Ni kwa kiasi gani watu wanakujua kwenye mitandao ya kijamii? Je, kuna hatari gani?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Ni rahisi kupeana habari na watu unaowasiliana nao mtandaoni. Majukwaa kama vile mitandao ya kijamii inafanya iwe rahisi kwa wewe kutangaza kwa familia yako na marafiki (na hata kwa watu usiowajua, kulingana na mipangilio yako ya faragha) unachofanya na mahali ulipo.

Mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Instagram hukuruhusu kuweka kwenye picha zako eneo ambapo picha hiyo ilichokuliwa. Wakati huo huo, Snapchat hukuruhusu kushiriki eneo ikiwa unarekodi video mubashara, kuwajulisha wafuasi wako (na umma, kulingana na mipangilio yako ya faragha) kuhusu mahali ulipo.

Baadhi ya lebo za eneo zinaweza kuonesha anwani halisi ya eneo lako, si tu jiji au eneo la jumla ulipo. Hii ina maana kwamba ukiweka taarifa za eneo lako mtu yeyote anayeweza kutazama machapisho yako ya mitandao ya kijamii anaweza kufika kabisa sehemu ulipo.

Ikiwa una watoto, huenda wanaweka taarifa hizi pia kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo linaweza kuwaweka katika hatari ya kuwasiliana na watu wasiowafahamu. Lakini pia kupiga picha na vitu kama kitambulisho cha sehemu ya kazi, kadi ya benki nk, ni njia rahisi ya kuweka taariza zako binafsi wazi ambapo zinaweza kutumiwa vibaya na watu wenye nia mbaya.

Walaghai nao wanaweza kujaribu kufanya urafiki nawe kwa kutumia akaunti bandia, au kwa kuchukulia utambulisho halisi wa watu au makampuni ambayo unaweza kujua au unaowaamini.

Lakini pia watu wengi wapo katika hatari ya kuibiwa taarifa zao kwakuwa hawalindi taarifa zao binafsi kwa kigezo eti siyo watu maarufu au matajiri hivyo kujiona hawapo kwenye hatari ya kuibiwa utambulisho wao na kutumiwa vibaya. Dhana hii potofu inawafanya wasione ukweli huu kwamba mtu kuiba utambulisho wako haijalishi kama wewe ni tajiri au la mradi taarifa zako zinaweza kutimiza lengo lake na kumfaidisha.

Mfano, mtu kuchukua picha au video zako za faragha na kuzuiuza au kutaka fedha kutoka kwako ili zisivujishwe, haitajalisha kama wewe ni tajiri au mwenye kipato cha chini utapata madhara ya moja kwa moja kutokana na taarifa hizo kutumiwa vibaya.

Na mara nyingine wanaoiba taarifa zako binafsi ni watu wa karibu akiwa na lengo la kukukomoa tu, hivyo hutakiwi kupuuzia ulinzi wa taarifa zako binafsi kwani hata kitu unachoona ni kidogo sana kinaweza kutumiwa na kukuletea madhara makubwa.

Kushirikisha taarifa zako binafsi mtandaoni kupita kiasi kunaweza pia kuweka vitu vyako vya thamani hatarini - kwa mfano, ikiwa unaonyesha kuwa upo mbali kwa mapumziko ya likizo, unatangaza kuwa haupo nyumbani kwako. Hili linaweza kuwapa wahalifu - ikiwa ni pamoja na wezi wa utambulisho, nafasi ya kulenga makazi yako, ikiwa wanajua ni wapi.

Unaweza kupunguza hatari hizi kwa kufanya haya yafuatayo;

~ Zuia machapisho yako kuonesha eneo ulilopo kwa kuzuia/kuzima mipangilio ya eneo (location settings) kwenye simu yako, hii inajumuisha kuondoa sehemu inayojulisha eneo picha ilipochukulia kwenye settings za simu yako, labda kama kwa kuacha eneo ulilopo kujulikana hakutarishi usalama wako wala taarifa zako binafsi.

~ Usiweke eneo lako wewe mwenyewe, yaani usiandike kwenye chapisho la mitandao ya kijamii, Hii ni pamoja na wakati na mahali ulipo kwenye mapumziko yako/likizo.

~ Usipige picha ukiwa na vitu ambavyo vitaweka wazi taarifa zako binafsi, mfano kupiga picha na kadi ya benki, cheti cha kuzaliwa au vyeti vya ngazi mbalimbali za elimu.

Bado unaweza kuungana na marafiki na familia kwenye mitandao ya kijamii bila kuweka taarifa nyingi binafsi, fikiria mara mbili kuhusu kuweka taarifa zako binafsi hadharani. Elewa kwamba taarifa yoyote unayotoa kwenye mitandao ya kijamii inaweza kuonekana hadharani.

EquiFax
 
Back
Top Bottom