Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI
· Mchakato wa katiba umetawaliwa na uvunjaji wa sheria na kanuni, udanganyifu, uchakachuaji, vitisho na mabavu.
· Katiba inayopendekezwa imepuuza maoni muhimu na ya msingi ya wananchi.
· Badala ya mchakato kutumika kuunganisha wananchi na kuboresha muungano, mchakato umeligawa taifa na kuuweka muungano katika hali ya hatari kuliko kipindi kingine chote cha umri wake wa miaka 50.
· Nchi imesimama, CCM inalazimisha kusonga mbele.
Mchakato wa Katiba mpya umekamilika na kubakisha hatua ya mwisho ambapo katiba inayopendekezwa sasa itapigiwa kura ya maoni. Katika kipindi cha miaka zaidi ya 50 ya huru wa Tanganyika, uhuru na mapinduzi ya Zanzibar, na muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wananchi wa pande zote mbili za muungano hawajawahi kupiga kura ya maoni juu ya suala lolote linalohusiana na katiba ya nchi au Mfumo wa utawala. Hii inafanya suala la kura ya maoni katika kipindi hiki lichukuliwe kwa uzito unaostahili na wananchi wa pande zote mbili za muungano, lakini muhimu zaidi, kuikataa katiba inayopendekezwa kwani kama tutakavyojadili, mchakato wake pamoja na yaliyopo ndani ya katiba inayopendekezwa yanaelekea kulitumbukiza taifa katika machafuko makubwa.
Kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya Katiba, Mchakato wa Katiba ulitarajiwa kupitia hatua kuu nne kama ifuatavyo:
1. Tume ya Katiba Kukusanya maoni ya Wananchi.
2. Rasimu ya Kwanza kuboreshwa kupitia Mabaraza ya Katiba ya Kata.
3. Rasimu ya Pili kujadiliwa ndani ya Bunge Maalum la Katiba kwa nia ya kuiboresha bila kugusa moyo rasimu ya wananchi (tume) ambayo ni muundo wa muungano wa shirikisho lenye serikali tatu.
4. Rasimu iliyoboreshwa na Bunge Maalum la Katiba kupigiwa Kura ya Maoni na wananchi wa Pande zote mbili za muungano chini ya Kanuni ya theluthi mbili ya kura (2/3) .
Lakini kama ambavyo tayari historia imekwisha andika, badala ya mchakato wa katiba kufuata hatua hizi nne, kilichotokea ikawa ni sintofahamu kubwa kutokana na uvunjaji wa kanuni, uvunjaji wa sheria, na kila aina ya uchakachuaji, yote ambayo yameshavunja matumaini ya watanzania kwa mara ya kwanza tangia uhuru na muungano, kujipatia katiba iliyotokana na wananchi. Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya matukio muhimu ambayo yamepelekea matumaini ya wananchi kujipatia katiba yao, kutoweka:
1. Muswada wa mabadiliko ya katiba ulipelekwa bungeni kwa hati ya dharura tarehe 15 Aprili, 2011 huku ukiwa umejaa mapungufu ya kila aina. Kwa mfano, muswada husika ulipiga marufuku mjadala juu ya muundo wa muungano. Hali hii ikapelekea muswada huu kupingwa katika kila kona ya nchi, na hata kufikia hatua ya kuchwana na kuchomwa moto mbele ya Samuel Sitta kule Zanzibar.
2. Uteuzi wa Wajumbe wa bunge maalum la Katiba. Kwanza, wananchi hawakushirikishwa moja kwa moja kuchagua wawakilishi wao, na pili, wengi walioteuliwa walikuwa ni makada wa CCM.
3. Muswada ulirudishwa ndani ya bunge la muungani mara tano kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho. Lakini pamoja na Spika wa bunge hilo, Anna Makinda kuagiza muswada kufanyiwa marekebisho ikiwa ni pamoja na kuandikwa kwa lugha rahisi ya Kiswahili ili wananchi wengi waweze kuusoma na kuelewa, hakuna agizo lililo tekelezwa.
4. Uchakachuaji wa kanuni: Kanuni zikapindwa ili kumruhusu Rais wa JMT (ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa) kungia na kuhutubia bunge maalum la katiba baada ya mwenyekiti wa tume ya katiba (Jaji Warioba) kuwasilisha rasimu ya wananchi bungeni, badala ya Rais kuanza kabla ya Jaji warioba. Shughuli ya uzinduzi wa Bunge Maalum la katiba ikageuzwa kuwa ni mkutano mkuu wa CCM, ambapo Rais wa JMT na mwenyekiti wa CCM (taifa) akatumia fursa ile kutoa maoni na kuweka msimamo wa chama cha mapinduzi. Matokeo yake yakawa kwamba, badala ya mchakato wa Katiba mpya kuunganisha taifa lililogawanyika kwa miaka 50, mchakato wa katiba mpya umezidi kuligawa taifa vipande vipande.
5. Bunge likajichukulia Mamlaka nje ya Sheria ambapo likangoa maoni ya wananchi na kubandika Sura Mpya.
6. Mwenyekiti wa Bunge Maalum (Samuel Sitta) akavunja kanuni nyingine juu ya utaratibu wa pigaji wa kura bungeni ambapo pakalazimishwa uwepo wa kura ya siri na kura ya wazi kwa pamoja, utaratibu ambao ni wa kwanza kufanyika duniani. Hali hii ikazuia wajumbe wa bunge maalum la katiba kusimamia rasimu ya wananchi (tume).
7. CCM ikaja na mikakati ya kuwafunga midomo wabunge wake.
8. Hatimaye, Umoja Wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ukasema, sasa basi, imetosha, na kuondoka bungeni ili kuacha CCM iendelee na utungaji wa katiba yenye maslahi ya Chama cha mapinduzi, na sio maslahi ya Taifa bila ya kujalisha itikadi na siasa za vyama.
9. Pamoja na mapungufu yote haya ambayo yalihitaji bunge kusitishwa ili kuokoa fedha za wananchi zisipotee bure kwa kuandika katiba ambayo wananchi hawakuipendekeza, Bunge la Katiba likageuka kuwa Bunge Maalum la CCM. Hata baadhi ya wabunge wa ccm walitamka wazi kwamba bunge hilo limekosa mvuto. Ndani ya bunge lile, wananchi hawakuona mjadala wa rasimu iliyotokana na maoni yao, badala yake, walichoona ni mipasho na matusi.
10. Hatimaye, ikaamuliwa kwamba - kura za kuamua hatima ya wananchi zipigwe kwa njia ya Fax, gmail, SMS, whatasap, facebook, twitter, instagram, n.k. Yote haya yalilenga kupata uhalali wa 2/3 (theluthi mbili) za kura kwa hila na udanganyifu. Wananchi wakasikia baadae kupitia vyombo vya habari kwamba wapo wajumbe wa bunge maalum la katiba ambao walipiga kura hata kutokea majumbani, vitandani hospitali wakiwa hoi, na wapo ambao usiku walikuwa ni wajumbe wa upande wa bara, lakini asubuhi wakahamia kuwa wajumbe wa upande wa Zanzibar. Hivyo ndivyo 2/3 (theluthi mbili) ya kura ilivyopatikana. Hadi leo, kura hazijahakikiwa, na Katibu wa Bunge (Kashililah) bado anaendelea kutafuta majina mengine zaidi, ili mradi tu CCM ipate 2/3 (theluthi mbili) ya kura inazozitafuta.
Kabla ya kupiga kura ya maoni ya NDIO kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kujiuliza, je:
· JE - Haya ndio wanataka kuyaridhia na kuyabariki kwa kupigia rasimu inayopendekezwa kura ya NDIYO katika kura ya maoni?
· JE - Wananchi wanajua madhara watakayopata wao pamoja na familia zao Katika muda mfupi ujao na muda mrefu ujao, iwapo wataipigia kura ya NDIYO Katiba inayopendekezwa?
Wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari mapema na kuikataa katiba inayopendekezwa kwa kuipigia kura ya HAPANA kwa nguvu na kwa moyo wote. Katiba waliyoipendekeza ni ile iliyowasilishwa na tume ya jaji warioba, katiba ambayo CCM na serikali yake imeamua kuidharau na kuikataa licha ya ukweli kwamba rasimu ile ndiyo iliyobeba matumani na ndoto za wananchi .
Inaendelea
Cc MwanaDiwani, chama, Kobello, Mtanganyika, ZeMarcopolo, Pasco, JokaKuu, Jasusi, Ritz, Mkandara, Nape Nnauye, Gamba la Nyoka, Mag3, King Suleiman, EMT

Last edited by a moderator: