvyohvyo kwa magufuli
 
Hii ni kauli ya mfanyakazi mmoja wa ngazi za juu anayefanya kazi taasisi ya bodi ya ugavi hapa nchini(PSPTB).

Leo nimetembelea bodi ya ugavi kwa mambo yangu binafsi na nikiwa hapo nilifanikiwa kubadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi ila nilichokigundua kinachozungumzwa maofini juu ya magufuli kwa wafanyakazi wa serikali ni tofauti kabisa na mijadala ilivyo humu mitandaoni.

"Kwa mara ya kwanza ninakwenda kuipigia kura CCM 2020"Hii ilikua ni kauli ya afisa huyo ambaye alisema tangu ameanza kupiga kura hajawahi kuipigia kura CCM kutokana na mambo yake ya hovyo ila kwa sasa Magufuli amekua kivutio kikubwa.

Aliongeza kwakusema,"Siwezi kumchagua raisi tofauti na Maguli kwani kura yangu siwezi kui risk kumpigia kura raisi tofauti nisiyefahamu atakuaje baada ya kua raisi".

Mwisho afisa huyu alisema na hapa namnukuu,"Tutarajie 2020 Maguli kushinda kwa zaidi 80% kwani kwa sasa huyu ndiye pekee aliyeonesha dira kuivusha nchi".

Hii ndio hali ya maofisini na kuhusu vijijini mapenzi kwa Magufuli ni zaidi ya hali ilivyo mijini wananchi huwaelezi chochote kuhusu Maguli.

Nimeona niliseme hili ili huyu inaeitwa Lowasa na wafuasi wake wajipange vizuri uchaguzi ujao ama waahirishe ili pesa za kampeni ziweze kujenga hata makao makuu ya chama.

umeagana na Mungu? hakuna aijuae kesho.
 
Hahaha wako wapi wale waliodai tatizo mfumo, sio mtu! Sidhani kama waliwahi kufikiri kuwa kila mtu ana mtazamo tofauti na hatuwezi kuwa sawa kiakili.
Hujui maana ya mfumo?! Hv Magufuli siku àkiondoka madarakani akaja mswahili kama Jk itakuwaje?
 
CHADEMA mwaka jana ingemsimamisha Dr. Slaa ingetoa changamoto kuliko wanavyofikiria. Tatizo lao ni kutojiamini tu.

Kama ni changamoto ni sawa lakini wasingechukua nchi kamwe.
Ila uki balance equation utaona el ni mzito zaidi ya Slaa. Ndio maana aliweza kumtoa kwenye nafasi pamoja na maanadalizi yake kuchukua nchi. Sasa kama aliweza kutolewa asigombee angeifanya nini dubwana kubwa kama ccm. CHADEMA kingebakia kua chama cha wanyonge tu.

Hata nape aliwahi kusema:-EL aliwapa changamoto zaidi kwasababu kuhama kwake alikua anajua mbinu halali za CCM kushinda uchaguzi kitu.

Mtu hatari ni yule anayekujua kwa kila kitu kisha akakugeuka.
Wimbo wa ufisadi usingeimbwa na chama tawala, kama el angebakia CCM. Viongozi wengi walikua wana vigugumizi katika hili. Ni lazima tutambue mchango mkubwa wa el katika hili. Mabadiliko ya CCM yamechangiwa kwakiasi kikubwa na kuhama kwa EL. Kupitia kuhama kwake alichochea fikra hizi za mabadiliko kwa jamii sana na kupelekea uasi mkubwa ndani ya CCM. Dk slaa asingeweza kufika hapa hata kidogo. Watanzania wake kwa waume wamejikuta wakijadili siasa na mustakabali wao kuliko kipindi kingine chochote katika historia ya nchi. Uchaguzi ulioleta tumbo joto kwa tawala ulioko madarakani kuliko wakati wowote ule.
 
Naomba upite Na mitaani nako uulize achana Na hao wafanyakazi wa maofisini.!
 
Aliongeza kwakusema,"Siwezi kumchagua raisi tofauti na Maguli kwani kura yangu siwezi kui risk kumpigia kura raisi tofauti nisiyefahamu atakuaje baada ya kua raisi".
Wewe na huyo afisa wako mnafanana akili!
Kwani ni nani alimfahamu magufuli kuwa yupo hivyo alivyo kabla ya kuwa raisi??
Halafu, mbona utafiti wako ni haba sana!
Yaani umeenda idara moja tu ukasikilliza mawazo ya mtu mmoja halafu ukatoa hitimisho!
Kitaalamu, wanasema hivi pasipo utafiti huna haki ya kusema ingaawa unaweza kuzungumza.
 
Kama ni changamoto ni sawa lakini wasingechukua nchi kamwe.
Ila uki balance equation utaona el ni mzito zaidi ya Slaa. Ndio maana aliweza kumtoa kwenye nafasi pamoja na maanadalizi yake kuchukua nchi. Sasa kama aliweza kutolewa asigombee angeifanya nini dubwana kubwa kama ccm. CHADEMA kingebakia kua chama cha wanyonge tu.

Hata nape aliwahi kusema:-EL aliwapa changamoto zaidi kwasababu kuhama kwake alikua anajua mbinu halali za CCM kushinda uchaguzi kitu.

Mtu hatari ni yule anayekujua kwa kila kitu kisha akakugeuka.
Wimbo wa ufisadi usingeimbwa na chama tawala, kama el angebakia CCM. Viongozi wengi walikua wana vigugumizi katika hili. Ni lazima tutambue mchango mkubwa wa el katika hili. Mabadiliko ya CCM yamechangiwa kwakiasi kikubwa na kuhama kwa EL. Kupitia kuhama kwake alichochea fikra hizi za mabadiliko kwa jamii sana na kupelekea uasi mkubwa ndani ya CCM. Dk slaa asingeweza kufika hapa hata kidogo. Watanzania wake kwa waume wamejikuta wakijadili siasa na mustakabali wao kuliko kipindi kingine chochote katika historia ya nchi. Uchaguzi ulioleta tumbo joto kwa tawala ulioko madarakani kuliko wakati wowote ule.

Hapo ndipo chadema mlipotea na hamtarudi kwenye mstari tena! Kuamini kwamba lowassa kwa kuwa ametoka ccm atachukua nchi kwa urahisi! Mkasahau itikadi yenu na kuitupa na sasa hatuwaamini tena. Subirini maporomoko wa kutisha 2019 serikali za mitaa na 2020 uchaguzi mkuu. Nani atawaamini vigeugeu. Mara leo hii ni nyeusi na haisafishiki kabisa. Tena mna ushahidi wa kutosafishika! Tena ni heshima kwa mungu kuitupa hiyo nyeusi. Mara, hapana! Ni nyeupe haina doa! Macho yetu hayakuona vizuri tulikosea jamani! Ubababishaji gani huu! Ccm oyeee! Hapa kazi tu!! Bla bla huko huko ufipa!!
 
Back
Top Bottom