Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

gombea wengi ambao wanasimamishwa na ccm huwa hawafikishi asilimia hamsini..... iweje leo? kuna mkono wa mtu hapa...
 
Bila CCM madhubuti nchi itayumba kabla ya kuchukuliwa na CDM!!

nashindwa kukuelewa unaposema nchi itayumba na kuchukuliwa na chadema,

nadhani nchi kuchukuliwa na chadema haina maana nchi imeyumba bali watanzania wametumia demokrasia yao, na suala la nchi kuyumba, to be honest nchi sasa INAYUMBA SANA TU
 
Hili jambo nilishangaa sana nilipoona matokeo. Katiba ya CCM inataka mshindi apatikane kwa zaidi ya nusu ya kura.

Sijui ilikuwaje kiongozi wa juu kama Mwigulu hakuliona hili?

Kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 walifuta hiki kifungu cha umuhimu wa nusu kwasababu kura zilikuwa zinapigwa na wanachama wote. Ilikuwa ngumu na gharama kuendesha uchaguzi mara mbili.

Kwenye chaguzi zote za mwanzoni ambazo zilikuwa zinafanywa na mkutano mkuu wa wilaya, nusu ni lazima.

Nafikiri wamefanya la maana kuamua kufuata katiba.
 
Kura za maoni zinarudiwa baina ya Sioi Sumri na W. Srakikya kwa kuwa hawakufukisha asilimia 50.Demokrasia CCM ni safu sana.Source: Nape kupitia Clouds FM
Katiba ya CCM inatamka chochote kuhusu kufikisha 50%? Au ni kwa ajili tu ya Jimbo la Arumeru?
 
Kura za maoni zinarudiwa baina ya Sioi Sumri na W. Srakikya kwa kuwa hawakufukisha asilimia 50.

Demokrasia CCM ni safu sana.

Source: Nape kupitia Clouds FM
Mkuu MAFILILI demokrasia gani unayo sema, ulevi wapombe na rushwa ndio demokrasia???? Kwa taarifa yako labda muwaweke TAKUKURU kwa vile wanawasikiliza bila hivyo fedha ya Mheshimiwa fulani itamwagwa tena na mtu wake apite!!!! Vueni magamba yatawaozesha mwili wote, poleni!!!!!

 
Unafiki mtupu,mbona za uraisi hawakusema zirudiwe?

hapo sarakikya imekula kwake kwani hatokuwa na hela ya kutoa rushwa tena na sioi atasonga mbele kwa kuwa anafadhiliwa na mamvi, kisima cha ela kisichokauka
 
Kura za maoni zinarudiwa baina ya Sioi Sumri na W. Srakikya kwa kuwa hawakufukisha asilimia 50.

Demokrasia CCM ni safu sana.

Source: Nape kupitia Clouds FM

CCM du ni noma ina maana hili hawakulijua tangu mwanzo hadi kumtangaz Sioi kuwa ndie mshindi? au kuna zengwe hapa kama ilivyo kawaida yao kwenye kura za maoni?
 
Kura za maoni za CCM kwa ajili ya kumpata mgombea wa jimbo la Uchaguzi Arumeru kurudiwa tarehe 1/03/2012!!
Hii ni kwa mujibu wa Nape akihojiwa na Clouds!!

Hakuna kanuni ya kufikisha asilimia hamsini kwenye kura za msono huu ni mkakati wa wazi wa kumnyang;anya kijana ushindi
 
Katiba ya CCM inatamka chochote kuhusu kufikisha 50%? Au ni kwa ajili tu ya Jimbo la Arumeru?

Katiba ya CCM inatamka hivyo. Ndio maana hata uchaguzi wa rais 1995 walirudia kati ya Mkapa na JK.

Nafikiri kilichowachanganya ni kwamba kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 walitoa waraka ambao uliruhusu washindi kupatikana kwa simple majority. Tatizo lilikuwa kwamba uchaguzi huo wanachama wote walipiga kura. Ingelikuwa ngumu na gharama kuandaa uchaguzi mwingine.

Kwenye changuzi ndogo, unatumika utaratibu ule ule kama wa zamani wa kutumia mkutano mkuu wa wilaya hivyo ingetakiwa mshindi apate zaidi ya nusu ya kura.

Nafikiri msimamizi alichemsha kwa kuamua kutumia taratibu zilizotumika kwenye mchujo wa CCM 2010.
 
Wemeogopa mpasuko...na hii ni janja ya kusubiri kuona CDM tutampitisha nani,nafahamu kuwa CCM wanmuogopa Joshua Nasari kwa kiasi kikubwa sana.Wanajua asipopita watapata mwanya wa kushinda kirahisi.
 
CCM ina vituko hahahahaa kuna wakati mtu unaamua unasema yetu macho! Ingawa nchi hii inajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno. Haya ngoja tuone keshokutwa nini kitajiri.
 
Kura za maoni zinarudiwa baina ya Sioi Sumri na W. Srakikya kwa kuwa hawakufukisha asilimia 50.

Demokrasia CCM ni safu sana.

Source: Nape kupitia Clouds FM

Sio safu sana ni safi sana kama sijakosea...nadhani furaha ilikuzidi baada ya kuona mgombea wako Sarakikya amerudishwa.Hongera sana mkuu,masalimie na mkeo.
 
Back
Top Bottom