TUTUO
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 3,253
- 2,023
Hali ya maofisini wakati umezungumza na mfanyakaz mmoja tu halafu unaconclude kwa kuonyesha ni ofisi zoteHii ni kauli ya mfanyakazi mmoja wa ngazi za juu anayefanya kazi taasisi ya bodi ya ugavi hapa nchini(PSPTB).
Leo nimetembelea bodi ya ugavi kwa mambo yangu binafsi na nikiwa hapo nilifanikiwa kubadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi ila nilichokigundua kinachozungumzwa maofini juu ya magufuli kwa wafanyakazi wa serikali ni tofauti kabisa na mijadala ilivyo humu mitandaoni.
"Kwa mara ya kwanza ninakwenda kuipigia kura CCM 2020"Hii ilikua ni kauli ya afisa huyo ambaye alisema tangu ameanza kupiga kura hajawahi kuipigia kura CCM kutokana na mambo yake ya hovyo ila kwa sasa Magufuli amekua kivutio kikubwa.
Aliongeza kwakusema,"Siwezi kumchagua raisi tofauti na Maguli kwani kura yangu siwezi kui risk kumpigia kura raisi tofauti nisiyefahamu atakuaje baada ya kua raisi".
Mwisho afisa huyu alisema na hapa namnukuu,"Tutarajie 2020 Maguli kushinda kwa zaidi 80% kwani kwa sasa huyu ndiye pekee aliyeonesha dira kuivusha nchi".
Hii ndio hali ya maofisini na kuhusu vijijini mapenzi kwa Magufuli ni zaidi ya hali ilivyo mijini wananchi huwaelezi chochote kuhusu Maguli.
Nimeona niliseme hili ili huyu inaeitwa Lowasa na wafuasi wake wajipange vizuri uchaguzi ujao ama waahirishe ili pesa za kampeni ziweze kujenga hata makao makuu ya chama.