Kwa hii kashfa, Mchungaji Anthony Lusekelo (Mzee wa Upako) atajisafishaje?

Kwa kweli siku hizi hawa viongozi wetu wa dini wamesahau kabisa miiko ya utumishi wao,inawezekana huyu akawa anasingiziwa lkn ukweli ni kwamba wengi wao wanatia kichefuchefu nadhani sadaka zetu wanazozipata bila jasho ndizo zinazo walevya.
Mbaya zaidi wanawapiga vita Sana wale waliosimama kwa uaminifu ktk imani zao.
Isitoshe wao wakituhumiwa hawawi na ujasiri wa kuja kusisimama mbele ya waumini kuthibitisha tuhuma zao Kama ni uongo au la?
Mungu atusaidie tu kwa kweli
 
Hizo hela za bapa mnamchangia nyie waumini wake mungu anawaona,mnamchangia mihela mingi mpaka anashindwa kuzitumia anaishia kuzipiga tungi,ebu mkazieni kidogo ataacha.
 
Bujibuji na video ipo,ila ninashindwa kuipakua na kuipakia humu.Nafikiri tatizo la network huku nilipo.Nipo Kiwangwa ya Bagamoyo,nimekuja kula mananasi...Si unajua ndio msimu mwenyewe huu??
Kipanya barafu mi nakuamini huyu jamaa ni wa ovyo sana watu hawajui tu kuna nyumba yangu moja tupo jirani najua visa vyake
 
Hii "kashfa" Mchungaji Lusekelo alias Mzee wa Upako, Bulldozer, tingatinga na kiboko ya mapepo atachomokaje?

Mzee wa Upako amekumbwa na kashfa ya ulevi na kuleta vurugu kwa majirani zake huko Kawe nyumbani kwake,jirani na ilipo Radio Times.

Inaandikwa katika mitandao kuwa, Mzee wa Upako alfajiri ya jana, wakati mvua kubwa ikinyesha ktk jiji la Dsm, yeye alikuwa mtaani kwake akifanya fujo kwa majirani zake. Mzee wa Upako alikutwa akiwa kalewa "tilatila" huku akiporomosha lugha kali kwa majirani zake hao kupitia kwenye lango la nyumba hiyo.

Nyumba hiyo #KAW/MZN/1348 ni jirani na kwa Mzee wa Upako, malalamiko ya Mch. Lusekelo ni kuwa majirani hao wamekuwa wanamfuatilia muda mwingi kwa kumuita mlevi, na kwamba yeye ni mchungaji fake. Hivyo alfajiri hiyo Mch Lusekelo alikuwa anaenda kuwapa "vidonge" vyao hao majirani wachokozi.

Taharuki hii ya Lusekelo ilimfanya kuegesha gari lake katikati ya barabara na kuzuia watumiaji wengine kupita. Gari hiyo #T 126 DFN ilisimama katikati mwa njia na kusababisha foleni kubwa. Timbwili hilo la mchungaji lilifanyika mpaka kunapambazuka.

Hata alipoombwa kutulia, ndio kwanza aliita walinzi wake(Mabaunsa) ambao walikuja kumpa support.

Waliokuwa eneo la tukio wanasema mchungaji alikuwa pekupeku huku akiwa amekunja suruali na akiwa na "hangover". Huku baadhi ya mashahuda wakisema walinzi wanasema "Baba" yao hakuwa amelala nyumbani usiku uliotangulia.

Kwa kero hiyo, majirani waliita polisi wa Kituo cha Kawe na walikuja kumbeba "bulldozer" na kumuweka ndani. Baadae alihamishwa kituo kingine baada ya pale Kawe kuendelea kufanya fujo mle "Behind Ze Baz"

Wanyetishaji wanasema Mzee wa Upako ni mpenzi wa bapa ndogo na kubwa. Inawezekana juzi aliwapigia bapa majirani wanaomsakama ili kutoa aibu ya kuja kuwabwatukia, sababu wahanga wanasema "In Wine, There is truth". Yaani wengi huongea ukweli wakipata mvinyo kidogo.

Hii ni kama kashfa kwa mzee wa Upako, mchungaji maarufu na mwenye wafuasi lukuki ndani na nje ya nchi. Bulldozer mwenye kipindi channel Ten sasa anakatisha tamaa waumini wake. Je "kashfa" hii Mzee wa Upako atatoka hadharani na kuitolea ufafanuzi? Tusubiri na tuone.

Note: Naomba wenye "Daddy yao" tusiparuane tu hapa. Leo tumjadili Baba kwa matendo haya(Samahanini)

View attachment 438846View attachment 438847

Sijaona kashfa yoyote hapa!
 
Huyu mchungaji ni wa ovyo sana ana nyumba yake nyengine kule Mbezi Beach Jogoo pembeni ya Art Gallery yaani anaingia na wanawake mpaka mnashangaa..Yaani ni aibu kabisa mi nikimuona anavyokemea mapepo kwenye tv huwana nacheka tu

Hiyo nyumba anayokaa hana mke wake, mpaka aingize wanawake hovyo mkuu?
 
Ile barabara aliyohaidiwa na mzee pombe tayari? Asije akatumia pesa za tetemeko maana lusekelo mwenyewe keshatetemeka. Heri mimi ninayekunywa na natangaza kuliko huyo anayeombea walevi huku yeye kajaza watoto na vyupa uvunguni.
 
Uyo jamaa mbona afananii na lusekelo, maana yeye ni mfupi kidogo na mwili wake ni mnene kias, pia lusekelo avaag mashat ya mikona milefu atasiku moja, upenda kuvaa nguo za vitenge mikono mfup na sut za mikono mifup so atumiag mashat ya haina iyo na gar yake anayo tumia n range sport namba nmesahau ila ina anzia na A na izo V8 anazo mbil moja n kijan flan iv na nyngne n nyeus ambayo n new model,
Mleta mada huenda mnayenu lusekelo ila umeshindwa kututhibitishia kama n yeye.

Mimi ni jiran yake huku kibangu na sio muhumun wake

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Jana tu nimetoka kubishana Na mama watoto kuhusu Mzee wa upako wakati tunaangalia kipindi chake Chanel ten.

Mimi nikamwambia Mama watoto, Mzee wa Upako anasura ya kilevi mno Na anaonekana mlevi tena wa pombe Kali.

Sasa Kwa tuhuma hizi nakubaliana kabisa kuwa jamaa Ni chapombe.
Alafu anapendwa na kinamama sana mimi sijui anawapa nini hata!
 
NIMERUDI:
Nimecheki huku na huku lakini ni kama vile watu wanatafuta traffic(vistors kwenye blog zao) kama wengine wanvyotafuta like humu JF.

Hakuna kitu. ni ubabaishaji tu. Inawezekana kunatukio kama hilo. lakini limetiwa chumvi mno. kama nilivyosema habari hii inatoka kwa mtu mmoja na kujaribu kisambaza. LAKINI CHA ajabu haisambaziki kila ukitafuta huikuti. Ninafikiri wengi wanaogopa mkono wa sheria. Hongera sana sheria ya mitandao wakati mwingine tunaichukia lakini imeleta adabu. Adabu inarudi kwa kasi sana katika kusambaza upuuzi. BADO ni uongo na uzushi kama kweli weka hapa video au audio ama umeamua kuchafua jina na heshima ya Mzee wa Upako. Kuna huyo Binti anadai katika makala yake kwamba alikaa katika tukia zaidi ya masaa 3 halafu hana video wala audio. Sheme!!!.

Lakini Labda ni wale majirani waliomkwaza mzee wetu na sasa kwa aibu wanajaribu kuvunja heshima yake.

Mnielewe sikatai inaweza kuwa kweli kabisa. Wekeni ushahidi bila hivyo mnavunje heshima ya mtu kwa kutafuta "like" au kupata visitors kwenye blog zenu.
Ni PM namba yako nikutumie video
 
Sio vizuri kumsema vibaya kiongozi wa dini,acha nimkabidhi Mungu baba wa Mbinguni
Acha UOGA na UNAFIKI na UJINGA !!! Kwahiyo hata kama ni kiongozi KANJANJA na TAPELI ndio usimseme?

Huyu ni Kiongozi anayeongozwa na roho mtaka vitu.

Achukuliwe Hatua.
 
Lusekelo sijawahi kumuamini kama Mtumishi wa Mungu kweli.

Ni mtaka pesa tu...wajinga ndio waliwao
 
Back
Top Bottom