Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
- Thread starter
- #41
Heshima mbele Mkuu MMKJJ:
Kielimu tu na kimaendeleo ni vigumu kuwalinganisha watu wa Scotland na Quebec na hawa Wazanzibari. Huko majuu wanafanya mambo yao kistaarabu zaidi, au tunaaminishwa wanbafanya hivyo.
Kutumia udini ktk malengo ya siasa yamefanyika mahala mengi kama historia inavyotuambia. Miaka ya karibuni ni Iran, pale udini ulitumika kumuondoa Shah mwaka 1979. Hii ni kwa sababu Iran ni Waisilamu kwa asilimia 95%.
Halafu tusisahau Ireland ya Kaskazini. Kuna udini unatumika kudai haki au kuiminya haki ya kujitenga kwa jimbo lile la uingereza (UK). Waprotestanti ambao ndiyo wengi kule wanatumia udini kutaka kubakia chini ya utawala wa London, na Wakatoliki wanataka kujiunga na Jamhuri ya Ireland (Ireland ya Kusini) ambayo ina Wakatoliki wengi.
Hali kadhalika huko Palestina ambako udini unatunmika sana kwa malengo ya kisiasa na Kashmiri, jimbo (state) pekee la India ambalo lina Waisilamu wengi (majority). Udini unatumika ktk harakati za kujitenga.
Huko Zanzibar Waisilamu ni kama 95 % hivyo kuitumia dini ktk malengo ya kisiasa yapo na yanaeleweka hasa katrika nchi zenye dini moja au dini moja kubwa. Ila swali la kujiuliza ni kwamba jee ni haki au dhambi kufanya hivyo?
Mmh! Kuna masuala ya msingi hapa aliyoleta NSM, na hasa katika ile dhana ya kwamba ni vigumu kutenganisha dini na siasa. Hata huko nchi za magharibi, udini unatumika sana katika harakati za siasa na kudai haki ingawa mara nyingi si kwa njia za ghasia. Ghasia hutokea pale tu ambapo ukandamizaji hupitiliza kipimo.
Mfano alioutoa NSM wa Ireland na Iran ni mizuri, lakini kuhusu Ireland, mauaji mengi sana yalifanyika dhidi ya kikundi cha IRA pale majeshi ya Uingereza yalipokwenda kuzima "uasi" kuanzia miaka ya 70.