Kwa jinsi DalaDala za Mbagala-Kawe, Gerezani-Kawe na Buza-Kawe zinavyopata tabu kugeuza, tutegemee ajali kubwa siku moja

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,127
GENTAMYCINE ni Mtetezi Huru wa kila Kada za Watu na leo nimeamua Kutetea DalaDala za Ruti tajwa hapo juu kwa jinsi zinavyonyanyasika wakati wa Kugeuza zikifika Kawe mwisho eneo la Masai.

Kinachonisikitisha zaidi ni kuona aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla Kushindwa kulitatua hili kwa kukaa na pande Mbili Hasimu Manispaa ya Kinondoni na Kambi ya Jeshi ya Lugalo kwa upande wa Kawe.

Cha Kushangaza zaidi eneo ambalo awali ndiyo lilitengwa kama sehemu ya Kugeuzia DalaDala za hizo Ruti tajwa hapo juu hivi sasa kumejengwa Baa na Ukumbi wa Burudani wa Jeshi uitwao DAR SERVICE PARK ambao huwa unajaa tu tarehe 21 hadi 27 na tarehe 30 au tarehe 1 za kila Mwezi pale Wajeda wakipokea Mishahara yao na Resheni zao na kuanzia tarehe za 3 hadi 20 za kila Mwezi Wajeda wakiwa Juu ya Mawe (Apeche Alolo kama GENTAMYCINE) katika huo Ukumbi utaona tu Kunguru, Paka na Tumbiri wa Pori jirani wamejazana huku Wakicheza Ndombolo na Masebene kwa Niaba ya Wanajeshi walioishiws Pesa.

Ilinichukua muda mrefu kwa GENTAMYCINE kufuatilia ni kwanini hakuna Kituo cha DalaDala za Kugeuzia kwa Ruti tajwa na Majibu niliyoyapata yalinisaidia kuamini ule Utafiti kuwa kwa sasa nchini Tanzania idadi ya Watu wenye Magonjwa ya Akili ni Milioni Nne na yawezekana ikazidi.

Ni kwamba Jeshi la Tanzania (Kambi ya Lugalo) kwa Nia Njema kabisa baada ya Kuona Wananchi wanapata hiyo Adha pamoja na DalaDala za Ruti hizo tajwa hapo juu waliamua kutoa hilo Eneo bure kabisa kwa Manispaa ya Kinondoni huku wakiwapa Sharti kuwa Kodi ya DalaDala za hapo zikusanywe na Jeshi kwakuwa hilo Eneo ni lao na pia wakisimamia Wao (Jeshi) hata Suala la Ulinzi na Usalama wa Raia ( Abiria ) litakuwa lao kupitia Kikosi chao cha SUMA JKT.

Kilichofuatia ni Upumbavu wa Watu wa Manispaa ya Kinondoni ambapo pamoja na kupewa Bure eneo hilo (namaanisha bila Kulinunua) na Kambi ya Jeshi ya Lugalo wao kwa Tamsa zao wakataka kuweka Watu Wao ili Kukusanya Kodi za Kimagumashi hali ambayo iliwakasirisha Jeshi na kuamua sasa Kuzuia DalaDala zote za Ruti tajwa hapo juu Kugeuzia eneo hilo na mwanzoni ilikuwa DalaDala zikigeuzia tu hapo Dereva, Kondakta na Abiria nyote mnaruka Kichurachura ndani ya DalaDala mliyomo huku Dereva akitakiwa Kugeuza DalaDala lake kwa mwendo wa Kichurachura huku akichungulia Dirishani asije sababisha Ajali.

Kiukweli kinachoendelea sasa si tu ni Kero bali ni Mateso na Manyanyaso kwa DalaDala za Ruti tajwa hapo juu na Abiria kwani kila Siku eneo la DalaDala hizo Kugeuzwa linasogezwa mbele na wenye Eneo (Jeshi la Lugalo) kiasi kwamba hivi sasa DalaDala zile Kubwa kabisa (EICHER) za Mbagala Kawe zinapata mno taabu Kugeuza na kuna moja leo ilibaki Kidogo sana isababishe Ajali Kubwa wakati nikiwa zangu Ukumbini DAR SERVICE PARK natongoza Baamedi aliyenikalisha muda mrefu huku Mbu wasio na Huruma wa Jeshini Lugalo ambao nahisi na Wao wameenda Kozi wakiningata bila Huruma na Baamedi Mwenyewe nimemkosa na sasa nimebakia na Usununu (Hasira) ru kwani nilishampakia mapema tu Vumbi la Kinshasa na Brazaville hivyo sasa cha Moto nakiona.

OMBI

Tafadhali Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam na Watu wa Manispaa ya Kinondoni nendeni mkazungumze Kiungwana na Jeshi (Kambi ya Lugalo) ili ikiwezekana waruhusu DalaDala Kugeuza katika hilo eneo lao bila ya Kubughudhiwa nao na kama ikishindikana kabisa msione Aibu au Uoga kuamuru sehemu Kubwa ya Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe ambavyo vinatumika na Wabakaji wa Mchana na Usiku na Machimbo ya Vibaka na Makao Makuu ya Watu waliokata Tamaa na Maisha magumu Kujinyonga utumike Kama Stendi Kuu ya DalaDala za Ruti tajwa na hata zingine kama za Mbezi Kawe, Segerea Kawe na Bunju Sokoni Kawe ambao nao Stendi yao ni mbaya, chafu na ina Kero nyingi (kama za Vibaka Abiria) Kuutumia pia.

Ni matumaini yangu makubwa nilichokiwasilisha hapa mtakifanyia Kazi haraka mno mkizingatia GENTAMYCINE (Mleta huu Uzi) nasomwa vyema (tena 24/7) na Rais Samia (Mama) hivyo hapa tayari ni kama vile Nimeshawachongea na Kuwasakizia Kwake Kimtindo hivyo litafuatiliwa na mtaulizwa nae au Wasaidizi wake kama mmelitatua na kama bado ndiyo mtamjua vyema Mtemi wa Kizanzibari (Chief Hangaya) sawa?

Kazi Kwenu!

Cc: Mjeda wa Lugalo King Kong III
 
GENTAMYCINE ni Mtetezi Huru wa kila Kada za Watu na leo nimeamua Kutetea DalaDala za Ruti tajwa hapo juu kwa jinsi zinavyonyanyasika wakati wa Kugeuza zikifika Kawe mwisho eneo la Masai....
Kwanini Daladala za Mbagala huwa ziko tofauti kabisa (hazifanani) kimwonekano na zile za Masaki?

Hivi mi mwenyewe sina hata Passo

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom