Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,920
- 2,798
Kuna changamoto kwenye sekta hii ya utumishi wa umma. Kubwa sana ni kukosa viwango (standards) na muendelezo (continuity). Hii continuity watu wa filamu wanaijua sana, la sivyo kazi zao zingekuwa vioja. Sasa vioja hivyo wanafanya hawa watumishi wa serikali.
Tukianza na standards nikiangazia idara mbili za umma (NHIF & RITA) Tunategemea pale ambapo mtafuta huduma anafika ofisi husika na kukutana na mtumishi ambaye anakuhudumia leo. Bahati mbaya ofisi za umma jambo lako haliwezi isha kwa siku moja. Sasa utakaporudi kesho na viambatanisho ulivyoagizwa unakutana na mtumishi mwingine ambaye naye anakosoa viambatanisho ulivyoagizwa awali. Unapoomba kuonana na yule wa awali pengine asiwepo muda huo au vyovyote tu.
Matokeo yake utaondoka na kwenda kufanya kadiri ya mtumishi wa pili alivyoelekeza. Pale unapoona sasa umekalimisha, hasa ujazaji wa nyaraka, makosa mengine yanaibuliwa katika nyaraka zako. Kwao kukuambia rudi kafanye hiki sio ishu. Hawaangalii muda na gharama utakazotumia katika ufuatiliaji.
Sambamba na hilo hawatoi taarifa sahihi kwa wateja kwamba utaratibu ni huu mwanzo hadi mwisho.
Najua kuwa wapo watumishi ambao wanajua kwa usahihi hatua kwa hatua nini cha kufanya ili mteja jambo lake likamilike kwa wakati. Tatizo linakuja pale ambapo utaelekezwa kwa mtumishi ambaye hayuko kwenye hiyo cheni ya huduma. Ndio hao hukosoa jambo ambalo awali lilishawekwa sawa
Kwenye suala la mwendelezo hapa napo pa kutazamwa. Leo unafika ofisi fulani. Unafanya yako kisha yanatokea mapungufu unaambiwa uje kesho. Kesho ukija unakutana na mtumishi nwingine au unaelekezwa kwa mwingine ambaye anataka uanze kumwelezea jambo lako upya. Inakera sana. Mwisho unamaliza jambo lako kwa kuchelewa, na pe gine ukiwa nje ya muda.
Utumishi wa umma ni sehemu muhimu sana. Hata kama nitaelekezwa kwa mtumishi mwingine kupata huduma ileile au mwendelezo wake, basi ajue afanyacho na sio kupiga ramli.
Lingine toka NHIF ni hiki kioja cha kulipia kumtoa au kurekebisha jina la mtegemezi. Kweli? Kwa vigezo vipi nataka kumtoa mtu kwenye list ya wategemezi wangu nipewe control numba nikalipie? Kufuta tu jina la mtu hata baada ya kuambatanisha vielelezo vyote nilipie? Hapa NHIF watupatie ufafanuzi kwa kweli.