Kuna ukweli khs uhusika wa makabila?

G M S

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
502
53
Wana jf naomba kujua kama kuna ukweli kwamba unapotaka kuoa unatakiwa kuwa makini kuna makabila yana utata wake pindi utakapoungana nao je nikweli? Ni makabila gani hayo? Na utata wao ni upi?
 
Imeanza kupitwa na wakati nadharia hiyo, makabila ambayo mfano ulikuwa ukitaka kuoa lazima watu wakushangae kidogo ilikuwa ni Wahaya, Wazaramo n.k lakini siyo kweli siku hizi watu wanaoana popote pale na kabila lolote bora tu tabia zao zinaendana na wanasikilizana.
 
Hiyo ni kweli kabisa.
Mojawapo ni hilo kabila lako.
Utata ni kuwa pamoja na wewe kufikia umri huo bado unatatizwa na maswali ya hivyo lol.
 
Wana jf naomba kujua kama kuna ukweli kwamba unapotaka kuoa unatakiwa kuwa makini kuna makabila yana utata wake pindi utakapoungana nao je nikweli? Ni makabila gani hayo? Na utata wao ni upi?

We oa tu bana................, hayo mambo ni imani zilizopewa nguvu na wazee wetu long time..............
 
kijana sikiliza....huo ni ukweli.
kila kabilia lina mila na desturi zake na mara nyingi hizi uwa sehemu ya makuzi ya binadamu...tuchukulie kwa mfano labda mtu amekuwa kwenye mazingira ambayo kumpiga mwanamke ni kawaida basi yeye pia ataona kuwa ni jambo la kawaida.
hivyo basi hivi vijitabia au malezi ni sehemu ya hiyo kabila (intrinsic characteristics) na hazikwepeki maa nyingi kwa kuwa umelelewa hivyo. kweli mtu anaweza kuzificha kwa muda lakini jua ya kwamba ipo siku itaibuka tuu.
sasa ni vyea ufahamu kiundani vijitabia vya makabila ili ujue mapema waingereza wanasema forewarned forearmed; kukuwezesha wewe kujua kama utaweza kuishi nae au lah. usipuuzie kabisa wala kudanganywa kuwa ni mambo yababu zetu....wale babu zetu walikuwa wanajua umuhimu wake!!!
 
Back
Top Bottom