Kwa wajuzi wa mila na desituli za makabila ya watanzania mje hapa mtujuze!

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,167
11,484
Kuna kitu kinaitwa 'watani'. Yaani kabila moja kuwa na kabila au makabila mengine na kujulikana kuwa ni 'watani zetu'.

Hiki kitu cha watani ukikichukulia poa unaweza kukosa fursa zilizo ndani yake! Kwa mfano: makabila yanayoitana 'watani' ni rahisi kukubalika katika kuoa/kuolewa hata urahisi wa kujenga urafiki kuliko makabila mengine ambayo hamuhitani 'watani'.

Sasa wajuzi wa mila na desituli hasa hasa za makabila ya kitanzania, hili jambo chimbuko lake ni wapi? Mfano: wahaya wana watani wengi kuliko (labda) makabila yote: watani wao ni: watu wa Musoma (wajaluo, wajita, wakulya), watu wa Kigoma (waha), watu wa Ukerewe (wazinza), watu wa Dodoma (wagogo).

Angalizo: kama uzi huu unakukwaza pitia huku! Karibu
 
Kuna watani hawaruhusiwi kuoana kuna mmoja anajiona superior kuliko mwingine,
anyway tumeyakuta tu haya mambo hata sijui yalianzaje kuna kabila niliwahi kutaka kuolewa nalo, nilipodokeza home mashangazi walikataa kwa kigezo hicho hapo aya ya kwanza
 
Inasemwa midomoni mwa watu eti kwamba. Utani wa makabila hapa Tanzania uliundwa/kutengenezwa katika Kipindi cha utawala wa Mwl Jk nyerere na sababu kuu ilikua ni kuwaweka watanzania pamoja

Yaani watu wa makabila yote kuwa sociable na kuua ile dhana ya ukabila, Hivyo ile complete circuit ya utani ktk haya makabila zaidi ya 10+ ndio tuseme ikaunda One huge firm of this watanzania.
 
Sina maelezo ya kutosha lakini nilicho na hakika nacho ni kwamba utani kati ya makabila ulikuwepo hata kabla ya Mwl. Nyerere hajazaliwa.
 
Kuna kitu kinaitwa 'watani'. Yaani kabila moja kuwa na kabila au makabila mengine na kujulikana kuwa ni 'watani zetu'. Hiki kitu cha watani ukikichukulia poa unaweza kukosa fursa zilizo ndani yake! Kwa mfano: makabila yanayoitana 'watani' ni rahisi kukubalika katika kuoa/kuolewa hata urahisi wa kujenga urafiki kuliko makabila mengine ambayo hamuhitani 'watani'. Sasa wajuzi wa mila na desituli hasa hasa za makabila ya kitanzania, hili jambo chimbuko lake ni wapi? Mfano: wahaya wana watani wengi kuliko (labda) makabila yote: watani wao ni: watu wa Musoma (wajaluo, wajita, wakulya), watu wa Kigoma (waha), watu wa Ukerewe (wazinza), watu wa Dodoma (wagogo).
Angalizo: kama uzi huu unakukwaza pitia huku! Karibu
Wahaya wanakuwaje na utani na wagogo!?..utani huja kutokana na migongano huko nyuma, mnyamwezi ana utani na wadigo,wagogo,wazaram,wangoni,wahehe..wagogo ni kwa sababu alikua akipita kwenda pwani wagogo wakiwapora mizigo yao,wahehe na wangoni ni sababu za Vita,mngoni akimsaidia mhehe
 
Inasemwa midomoni mwa watu eti kwamba. Utani wa makabila hapa Tanzania uliundwa/kutengenezwa katika Kipindi cha utawala wa Mwl Jk nyerere na sababu kuu ilikua ni kuwaweka watanzania pamoja

Yaani watu wa makabila yote kuwa sociable na kuua ile dhana ya ukabila, Hivyo ile complete circuit ya utani ktk haya makabila zaidi ya 10+ ndio tuseme ikaunda One huge firm of this watanzania.
Nyerere mnamsingizia vitu vingi vizuri..utani wa wanyamwezi na wahehe, wazaram,wadigo,wangoni,wagogo umeanza kabla hata mama yake Nyerere hajazaliwa,watanzania walikua wamoja,waungwana,wakarimu kabla ya huyo mtu wenu,ndiyo maana mnyamwezi akaoa kwa chifu mkwawa,abushiri na mkwawa marafiki wa damu
 
Wahaya wanakuwaje na utani na wagogo!?..utani huja kutokana na migongano huko nyuma, mnyamwezi ana utani na wadigo,wagogo,wazaram,wangoni,wahehe..wagogo ni kwa sababu alikua akipita kwenda pwani wagogo wakiwapora mizigo yao,wahehe na wangoni ni sababu za Vita,mngoni akimsaidia mhehe
Ndo unijuze! Wahaya ni watani wa wagogo pia!
 
Utani huwa unatakiwa kufanywa kwa heshima. Ule utani wa kuzuia sijui jeneza, sijui kuwadhihaki wafiwa ni ujinga wa watu waliojitengenezea. Ila utani hautakiwi kumaanisha hadi mtu kukosea adabu mwingine.

Inatakiwa utani liwe jambo kufurahia pande zote mbili sio pande moja pekee.
 
Kuna watani hawaruhusiwi kuoana kuna mmoja anajiona superior kuliko mwingine,
anyway tumeyakuta tu haya mambo hata sijui yalianzaje kuna kabila niliwahi kutaka kuolewa nalo, nilipodokeza home mashangazi walikataa kwa kigezo hicho hapo aya ya kwanza
sijui
 
Watani ni yale makabila yaliyowahi kupigana vita baina yao.
 
Sina maelezo ya kutosha lakini nilicho na hakika nacho ni kwamba utani kati ya makabila ulikuwepo hata kabla ya Mwl. Nyerere hajazaliwa.
Naam

Pengine hata kabla ya biashara ya utumwa huko. Kama lugha ya kiswahili tu. Nyerere alifanya kui-promote tu ikasambaa zaidi.

Vivyo hivyo utani
 
Utani huwa unatakiwa kufanywa kwa heshima. Ule utani wa kuzuia sijui jeneza, sijui kuwadhihaki wafiwa ni ujinga wa watu waliojitengenezea. Ila utani hautakiwi kumaanisha hadi mtu kukosea adabu mwingine.

Inatakiwa utani liwe jambo kufurahia pande zote mbili sio pande moja pekee.
Hivyo ndivyo utani ulivyokuwa toka zamani.
 
Utani haukuwa kati ya makabila. ulikuwa kati ya mtu na rafiki zake, ndani ya kabila moja. Waliuleta kwenye makabila ili kuondoa ile chuki ya makabila. Ni jambo zuri.
Mkuu mara nyingi watani ni makabila yaliyowahi kupigana
 
Back
Top Bottom