Kuna ndugu tulisoma naye, hayupo kabisa kwenye mitandao ya kijamii

Cybergates

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
673
1,391
Wakuu,

Hili jambo linawezekana kuonekana kawaida, lakini limenishangaza kidogo.

Leo nilikua napitia habari huko mitandaoni, nikapata wasaa wa kuongalia taarifa za baadhi ya jamaa tulio kuwa pamoja kipindi cha nyuma.

Kitu kilicho nishangaza ni kuona kuna account moja ya mtu tulikua tunasoma wote darasa moja ipo empty (haina kitu, picha, post, like, page alizo follow au comment etc) ni sawa na account iliyo telekezwa.

Nikaona isiwe tabu, nikajaribu kumtafuta mitandao mingi, huko nako hayupo, hamna picha wala taarifa inayo muhusu.

Japo tulisoma darasa moja, nika mtafuta jamaa aliekuwa best yake kipindi hicho, nika jaribu ku mdodosa huyu ndungu yetu yupo wapi?

Akaniambia kipindi tulichomaliza, jamaa aliendelea kujuendeleza lakini baada ya mda aliondoka kwenda kusoma nje (Jina Kapuni). Baada ya hapo akaniambia hana tena taarifa zake.

Hapa ndio nemeshangaa inawezekanaja mtu uka potea jumla jumla, uka delete kila kitu kwenye account yako?

Nimejiuliza amebadilisha identity au nini kimetokea, au amepata dili za TISS au idara za usalama?

Hii weekend nitajaribu ku go-deep kumtafuta mtu asiye taka kupatikana.
 
Mkuu mbna unaumiza sana kichwa sio kila mtu anapenda ku expose maisha yake kwa ujumla wengne unakuta mitandaoni yupo ila kwa majina tofauti na uliomzoea na bdo hapost kitu wengne hutumia majina ya wanawake humo mitandaoni.
 
Sio yeye tu hata mimi sipo huko. Maisha yangu ni private sina sababu ya kujianika mitandaoni. Mambo ya kununua gari umepost, umepata mtoto umepost, umenunua kanzu mpya umepost, unafuga bata umepost n.k mimi yamenishinda kabisa.
 
Mbona simpo tu kafanya kama mimi unatumia id fake kama JF mi niliosoma nao degree ufaransa wote tupo mitandaon ila wana kili kama wewe hawajawai niona huko, unajua ukipenda ujulikane sana kwa uhalisia wako sisi wengine ni binadamu wa hovyo.

Kuna muda unataman umchane jamaa na kumnanga matus pale anapozingua, ila ukikumbuka ananijua unaishiwa poz ndio mana tunatumia short cut hatuweki utambulisho halisi ili tupete kwa uhuru.

Hata zile vidio tutumiane kwa uhuru pasipo kujuana kuna siku jf kuna mdada aliniboa tulichambana sana, na vile sina dogo nikampa madongo, and the mwisho nakuja kucheki simu ya wife kumbe mwenye ile id ni yeye nikaamua kum blok kimya kimya na hajanijua mpaka leo.
 
Huyo alichukuliwa kitengo muda mrefu tu ndio maana humuoni mitandaoni maana amewekwa sehemu ambayo ni nyeti sana.

Usishangae kabisa wapo ambao hutengenezewa vifo fake yaani msiba kabisa na mazishi kumbe mwamba amehamishwa kikazi amepewa jukumu kubwa sehemu kiasi kwamba hatakiwi kuwasiliana na ndugu wala familia yake tena.

Yaani anabadirishiwa mpaka identity details huyo harudi tena labda miaka ya badae sana akimaliza salama kilichompeleka
 
Hiyo kawaida kuna jamaa yetu toka tunakuwa hajawahi kufungua akaunti yoyote ya kijamii mpaka watsap hatumii ukitaka kumtumia kitu anakupa email yake ndo umtumie, nakupita chuo kote mpka sasa hajabadilika hiyo ndo misimamo yake na maisha yanaenda
 
Huyo alichukuliwa kitengo muda mrefu tu ndio maana humuoni mitandaoni maana amewekwa sehemu ambayo ni nyeti sana.
Usishangae kabisa wapo ambao hutengenezewa vifo fake yaani msiba kabisa na mazishi kumbe mwamba amehamishwa kikazi amepewa jukumu kubwa sehemu kiasi kwamba hatakiwi kuwasiliana na ndugu wala familia yake tena
Yaani anabadirishiwa mpaka identity details huyo harudi tena labda miaka ya badae sana akimaliza salama kilichompeleka
Na ukimaliza salama unauwawa au unachizishwa simple..
 
Back
Top Bottom