Kura za wabunge inakuwaje zinaharibika?

watu wengine wanavyo argue inakera sana...walioharibu kura kina nani eti lyatonga lusinde (mind kura zilikuwa ni siri) sijui nani! mbona hamfikirii wale ambao walitaka tena kwa nia kabisa kususia uchaguzi huo ndani ya bunge lenyewe kuwa ndio wasie 1st suspect wa kuharibu kura na tumewasikia humu wanachama/washabiki wao wakilalamika na kutaka maelezo kwa kutomwandaa vyema mgombea wao. tuache hizi habari jamani....bila vitendo vya dhati tutalalamika humu kwenye forum 24/7 bila majibu! hoja zitakuja na kujadiliwa na kupita...wote tunaochangia humu hamjui mwenzie nani ni nani huu ni uppuzi kwa faida ya nani...kama tunavyovisema ni vya kweli! sipendi matusi na wala simtetei (lusinde kwa matusi yake) lakini kuna watu wangapi humu forumini wanatoa matusi tena ya nguoni kwa watu! Issue ni kuijenga TZ tunayoitaka! watu tumekuwa wanafiki sana tunadiriki hata kujifananisha na wanaoitwa simba wa Afrika inauma sana! wao walitoaka hadharani na kulitetea bara hili leo hii sisi kama vijana tunashindwa nn kutoka kifua mbele na kutetea haya tunayoyaona hayafai ukizingatia tunafacilities za kutosha kuliko enzi nzile tunabaki na sintofaham za kipumbavu mf Millya kuhamia CDM hakika sina ninalolijua kuhusu kuhama kwake chama...lakini sioni sababu ya wanaompokea kuwa na wasiwasi nay kwani kumpokea mtu si umemwamini tatizo nn! turekebishe siasa zetu tujenge nchi yetu....mimi ni mwanachama wa ccm ila naamini kweli ndani ya ccm kuna matatizo lakini hakika yanazungumzika na kuweza kutatatulika! ccm oyeee!
 
Akitangaza matokeo ya wagombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki Katibu wa bunge anasema kwamba kati ya kura 305 zilizopigwa kura 16 ziliharibika sawa na asilimia 6.2. Hivi inakuwaje wabunge wanakosea kupiga kura??

...Mbunge hakuridhika na rushwa aliyopokea toka kwa Wabunge watarajiwa au hakupata kabisa mgao wa rushwa hivyo kuamua kwa makusudi kuharibu kura.
 
Watakua akina Maji marefu, Komba (kalala), Wasirra (kalala), walipokurupuka tu wakaandika majina yao

wengine labda walikua hata hawajui kwanini wapo bungeni wakati ule
 
Hili ni tatizo kubwa sana kuliko tunavyolichukulia. Hapa tunazungumzia kwa kiingereza "the best of the best" yaani watu bora kati ya bora kwenye jamii. Mbunge anayewakilisha maelfu ya watu inakuwaje asiwe makini kwenye kupiga kura wakati hakuna hamaniko (tension) yoyote kwake wala shinikizo la kumfanya aogope kupiga kura vizuri.

Kura zimepigwa kwenye ukumbi mkubwa wenye usalama wa hali ya juu kukiwa na usiri mkubwa sana kwa wabunge wenyewe. Hawa kama ndiyo watu tulipowapeleka bungeni iwe kwa rushwa au kwa kupenda kwetu ni lazima kama taifa tujue kwamba tunalipa gharama kubwa sana ya kuwachagua kuwa wawakilishi wetu.

Majina ya walioharibu siyo ishu sana bali ni kwa nini wameharibu ndiyo jambo la kujadili!!
 
Je hawa ni aina ya wabunge wale waliosoma Primary school kwa miaka 9? Inashangaza sana sana Mheshimiwa mbunge kukosea kupiga kura. Nashindwa kuelewa kama ni suala la udhaifu wa kibinadamu au ukilaza!
 
Kama mbunge analala bungeni kama wasira, anashinda bungeni akigonga meza, akizomeazomea ovyo atashindwa kuharibu kura?
 
Hatujui form za kupigia kura zilikuwaje lakini maelezo ya Spika yanaweza kuwa yaliwachanganya baadhi ya watu

1. Kati ya makundi manne, matatu unatakiwa kuchagua watu wawili na moja uchague watu watatu [Ukichagua watatu kwenye kundi linalotakiwa uchague wawili kura imeharibika]

2. Kulikuwa na kundi maalum la wanawake na pia katika makundi mengine kama Zanzibar na Vyama vya Upinzani kulijitokeza wagombea wa kike. Wabunge waliulizia wanatakiwa kufanyaje hapo [Ukichagua wawili wanaume na mmoja mwanamke kwenye kundi hilo hilo moja, kura imeharibika]
 
Back
Top Bottom