Kupunguza gharama za uzalishaji, kuongeza bidhaa na faida

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
459
643
ECONOMIES OF SCALE

Hiki ni kitendo cha kupungua kwa gharama ya uzalishaji (Average cost) kadri ya uzalishaji wa bidhaa unavyoongezeka.

Njia ambazo zitamsaidia mfanyabiashara kupata economies of scale ni kama zifuatazo:

1. Kununua mahitaji yanayohitajika katika uzalishaji kwa bei ya jumla

Mfano:

Una miliki mgahawa, basi ni vyema ukanunua mchele, maharage, unga, mafuta kwa bei ya jumla ili kupunguza gharama za usafirishaji, na kukwepa kuuziwa bei ya rejareja.

2.Kuajiri wafanya kazi sahihi katika biashara yako.

mfano:

Umefungua biashara ya saloon ya kike, ni vyema kumuajiri mtu mwenye mkono mwepesi ambae anaweza kusuka, kufumua, kuosha nywele, kuweka dawa. Ili kupunguza gharama za kuajiri watu wengi kwa wakati mmoja wakati biashara bado ni changa.

Ni kheri umuajiri mmoja kwa mshahara mkubwa kuliko kuajiri watu 3 kwa mishahara midogo.

3. Kwenda na wakati kiteknolojia

Mfano:

Unamiliki parking ya magari, sasa badala ya kuajiri walinzi 10 kwaajili ya kulinda, uki install camera system au any other security system utakua umepunguza gharama na kuongeza faida

Mfano 2:
Muuza chips badala ya kuajiri wamenya viazi 5, basi ni vyema kununua machine ya kumenya na kukata viazi ili kazi iende kiurahisi.

4. Kuuza bidhaa mpya inayoendana na biashara yako.

Mfano:

Wewe ni muuzaji wa viungo vya chai kwenye mitandao ya kijamii na unalipia matangazo, ni vyema kuongeza bidhaa kama kuanza kuuza pia dawa za kupunguza unene nk

Gharama itapungua maana kulipia tangazo mfano instagram unaruhusiwa ku post picha 7 tofauti, kwaio gharama ya tangazo itabaki kuwa ile ile , ila mauzo yako yataongezeka kutokana na kuingiza bidhaa mpya .

Mfano 2:

Wewe ni mkulima wa maharage, unaweza panda maharage na mahindi kwa pamoja ili kuongeza uzalishaji wako.

Gharama ya kukodi shamba ni ile ile, wafanyakazi mshahara ni ule ule, umwagiliaji ni wa pamoja, gharama inayoongezeka ni mbegu ya mahindi tu. Ila faida itakuwa kubwa maana umeongeza production ya mahindi.

Mfano 3:
Wewe ni muuza vitumbua, unaweza anza kuuza pia mkate wa kumimina maana ingridients ni zile zile.

5.Kuuza bidhaa ya aina moja

Mfano:

KFC, MacDonald, vibanda vya chips, Wakala wa Bank, Wakal wa Coca, WWakala wa Pepsi nk

Kama kwenye biashara yako , wateja wako wakubwa ni wakitu kimoja kuzidi vyengine basi ni kheri kuuza hio bidhaa kwa wingi na kuongeza nguvu kwenye hio bidhaa .

Hii itakusaidia kupunguza gharama ya uzalishaji wa bidhaa nyengine ambazo hazikupi faida.

Wewe ni wakala wa makampuni ya simu, ila wateja wako wengi ni wa M-pesa , ni vyema kuamisha ule mtaji kwenye M-pesa na kuachana na vyengine ili uweze kupata faida na kupunguza gharama kama nauli kwenda kuweka hela kwenye mtandao flani nk

6. Kufanya biashara ambazo zinapewa ruzuku na serikali
Mfano:
Wakulima wa bidhaa ambazo zinauzwa nje kuna ruzuku wanapewa na serikali ambazo huwasaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza faida

7.Kufanya biashara ambazo zina bei zake ni elekezi
Mfano:
Petrol station (Bei za mafuta), Bus (nauli za mabus na madaladala) nk

8.Kuongeza ubunifu (Kuwaza nje ya box)
Mfano:
Wewe ni fundi cherehani, basi anzisha darasa la kufundisha wengine kuwa mafundi, hapo unakuwa umejipatia volunteers, pia umepata kipato chengine kwaajili ya kufundisha

9.Using the right equipment for the job
Mfano:
Unamiliki stationary, sasa badala ya kununua printer kivyake, scanning machine kivyake ni bora ukanunua machine kubwa moja ambayo itaweza kufanya majukumu yote kwa wakati mmoja. Hii itakusaidia kutumia nafasi yako vizuri katika frame uliyopanga, pia itakusaidia kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.

Mfano 2:
Fundi cherehani, ni bora kununua cherehani 1 ambayo itaweza kuweka zipu, kushona suti, kushona magauni ya harusi nk, kuliko kuwa na machine tofauti tofauti.

Mfano 3:
Unamiliki dry cleaner, ni vyema kununua washing machine ambayo, inafua, inasuuza na kukausha ili kupunguza gharamA, Pia badala ya kuwa na pasi ni kheri kuwa na steame ambayo itakusaidia kunyoosha nguo za wateja kiurahisi.

Kumbuka , biashara zinatofautiana, kuna vitu ambavyo vitasaidia katika kukuza biashara flani ila visiwe vitu sahihi vya kufanya ili kukuza biashara nyengine.

Karibuni kutoa maoni
diseconomies_of_scale_final-db85c494049d42aca10deb37e214a013.png

#bank #security #instagram #parking #economiesofscale #kuongezafaida #gharama #cost #productivity #economics #swahili
 
Hivi hizo mashine za kumenya viazi(kwa wauza chips) bei zake zimekaaje?
..... Na ubora pia uko vipi?
 
Karibuni kutoa maoniView attachment 2123738

#bank #security #instagram #parking #economiesofscale #kuongezafaida #gharama #cost #productivity #economics #swahili
Ahsante mkuu
 
Daah mendeleo yapo juu hadi viazi vina mashine za kuvimenya
 
Back
Top Bottom