Kupima uwezo wa Rais Jakaya Kikwete??

Hilo la bei ya bidhaa kupanda masokoni ni kweli ..nafikiri ni katika failures zake mpaka sasa lakini uchumi wa dunia Baba ..kuna external force behind this kitu ambacho chumi ndogondogo kama zetu muhali ku-escape..financial crisis,
 
Pole kaka, na pia asilimia kubwa ya barabara za Mkapa, zilikuwazishapangwa na kutafutiwa wafadhili na Mwinyi.

So kuna issue ya kupokezana vijiti mzee, ukiona mkandarasi yuko site, ujue kazi ya ujenzi na uchoraji ilianza miaka mitatu nyuma... okay!!!

So do not expect... unasanifu mwaka huu, unatoa tenda mwaka huu, ujenzi unaanza mwaka huu na unaisha mwaka huu... tulia kidogo ufikiri kaka... kujenga barabara sio sawa na kununua ndizi sokoni tandale.
Mkuu, tangu serikali ya awamu ya 4 iingie madarakani, ujenzi wa barabara mpya umesimama kabisa.

Umezungumzia kuwa awamu ya 3 ilijenga asilimia kubwa ya barabara zilizobuniwa na kufadhiliwa na wafadhili waliotafutwa awamu ya pili. Nadhani hapo kuna upotoshaji mkubwa.

Ukweli ni kwamba, awamu ya 2 iliiacha nchi ikiwa haikopesheki licha ya kufadhilika. Awamu ya 2 ilijenga barabara nyingi katika kipindi chake cha kwanza. Kipindi cha pili kilikuwa kitupu kabisa.

Ni kweli kuwa awamu hupokezana vijiti. Ila ni hakika kuwa kama mambo yataendelea kama yanavyoendelea sasa, hakuna ambacho kitapokelewa na awamu inayokuja, zaidi ya madeni na akaunti zilizokauka.
 
Haki-ya-Mungu, inamaana kukubalika kwa raisi Karume huko zenji na CUF tena ime change mwelekeo bwana Tumain. Mbona umenitisha mi najua we CUF to the bone.

Leo tena wana JF wamekua hawana shukurani haki ya Mungu au mwezi mchanga tena(joke).
 
Pole kaka, na pia asilimia kubwa ya barabara za Mkapa, zilikuwazishapangwa na kutafutiwa wafadhili na Mwinyi.

So kuna issue ya kupokezana vijiti mzee, ukiona mkandarasi yuko site, ujue kazi ya ujenzi na uchoraji ilianza miaka mitatu nyuma... okay!!!

So do not expect... unasanifu mwaka huu, unatoa tenda mwaka huu, ujenzi unaanza mwaka huu na unaisha mwaka huu... tulia kidogo ufikiri kaka... kujenga barabara sio sawa na kununua ndizi sokoni tandale.
Mkuu, tangu serikali ya awamu ya 4 iingie madarakani, ujenzi wa barabara mpya umesimama kabisa.

Umezungumzia kuwa awamu ya 3 ilijenga asilimia kubwa ya barabara zilizobuniwa na kufadhiliwa na wafadhili waliotafutwa awamu ya pili. Nadhani hapo kuna upotoshaji mkubwa.

Ukweli ni kwamba, awamu ya 2 iliiacha nchi ikiwa haikopesheki licha ya kufadhilika. Awamu ya 2 ilijenga barabara chache katika kipindi chake cha kwanza. Kipindi cha pili kilikuwa kitupu kabisa. Nchi ilikuwa hoi.

Ni kweli kuwa awamu hupokezana vijiti. Ila ni hakika kuwa kama mambo yataendelea kama yanavyoendelea sasa, hakuna ambacho kitapokelewa na awamu inayokuja, zaidi ya madeni na akaunti zilizokauka.
 
All of those will be great mkuu. Just support your point with facts & figures. Tupe data mkuu kuthibitisha yote usemayo.
Statistics zipo kaka..hivi vyote ni vitu unaona kwa macho yako yote mfano:-
1. Watu wanaotuhumiwa wako mahakamani (baadhi) hilo nalo huoni?? rais gani amewahi kufanya acha tanzania hata hapo karibu kenya...ambayo ni 20 most corrupt country in the world
2. Barabara zote nilizosema nimeziona na kupita kwasababu ya kazi zangu..Rukwa-mbeya, rukwa-kigoma, dodoma-singida, Aursha-Dodoma (inaendelea), Arusha- singida (inaendelea) jamani kwa miaka minne ..he has done something worth ...
3. Shule na Zahanati zimeanza kujengwa kila kata..shule ofcourse imeanza wakati wa mkapa..lakini zahanati ni Kikwete iniative, vyuo vikuu vimejengwa (state university of dodoma for example)..enrollment kuanzia primamry mpaka chuo kikuu ni kubwa kupita wakati wowote nchini..need more..ni mafanikio hayo???
 
Tumain,
Mkuu wangu hakuna mtu anayesema JK hajafanya kitu chochote..basi nchi ningekuwa sii nchi tena labda Somalia...kafanya alofanya na ndio yamezua mapungufu yake.
Tunapozungumzia Uongozi bora ni pamoja na kutambua matatizo, mahitaji mbele ya kutafuta sifa..
UFISADI ni swala dogo sana lakini lenye uzito na impact kubwa ktk maendeleo ya nchi..Ufisadi ni sawa na pacha ya tairi la gari ambayo inaweza kuipeleka gari msituni pamoja na kwamba matairi mengine matatu ni mazima.
Sasa ni ujinga kwangu kuamini kwamba dereva mzuri ataendesha tu hilo gari lenye pacha kwa kutafuta sifa wakati gharama ya kuziba pancha (Ufisadi) sii kubwa kama ufisadi unavyoharibu program zote ulozitaja.
Leo hii Hospital kubwa MUhimbili haina dawa iweje hizo Zahanati zipewe sifa kwa sababu zimejengwa kila kata. Shule kubwa za serikali hazina vitabu, walimu wenye uwezo malipo hafifu na hata wafanyakazi wa serikali wanalipwa chini ya kiwango.. Ni ujenzi gani wa shule kila kata utasaidia elimu yatu kama sii ongezeko la hesabu ya Majengo.
Uhuru wa habari na tolerance inaweza tu kuwa na sifa kwa rais ikiwa kuna lengo. Hii sheria imewekwa kwa maana kamili ya demokrasia nayo ni pamoja na kukubali kukosolewa lakini hufanyi kitu zaidi ya kuendeleza Libeneke, basi haina maana kabisa.

Sisi sote mkuu wangu tulitumaini mengi mazito kuotka kwa JK, na hasa mimi ilinichukua muda mrefu sana kuamini haya nayoamini leo..JK anaweza kuwa kiongozi mzuri lakini sii kwa nafasi hiyo!
 
Rais anasifiwa matokeo yakionekana, hauwezi kulazimisha sifa zisipostahili.
- Rais amefanya ziara bandarini, kuna uozo wa hali ya juu pale, akaishia zake. hamna maagizo wala nini. Watu bado wanapitisha mizigo Mombasa kusiko na rushwa.Sasa alienda bandarini kufanya nini?
- Alifanya ziara Magereza, hamna mabadiliko yoyote.
- Alifanya ziara moja USA akapata msaada wa $ 2 million akaitisha press conference na kutaja hiyo kama mafanikio ya ziara, wakati EPA zimeibiwa hela mara 70 ya hizo alizoopewa.
- Ardhi takribani ya ukubwa wa kisiwa cha Unguja amepewa mwekezaji na kufukuza wazawa Loliondo, hii ni mwaka huu.
- Alitembelea TRA akasema "nina majina ya wala rushwa wote hapa", sasa alifanyia nini majina yale?
- Amechagua baraza la mawaziri limejaa vihiyo na "wezi" haya ni maneno ya naibu waziri wa fedha juzijuzi , siyo yangu.

Rais wetu siyo decisive.
 
Haki-ya-Mungu, inamaana kukubalika kwa raisi Karume huko zenji na CUF tena ime change mwelekeo bwana Tumain. Mbona umenitisha mi najua we CUF to the bone.

Leo tena wana JF wamekua hawana shukurani haki ya Mungu au mwezi mchanga tena(joke).
Duh! wewe mimi CUF you are kidding..go on guessing? sijawi na sintaipigia CCM mpaka ikulu imeingia chama kingine...lol
 
Kweli tuna rais ambaye ni figure/symbol, maamuzi yana fanywa na watu wengine.
 
Mkuu, tangu serikali ya awamu ya 4 iingie madarakani, ujenzi wa barabara mpya umesimama kabisa.

Umezungumzia kuwa awamu ya 3 ilijenga asilimia kubwa ya barabara zilizobuniwa na kufadhiliwa na wafadhili waliotafutwa awamu ya pili. Nadhani hapo kuna upotoshaji mkubwa.

Ukweli ni kwamba, awamu ya 2 iliiacha nchi ikiwa haikopesheki licha ya kufadhilika. Awamu ya 2 ilijenga barabara chache katika kipindi chake cha kwanza. Kipindi cha pili kilikuwa kitupu kabisa. Nchi ilikuwa hoi.

Ni kweli kuwa awamu hupokezana vijiti. Ila ni hakika kuwa kama mambo yataendelea kama yanavyoendelea sasa, hakuna ambacho kitapokelewa na awamu inayokuja, zaidi ya madeni na akaunti zilizokauka.
Nilipo highlight ndugu hiyo si Kweli..unataka kufurahisha baraza..au una personal bifu na JK..nimekuonyesha barabara zinazojengwa na zinazoendelea kujengwa hapo juu...kwa spidi ya kufa mtu...
 
Hii ndio kazi kina Saliva na January wameshindwa kufanya. Naona Tumaini anawafanyia spin nzuri kuhusu aliyofanya Kikwete. Mpisheni afanye kazi ya usemaji wa raisi maana nyie mmeshindwa kazi.
 
Haki-ya-Mungu, inamaana kukubalika kwa raisi Karume huko zenji na CUF tena ime change mwelekeo bwana Tumain. Mbona umenitisha mi najua we CUF to the bone.

Leo tena wana JF wamekua hawana shukurani haki ya Mungu au mwezi mchanga tena(joke).

Tumaini hajawahi kuwa CUF huyo. Ni ccm to the bones.
 
inasikitisha pale mafanikio ya Rais yanapokuwa kujenga ma-gofu yanayoitwa shule na wananchi wanapigia makofi ujinga huu.

hakukuwa na sababu yoyote ya kujenga shule hovyohovyo 100 kwenye wilaya moja.wangeweza kujenga shule 30 standard na kuhakikisha fedha za magofu mengine 70 zinatumika kuimarisha shule zilizokuwepo.waaalimu wakifuzu huko mavyuoni then wangeendelea.modular format ingefaa hapa sio huu usanii walioleta.

kumsifia raisi kwa kujenga barabara ya Lami ya km 1000 au kujenga daraja moja kwa muda wa miaka minne ni kutazama chini ya pua.HE IS THE PRESIDENT,to be successful he should have done more than that.
hizo sifa za kupewa waziri sio Raisi.Viongozi wetu Afrika tunawasifia kwa kutimiza majukumu yao,viwango vyetu vya kutoa sifa viko chini sana ndio maana kiongozi anaiba weeee,kisha anajenga daraja na uwanja mnamuita kiongozi bora.huyu jamaa nae atasifiwa kwa kufungulia watu mashtaka,sio kuondoa rushwa.

siwezi kumsifia kiongozi hata mmoja Tanzania hamna anyestahili.kama angekuwepo,kina mama wajawazito wasingekuwa wanajifungua kwenye sakafu,umasikini usingekuwa katika kiwango cha sasa.ambapo do called middle income families wanakula milo miwili kwa siku.

hakuna wa kumpa sifa...,wote wameharibu.ndio maana tupo tulipo!
 
Tumaini hajawahi kuwa CUF huyo. Ni ccm to the bones.
Hunijui sikujui ..agh nikiwa chama chochote what is your point...vyote kihalali kikatiba...hapa tunaomgelea vigezo vya kupima uwezo wa rais na mafanikio ya urais wake finito
 
inasikitisha pale mafanikio ya Rais yanapokuwa kujenga ma-gofu yanayoitwa shule na wananchi wanapigia makofi ujinga huu.

hakukuwa na sababu yoyote ya kujenga shule hovyohovyo 100 kwenye wilaya moja.wangeweza kujenga shule 30 standard na kuhakikisha fedha za magofu mengine 70 zinatumika kuimarisha shule zilizokuwepo.waaalimu wakifuzu huko mavyuoni then wangeendelea.modular format ingefaa hapa sio huu usanii walioleta.

kumsifia raisi kwa kujenga barabara ya Lami ya km 1000 au kujenga daraja moja kwa muda wa miaka minne ni kutazama chini ya pua.HE IS THE PRESIDENT,to be successful he should have done more than that.
hizo sifa za kupewa waziri sio Raisi.Viongozi wetu Afrika tunawasifia kwa kutimiza majukumu yao,viwango vyetu vya kutoa sifa viko chini sana ndio maana kiongozi anaiba weeee,kisha anajenga daraja na uwanja mnamuita kiongozi bora.huyu jamaa nae atasifiwa kwa kufungulia watu mashtaka,sio kuondoa rushwa.

siwezi kumsifia kiongozi hata mmoja Tanzania hamna anyestahili.kama angekuwepo,kina mama wajawazito wasingekuwa wanajifungua kwenye sakafu,umasikini usingekuwa katika kiwango cha sasa.ambapo do called middle income families wanakula milo miwili kwa siku.

hakuna wa kumpa sifa...,wote wameharibu.ndio maana tupo tulipo!
1.sababu ya kujenga shule kila kata ilikwisha pita kama sera ya taifa tangu wakati wa mkapa na sera halali kwa ajili ya enrollmet ya wanafunzi Tanzania..unachongelea ni hatua ya pili ya uboreshaji wa shule zote kwa kuweka vifaa, walimu na vitabu ili tuweze kutoa elimu bora..step step by by brother resorces ni scarce always
2. Rais hatasifiwa kwa kujenga barabara?? lol asiyeshukuru kwa kidogo hata kubwa hata shukuru wewe una bifu lako mwenyewe..huo ni mwanzo tu...na barabara nilizotaja ni zaidi ya kilometa unazosema..get your record right..
 
Unapoongelea kuongeza idadi ya wanafunzi katika nyanja zote unamaanisha nini? Je kiwango cha kutojua kusoma na kuandika katika kipindi chake kimepungua au kimeongezeka? haalafu Je, ongezeko la wanafunzi linanakwenda sambamba na ongezeko na majengo, walimu vifaa vya kufundishia na mazingira mazuri ya kusomea? au ndo bora elimu? Mwanafunzi wa secondary anayesoma sayansi hajawahi kuiona test tube na unajivunua kuwa nimeongeza wanafunzi. Angalia vijana wa UDSM wanasomea madirishani hapo kweli kuna elimu au kudanganyana? sehemu za kulala shida wanafunzi wanapeana zamu kulaala! vitabu je? huduma ya internet? Ni afadhali uwe na kiasi kidogo cha wanafunzi lakini wanasoma vizuri na kuelewa na wanaweza kushindana kimataifa. tusipende sana kuangalia quantity bali tuangalia quality (what is our end product)
 
huyu n i raisi kimeo kuliko wote ambao Afrika imewahi kushuhudia, ila basi tu.
 
Kwa maoni yangu Kikwete uongozi umemshinda na mimi sioni chochote cha kumpongeza. Alipata ushindi wa "kishindo" kwa kuahidi kuipitia mikataba upya ya uchimbaji madini yetu ambayo ilisainiwa na Mkapa hadi hii leo pamoja na kuunda kamati ya madini bado mapendekezo yaliyotolewa na kamati hiyo hadi hii leo bado tunaendelea kupata 3% ya mapato yote ya dhahabu na kuwaachia wageni 97% ya mapato. Pamoja na bei ya dhahabu kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana (Wakati Mkapa anasaini Bei ya dhahabu ilikuwa ni dola 233 na sasa ni zaidi ya dola 1,100. Kwa kifupi bado tunaliwa kwenye rasilimali zetu.

Aliahidi Maisha bora kwa kila Mtanzania, sijui kama alikuwa na mikakati ya kuhakikisha hili analifanikisha vipi kama kiongozi au ilikuwa na kauli tu ambayo haikuwa na mikakati yoyote bali ni katika kupata kura nyingi toka kwa Watanzania.

Kwenye swaala la ufisadi mpaka sasa hivi ameshindwa katika kila ufisadi uliofanywa dhidi ya nchi yetu. Tukianzia Kiwira ambayo Mkapa alijiuzia kiwiziwizi mgodi ule wenye thamani ya shilingi bilioni 7 kwa shilingi milioni 700 tu na kulipa shilingi 70 millioni. Hadi leo Mkapa hajachunguzwa iliWatanzania tufahamu ni nani aliyeidhinisha uuzwaji wa mgodi ule. Mkapa pia alichukua mkopo wa shilingi bilioni 7 toka NSSF na hadi hii leo hakuna anayefuatilia mkopo huo ili Mkapa na Yona waanze kuurudisha. Pia si ajabu Mkapa na Yona wanaweza kulipwa mabilioni ya shilingi na Serikali eti kuwafidia katika "gharama" walizoingia kuhusiana na Kiwira.

Tukija EPA kitendo cha kutwambia kwamba wahusika wa EPA wamerudisha shilingi bilioni 70 na wakati huo huo kushindwa kuyaweka majina ya watuhumiwa hao hadharani na kiasi kilichorudishwa na kila mmoja kwa maoni yangu ni usanii wa hali ya juu. Na mimi siamini kama watuhumiwa wa EPA wamerudisha hata senti tano vinginevyo sioni ugumu wowote wa majina yao na kiasi walichorudisha kuwekwa hadharani. Kesi za EPA nazo zimejaa usanii mtupu hili siyo siri kabisa wote tunalijua. Balozi wa Marekani nchini wakati ule aliahidi nchi yake kuisaidia Tanzania kumrudisha nchini mhusika mkuu Balalli kama Serikali ingewaomba msaada huo, lakini Kikwete akaamua kukaa kimya bila ya kuchangamkia msaada ule mpaka Balalli "akafa"

Tukija kwenye ufisadi wa Kagoda wa $40 millioni tunajua fika kwamba muhusika na ufisadi wa Kagoda papa fisadi Rostam hawezi kabisa kuguswa hivyo hadi hii leo hakuna uchunguzi wowote unaofanywa ili Watanzania tuweze kufahamu nini kilichojiri katika ufisadi wa Kagoda ambapo zilichotwa

Tukija kwenye Rada yule mtuhumiwa Vithlani alikuwa nchini anahojiwa na vyombo vya dola, lakini kwa kuwa ufisadi ule unawagusa vingune wengi katika awamu ya tatu na ya nne basi wakampa upenyo akimbie nchi ili kuwasitiri wahusika wa ufisadi ule wa $12 millioni

Kwenye Richmond/Dowans nako mapendekezo ya kamati iliyoundwa na Bunge mpaka leo Kikwete na Serikali yake imeshindwa kuyafanyia kazi bila kuwa na sababu zozote zile za msingi na wahusika waliochota $172 millioni bila kuzifanyia kazi bado wanapeta mtaani na huku mjadala wake ukiendelea kwa mwaka wanne sasa

Meremeta ambapo $155 millioni zilichotwa, hii tumeambiwa kwamba inahusiana na usalama wa Taifa na wizi wowote unaohusiana na usalama wa taifa haustahili kujadiliwa popote pale!!! Mhhh!

Rukia "Mipasho" Simba anasema hawezi kujiuzulu hadharani. "Mzee wa Vijisenti" Chenge "Mnyunyizaji" anatamka hadharani kwamba hakuna anayemchunguza kama yupo amfuate jimboni kwake. Papa fisadi Rostam kwa mara ya pili anaomba uchunguzi wa Richmond ufanyike tena kwa sababu hakubaliani na ripoti ya kamati ya Bunge mara ya kwanza alitaka uchunguzi mpya ufanywe na majaji. Haya yote yanaonyesha kwamba hawa wameshafahamu fika kiongozi wa nchi ambaye ana madaraka makubwa aliyokabidhiwa na Watanzania baada ya kumchagua kwa "kishindo" hana kabisa ubavu wa kuyatumia madaraka aliyokabidhiwa. Hawa kila mtu anaropoka kivyake vyake tu maana wanajua hakuna athari yoyote itakayowapata kutokana na kuropoka huko.

Mashule yetu bado mengi majengo yake hayana hata hadhi ya kuitwa ****** wachilia mbali madarasa, asilimia kubwa ya Wanafunzi bado wanakaa chini walimu ndiyo wa kubahatisha na wakti mwingine hawako kabisa, huko CCM kutokana na uongozi wake dhaifu migongano chungu nzima isiyokwisha na kuonyeshana ubabe hadharani, na mipasho ya hali ya juu na wengine hata kutishiwa maisha yao!!

Mimi kwa maoni yangu ukitilia maanani ufisadi wa Richmond, $172, EPA $133 millioni, Rada $12 millioni, Meremeta $155 millioni Kagoda millioni $40 basi ni haki kabisa kutumia ufisadi kama kigezo cha kumpima Kikwete na hata tukitumia vigezo vingine vyovyote vile hakuna hata kigezo kimoja ambacho anastahili kupewa pongezi.

Sasa tukitilia maanani hayo yote niliyoyaandika hapo juu tutaona kwamba Kikwete siyo tu hastahili pongezi zozote bali pia hastahili kugombea tena 2010. . Tumeshaona Kikwete kama kiongozi alivyo dhaifu katika mambo mbali mbali na hii kwa maoni yangu ni sababu tosha kabisa ya kuhakikisha tunapata kiongozi mpya 2010 ambaye atakuwa tayari kuyatumia madaraka aliyonayo bila kumuogopa yeyote yule.
Kama kiongozi mwenye mediocre perfomance kiasi hiki anashindwa kuambiwa kwamba kazi tuliyokupa imekushinda hivyo kaa pembeni ili tumtafute kiongozi mpya basi Tanzania tuna matatizo makubwa sana

Mchango wangu wa thumni huo
 
Kikwete ni tumaini lililopotea. Wasaidizi wake ni ushahidi tosha na kigezo kizuri cha kupimia uwezo wake kwani udhaifu unapogeuka na kuwa sifa kuu ya kiongozi, ujue utawala wake uko rehani. Kiongozi dhaifu hukwepa majukumu na si ajabu wanafiki wakamsifia huku wakitoa lawama lukuki kwa wapambe - hapana tatizo ni Kiongozi mwenyewe, period.
 
Back
Top Bottom