Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,437
- 52,086
Kwema Wakuu!
Wapo Watu Wanazodoa baadhi ya wanaJF wakija kutoa malalamiko yao huku JF licha ya kuwa hatujuani. Wengine wakieleza mpaka mambo ya siri ya maisha yao. Wapo wanaoleta mambo ya kifamilia, wengine kazi, wengine kuwasema wazazi au ndugu zao. Wengine ishu za kazi.
Elewa kuwa kuna Watu humu waliotengwa na Ndugu. Elewa kuna Watu humu waliosalitiwa na Watu wao wa karibu kiasi kwamba wameona ni bora wajihusishe na Watu wasiofahamiana sura wala majina kuliko wanaowafahamu.
Elewa kuwa humu JF kuna Watu wanaodharauliwa mitaani, wasiosikilizwa hisia wala maoni yao. Lakini wakija humu wanasikilizwa na baadhi ya Member.
Elewa kuwa humu JF kuna Watu hawana wapenzi hata wa kuwatania lakini wakiwa humu wanawapenzi wao licha ya kuwa hawajuani kwa sura na majina.
Elewa kuwa, Humu JF kuna Watu waliotamani kusoma na kuwa na elimu za juu lakini maisha na hali ngumu za. Familia zao wakashindwa. Hivyo humu JF kwao ni shule wanajifunza mambo mengi kutoka kwa Member waliojitolea kutoa elimu buree bila malipo yoyote na wananufaika.
Mimi ni miongoni mwa Member ambao napigiwa simu na kufuatwa inbox na Watu mbalimbali wenye changamoto mbalimbali. Naelewa nikisema hivyo.
Hivyo kuna wale waliobahatika kuwa na uelewa mkubwa au kwenda shule za juu, au kwenda nje ya nchi wanaweza kuzuia wengine wasiandike kisa wao wanajua bila kujua kuwa wapo wenye uhitaji.
Elewa kuwa, wapo Watu humu wanakumbwa na majanga ambayo hawana Watu wakuwaambia pole hata moja. Hivyo wanapopost humu wanahitaji faraja hata ya mtu mmoja.
Kwa mfano mamamzungu ametoa post ya kufiwa na mchumba wake ambaye alikuwa mbioni kumuoa. Wapo waliomkejeli, wapo waliotaka kujua ukweli wa taarifa yake.
Kwenye mitandao ya kijamii kama hii ni vizuri jambo kama umeonelea halikuhusu sana ni bora upite kushoto.
Elewa kuwa wengine humu JF ni kama kijiweni, kijiwe cha kupiga soga na stori. Sio kila mtu anaweza kwenda kijiweni kwenye miti au anawashikaji huko mitaani. Wengine humu ndio wamawashkaji zao wanaopiga stori kwa uhuru kwani hawajuani na kuonyesha hisia, mitazamo yao kwa uhuru.
Wengine humu ni jobless, waende wapi, wakaongee na nani, ndugu na marafiki mtaani wamewakimbia. Kimbilio pekee ni humu JF kupiga Stori na kupoteza muda kuona kama upepo utabadilika. Wewe kama unakazi na unashughuli ya kufanya usidharau kwa kuwaona wanashinda mtandaoni au usiwaone umewazidi akili. Ni upepo tuu.
Elewa kuwa, kuna Watu humu hawana connection yoyote na hawana Watu wanaowajua lakini kupitia JF wamejuana na Watu waliosaidiana nao.
Unapomwambia mtu amalizane na familia yake, usiwe na akili fupi kama pipi kifua. Unauhakika kwamba anafamilia? Unauhakika familià yake ipo kumsaidia?
Wengine JF kwao ni familia yao. Humu wapo Baba zake, Mama zake, Kaka na dada zake. Anajua atapata kile atakachowaletea.
Nafahamu kuna Watu hawawezi kuvaa viatu vya wengine. Najua kuna Watu hawawezi kufanya imagination na kukadiria yanayowapata wengine. Tuache tabia ya Ubinafsi.
Acha nipumzike sasa
Mtibeli