timu ya bunge, mpira wa miguu na pete zimeshinda kwenye mechi za jumamosi!
Hotuba muhimu za bajeti ni mbili tu. Ile ya Bajeti yenyewe inayosomwa na waziri wa fedha na ya ofisi ya Waziri Mkuu. Hizi nyingine ni kwa ajili ya posho kwa Wabunge masikini. Wabunge na mawaziri wengi wako hapa Dar sasa hivi.Ni kweli, so far sijaona wachangiaji wa maana aliowasoma!
magamba bwana: Eti tunamlaumu bure mh ngeleja amepewa fedha kidogo kwenye bajeti yake! Mbunge wa kwanza kuchangia ndio kaunga hoja mkono ila amedai kuwa mwakani kama tatizo la umeme likiendelea eti "hawatapitisha bajeti ya nishati na madini!"
.....walicheza na wale waomba nauli.......wabunge wakatumia ''posho''
CCM yamwaga pikipiki Kawe
Monday, 18 July 2011
NA KHADIJA MUSSA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa pikipiki 15 kwa vijana wa jimbo la Kawe, Dar es Salaam, ambapo pia kimezoa wanachama wapya 200, baadhi wakiwa kutoka vyama vya upinzani.
Pikipiki hizo ni sehemu ya 26 zilizotolewa na Chama kwa ajili yavijana, ambapo 11 zimepelekwa mkoani Singida. Jumla ya gharama ya pikipiki hizo ni sh. milioni 46.8. Wanachama hao walijiunga na CCM jana, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Tegeta, ambao uliohutubiwa na Katibu wa NEC yaCCM, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba.
Kwa mujibu wa wanachama wapya, wamevutiwa na sera za CCM, hivyo kuamua kujiunga na Chama. Nchemba katika mkutano huo uliohudhuriwa na umati wa wananchi, wanachama na wapenzi wa CCM, alikabidhi pikipiki 15 kwa vijana wa jimbo hilo. Alisema pikipiki hizo zimetolewa kwa mkopo, ambapo vijana watatakiwa kuunda vikundi na kukabidhi sh. 30,000 kila wiki kwa kiongozi wa kikundi, yakiwa ni marejesho ili kuwezesha kununuliwa nyingine.
Katibu huyo wa NEC alisema fedhahizo zitatumika kununua pikipiki nyingine zitakazogawiwa kwa vijana wengine, ambapo kila mwezi mmoja atapatiwa. Aliwataka vijana hao kuwa waaminifu, kwani wakirejesha fedha hizo kwa wakati zitawezesha vijana 360 kupata pikipiki katika kipindi cha miaka mitano.
Nchemba alisema pikipikihizo zitawasaidia vijana kujipatia ajira, ikiwa ni utekelezaji wa Ilaniya uchaguzi ya CCM kwa vitendo. Aliwataka viongozi wa vyama vya upinzani kutumia nguvu na akili katika kubuni vitu ambavyo vitawakwamua wananchi kimaendeleo, na si kuchochea vurugu na maandamano, kwani hayana tija kwa taifa. Nchemba aliingia kwenye mkutano huo akiwa amepanda pikipiki, akiwa amefuatana na Katibu wa UVCCM Taifa, Martine Shigela.
Ngeleja jana tulikutana pharmacy akinunua VALIUM!!