Kura Ya Maoni Na Hatima Ya Muungano

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI

· Mchakato wa katiba umetawaliwa na uvunjaji wa sheria na kanuni, udanganyifu, uchakachuaji, vitisho na mabavu.
· Katiba inayopendekezwa imepuuza maoni muhimu na ya msingi ya wananchi.
· Badala ya mchakato kutumika kuunganisha wananchi na kuboresha muungano, mchakato umeligawa taifa na kuuweka muungano katika hali ya hatari kuliko kipindi kingine chote cha umri wake wa miaka 50.
· Nchi imesimama, CCM inalazimisha kusonga mbele.

Mchakato wa Katiba mpya umekamilika na kubakisha hatua ya mwisho ambapo katiba inayopendekezwa sasa itapigiwa kura ya maoni. Katika kipindi cha miaka zaidi ya 50 ya huru wa Tanganyika, uhuru na mapinduzi ya Zanzibar, na muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wananchi wa pande zote mbili za muungano hawajawahi kupiga kura ya maoni juu ya suala lolote linalohusiana na katiba ya nchi au Mfumo wa utawala. Hii inafanya suala la kura ya maoni katika kipindi hiki lichukuliwe kwa uzito unaostahili na wananchi wa pande zote mbili za muungano, lakini muhimu zaidi, kuikataa katiba inayopendekezwa kwani kama tutakavyojadili, mchakato wake pamoja na yaliyopo ndani ya katiba inayopendekezwa yanaelekea kulitumbukiza taifa katika machafuko makubwa.

Kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya Katiba, Mchakato wa Katiba ulitarajiwa kupitia hatua kuu nne kama ifuatavyo:

1. Tume ya Katiba Kukusanya maoni ya “Wananchi”.
2. Rasimu ya Kwanza kuboreshwa kupitia Mabaraza ya Katiba ya Kata.
3. Rasimu ya Pili kujadiliwa ndani ya Bunge Maalum la Katiba kwa nia ya ‘kuiboresha’ bila kugusa moyo rasimu ya wananchi (tume) ambayo ni muundo wa muungano wa shirikisho lenye serikali tatu.
4. Rasimu ‘iliyoboreshwa’ na Bunge Maalum la Katiba kupigiwa Kura ya Maoni na ‘wananchi wa Pande zote ‘mbili’ za muungano chini ya Kanuni ya “theluthi mbili” ya kura (2/3) .

Lakini kama ambavyo tayari historia imekwisha andika, badala ya mchakato wa katiba kufuata hatua hizi nne, kilichotokea ikawa ni sintofahamu kubwa kutokana na uvunjaji wa kanuni, uvunjaji wa sheria, na kila aina ya uchakachuaji, yote ambayo yameshavunja matumaini ya watanzania kwa mara ya kwanza tangia uhuru na muungano, kujipatia katiba iliyotokana na “wananchi”. Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya matukio muhimu ambayo yamepelekea matumaini ya wananchi kujipatia katiba yao, kutoweka:

1. Muswada wa mabadiliko ya katiba ulipelekwa bungeni kwa hati ya dharura tarehe 15 Aprili, 2011 huku ukiwa umejaa mapungufu ya kila aina. Kwa mfano, muswada husika ulipiga marufuku mjadala juu ya “muundo wa muungano”. Hali hii ikapelekea muswada huu kupingwa katika kila kona ya nchi, na hata kufikia hatua ya kuchwana na kuchomwa moto mbele ya Samuel Sitta kule Zanzibar.

2. Uteuzi wa Wajumbe wa bunge maalum la Katiba. Kwanza, wananchi hawakushirikishwa moja kwa moja kuchagua wawakilishi wao, na pili, wengi walioteuliwa walikuwa ni makada wa CCM.

3. Muswada ulirudishwa ndani ya bunge la muungani mara tano kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho. Lakini pamoja na Spika wa bunge hilo, Anna Makinda kuagiza muswada kufanyiwa marekebisho ikiwa ni pamoja na kuandikwa kwa lugha rahisi ya Kiswahili ili wananchi wengi waweze kuusoma na kuelewa, hakuna agizo lililo tekelezwa.

4. Uchakachuaji wa kanuni: Kanuni zikapindwa ili kumruhusu Rais wa JMT (ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa) kungia na kuhutubia bunge maalum la katiba baada ya mwenyekiti wa tume ya katiba (Jaji Warioba) kuwasilisha rasimu ya wananchi bungeni, badala ya Rais kuanza kabla ya Jaji warioba. Shughuli ya uzinduzi wa Bunge Maalum la katiba ikageuzwa kuwa ni mkutano mkuu wa CCM, ambapo Rais wa JMT na mwenyekiti wa CCM (taifa) akatumia fursa ile kutoa maoni na kuweka msimamo wa chama cha mapinduzi. Matokeo yake yakawa kwamba, badala ya mchakato wa Katiba mpya kuunganisha taifa lililogawanyika kwa miaka 50, mchakato wa katiba mpya umezidi kuligawa taifa vipande vipande.

5. Bunge likajichukulia Mamlaka nje ya “Sheria” ambapo likang’oa maoni ya wananchi na kubandika Sura Mpya.

6. Mwenyekiti wa Bunge Maalum (Samuel Sitta) akavunja kanuni nyingine juu ya utaratibu wa pigaji wa kura bungeni ambapo pakalazimishwa uwepo wa ‘kura ya siri’ na ‘kura ya wazi’ kwa pamoja, utaratibu ambao ni wa kwanza kufanyika duniani. Hali hii ikazuia wajumbe wa bunge maalum la katiba kusimamia rasimu ya wananchi (tume).

7. CCM ikaja na mikakati ya kuwafunga midomo wabunge wake.

8. Hatimaye, Umoja Wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ukasema, “sasa basi, imetosha”, na kuondoka bungeni ili kuacha CCM iendelee na utungaji wa katiba yenye maslahi ya Chama cha mapinduzi, na sio maslahi ya Taifa bila ya kujalisha itikadi na siasa za vyama.

9. Pamoja na mapungufu yote haya ambayo yalihitaji bunge kusitishwa ili kuokoa fedha za wananchi zisipotee bure kwa kuandika katiba ambayo wananchi hawakuipendekeza, Bunge la Katiba likageuka kuwa Bunge Maalum la CCM. Hata baadhi ya wabunge wa ccm walitamka wazi kwamba bunge hilo limekosa mvuto. Ndani ya bunge lile, wananchi hawakuona mjadala wa rasimu iliyotokana na maoni yao, badala yake, walichoona ni ‘mipasho na matusi’.

10. Hatimaye, ikaamuliwa kwamba - kura za kuamua hatima ya wananchi zipigwe kwa njia ya Fax, gmail, SMS, whatasap, facebook, twitter, instagram, n.k. Yote haya yalilenga kupata uhalali wa 2/3 (theluthi mbili) za kura kwa hila na udanganyifu. Wananchi wakasikia baadae kupitia vyombo vya habari kwamba wapo wajumbe wa bunge maalum la katiba ambao walipiga kura hata kutokea majumbani, vitandani hospitali wakiwa hoi, na wapo ambao ‘usiku’ walikuwa ni wajumbe wa upande wa bara, lakini ‘asubuhi’ wakahamia kuwa wajumbe wa upande wa Zanzibar. Hivyo ndivyo 2/3 (theluthi mbili) ya kura ilivyopatikana. Hadi leo, kura hazijahakikiwa, na Katibu wa Bunge (Kashililah) bado anaendelea kutafuta majina mengine zaidi, ili mradi tu CCM ipate 2/3 (theluthi mbili) ya kura inazozitafuta.

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya “NDIO” kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kujiuliza, je:
· JE - Haya ndio wanataka kuyaridhia na kuyabariki kwa kupigia rasimu inayopendekezwa kura ya “NDIYO” katika kura ya maoni?
· JE - Wananchi wanajua madhara watakayopata wao pamoja na familia zao Katika muda mfupi ujao na muda mrefu ujao, iwapo wataipigia kura ya “NDIYO” Katiba inayopendekezwa?

Wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari mapema na kuikataa katiba inayopendekezwa kwa kuipigia kura ya ‘HAPANA” kwa nguvu na kwa moyo wote. Katiba waliyoipendekeza ni ile iliyowasilishwa na tume ya jaji warioba, katiba ambayo CCM na serikali yake imeamua kuidharau na kuikataa licha ya ukweli kwamba rasimu ile ndiyo iliyobeba matumani na ndoto za wananchi .


Inaendelea…


Cc MwanaDiwani, chama, Kobello, Mtanganyika, ZeMarcopolo, Pasco, JokaKuu, Jasusi, Ritz, Mkandara, Nape Nnauye, Gamba la Nyoka, Mag3, King Suleiman, EMT
 
Last edited by a moderator:
SEHEMU YA PILI

· Wananchi wanatakiwa kuelewa nini ni maana ya “Kura ya Maoni.”
· Wananchi wanahitaji kuelewa kwamba kuna tofauti kubwa baina ya “kura ya maoni” na kura ya kawaida katika uchaguzi mkuu na uchaguzi wa serikali za mitaa.
· Wananchi wanapaswa kujua kwamba uamuzi watakaoufanya kupitia kura ya maoni unaweza kuwa ni uamuzi ambao hawataweza kuubalidisha katika maisha yao yote.
· Kura ya maoni juu ya Mfumo wa muungano na katiba ya nchi imechelewa kwa miaka 50.

Hivi karibuni, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alinukuliwa akisema kwamba kuna haja ya taifa kumalizana na suala la Katiba Mpya haraka iwezekanavyo ili taifa liendelee na masuala mengine muhimu. Waziri Mkuu Pinda akaenda mbali zaidi na kusema kwamba kama ikiwezekana, wananchi wapige kura ya kuchagua viongozi wao pampoja na kura ya maoni kwa wakati mmoja – yani uchaguzi mkuu ujao mwakani (2015). Wananchi wana haja ya kuangalia mtazamo huu wa Waziri Mkuu Pinda kwa umakini mkubwa kwani bila ya uangalifu, wakiruhusu hali hiyo itokee, wataishi kwa kujuta kwa maisha yao yote.

Hakuna taifa duniani ambalo limewahi kuchanganya pamoja tukio la kura ya maoni inayohusu katiba mpya na tukio la kura ya kumchagua rais na wawakilishi wao. Iwapo wananhci watakubali hali hiyo itokee, Tanzania itakuwa ni nchi ya kwanza duniani kuruhusu suala hili litokee

Nini Maana Rahisi ya Kura ya Maoni? Tofauti yake na Kura ya kumchagua rais, wabunge na madiwani ni nini?

Tukianza na KURA YA MAONI, tofauti na kura katika chaguzi kuu ambazo huja kila baada ya miaka michache, kura ya maoni mara nyingi huwa ni tukio la mara moja katika maisha ya wananchi walio wengi, na ikitokea kwamba tukio hili likajirudia, basi ni mara chache sana.

Kura ya maoni:
Kura ya Maoni ni kura ya moja kwa moja(direct vote), inayolenga kuuliza wananchi juu ya suala Fulani la kisiasa, kijamii au kiuchumi kwa lugha nyepesi na inayoeleweka. Kura ya maoni huja baada ya serikali kufanya juhudi kubwa kuelimisha wananchi juu ya nini kilichomo lakini pia, juu ya umuhimu wa kura husika ya maoni. Kura hii huwa ni matokeo ya mahitaji yatokanayo na ‘legal framework’ ya nchi au mahitaji juu ya suala Fulani linalohusiana na sera ya umma (an issue of public policy). Tofauti na kura za chaguzi kuu, wananchi wanapoenda kupiga kura ya maoni, hawaendi kuwasilisha itikadi au siasa za vyama, bali maslahi yao kama wananchi wa taifa husika. Kwa maana nnyingine, Kura ya maoni huwa haina mahusiano yoyote na vyama vya siasa, badala yake, zinahusiana na masuala ya kitaifa bila ya kujalisha itikadi na siasa za vyama, au itikadi za kisiasa bali suala la utaifa au kitaifa.

Kura ya uchaguzi mkuu:
Kwa upande mwingine, Kura ya uchaguzi mkuu (uchaguzi wa rais, wabunge, madiwani, au serikali za mitaa), ni kura ambazo hujirudia rudia katika vipindi vifupi vifupi kuendan ana ratiba za chaguzi mbalimbali ndani ya taifa husika. Tofauti na kura za maoni ambazo mtazamo au orientation yake huwa ni ya “kitaifa”, kuta za chaguzi kuu zina uhusiano wa moja kwa moja na itikadi za vyama, siasa za vyama, mvuto (sura, tabia, msimamo) wa wagombea uongozi katika nafasi mbalimbali za kuchaguliwa n.k. Kura za aina hii huwa zina akisi kile au yale ambayo wananchi/wapiga kura huwa na “individual preference”, over and above/tofauti na masuala ambayo yanawaunga wananchi kama taifa bila ya kujalisha itikadi zao za vyama (e.g. muundo wa muungano, n.k). Kwa mfano, suala la muundo wa muungano halitakiwi kuwa ni sera ya chama cha siasa, bali linatakiwa kuwa ni suala la kitaifa. Na hii ndio maana mkataba wa Muungano (1964) haukutaja vyama vya siasa kwa ujumla wake, au chama kimoja kimoja kama vile TANU, ASP n.k. Suala la vyama lilikuja ingizwa katika makubaliano ya muungano kwa hila kupitia katiba iliyoitwa – katiba ya muda (1965), ambapo kwa mara ya kwanza, katiba ya chama ikawa ni sehemu ya katiba ya jamhuri ya muungano. Makosa haya ndio tunavuna hasara zake miaka 50 baadae.

JE - Kwanini hakujawahi kutokea “Kura Ya Maoni” inayohusiana na muundo wa Utawala na katiba ya nchi Tanzania?

Mbali ya sababu tulizogusia kidogo hapo juu, sababu za msingi juu ya kwanini taifa halijawahi kupiga kura ya maoni juu ya jambo linalohusiana na Mfumo wa Utawala au katiba ya nchi ni hizi zifuatazo:


  1. Utawala wa mwalimu ulipata uhalali kutoka kwa wananchi bila ya kujalisha sana katiba ya nchi.
  2. Uwoga wa watawala juu ya matokeo ya kura ya maoni.

Tukianza na sababu ya kwanza, uhalali wa utawala wa mwalimu nyerere chini ya chama kimoja cha siasa ulitokana na vyanzo vingine na nje kabisa ya katiba ya nchi. Vyanzo hivyo vya uhalali wa utawala wa Mwalimu Nyerere vilikuwa ni pamoja na:
· Itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyoweka mbele maslahi ya wananchi.
· Historia, Malengo na mafanikio ya Chama Cha TANU kutetea wanyonge ndani na nje ya nchi.
· Uwezo mkubwa wa kioungozi, Umaarufu na ‘Charisma’ ya kipekee ya Mwalimu Nyerere ambae hakutumia uongozi kujinufaisha binafsi na familia yake bali kwa manufaa ya watanzania wote. Katika mazingira haya, suala la katiba ya nchi halikuwa suala ambalo wananchi wengi walijali sana. Mwalimu alifanya mazuri na mabaya kwa nchi yake, na yeye alikiri hilo na hata kuomba msamaha kwa wananchi. Lakini mengi ya mabaya aliyofanya mwalimu, ubaya wake unaweza kupimwa zaidi katika muktadha wa “MATOKEO” au “MCHAKATO” uliohusisha sera au maamuzi fulani, lakini sio kwa kuangalia “NIA” ya sera au maamuzi husika. Moja ya mapungufu ya mwalimu ni pamoja na mfumo wa muungano wa serikali mbili, mfumo ambao uliundwa katika zama za mfumo wa chama kimoja, lakini muhimu zaidi, kwa mtazamo wa “panafricanism”.

Baada ya kuondoka kwa mwalimu madarakani, licha ya mazingira mengi ya kisiasa, kijamii na kiuchumi kuhitaji kura ya maoni, kwa muda mrefu watawala walikuwa waoga sana juu ya suala hili, hasa woga iwapo maamuzi ya “watawaliwa” (wananchi) yangeweza kwenda kinyume na matakwa ya “watawala”.

Masuala ambayo hufanya nchi kuingia katika “Kura Ya Maoni”.

Kama tulivyokwisha ona, kura ya maoni hutokea kwa nadra sana katika taifa lolote. Hii ni kwa sababu kura ya maoni huwa ni zao la matukio ambayo huwa hayajitokezi mara kwa mara ndani ya taifa, na hii ni sababu ambayo hufanya ‘kura ya maoni’ kuwa ni tukio la mara moja katika maisha ya wananchi wengi katika mataifa mbalimbali duniani. Matukio ambayo huzaa kura ya maoni ni haya yafuatayo:


  1. Pale Taifa jipya linapoanzishwa (new sovereign state or change of sovereignty), kwa mfano kilichojiri katika nchi ambazo zilizokuwa sehemu ya USSR, baada ya kuvunjikika kwa muungano huo miaka ya 1980s..
  2. Pale nchi inapoanzisha mchakato wa Katiba Mpya, mchakato ambao huitimishwa kwa kura ya maoni.
  3. Pale Taifa linapotaka kujiunga na nchi nyingine, shirikisho au jumuiya ya kimataifa (kwa mfano Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Ulaya (EU), n.k.
  4. Pale nchi moja inapotaka kupata mamlaka yake nje ya masuala ya muungano, ya pamoja au ya shirikisho (Sub - State Autonomy).
  5. Pale panapotokea mabadiliko makubwa ndani ya jamii (major social changes or tranformation), kwa mfano mageuzi ya mfumo wa utawala kutoka chama kimoja kwenda vyama vingi au mabadiliko kutoka utawala wa kijeshi kwenda utawala wa kiraia.

JE – historia inatuambia nini juu ya masuala haya katika muktadha wa muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar?
Tayari imeshaandikwa katika Historia kwamba - mchakato wa katiba mpya haikuwa agenda ya CCM bali ya shinikizo nje ya CCM na serikali yake kama vile vyama vya upinzani, asasi za kiraia, wasomi na makundi mbalimbali ya kijamii. Hii ndio sababu ya msingi kwanini leo mchakato huu umegubikwa na sintofahamu nyingi. Kuna ushahidi wa wazi juu ya hoja hii:


  1. Katika uchaguzi mkuu wa 2010, suala la katiba mpya halikuwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM. Hii ni tofauti na Chadema ambao waliweka suala hili kama sehemu ya ilani yao ya uchaguzi.
  2. Rais Kikwete amekiri kwamba alipata upinzani mkali sana ndani ya chama chake (CCM) ambapo viongozi wake hawakupendezwa na wazo lake la kukubali kuanzishwa kwa mchakato wa katiba mpya.
  3. Waziri mwenye dhamana ya Katiba – yani aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba wa wakati huo, Celina Kombani, alitamka wazi kwamba taifa halihitaji katiba mpya, na kwamba katiba iliyopo (katiba ya 1977), inatosha.
  4. Mwanasheria mkuu wa serikali – Jaji Werema, nae alirudia maneno haya ya kiongozi mwenzake wa serikali kusema kwamba taifa halihitaji katiba mpya, iliyopo (katiba ya 1977) inatosha.

Kama tulivyogusia awali, historia ya Tanganyika na historia ya muungano, zote zimechakachuliwa, huku mshirika mmoja wa muungano (Zanzibar) akiendelea kupambana kufa na kupona ili historia yake, utambulisho wake (identity) na mamlaka yake (Autonomy) visipotezwe na mfumo mbovu wa serikali mbili kama ilivyotokea kwa historia, utambulisho na mamlaka ya mshirika wake mwenza wa muungano (Tanganyika). Uchakachuaji huu ndio sababu ya msingi kwanini muungano wa miaka 50 baina ya Tanganyika na zanzibar umetawaliwa zaidi na kero kuliko mafanikio. Kwa miaka 50, Muungano umekuwa ukiendeshwa kwa mabavu na vitisho badala ya ridhaa ya wananchi. Serikali ya CCM inasahau kwamba mlinzi wa kweli wa muungano wowote ule duniani ni wananchi walioridhia mfumo wa muungano. Mlinzi wa kweli wa muungano wowote haijawahi kuwa ni Vifaru na mabomu ya nyuklia, na muungano huo ukadumu. Hivyo tutakuwa sahihi tukisema kwamba kura ya maoni juu ya mfumo wa muungano imechelewa kwa miaka 50.

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya “NDIO” kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kujiuliza, je:
· Wananchi wanaelewa kwamba kupigia kura ya “NDIYO” rasimu inayopendekezwa ni kukubali kuzika moja kwa moja na kwa mujibu wa sheria, hadhi, historia, utambulisho na mamlaka ya Tanganyika ndani ya muungano? Ikumbukwe kwamba kura ya NDIYO itaipa serikali ya CCM uhalali wa kudumu katika hili, tofauti na hali ya sasa ambapo CCM inajua wazi kwamba mapungufu yote ya mfumo wa serikali mbili hayajawahi kupata ridhaa ya wananchi.

Inaendelea……
 
SEHEMU YA TATU
· Wananchi watakuja jutia Kura yao ya NDIYO
· Rasimu ya Chenge tayari imewachagulia mfumo wa muungano ambao ni tofauti na walichopendekeza wananchi kwa tume.
· Rasimu ya Chenge inawataka wananchi kupigia muundo wa muungano bila ya kuwapa fursa ya kuamua kama wanautaka muungano au hawautaki.

Kauli ya hivi karibuni ya waziri mkuu mizengo panda kukiri kwamba tulifanya makosa kuanzisha mchakato wa katiba bila ya kura ya maoni juu ya muundo wa muungano ni ushahidi tosha kwamba hata viongozi wa CCM na serikali yake wanatambua kwamba, kwanza muungano uliopo hauna ridhaa ya wananchi, lakini pili na muhimu pia, mchakato wa katiba mpya umejaa kasoro kubwa. Mtazamo wa Waziri Mkuu Pinda ni sababu tosha kwa wananchi kuelewa juu ya umuhimu wa kuipigia kura ya HAPANA katika inayopendekezwa.
· Ikiwa Waziri Mkuu anakiri kwamba kuna tatizo, kwanini hii isiwe ni sababu tosha ya wananchi kuamua kwa kura ya HAPANA ili kama taifa, tuanze upya?Kwa hali hii, wananchi wanatakiwa waikatae katiba inayopendekezwa ili taifa lianze upya.

Vinginevyo wananchi wakae wakijua kwamba kura yao ya NDIYO itakuwa ni kura ya kujuta na kusaga meno kwa maisha yao yote kwani kura ya NDIYO itakuwa ni kuhahalisha uchakachuaji wa hadhi, historia, utambulisho na mamlaka ya Tanganyika ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Swali muhimu kwa wananchi:
· JE, wananchi wanaelewa ni kitu gani wanachoambiwa na serikali ya CCM kwamba wakipigie kura ya NDIYO?

Pengine wananchi hawafahamu kutokana na njama nyingi za CCM katika kampeni kuanzia sasa, ambazo zinalenga kuwaondoa wananchi katika uelewa kwamba roho ya rasimu ya katiba ya wananchi (tume) ni muundo wa muungano, vinginevyo masuala mengine kama haki za vijana, watoto, akina mama, pamoja na umuhimu wake, ni haki ambazo zimekuwepo muda wote kikatiba. Tofauti kubwa baina ya katiba ya JMT (1977), na Katiba inayopendekezwa (2014) ni kwamba, haki hizi zimeongezewa maneno matamu zaidi.

Wananchi wanatakiwa waelewe kwamba katiba inayopendekezwa haitoi maelezo kwamba vijana, watoto na kina mama watadai haki zao kivipi au kwa mujibu wa sheria zipi. Badala yake Katiba inayopendekezwa inasema wazi kwamba sheria husika zitakuja kutungwa na bunge baadae. Huu ni mtego ambao vijana na akina mama hawajauona bado. Watapiga kura ya NDIYO kuunga mkono rasimu ya chenge na kuishia kuja kujuta na kusaga meno baadae.

Katiba inayopendekezwa haisemi bunge litakalotunga sheria za kulinda haki za wahusika ni bunge lipi. Iwapo rasimu hii inamaanisha bunge la JMT, ukweli ni kwamba – ni jadi na utamaduni kwa miswaada mingi ndani ya bunge la JMT kupitishwa kwa maslahi ya CCM, badala ya maslahi ya taifa. Kwa mfano, rejea muswada juu ya uhuru wa vyombo vya habari. Pamoja na umuhimu wa muswada huu kwa umma bila ya kujalisha itikadi zao za kisiasa, bado serikali ya CCM ilihakikisha kwamba muswaada huu unakidhi kwanza maslahi ya CCM kwanza, kabla ya maslahi ya taifa.

Ni haya haya pia yatafanyika katika miswada ya sheria juu y ahaki za akina mama, vijana n.k. Kuna haja ya wananchi kujifunza kutoka kwa majirani zao KENYA ambako, ndani ya katiba yao mpya, haki na fursa kwa makundi yote ya kijamii zimewekwa bayana ikiwa ni pamoja na jinsi gani na pia sheria gani zitatumika kwa makundi haya kudai haki na fursa husika pale ambapo haki na fursa hizo zinakosekana. Rasimu ya Chenge ipo kimya juu ya hili.

Swali linalofuata:

· Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIYO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, JE Wananchi wanaelewa kinachopendekezwa kupigiwa kura ya maoni na Rasimu ya Chenge?

Kinachotajwa katika ukurasa‘108', Rasimu ya Chenge, ni hiki:

["Mambo ambayo mabadiliko yake yanahitaji kuungwa mkono kwa zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa ma wananchi wa Tanzania Bara, na zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa na wananchi wa Tanzania Zanzibar katika kura ya maoni":


  1. Muundo wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
  2. Kuwepo kwa Jamhuri ya muungano.
  3. Kubadilisha mashrti ya ibara ya 129(1) (c) ya katiba hii.

Kuna utata hapa. Tutafananua:

Kwanza, kinyume na utaratibu duniani kote ambao unaweka utaratibu wa kura ya maoni kuwa ni robo tatu ya kura halali, rasimu ya chenge imechakachua kanuni iliyowekwa na tume ya jaji warioba (robo tatu ya kura halali), na kuweka kanuni yake ambayo sasa ni: ‘zaidi ya nusu ya kura halali", ikiwa na maana kwamba rasimu ya chenge sasa itahitaji 50.01% tu ya kura kupita na kuwa Katiba rasmi ya JMT. Kwa suala zito na nyeti kama katiba ya nchi, kanuni hii inaweka mazingira hatarishi ya kuligawa taifa juu ya muundo wa muungano kwani suala hili linatakiwa lipate ushindi wa kishindo (robo tatu ya kura), na sio ushindi wa tundu la sindano kama ambavyo huwa inatokea katika chaguzi kuu kwa mfano kule zanzibar na kupelekea hali ya instability isiyokwisha.

Pili, iwapo Wananchi watapiga kura ya NDIYO, basi wajue kwamba watakuwa wanaunga mkono mfumo wa muungano ambao hawakupendekeza kwa tume, yani mfumo wa serikali mbili. Kwa maana nyingine, kura ya NDIYO itakuwa ni kubariki suala la muundo wa muungano kuwa ni sera ya chama cha siasa. Suala la mfumo wa utawala wa nchi linatakiwa kupewa uzito wa kitaifa, sio uzito wa kichama. Wananchi wakifanya kosa hili, huko mbeleni, kila chama cha siasa kitakachoingia madarakani kitakuja na mfumo wake wa muungano. Hii ni hatari ambayo wananchi lazima waizuie sasa.

Tatu, wananchi wajue kwamba wanalazimishwa kupiga kura juu ya uwepo au kutokuwepo kwa jamhuri ya muungano bila ya kupewa fursa ya kuamua ni aina gani ya muungano wanaopendelea. Hili ni tatizo la kiufundi ambalo litakuja kuleta madhara makubwa sana kwa taifa siku za usoni. Vinginevyo, wananchi walishaamua kupitia rasimu ya tume kwamba, muundo wa muungano wenye serikali tatu, hivyo ni wajibu wa wananchi kuonyesha msimamo wao usiyo yumba katika suala hili.

Inaendelea…….
 
SEHEMU YA NNE

· Agenda ya Katiba mpya haijawahi kuwa ni agenda ya CCM.
· CCM haikuwa na lengo la kuwapatia wananchi katiba kwa mujibu wa matakwa ya ‘wananchi.'
· CCM kuwaambia wananchi katiba haina umuhimu kama huduma za kijamii ni kuwapotosha wananchi.

Wakati wananchi wanaendelea kupokea makada wa CCM majukwaani ambao wameanza kuzunguka nchi nzima kunadi katiba wanayopendekeza, kuna haja ya wananchi/wapiga kura kufahamu japo kwa ufupi historia ni jinsi gani na ni kwa hoja gani serikali ya CCM ilipinga ujio wa katiba mpya. Hii itasaidia wananchi waelewe kwamba CCM bado haina

Tukirudi nyuma kidogo katika historia, tunaona kwamba msimamo huu wa serikali kupinga katiba mpya haukuanza na awamu ya nne, bali ni msimamo wa miaka mingi ndani ya chama cha mapinduzi na serikali yake. Kwa mfano, miaka kumi na sita iliyopita, serikali ya CCM ilitoa "White Paper" (White Paper #1 of 1998) mahususi kwa ajili ya kuweka msimamo wake kupinga umuhimu wa katiba mpya. Nyaraka hii ya serikali ya CCM ilijenga hoja kwamba zipo sababu za msingi kwanini taifa huhitaji katiba mpya na kwamba sababu hizo bado hazijajitokeza nchini. White Paper hiyo ya serikali ikaorodhesha sababu kuu mbili za kwanin nchi hutaji Katiba Mpya:


  1. Sababu ya kwanza ni iwapo panatokea mabadiliko makubwa ya kijamii au mabadiliko makubwa ndani ya jamii (major changes in the society).
  2. Sababu ya pili ni iwapo panapotokea mabadiliko ya kimamlaka (Change of sovereignity).

White paper ya serikali ikaendelea kusema kwamba – tangia 1977, mwaka ambao katiba ya sasa ya JMT iliandikwa, sababu hizi mbili hazijajitokeza, kwahiyo taifa halikuwa na haja ya kuandika katiba mpya.

Tukianza na hoja ya kwanza kwamba moja ya sababu zinazopelekea taifa kuanzisha mchakato wa Katiba mpya ni ‘mabadiliko makubwa ya kijamii' (major changes in the society), katika hili, serikali ya CCM iliamua kuja na ‘definition' yake yenyewe juu ya nini maana ya ‘mabadiliko makubwa ya kijamii' (major changes in the society). Kwa maana nyingine, serikali ya CCM iliamua kuchachakua maana halisi ya ‘mabadiliko makubwa ya kijamii' (major changes in the society). Tutafafanua:

Mabadiliko ya kutoka mfumo wa chama kimoja cha siasa kwenda vyama vingi vya siasa mwaka 1992 kufuatia kazi ya tume ya jaji nyalali ‘qualified' suala la ‘mabadiliko makubwa ya kijamii' (major changes in the society). Kwa maana hii, wananchi walikuwa wamenyimwa haki yao ya kuandika katiba mpya kwa karibia miaka 20 (i.e 1992 hadi mwaka 2011 Rais Kikwete alipokubaliana na hoja ya muda mrefu ndani ya jamii kwamba Taifa linahitaji Katiba Mpya.

Tukija kwenye hoja ya pili inayohusu ‘change of sovereignty" kama sababu ya taifa kuandika katiba mpya, white paper ya serikali ya CCM ilijenga hoja kwamba tangia uhuru, tangia uhuru na tangia muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ‘change of soveregnity' zimetokea mara tatu tu, na changes hizi zilizaa katiba mpya katika nyakazi tofauti, na kuongeza kwamba, tangia muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hapajatokea tena ‘changes of soveregnity'. Hoja ya serikali ni kwamba:


  1. Katiba ya Kwanza ilikuwa ni ya Mwaka 1961, Tanganyika ilipopata uhuru wake kutoka kwa Mwingereza, na kupelekea Tanganyika kupata katiba mpya ‘as a new sovereign state'.
  2. Katiba ya Pili ikaja mwaka 1962, mwaka ambao Tanganyika ikawa jamhuri (a republic) rasmi, hivyo kujipatia katiba yake mpya.
  3. "HATIMAYE" - Katiba ya tatu ni hii ya sasa iliyopatikana mwaka 1977 baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Muungano huu ukazaa new sovereign entity – jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Haya ndio yalikuwa maelezo na msimmao rasmi wa serikali ya ccm (1998) juu ya kwanini taifa halihitaji katiba mpya. Kwa kifupi, white paper ya serikali (1998) ikahitimisha kwamba hapajwahi kuwa na ‘mabadiliko makubwa ya kijamii' (major changes in the society) yaliyohitaji katiba mpya, na badala yake, kumekuwa na change of sovereignity mara tatu, na mabadiliko yote haya yalipelekea kuandikwa kwa katiba mpya.

Swali la msingi linalofuata ni je:
· Iwapo huu ndio umekuwa msimamo wa serikali kwa kipindi kirefu, ni kitu gani kilibadilisha msimamo huu mwaka 2011, mwaka mmoja tu baada ya uchaguzi ambapo suala la katiba mpya halikuwa sehemu ya ilani ya uchaguzi?

Kwa mtazamo wetu finyu, upo uwezekano tena mkubwa sana kwamba kilichosukuma serikali ya CCM kuanzisha mchakato wa katiba mpya ilikuwa ni mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ambayo sasa yalitambua Zanzibar kama nchi. Mtazamo wetu finyu unaendelea kutufanya tuamini kwamba, kitendo cha Zanzibar kujitambua rasmi kama "nchi" kwa mujibu wa katiba yake (2010) kingepelekea umma (hasa wa Tanganyika) kuhoji juu ya ‘sovereignity status' ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya mabadiliko ya katiba ya Zanzibar (2010). Kwa maana nyingine, sababu ya CCM kuvaa kichwa kichwa mchakato wa katiba mpya ulitokana na matukio ya Zanzibar, na sio mahitaji ya wananchi, hasa watanganyika kama wananchi wengi wa Tanganyika wanavyoendelea kuaminishwa kwenye kampeni zilizoanza za kuhamasisha upigaji wa kura ya ndio kwa rasimu iliyopendekezwa katika kura ya maoni. Iwapo hatupo sahihi katika hili, basi wacha historia ije kutuhukumu.

CCM wamekabidhiana rasimu wakitambua wazi kwamba haina uungwaji mkono. Ndio maana wanaacha kunadi kwa wananchi moyo wa rasimu (muundo wa shirikisho la serikali tatu), na badala yake wananadi viungo kama vile vidole, magoti, makalio, n.k, viungo ambavyo bila ya moyo, ni viungo ambavyo havina kazi.

CCM wanaotambua kwamba walipobaki wenyewe ndani ya BLK, hakukuwa na cha maana zaidi ya uhuni wa kura ambao hauhitaji akili kubwa kubaini. CCM wanatambua kwamba katiba yao haikubaliki kwa wananchi na ni suala la muda tu kukataliwa hata kama watalazimisha iwe kama wanavyotaka.

Kwa sasa, mkakati wa CCM ni kuwasahaulisha wananchi mambo muhimu. Hivyo CCM inajitahidi kuwaaminisha wananchi kwamba mchakato umekamilika. Wanaaminisha wananchi hivyo ili wasahau uhuni uliofanyika kuanzia mwanzo hadi mwisho (rejea hoja za awali). Jitihada za CCM ni kuona wananchi wanajadili rasimu yao ya mafichoni kwa lengo la kuwasahaulisha kwamba mtiririko wake umejaa dhambi, uchafu na najisi kwa demokrasia.

Kama tulivyokwisha jadili, Rasimu ya CCM imeonekana kujibu hoja za wazanzibari badala ya matakwa ya watanzania kikatiba. Na katika kuficha ukweli, CCM wametumia mwanya wa kusema zipo haki za akina mama, watoto, wafugaji, vijana, wasanii n.k kama mkakati wa kutumia makundi haya kupitisha katiba haramu inayopendekezwa. Huku ni kuendelea kuwalaghai wananchi ili kuficha makosa, dhambi na uhuni uliotendeka dhidi ya taifa. Isitoshe, ni kusema kwamba kwa miaka 50, CCM haikujali haki za wananchi, lakini sasa imeona haja ya kuanza kujali haki hizo:

· Je hivyo ndivyo CCM inataka kuambia wananchi?

Lengo kubwa la CCM ni kuondoa umma katika mjadala halisi, mjadala muhimu kwa maisha yao ya sasa na baadae, na badala yake kuwatupia viungo vya katiba ili waridhike. CCM wanafahamu katiba yao imekosa ‘moyo' na ndio sababu hawakujadili muundo wa muungano katika vifungu husika.

Ni aidha:


  1. Walikwepa ukweli kuhusu muungano.
  2. Hawakuwa na majibu ya kero za muungano.
  3. Walikwepa ili waendelee na ulaghai wa miaka 50 iliyopita, na waendeleze ulaghai kwa miaka mingine ijayo.

Hali ya muungano leo ni mbaya zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Tofauti na muungano ambao waasisi wa muungano waliuacha – nchi moja, serikali mbili, leo muungano ni wa nchi mbili na serikai mbili. Muungano wa aina hii haupo na hauwezekani kutumika duniani popote, badala nchi mbili zinapoungana na kuwa moja, muungano unaozwaliwa ni aidha wa serikali moja, au serikali tatu. Basi.

Kama tulivyojadili awali, kwa sasa madai si wazanzibari bali watanganyika waliopuuzwa na kuendelea kubebeshwa mzigo mzito sana kwa maslahi ya Zanzibar. Madai ya watanganyika ni mazito na yanahitaji majibu. Ikizingatiwa kwamba ni watanganyika ndio wameshika muungano kwa asilimia zaidi ya 90, Kura ya maoni ya NDIYO katika mazingira ya mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa itakuwa ni pamoja na uwezekano mkubwa ‘uprising' (maasi) yatakayovunja muungano ni mkubwa.

Kwa wenzetu waingereza, Waziri mkuu wao – David Cameroon, ameliona hilo, ni kwa sababu hizo, Scotland kumefanyika kura ya maoni. Na kitendo cha wananchi wa Scotland kuamua kubaki ndani ya muungano kilitokana na ahadi walizopewa na uingereza juu ya utambulisho na pia mamlaka kamili katika masuala nje ya muungano. Na baada ya kura hiyo mengi yanaendelea kujitokeza. England sasa wana madai mazito kuhusu nafasi yao katika muungano, kama ilivyo kwa nafasi ya Tanganyika katika muungano. Hivyo kwetu sisi tumechelewa. Kama tulivyokwisha ona, Waziri mkuu Pinda alisikika akitamka kwamba laiti serikali ingelijua basi kura ya maoni ingetangulia kwanza. Na viongozi wangi wasiotajwa wana msimamo kama huo ambao umejadiliwa na wadau wengi kwa miaka kadhaa sasa humu jamvini na kwingineko.

Hapa tulipo sasa hakuna namna ya kusonga mbele. Kura ya maoni kwa rasimu ya CCM haitatoa majibu tofauti na wizi na uhuni uliofanyika ndani ya Bunge maaluum la katiba. Leo hii iwapo kura zinaibiwa bungeni, nani ataweza kuzuia wizi wa kura ya maoni Tukuyu, Namtumbo, Isevya, Muheza au kanyigo? Itakuwa ni busara kwa serikali ya CCM kuachana na kura ya maoni kwa katiba wanayopendekeza ili kuepuka sintofahamu nyingi zitakazojitokeza. Huu ni wakati sasa wa CCM kurudi ubaoni na kuanza kuchora upya. Mahali pazuri pa kuanzia ni kura ya maoni ambayo itahoji iwapo wananchi wa Tanganyika na Zanzibar bado wanautaka muungano, na kama wanautaka, ni mfumo gani ambao wangeupendelea zaidi. Mfumo utakaotokana na utaratibu huu, utalindwa na wananchi kwa nguvu zote tofauti na sasa ambapo mfumo wa serikali mbili ni sera ya chama cha mapindizu ambayo mlinzi wake ni vifaru, magari ya washaswasha, mbwana aina ya germany shepperd pamoja na farasi wa FFU.

Kura ya maoni inahitaji kufanyika kwa pande mbili za muungano kwani madai ya watanganyika hayawezwi kupuuzwa tena.
 
SEHEMU YA TANO

· Rasimu ya Chenge imefinyanga roho ya rasimu ya wananchi (muungano wa shirikisho la serikali tatu).

Rasimu ya chenge imeondoa Sura mbili muhimu za rasimu ya wananchi: Sura ya KWANZA na sura ya SITA. Sura ya kwanza iligusia masuala ya - jina, mipaka, alama, lugha na tunu za taifa. Na sura ya Sita iligusia suala la muundo wa jamhuri ya muungano. Kwa mujibu wa nyaraka za tume, maoni ya wananchi walio wengi yaligusa zaidi sura hizi mbili kuliko masuala mengine yote, hivyo kufanya sura hizi, hasa sura ya sita kuwa ndio moyo wa rasimu ya katiba ya wananchi (tume).

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya “NDIO” kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kwanza kufanya tathimini juu ya muundo wa muungano unaopendekezwa na rasimu ya Chenge, na kisha kufafanisha na maoni waliyoyatoa mbele ya tume ya jaji warioba. Iwapo wananchi watabaini mapungufu, hiyo itakuwa ni sababu tosha juu ya kwanini wanatakiwa kuipigia kura ya HAPANA rasimu ya Chenge kwa nguvu na mioyo yao yote, kwa manufaa yao ya sasa, na ya baadae.

Katika sehemu iliyosalia, tutafanyia tathmini rasimu ya chenge, na kuifafanisha na rasimu ya tume ya jaji warioba (rasimu ya wananchi), kwa nia ya kubaini mapengo yaliyopo.

Kuanzia kwenye utangulizi wa Rasimu ya Chenge, wananchi hawana sababu yoyote ya kuipigia rasimu hii kura ya NDIO ya ndio kwani haikidhi matarajio waliyokuwa nayo wananchi wakati wa mchakato wa kukusanya maoni yao uliofanywa kwa umakini mkubwa sana na tume ya katiba. Kwa mfano, rasimu ya wananchi (tume) inatamka hivi katika utangulizi wake:

[Na Kwa kuzingatia urithi ulioachwa na waasisi wa taifa letu wa kujenga nchi yenye umoja wa watu wake ambao hawabaguani kwa misingi ya ubakila, dini, rangi, jinsia au ubaguzi wa aina yoyote...”]

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya “NDIO” kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa wakumbuka kwamba:

· Kwanza, Waasisi wa muungano (Nyerere na Karume) walituachia muungano wenye serikali mbili na nchi moja. Tofauti na walichotuachia waasisi wa muungano wetu, Rasimu ya Chenge inahalalisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye “serikali mbili”, na “nchi mbili”. Rasimu ya tume ya jaji warioba ilijiridhisha kwamba uamuzi wa Zanzibar kuwa ‘nchi” kamili (2010), ni uamuzi ambao kamwe wazanzibari hawatorudi nao nyuma. Ni kwa sababu hii, tume ya warioba ikaja na mapendekezo ya mfumo wa serikali tatu ambao ulipunguza masuala machache ya muungano kama njia ya kulinda na kuboresha muungano uliopo.

· Pili, ni Viongozi wa serikali ya CCM kama vile William Lukuvi ndio walitamka wazi maneno ya kibaguzi (udini) kupinga serikali tatu. Ubaguzi huu haukuachwa na waasisi wa muungano.

Tukiendelea na sehemu ya utangulizi wa rasimu ya Chenge, pia inasema kwamba:

[“Na kwa uzoefu wa zaidi ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar na miaka 50 ya muungano wa jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu wa Zanzibar, na umuhimu wa ushiriki mpana na bayana wa wananchi katika utungaji wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.”]

Katika hili pia, kabla ya kupiga kura ya maoni ya “NDIO” kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:

· Je ni kweli kwamba wananchi walishirikishwa?
· Je, yaliyomo kwenye rasimu ya Chenge ndio maoni waliyotoa mbele ya tume ya jaji warioba?
Rasimu ya Chenge katika sehemu yake ya utangulizi inaendelea:

[“Hivyo basi katiba hii ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inayopendekezwa na bunge maalum la katiba imetungwa na sisi wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia kura ya maoni kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo na kuhakikisha kuwa jamhuri ya muungano wa Tanzania inaongozwa na serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia, utawala wa sheria, kujitegema na isiyofungamana na dini.”]

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya “NDIO” kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:

· Je, mchakato wa katiba inayopendekezwa ulizingatia sheria na kanuni husika?
· Je, bunge maalum la katiba lililopitisha rasimu inayopendekezwa ilikuwa na uhalali gani wa kisheria kufanya kazi hiyo?
· Je, ni kweli kwamba yaliyomo kwenye katiba inayopendekezwa yameheshimu maoni ya wananchi?

Kama tunavyo fahamu, roho ya rasimu ya wananchi (tume) imefutwa na Rasimu ya Chenge. Rasimu ya Chenge imefuta Sura ya KWANZA na sura ya SITA ya Rasimu ya wananchi (Tume ya Jaji Warioba). Tujadili yaliyofutwa ndani ya rasimu ya wananchi na kuyafafanisha na yaliyoingizwa ndani ya rasimu ya Chenge ili tubaini iwapo yana uhalali wowote, na iwapo yanaendana na matakwa ya wananchi walio wengi.

Sura ya Kwanza Ya Rasimu ya Wananchi (Tume), inazungumzia – Jina, Mipaka, Alama, Lugha na Tunu Za Taifa kama ifuatavyo:

[“Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Ni nchi Na Ni shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana Na muungano wa nchi mbili za jamhuri ya Tanganyika Na Jamhuri ya Watu WA Zanzibar ambazo kabla ya hati ya makubaliano, zilikuwa nchi huru.”]

Rasimu ya tume iliandika haya kwa nia ya kuokoa mgogoro uliojitokeza kutokana na hatua ya Zanzibar (2010) kuamua kujitambua Zanzibar kama nchi, yenye bendera yake, wimbo wa taifa, majeshi na amiri jeshi wake mkuu. Licha ya hatari hii kwa muungano, rasimu ya chenge inatamka yale yale ya miaka 50 ambayo yamepelekea Zanzibar kufanya iliyofanya 2010 kupitia katiba yake. Rasimu ya Chenge inatamka hivi:

[“Jamhuri ya Muungano WA Tanzania Ni nchi yenye mamlaka kamili ambayo imetokana Na muungano WA nchi mbili za jamhuri ya Tanganyika Na jamhuri ya watu WA Zanzibar ambazo kabla ya hati ya makubaliano ya muungano ya tarehe 22 Aprili, zilikuwa nchi huru”]

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya “NDIO” kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:
· Je, kwanini rasimu ya Chenge inawadanganya wananchi kwamba Jamhuri ya muungano ni nchi yenye mamlaka kamili wakati kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar (2010), Zanzibar nayo ni nchi, hivyo kufanya Jamhuri ya Muungano kuwa na nchi mbili – nchi ya kwanza ikiwa ni Zanzibar, na nchi ya pili ikiwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

inaendelea...
 
Katika Sura ya Kwanza, Rasimu ya wananchi (Tume) pia inatamka kwamba:

["Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni shirikisho la kidemokrasia linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa wa binadamu, kujitegemea, utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na lisilofungamana na upande wowote."].

Rasimu ya Chenge inatamka kwamba:
["Jamhuri ya Muungano WA Tanzania Ni nchi ya kidemokrasia inayofuata mfumo WA vyama vingi vya siasa, utawala WA sheria, inayoheshimu misingi ya haki za binadamu, isiyofungamana na dini yoyote na inayojitegemea".]

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:

· Je, kwanini rasimu ya Chenge inawadanganya wananchi kwamba Jamhuri ya muungano ni nchi yenye mamlaka kamili wakati kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar (2010), Zanzibar nayo ni nchi, hivyo kufanya Jamhuri ya Muungano kuwa na nchi mbili – nchi ya kwanza ikiwa ni Zanzibar, na nchi ya pili ikiwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
· Je, kwanini rasimu ya chenge imefuta maneno "usawa wa binadamu" na badala yake kuweka "haki za binadamu"?
· Je hii ni kwa sababu ndani ya muungano, hakuna USAWA wa binadamu kwa vile katiba inawapa wananchi wa upande mmoja tu wa muungano (Zanzibar) haki zaidi?
· Iwapo maneno "usawa wa binadamu" yangeachwa yawepo ndani ya rasimu ya chenge, je hilo lingechochea wananchi wa Tanganyika kuhoji mahakamani kwanini watanganyika na wazanzibari hawapo treated katika hali ya usawa?

Vile vile, Katika Sura ya Kwanza, Rasimu ya wananchi (Tume) inatamka kwamba:

["Hati ya makubaliano ya muungano iliyorejewa katika ibara ndogo ya (1) ndio msingi mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na katiba hii, kwa kadri itakavyorekebishwa itakuwa ni mwendelezo wa makubaliano hayo."]


Rasimu ya Chenge haijabadilisha ibara hii. Pamoja na hayo, lakini kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIYO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:

· Ipo wapi Hati ya Muungano?
· Iwapo hati halisi ya muungano ipo, kwanini upatikanaji wake ulitawaliwa na sintofahamu kubwa?

Moja ya masuala ambayo yaliainishwa chini ya mkataba wa muungano (1964) lilikuwa ni orodha ya mambo ya muungano ambayo ilikubaliwe iwe katika maeneo kumi na moja tu. Baina ya rasimu ya chenge na rasimu ya warioba (wananchi), ni rasimu ipi ambayo imelenga kuondoa kero katika suala hili:
· Je ni rasimu ya Chenge yenye mambo 15 ya muungano (kutoka 20) au rasimu ya warioba yenye mambo 7 ya muungano (kutoka 22)?

Katika sura yake ya kwanza , sehemu ya pili, rasimu ya tume, inatamka kwamba:

["Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni eneo lote la Tanganyika likijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar likijumuisha sehemu yake ya bahari"].

Rasimu ya Chenge inatamka maneno kwamba:

["Eneo la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni (a) eneo lote la Tanzania bara, ikiwa ni pamoja na eneo lake la bahari ambalo kabla ya muungano lilikuwa likiitwa jamhuri ya Tanganyika pamoja na maeneo mengine yatakayoongezeka; na (b) eneo lote la zanzibar, ikiwa ni pamoja na eneo lake la bahari ambalo kabla ya muungano lilikuwa likiitwa jamhuri ya watu wa Zanzibar pamoja na maeneo mengine yatakayoongezeka.

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIYO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:

· Ni maeneo yepi hayo ya muungano ambayo yataongezeka?
· Kwanini matumizi ya jina "Tanzania Bara" yasiendane sambamba na matumizi ya jina "Tanzania Visiwani?
· Kwanini jina la Tanganyika linafichwa huku jina la mshirika mwenzake wa muungano (Zanzibar) likiachwa liendelee kutumika?
· Kwanini Tanganyika inafichwa wakati mipaka yake (Tanganyika) na mipaka ya Tanzania bara ni ile ile kwani haijawahi kubadilishwa tangia uhuru wa Tanganyika?
· Yupi ni mshirika mwenza wa Zanzibar katika muungano, je ni Tanganyika na Tanzania bara? Kwanini Katiba ya Zanzibar inamtambua Tanganyika tofauti na Rasimu ya Chenge ambayo haimtambui Tanganyika?

Kwa mujibu wa rasimu ya Tume sehemu ya 3(2), sikukuu za kitaifa zitakuwa pamoja na:

1. Sikukuu ya uhuru wa Tanganyika itakayoadhimishwa tarehe 9 Disemba.
2. Siku ya mapinduzi ya Zanzibar itakayoadhimishwa tarehe 12 January.

Rasimu ya Chenge pia inatambua sikuu kuu hizi za kitaifa. Katika hili, lakini Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:

· Kwanini Rasimu ya Chenge kwa upande mmoja haitaki kuitambua Tanganyika lakini kwa upande mwingine inatambua siku kuu ya kuadhimisha uhuru wake?
· Kama Rasimu ya Chenge inatamka wazi kwamba Tanzania Bara ni nchi ambayo awali ilijulikana kama Tanganyika, kwanini basi sikuu kuu ya uhuru wa Tanganyika isitambuliwe na rasimu ya chenge kama "siku kuu ya uhuru wa Tanzania bara ambayo awali ilikujulikana kama Tanganyika? Consistency ipo wapi?

Katika sura ya Sita ya Rasimu ya Wananchi (tume) juu ya Muundo wa jamhuri ya Muungano, Rasimu hii inatamka kwamba, 60(1):

["Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni (1) Serikali ya jamhuri ya muungano (2) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (3) Serikali ya Tanganyika"].

Rasimu ya Chenge imefuta sura hii ya rasimu ya wananchi, na badala yake, katika sura yake ya saba, inatamka kwamba, 70 (1):

["Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa serikali mbli ambazo ni (1) Serikali ya jamhuri ya muungano (2) Serikali ya Zanzibar."].

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:

· Iwapo wakati tume inakusanya maoni ya wananchi, wananchi walio wengi walitumia muda wao mwingi zaidi kujadili juu ya muundo wa muungano, kwanini rasimu ya Chenge imepindua mapendekezo yao ya mfumo wa serikali tatu na kurudisha mfumo ule ule uliojaa kero ambazo zimekosa jawabu kwa miaka 50 (mfumo wa serikali mbili)?

Hivi karibuni, Katibu Mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alitoa kauli kwa niaba ya serikali kwamba – ‘ni sahihi kwa bunge maalum la katiba kuweka kando mjadala juu ya muundo wa muungano kwa vile suala hili limeligawa taifa'. Balozi Sefue akaendelea kusema kwamba "Muundo wa sasa wa muungano utabaki kama ulivyo sasa kwa kuwa bunge la katiba limeshindwa kupata maridhiano juu ya jambo hilo".

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:
· Ikiwa hakuna maridhiano juu ya muundo wa serikali tatu, yapo wapi maridhiano juu ya muundo wa serikali mbili? Maridhiano yake yametokana na nini? Hoja za akina nani? Maridhiano yalifanyika lini, wapi, na yalihudhuriwa na akina nani?

inaendelea...
 
sitaki muungano huu wa chuna buzi,wazanzibar wanatuchuna,fedha zetu zinawasaidia bure huku sisi bara huku tukinyanyasika,mafano hapa Rorya tunaishi kama wanyama vile hakuna maji,nymba za nyasi,ujinga na maradhi.....tuwe na ushirikiano wa kibiashara tu lakini si aina hii ya muungano ambayo yetu chao,chao chao
 
Tukizidi kuangalia hoja ya balozi Sefue kwa undani zaidi – hoja kwamba mjadala wa serikali tatu umeligawa taifa, kitendo cha Rasimu ya chenge kupindisha kanuni ya kura ya maoni kutoka 2/3 (robo tatu) kama iliyopendekezwa na rasimu ya wananchi (tume) na badala yake kuchakachuliwa na sasa kuhitaji "zaidi ya nusu" (kwa maana ya 50.01%), je:

· Ni matokeo yepi ambayo yataligawa taifa baina ya matokeo ya 50.01% na matokeo ya
· Ni matokeo yepi ya kura ya maoni juu ya muundo wa muungano ambayo yataligawa taifa baina ya matokeo ya kura ya maoni chini ya kanuni ya rasimu ya wananchi (robo tatu ya kura) na matokeo ya kura ya maoni chini ya kanuni ya rasimu ya chenge (50.01% ya kura)?

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa wakumbueka kwamba:

Hoja ya serikali tatu sio ngeni, na haijaletwa tume ya warioba, Chadema, Wala UKAWA, bali hoja imekuwepo kwa zaidi ya miaka 30. Kwa mfano:

· Kwanza suala la serikali tatu lilijitokeza kwa nguvu na kwa hisia kali kwa mara ya kwanza mwaka 1984 katika kipindi kilichoitwa "kuchafuka kwa hali ya hewa kisiasa Zanzibar". Wahusika wote katika sakata hili walikuwa ni wanachama hai na waaminifu wa CCM. Hapakuwa na tume ya jaji warioba, chadema, ukawa wala upinzani.

· Mwaka 1991, tume ya nyalali ilipendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika kipindi hiki, CCM ilikuwa ni chama pekee cha siasa, lakini muhimu zaidi ni kwamba, watumishi wote wa umma walitakiwa kuwa ni wanachama wa CCM kwa mujibu wa sheria. Kwahiyo wajumbe wote wa tume ya nyalali walikuwa ni wanachama hai na waaminifu wa CCM. Hapakuwa na tume ya jaji warioba, chadema, ukawa wala upinzani.

· Miaka miwili baadae, likaibuka sakata la G55 ndani ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao walidai uzinduzi wa Tanganyika. Wabunge wote 55 walikuwa ni wanachama wa CCM, akiwemo pia Spika wa Bunge maalum la katiba, Samuel Sitta. Serikali iliridhia hoja hii, na Samuel Sitta akiwa waziri mwenye dhamana husika (waziri wa sheria na katiba) akapewa jukumu la kuandaa ujio wa Tanganyika. Hapakuwa na tume ya jaji warioba, chadema, ukawa wala upinzani.

· Mwaka 1999, kamati ya jaji kisanga ilipendekeza mfumo wa serikali tatu, na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo alikuwa ni Asha Migiro, mwana ccm ambae leo hii ni mmoja wa makada wa ccm waliosimamia vilivyo kupinga rasimu ya wananchi (tume), hasa mfumo wa muungano wa serikali tatu.

· Pia mfumo wa serikali tatu ukapendekezwa na tume nyingine mbalimbali kama vile tume ya Amina Salum Ali, na Tume ya William Shelukindo, wote hawa wakiwa ni wanachama hai na waaminifu wa chama cha mapinduzi.

Hoja na sababu zilizotolewa katika matukio yote haya juu ya umuhimu wa serikali tatu zinafanana na hoja ambazo zilitolewa na wananchi mbele ya tume ya jaji warioba. Kila upande wa muungano ulitoa malalamiko yake (kitaasisi, lakini pia kwa mtu mmoja mmoja). Katika hotuba yake ya kukabidhi rasimu ya pili kwa rais kikwete viwanja vya karimjee mapema mwaka huu (2014), jaji warioba alitamka yafuatayo:

"Mheshimiwa Rais, Katika ripoti tunayokukabishi leo, tumeorodhesha malalamiko kumi kwa upande wa Zanzibar na malalamiko manane kwa upande wa Tanzania bara. Kwa upande wa Zanzibar, malalamiko matatu makubwa ni:

1. Serikali ya Tanganyika kuvaa koti la serikali ya muungano ambalo linasaidia Tanganyika zaidi kuliko Zanzibar. Koti hilo limeifanya Tanganyika kuwa ndio Tanzania.

2. Mambo ya Muungano yamekuwa yakiongezeka na hivyo kuathiri madaraka ya Zanzibar (autonomy) na kufifisha hadhi ya Zanzibar (identity) na Zanzibar inaendelea kumweza.

3. Kumwondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano.

Kwa upande wa Tanzania bara, malalamiko makubwa ni:
1. Zanzibar imekuwa nchi huru, ina bendera yake, ina wimbo wake wa taifa, ina serikali yake na imebadili katiba yake ili ijitambue kama nchi, wakati Tanzania bara imepoteza utambulisho wake wa Tanganyika. Katiba ya jamhuri inasema Tanzania ni nchi moja lakini katiba ya Zanzibar inasema Tanzania ni nchi mbili.

2. Zanzibar imebadili katiba yake na kuchukua madaraka ya jamhuri ya muungano, kama vile kuelekeza sheria za muungano zilizopitishwa na bunge la muungano zipelekwe kwenye baraza la wawakilishi. Maana yake ni kuwa katiba ya Zanzibar sasa ipo juu ya katiba ya jamhuri ya muungano.

3. Wananchi wa Tanzania bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi wakati wenzao wa Zanzibar wana haki hiyo Tanzania bara.

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:

· Iwapo wananchi walio wengi kutoka Tanganyika na Zanzibar waliwasilisha malalamiko haya juu ya muundo wa serikali mbili, je rasimu ya Chenge imejibu vilio vyao?
· Kwanini mshirika mmoja wa muungano aruhusiwe kuwa na utambulisho wake (Zanzibar) huku mshirika mwienzake wa muungano (Tanganyika) akiendelea kunyimwa haki hiyo ya Kikatiba?

Rasimu ya wananchi ilipendekeza suala la ardhi lisiwe moja ya masuala ya muungano ili kuondoa kero zilizopo juu ya suala hili.

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:

· Kwanini rasimu ya Chenge imeamua kufanya ardhi ya Tanganyika kuwa halali kwa wazanzibari kwa mgongo wa "utanzania" huku watanganyika wakinyimwa haki hiyo wakienda Zanzibar?

Rasimu ya Wananchi (tume) imeweka wazi suala la vyanzo vya mapato, matumizi na michango ya washirika wa muungano, ikiwa ni pamoja na kutamka kwamba kuanzia sasa, washirika wote wa muungano watatakiwa kuchangia kwenye gharama za kuendesha muungano. Tofauti na rasimu ya wananchi, rasimu ya Chenge katika sura yake ya SITA haitamki juu ya uchangiaji wa washirika wa muungano, na badala yake inaliacha tatizo hili libakie kama lilivyo kwa miaka 30 sasa.

Vile vile, katika sura ya SITA, rasimu ya chenge inatamka kwamba:

["Mamlaka ya kutoza kodi kwa mambo yote ya muungano kwa mambo yasiyo ya muungano yanayoihusu Tanzania bara yatakuwa chini ya serikali ya jamhuri ya Muungano."]

["Mamlaka ya kutoza kodi kwa mambo yote yasiyo ya muungano yanayoihusu Zanzibar yatakuwa chini ya seriklai ya Zanzibar".]

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:
· Kwanini Wazanzibari waruhusiwe kutumia fedha zao kwa masuala yasiyohusu Muungano, lakini watanganyika mapato yao yatumike kwa wazanzibari kupitia koti la muungano (Tanzania)?

Rasimu ya Chenge katika sura hii ya SITA pia inatamka kwamba:

["Mamlaka ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kukopa: Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka ya kukopa fedha ndani na nje ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa ajili ya kugharamia shughuli zilizo chini ya mamlaka yake"].

["Endapo mkpo utahitaji dhamana, serikali ya jamhuri ya muungano baada ya kushauriana na kukubaliana na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, yaweza kutoa dhamana kwa mkopo unaoombwa."]

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:
· Kwanini Tanganyika ikope halafu izuie kutumia fedha hizo kugharamia shughuli zilizo chini ya mamlaka yake – yani shughuli zisizohusu Zanzibar, kama ilivyokuwa kwa upande wa Zanzibar?
· Kwanini rasimu ya chenge haiji na maelezo juu y ajinsi gani Zanzibar italipa mikopo yake, hivyo kumaanisha kwamba anayelipa mikopo hii ya Zanzibar ni mtanganyika wa Tukuyu, Ikwiriri, Bumbuli, mtama, chalinze, na maeneo mengine ya Tanganyika?

Wananchi sasa wana fursa ya kutumia kura ya maoni kukataa mfumo kandamizi wa muungano kwa kupigia rasimu ya chenge kura ya HAPANA.


Tusemezane.
 
Kama wameweza kuchakachua kura bungeni la katiba basi ambapo watanzania tumeona kwa macho yetu na tumekaa kimya kura ya maoni ndo kabisaa itapita kwa kishindo
 
Wananchi wanatakiwa kuhoji:
· Kwanini Rasimu ya Chenge kwa upande mmoja haitaki kuitambua Tanganyika lakini kwa upande mwingine inatambua siku kuu ya kuadhimisha uhuru wake?

· Kama Rasimu ya Chenge inatamka wazi kwamba Tanzania Bara ni nchi ambayo awali ilijulikana kama Tanganyika, kwanini basi sikuu kuu ya uhuru wa Tanganyika isitambuliwe na rasimu ya chenge kama "siku kuu ya uhuru wa Tanzania bara ambayo awali ilikujulikana kama Tanganyika? Consistency ipo wapi?

Katika sura ya Sita ya Rasimu ya Wananchi (tume) juu ya Muundo wa jamhuri ya Muungano, Rasimu hii inatamka kwamba, 60(1):

["Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni (1) Serikali ya jamhuri ya muungano (2) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (3) Serikali ya Tanganyika"].

Rasimu ya Chenge imefuta sura hii ya rasimu ya wananchi, na badala yake, katika sura yake ya saba, inatamka kwamba, 70 (1):

["Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa serikali mbli ambazo ni (1) Serikali ya jamhuri ya muungano (2) Serikali ya Zanzibar."].

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:

· Iwapo wakati tume inakusanya maoni ya wananchi, wananchi walio wengi walitumia muda wao mwingi zaidi kujadili juu ya muundo wa muungano, kwanini rasimu ya Chenge imepindua mapendekezo yao ya mfumo wa serikali tatu na kurudisha mfumo ule ule uliojaa kero ambazo zimekosa jawabu kwa miaka 50 (mfumo wa serikali mbili)?

Hivi karibuni, Katibu Mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alitoa kauli kwa niaba ya serikali kwamba – ‘ni sahihi kwa bunge maalum la katiba kuweka kando mjadala juu ya muundo wa muungano kwa vile suala hili limeligawa taifa'. Balozi Sefue akaendelea kusema kwamba "Muundo wa sasa wa muungano utabaki kama ulivyo sasa kwa kuwa bunge la katiba limeshindwa kupata maridhiano juu ya jambo hilo".

Kabla ya kupiga kura ya maoni ya "NDIO" kuunga mkono Katiba inayopendekezwa, Wananchi wanatakiwa kuhoji:
· Ikiwa hakuna maridhiano juu ya muundo wa serikali tatu, yapo wapi maridhiano juu ya muundo wa serikali mbili? Maridhiano yake yametokana na nini? Hoja za akina nani? Maridhiano yalifanyika lini, wapi, na yalihudhuriwa na akina nani?
Hoja kubwa kutoka kwa wapotoshaji ni kuwa tume ya Warioba ilihoji watu wachache na hivyo kukosa 'uhalali'' wa muundo wa Muungano.
Swali; Tume ya Sitta ilihoji watu wangapi kiasi kwamba Rasimu ya Chenge imeamua kubaki na mfumo ule ule wenye matatizo miaka 50.

Pili, kama suala la muungano linagawa taifa, kwa miaka 50 tatizo linazidi kukua badala ya kupungua
Swali; Hivi watu wenye akili huwa wanakabili tatizo au wanakimbia tatizo? Na lini na nani atakuja kukabili tatizo linaloonekana kuligawa taifa si kwa S3 hata S2 au S1. Ni nani na lini atakuja kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu.

Tatu, kulikuwa na haja gani ya kuunda tume kwa mabilioni ya pesa iwapo Serikali ilijua muundo wa muungano unaligawa taifa. Je, sasa hivi taifa li pamoja kuliko ilivyokuwa miaka 2 au 3 iliyopita?
 
Kuna swali Mchambuzi kauliza kama yaliyopitishwa na BMK-CCM yaliheshimu maoni ya wananchi.

Ninaweza kutoa jibu hapana. Sababu ni kuwa hata yale waliyoondoa hawakuwa na majibu yake.
Kwa mfano, kuacha kujadili muundo wa muungano kama ulivyotolewa maoni na wananchi si kuheshimu mawazo yao.
Kwamba, kuondoa bila kuwaambia sababu zenye mashiko ni kuwadharau.

Sababu hafifu ni kuwa muundo wa muungano unaligawa taifa. Well, labda wangejiuliza, je miaka 50 ya muundo uliopo umelisaidiaje taifa? Je, matatizo yanayojitokeza yakiwemo kufungwa, kupigwa watu ni kuheshimu mawazo yao ya kutafuta ufumbuzi?

Kuheshimu mawazo ni pamoja na kuyatolea ufumbuzi. Jambo linapoachwa tu bila sababu kwasababu Chenge na Sitta wameamua ni dharau kubwa sana kwa maoni ya wananchi.

Tulipopata uhuru tulikwenda Lancaster house London kujadili namna tunavyoweza kuachwa tujitawale.
Miaka 50 ya kujitawala hatuwezi kutoa majibu ya matatizo yanayotukabili. Hivi kweli tumejitawala?

Tunaambiwa hilo jambo lisubiri wakati wake. Wakoloni wangemwambia Nyerere hivyo, hivi leo kweli tungekuwa huru!
Uhuru wetu ni wa nini kama si kuamua hatma ya taifa letu.

Katiba ndio mwongozo, tunapoogopa kujadili au kuheshimu maoni ya wananchi, maana hasa ya katiba ni nini?
 
Last edited by a moderator:
Katika badiko #8 kuna hoja alizoongelea rais wa Jamhuri ya muungano wakati anapokea rasimu ya Chenge iliyotokana na tume ya kukusanya maoni ya Sitta iliyohoji wananchi takribani 30.

1. Rais katika hotuba amesema '' Zanzibar sasa huru kukopa nje tena kwa dhamana ya JMT kikatiba'' misaada na madeni.
Sidhani kama Rais alishuriwa vema kutoa kauli hiyo. Ninasababu za kusema hivyo.
a) Znz inapopewa dhamana hiyo na JMT ina maana mzigo watakaochukua huko nje mwenye dhamana ni JMT.
Ndivyo ilivyotokea siku za karibuni wakati Kikwete alipowaruhusu wakope mchele Kenya kwa dhamana ya JMT.
Matokeo yake deni la mchele uliokwenda znz linalipwa na mkazi wa Mtimbira, Kicheba na Manyoni.

b) Zanzibar inakopa nje itatumia mikopo na misaada hiyo kwa ajili ya znz.
Kwa mujibu wa waziri Wassira, asilimia 4.5 ya pato la Tanganyika inayopewa znz ni kutokana na misaada na mikopo kwa JMT. Hapa ina maana Tanganyika inakopa na kuwapa wznz, wakati wao wanakopa na kubaki nacho.

c)Mikopo na misaada wanayosema akina JK ni deni la JMT ambalo ni la Tanganyika. Kuna nyakati inatumika katika shughuli kama ulinzi na usalama, mambo ya ndani na nje na uendeshaji wa JMT na SMZ.
Ulipaji wa deni hilo ni jukumu la Tanganyika, znz haina eneo inaloonyesha imelipa vipi deni hilo.

Hivyo wakati wao wanakopa kwa ajili ya shughuli zao, Tanganyika itakopa kwa shughuli zetu sote na wao, lakini deni la JMT linamkabili Mtanganyika. Hapa ndipo wananchi wanatakiwa kuona.

Swali, kama Rais Shein anasema znz ni sehemu ya JMT, wapi Tanga, Morogoro na Mbeya wamepewa fursa ya kukopa kwa ajili yao bila kupitia JMT na wakati huo huo walkichota kupitia JMT?

Mambo kama haya ni bomu lilotegwa kwasababu ipo siku, akina Chenge, Sitta na Kikwete hawatakuwa na nguvu za kiutawala. Mambo yanaweza kugeuka kwa usiku mmoja na kikatokea kisichotarajiwa tena kwa masikitiko.

cc Mag3
 
Last edited by a moderator:
Hivi itakuwaje, kwa mfano, Tanzania Bara wakipiga kura ya Ndiyo na Zanzibar kura ya Hapana?

Nauliza tuu in theory maana sidhani kama hili linaweza kutokea in practice anyway.

Huwa nawashangaa sana wale wanaodai kuwa wanaisubiri katiba inayopendekezwa kitaani wapigie kura ya Hapana.

Hata kama wengi wakipiga kura ya Hapana lazima kura za Ndiyo zitoshelezwe kwa namna yoyote ile.

Huo ndiyo ukweli wenyewe ambao wengi hawataki kuuamini. Lazima watu wakubali kuvuna walichopanda.
 
Hivi itakuwaje, kwa mfano, Tanzania Bara wakipiga kura ya Ndiyo na Zanzibar kura ya Hapana?

Nauliza tuu in theory maana sidhani kama hili linaweza kutokea in practice anyway.

Huwa nawashangaa sana wale wanaodai kuwa wanaisubiri katiba inayopendekezwa kitaani wapigie kura ya Hapana.

Hata kama wengi wakipiga kura ya Hapana lazima kura za Ndiyo zitoshelezwe kwa namna yoyote ile.

Huo ndiyo ukweli wenyewe ambao wengi hawataki kuuamini. Lazima watu wakubali kuvuna walichopanda.

Two thirds kwa Zanzibar haiwezekani, na hata kwa Tanzania bara, hakuna guarantee. Ndio maana rasimu ya Chenge imechakachua kanuni ya two thirds na kuipunguza to 50.01% ili Ile michezo ya kura baina ya CCM na CUF Zanzibar ifuate mkondo wake. Je CCM itafanikiwa?inategemea how one defines mafanikio, Vinginevyo Leo nape kasisitiza Kwamba kwa Mujibu wa Sheria husika, kura Hii inatakiwa ifanyike siku 84 baada ya bunge la Katika kumalizika. Tuombe uzima kushuhudia tukio Hilo muhimu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hiyi ni ilani ya ccm sio katiba,chenge kwenye ilani yake ameweka kanuni ya 50.1 ili kura ya ndio iweze kupita amesahau kuwa huku kwetu zanzibar kanuni hiyo hatuitambui coz tuna katiba yetu inayo elekeza kanuni y 2/3 ilikura ya ndio iweze kupita,katiba ya zanzibar inatuelekeza kuwa sheria yoyote inayohusu muungano lazima ije kwenye baraza la waakilishi ije kujadiliwa na lazima kanuni ya 2/3 itumike,je chenge amekwisha semezana na ccm zanzibar ambao wakiwepo zanzibar wapo pamoja na wazanzibar lakini wakiwepo machinjioni (dodoma)wanaufyata?
 
Hivi itakuwaje, kwa mfano, Tanzania Bara wakipiga kura ya Ndiyo na Zanzibar kura ya Hapana?

Nauliza tuu in theory maana sidhani kama hili linaweza kutokea in practice anyway.

Huwa nawashangaa sana wale wanaodai kuwa wanaisubiri katiba inayopendekezwa kitaani wapigie kura ya Hapana.

Hata kama wengi wakipiga kura ya Hapana lazima kura za Ndiyo zitoshelezwe kwa namna yoyote ile.

Huo ndiyo ukweli wenyewe ambao wengi hawataki kuuamini. Lazima watu wakubali kuvuna walichopanda.
Hili swali lako umeliuza mara nyingi. Lina mantiki sana, na sijui kama wameliona hilo tatizo.

CCM ni wazuri sana wa kuandaa ''mikakati''
Tayari wamebasdili sheria ili iwe 50.01%, kwa mfano znz wakiwa na 50%, basi Zakhia Meghji atapelekwa huko na Hamad Rashid. wanatosha kutengeneza 50.01.

Si unaona jinsi katibu wa BMK-CCM anavyotoa matokeo kila siku?
Leo anasema Zakhia amezaliwa znz. Gazeti la serikali lilimtaja katika kundi la bara. All spinning going on.

Spinning kama hizi mkuu Mkandara anaita 2/3
 
Last edited by a moderator:
Hiyi ni ilani ya ccm sio katiba,chenge kwenye ilani yake ameweka kanuni ya 50.1 ili kura ya ndio iweze kupita amesahau kuwa huku kwetu zanzibar kanuni hiyo hatuitambui coz tuna katiba yetu inayo elekeza kanuni y 2/3 ilikura ya ndio iweze kupita,katiba ya zanzibar inatuelekeza kuwa sheria yoyote inayohusu muungano lazima ije kwenye baraza la waakilishi ije kujadiliwa na lazima kanuni ya 2/3 itumike,je chenge amekwisha semezana na ccm zanzibar ambao wakiwepo zanzibar wapo pamoja na wazanzibar lakini wakiwepo machinjioni (dodoma)wanaufyata?
Ahh wapi, ikifika wakati CCM wanafanya vitu vyao hakuna cha znz. Kwani si wamechakachua matokeo yao wenyewe Dodoma wznz wakiwa macho wanaona. Tena ni hao wznz walioshirikia kuchakachua, akina Hamad Rashi walioenda znz usiku na kukutana na maruhani, wakayashawishi hadi maruhani hao wakapiga kura 2.

Hapa ilikuwa kutotambua tu hiyo kura ya maoni, CCM waitane wamalize wanachotaka, sisi tufikirie mchakato kwa njia nyingine.

Bobwe kwani hujui unafiki wa nduguzo?
 
Ndio maana rasimu ya Chenge imechakachua kanuni ya two thirds na kuipunguza to 50.01% ili Ile michezo ya kura baina ya CCM na CUF Zanzibar ifuate mkondo wake.

Tayari wamebasdili sheria ili iwe 50.01%, kwa mfano znz wakiwa na 50%, basi Zakhia Meghji atapelekwa huko na Hamad Rashid. wanatosha kutengeneza 50.01.

Najua nimeuliza sana maana siku hizi sifuatilii tena huo mchakato wa katiba mpya. Kuna sehemu nili-quote haya meneno ya Mama Fatma Karume.

So how will a party that is isolated win the necessary two thirds majority required to pass the Draft Constitution in Zanzibar?. I am told that there is a very simple, but effective way of doing it. So I am sharing this theory with all of you, if you care to know.

There are two electoral commissions responsible for voting in Zanzibar, the National Electoral Commission and the Zanzibar Electoral Commission. The former registers all persons resident in Zanzibar for the purpose of voting for the President of the United Republic of Tanzania and the latter registers Zanzibaris only, who have the right to vote for the President of Zanzibar.

The theory is that the definition of a Zanzibari for the purpose of the referendum will be expanded to include all those who are registered by the National Electoral Commission and who claim they are Zanzibaris.

This is despite the fact that there is a law in Zanzibar that defines what a Zanzibari is. In theory therefore, all Tanzanians who claim to be Zanzibaris, wherever they may be will have the right to vote in the referendum as Zanzibaris. You will no doubt all agree that it is a simple and effective theory because suddenly the voice of 1.2 million Zanzibaris can be drowned by the cacophony of 44 million Tanzanians.

In the end though, CCM will have to govern 1.2 million Zanzibaris in Zanzibar and the momentary drowning of their voices will only increase resentment and tension - By Fatma Amani Karume

Lakini bado wapo wenye moyo kama huyu.

Hiyi ni ilani ya ccm sio katiba,chenge kwenye ilani yake ameweka kanuni ya 50.1 ili kura ya ndio iweze kupita amesahau kuwa huku kwetu zanzibar kanuni hiyo hatuitambui coz tuna katiba yetu inayo elekeza kanuni y 2/3 ilikura ya ndio iweze kupita,katiba ya zanzibar inatuelekeza kuwa sheria yoyote inayohusu muungano lazima ije kwenye baraza la waakilishi ije kujadiliwa na lazima kanuni ya 2/3 itumike,je chenge amekwisha semezana na ccm zanzibar ambao wakiwepo zanzibar wapo pamoja na wazanzibar lakini wakiwepo machinjioni (dodoma)wanaufyata?

Time will tell. Waliweza kuchakachukua kura za wajumbe wa Zanzibar ndo sembuze kura za Wazanzibari?

Mlipanda mawe sasa ndo mnalazimisha kuvuna mahindi?

Tena mjiandae kabisa Zakia Meghi anakuja kupiga tena kura yake ya Ndiyo huko Zenchi.
 
Back
Top Bottom