Tumain
JF-Expert Member
- Jun 28, 2009
- 3,154
- 70
- Thread starter
- #41
Labda ni style yake..wengine wanaiita tolerance wewe unasemaje?, wanafiki wanaomsifia ni kina nani? wakati tunaongelea vitu vinavyonekana kwa macho yenu kila siku...kila mahali unaweza kuficha barabara? unaweza kuficha watuhumiwa wanaohaha mahakamani na kesi?..Kikwete ni tumaini lililopotea. Wasaidizi wake ni ushahidi tosha na kigezo kizuri cha kupimia uwezo wake kwani udhaifu unapogeuka na kuwa sifa kuu ya kiongozi, ujue utawala wake uko rehani. Kiongozi dhaifu hukwepa majukumu na si ajabu wanafiki wakamsifia huku wakitoa lawama lukuki kwa wapambe - hapana tatizo ni Kiongozi mwenyewe, period.