Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

MADAI YALIOMUUA KOLIMBA CCM JUU YA 'UKWELI ALMASI' WA CHAMA KUKOSA DIRA WALA HAYANA TOFAUTI KUBWA NA YALE YA MWANASAYANSI GALILEO GALILEI KWA VIONGOZI WA DINI DUNIANI

Hata Mwanasayansi Galileo Galilei alipata kukatwa kichwa kwa maagizo ya viongozi wa dini baada ya kuelezea kwamba sura ya dunia ni dwara na kwamba inakwenda inachukua umbo mchongoko mfano wa yai.

Ni majuzi tu baada ya miaka zaidi ya 400 kupita ambapo Marehemu Galileo ametokea kuombwa radhi na viongozi wa dini baada ya kubainika wazi kwamba madai yake ki-uhakika ndio hasa ukweli wa mambo ulivyo.

Kwa nini mtu aje aone ajabu hii CCM Kombokombo ya 'Kamanda' Kikwete kuja kujikamua ujasiri wa kumuomba radhi Horrace Kolimba badala ya kumhonga mwanaye na viji-cheo cha U-DC, wakati Kolimba mwenyewe wala hajamaliza hata robo karne tangu auweke wazi huo 'udhaifu almasi' wa Chama Cha Mapinduzi miaka kadhaa iliopita????


CCM walikosea sana kumuua Kolimba kwani aliwaambia ukweli mtupu.
 
Katiba ya CCM inatamka chochote kuhusu kufikisha 50%? Au ni kwa ajili tu ya Jimbo la Arumeru?
Hayo ni marudio, technic hii ilitumiwa na Nyerere kipindi kile cha kumuweka Mh Ben kuwa mgombea toka CCM!!!!!!!!! Maji hayasahau mkondo!!!!!

 
Sasa wale wajumbe kutoka leguruki walotupa kadi zao pale ukumbini watakuja tena kupiga kura?? Au wataletwa wajumbe wapya toka monduli(sio arumeru mashariki).?????
 
Mbona MIGULU Baja Njemba alipata asilimia 42 iramba,ama nape aeleze labda marekebisho ya katiba ya chama cha magamba yamenza kazi.
 
hii ni kwa mujibu wa katiba yao au wao tu wameamua hivyo?naomba kufahamishwa wana jamvi.
 
Lengo la CCM ni kuhakikisha Sioi hagombei maana itaweka chama katika sura ya kiukoo zaidi. Mi nisema huko nyuma https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...aba-yake-arumeru-mashariki-3.html#post3360164 kuwa CCM haiwezi ku-affort' nepotism politics kwani wananchi wengi wamewashitukia kuwa viongozi wanaandaa watoto wao kuja kutawala watoto.

Kwa kuwa wagombea wote walioshindwa hawamuungi mkono Sioi, maana yake wafuasi wao pia, na hiyo ni ishara ya wazi kuwa Sioi hatagombea kwa ticket ya CCM.
 
Kama ni suala la katiba nadhani lilikua wazi na hakukua na sababu ya kamati kuu kukaa na kufanya hesabu na kugundua 50/50 haikuaaply so kura zirudiwe, baada ya matokeo ilitakiwa duru ya pili itangazwe hapo hapo na wagombea wajipange na si kwenda cc kuhesabu kura? (au ni utaratibu akikosekana mwenye 50% cc ndo inakaa na kutangaza duru ya pili au kamati ya uchaguzi husika?" MASWALI MAGUMU") hapa kwa maoni yangu SIOI atachinjwa kimya kimya duh... VITA YA MAKUNDI HII.
 
Kura za maoni zinarudiwa baina ya Sioi Sumri na W. Srakikya kwa kuwa hawakufukisha asilimia 50.

Demokrasia CCM ni safu sana.

Source: Nape kupitia Clouds FM
Red:- una maana gani ;chafu /safi sana

hakunacha demokrasia tumesikia leo kisa wanasema Sioi MTz sijui babaye alikuwaje mbunge hapa kuna harufu ya kumchakachua Sioi ndilo lengo ngoja tusubiri tuone
 
Muda wote katiba ya CCM inasema hivyo. Kwenye kura za maoni za mwaka 2010 CCM walibadili utaratibu na wakaamua wanachama wote wapige kura. Kwasababu ya ugumu wa ku organise uchaguzi wa wanachama wote mara mbili, wakaweka waraka wa uchaguzi ambao ulikuwa unasema mshindi atapatikana kwa a simple majority.

Kwenye by-elections kama hii ya Arumeru au ile ya Igunga wanatumia utaratibu ule ule wa zamani wa Mkutano mkuu wa CCM wa wilaya kwenye kura za maoni. Kwahiyo kwa maoni yangu mimi nilitegemea hata hicho kifungu cha asilimia 50 kitumike. Nilishangaa kwenye hili la Arumeru wakatumia simple majority.

Nafikiri msimamizi alichemsha na akatumia waraka wa uchaguzi wa 2010 kuendesha kura ya maoni kwa kutumia mkutano mkuu wa CCM wa wilaya. Kitu ambacho kilikuwa makosa.

wanaojua zaidi wamesahihisha na kwa mawazo yangu mimi wako sahihi.
 
...the funny thing is wanagombea nafasi ya pili nyuma ya Nassari, Chadema inatisha.

Kumbe Chadema wameishapitisha jina la mgombea wa kiti cha ubunge Arumeru, kwa hiyo March 3 mlisema mtatangaza jina la mgombea ni zuga bwegee.
 
Mnazungusha uongo weee wakati inajulikana wazi kwamba huyo Sioi Nassari ni chaguo la Lowassa, na wanataka kumpiga chini -Vita ndani ya chama inaendelea..
 
Back
Top Bottom