sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
1. Wachaga - Kama kawaida yao sio watu wa kujisifia iwe ni biashara, maendeleo ya vijini kwao, n.k. Kiufupi hawa suala la elimu wapo Mbali tangu enzi za ukoloni, Mkoa wa Kilimanjaro ni mdogo ila ndio unaongoza kwa shule nyingi hasa maeneo ya uchagani, Kitu cha ziada ambacho wengi hawakijui ni kwamba wana mwamko wa shule za kimataifa na hata miji wanayoishi ya Moshi na Arusha kuna shule hizi nyingi kama St Constatine, Braeburn, INternational school of Moshi, Kennedy house, n.k. Kwenye shule hizi watoto utaowakuta kutoka Tz ni wachache ila majority huwa ni wachaga, sio suala la mzazi kuwa na pesa pekee bali na mwamko wa kuwapa watoto elimu ya kimataifa, na hata zile nafasi za udhamini watanzania kusoma bure huwa ni watoto wa kichaga. Ikumbukwe shule hizi ni tofauti kabisa na hizi za Necta, huku ukisoma kuna guarantee kubwa kusoma vyuo bora duniani, Luhgha za wazungu walimu ni wazungu, connections nzito za watoto wa wazito, n.k.
2. Wahaya - Yes, Ni nani asiewajua watu hawa waliowekewa kizuizi na Nyerere kwa alama za kufaulu darasa la saba ? Hawa watu wanaipenda shule jamani, Shida ni kwamba kuna changamoto za kiuchumi mkoani Kagera, wapo wengi wanaotamanigi kuendelea na shule na uwezo upo ila inawalazimu waendelee na maisha mengine, halafu pia wao na makabila mengine wana mwamko mdogo sana na International schools, Mhaya mwenye pesa za kutosha atapeleka mtoto wake Kaizarage ya Bukoba ama saint Francis huko Mbeya yani hana mwamko kabisa kujua kwamba kuna shule International.
3. Wanyakyusa - Ughonile, Nimeishi nao so nawajua vizuri hawa kina Mwakyusa, Mwakatobe, Mwakyembe, Bukuku, n.k., wazazi wa kinyakyusa hasa wamama wanaasa sana watoto wasome, wapo tayari kujinyima kwa lolote mtoto asome shule nzuri, Nakumbuka nikiwa Mbeya mtu anaweza kuresit form 4 hata mara 3 kutafuta credit, hawana jambo dogo kwenye elimu !! kuhusu uwezo darasani wanao wa kawaida ila wapo wachache nishawai kutana nao ni ma genius, Kwa sasa Mbeya ndio mkoa inaoongoza kwa vyuo ukiitoa Dsm, Kuba shule za kiingereza 4 za serikali za msingi, Shule za Sekondari zipo nyingi
4. Wasukuma - wasukuma wapo wengi sana hii nchi ila tatizo maeneo yao mengi hawaipi elimu kipaumbele, mikoa waliyojazana wasukuma kama Simiyu, Geita, Shinyanga, n.k elimu haipewi uzito na shule ni chache, Mwanza ndio inawabeba.... Laiti wasukuma wangejiongeza kielimu lingekuwa ni tishio kubwa sana hapa nchini maana katika kila watanzania sita kuna msukuma moja, Huenda mkoloni hakupeleka elimu usukumani alishaona watadominate sana, na pia licha ya Mwanza kuwa jiji la pili kwa ukubwa Tz hawana chuo kikuu.
5. Wakerewe - wakerewe wapo katika kisiwa kidogo cha Ukerewe, kwa mipaka ya ramani kipo mkoa wa Mwanza lakini kiuhalisia kipo mkoa wa Mara, wakerewe ndio wanaongoza nchi nzima kwa kuwa na maprofesa wengi zaidi wenye phd za kutafuta darasani, Sababu ya kuwa namba tano ni idadi yao (population) kuwa ndogo.
Bonus....
Watu wa Mara - sijajua ni kabila lipi kati ya wajita, wakurya, wajaluo au wazanaki lakini nimesoma vyanzo mbali mbali kwamba mkoa huu ni kinara wa kutoa wasomi wengi, Majimbo kama Musoma vijijini ule mchujo tu wa kupata mbunge wa kupitishwa ni phd tupu.
Makabila mengine ni Wapare, wamasai wa Meru, Wamatengo wa Ruvuma, n.k.