Kuwa na Tabia Njema / Mbaya huwa ni Maamuzi ya Mtu binafsi

Mivyumba

JF-Expert Member
Apr 20, 2017
275
532
Habari za Wakati Huu wakuu!!
Nina Ushauri Mdogo kwa Wale wanaokatishwa kuingia Kwenye Mahusiano na Baadhi ya Makabila Eti Kisa Sifa flani ulizisikia kutoka kwenye hayo Makabila.
Je,Ulishawahi kufanya uchunguzi kwenye Kabila lako/ ukoo wako ukazikosa hizo Tabia??? Kama MOYO wako Umempenda mtu acha kusikiliza maneno na Ushauri wa Watu ambao hawajui Hata hatma ya Maisha Yenu!! Ni wangapi waliooa mabamedi leo hii wanafuraha na Ndoa zao?? Maamuzi ya Mabadiliko ya Mtu,Yako ndani ya Mtu binafsi!! Hivyo mwenye Tabia mbaya/nzuri akiamua ndani ya Moyo wake kubadilika Kabila lake haliwezi kumzuia!!.
NGOJA NIKUPE USHUHUDA MFUPI.
Nilipokuwa niko Form two ,Shuleni Kwetu walihamia walimu wa 3! Mmoja wa Hao walimu alikuwa hajaoa na tulikuwa tunasali nae katika moja ya Makanisa ya Kipentecoste! Basi,tukazoeana na Yule Mwalimu na baadae akaomba nimtafutie Mke kama nina dada!! Nilichukulia masikhara,Kwahiyo nikawa nikikutana nae nikiwa na Marafiki zangu namuuliza Umempenda yupi😆Nayeye ananijibu Hakuna niliyempenda!!!
Siku Moja Alikuja Kunitembelea nilipokuwa nimepanga( Nilisoma Day- Igunga Day)Akamkuta mdada wa Nyumba Jirani Amekuja Kuomba kitu. Baadae huyu dada alipoondoka,akaniomba namba yake ya Simu akaniambia Amempenda. Nikamuuliza Utamuweza??? Akaniuliza Kwanini?? Sikutaka kumuelezea,ila Nikamwambia nikionana nae Nitamwambia then nitamuomba Namba yake!! Kimtazamo wa Kibinadamu nilidhani Yule Teacher Akizisikia zile Sifa za huyu binti asingekubali kabisaaaa,maana ni binti aliefukuzwa Shule mbili tofauti kutokana na Umalaya lakini pia alikuwa anachukuliwa na Maagent wa Magarii,lakini pia Wale madreva wa Malori kutoka Igunga hadi Dar na anaweza kumalizia hata wiki hayupo Nyumbani. Baba Yake alishamzila na mama yake alimsababishia hadi Pressure Kupanda yaani Kiufupi ule Mtaa Hadi mashuleni hakuna ambae alikuwa Hamjui.
Mimi nilienda Kuongea nae,akaniruhusu nimpatie ticha no then wakaanza muwasiliane hadi wakafikia process za Uchumba. Maneno yalikuwa mengi sana,nakumbuka hadi wazee wa Kanisa walimuita Kumzuia na Wakamshauri wamtafutie binti alietulia lakini aliwakatalia!! Alikuwa Akiniambia hii ni foolish Age,lakini Pia inawezekana Anafanya hivi kwasababu ya tamaa!! Nitaongea nae Atabadilika!!!. Ni Kweli walioana,Mungu akawabariki now Wana watoto 4 ! Huyu dada Ametulia sana na Wamestawi katika Mambo Yote( Kazi& biashara).
Hivyo basi,Angalia Moyo wako unazungumza nini Juu ya huyo mtu Halafu Muombe Mungu maana Yeye Haangalii kama Jinsi wanadamu wanavyotazama!! Utapishana na Mibaraka Yako kwa Kufuata historia za Makabila ambazo hazina uhalisia!!✍️
 
Back
Top Bottom