Muungano wa Makanisa ni hatari

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,301
3,414
Ili kufanikiwa katika malengo yao ya kuitawala dunia kupitia Dini, uchumi, siasa na
Ajira/kazi, Illuminati walifanikiwa kuanzisha taasisi za Kidini, kiuchumi, kisiasa na kazi na ajira, zote hizo zikiwa zinafanya kazi kwa mwongozo wa Illuminati.

Katika taasisi za kidini tunakuta Baraza la Umoja wa makanisa ulimwenguni (World Council of Churches) ambalo lilianzishwa na Illuminati kwa makusudi ya kuunganisha dini zote za Kikristo na kutengeneza “Mnara wa Babeli” wa kiroho

Tayari kuna makanisa mengi ambayo yamejiunga kwenye umoja huo. Wengi hawajui kama umoja huo uko chini ya chama cha siri cha Illuminati ambacho kina siri kubwa sana katika kutawala dini na dunia kwa ujumla.

Ukitaka kujua kama kanisa lako ni mwanachama wa Baraza hilo unaweza
kutembelea mtandao wa Baraza hilo kwenye website hii


Ieleweke kwamba WCC ina vitengo kama Christian World Communion, Global Christian Forum, nk. ambapo kanisa linaweza lisiwe member wa WCC moja kwa moja ila likawa member wa vitengo vilivyo chini ya WCC.

Siri ambazo Illuminati/Freemason hawataki zifahamike kwa watu Kuna siri muhimu ambazo Freemason na Illuminati hawataki zifahamike kwa watu. Siri hizo ni:

– Viongozi wa dini wamefanikiwa kuwatawala mamilioni ya wanaume na
wanawake, ambao wamekuwa wakifundishwa tangu utoto wao, kwamba viongozi
hao ni wajumbe kutoka kwa Mungu.

– Leo viongozi hao wamezungukwa na mamia ya alama na mavazi ya Freemason
kama vile pete, kofia nk kiasi kwamba watu wengi hawajui hilo.

images (9).jpeg

images (8).jpeg


Alama au logo ya Muunganano wa makanisa ni Boti lenye Msalaba ,mkikokotwa kupelekwa shimoni

download.png


Kwa hiyo dhehebu lolote ambalo Nembo yake Ina msalaba, Ina maana limekubali kurudi Katoliki.



Mfano: dhehebu la SDA zamani lilikuwa haliamini fundisho la Utatu, na hata Nembo yake ilikuwa ni ya malaika Watatu, lakini baada ya miaka ya 1981 kupitisha rasmi Fundisho la Utatu, Basi hata Nembo ilibidi ibadilishwe na ili iwe na alama ya Msalaba ambao ni alama ya Nembo ya EKUMENE.

Waasisi wa SDA hawakufundisha fundisho la Utatu mtakatifu


Katika Kitabu kinachoitwa EKUMENE wanakiri kwamba ipo siku Kanisa moja litasimamishwa Uk 63, wanasema:

"Siku moja itakapowadia, ambapo Makanisa hayo yataungana katika umoja wa imani na uongozi, ndipo Baraza la Makanisa la Ulimwengu litaweza kutoweka. Lengo lake ni kwamba Kanisa Moja Takatifu sharti litokee."


Sasa ili kukamilisha Umoja huu ndipo mwaka 1975, ilipitishwa rasmi kwamba fundisho la Utatu ndio liwe Fundisho la Imani linaloyaunganisha makanisa yote.
EKUMENE Uk 63 wanasema"Mkutano wa Wote katika mji wa Nairobi( mwaka 1975) uliyahimiza tena Makanisa kuutafuta umoja wa imani ambao ungejidhihirisha katika ekaristi moja na kanuni ya Imani moja. Hatimaye, Baraza la Makanisa lilikamilisha msingi ule wa imani tuliokwisha kuutaja, kwa kuliingiza neno moja linalohusuUtatu_Mtakatifu. (Mwisho wa kunukuu)


Kwa hiyo dhehebu lolote linaloamini fundisho la Utatu Ina maana limekubali kurudi Katoliki kupitia mkakati wa EKUMENE.


Na ndio maana Utatu ni Fundisho linalokubalika na karibu Madhehebu yote ya Kikristo, na hata mtu akionekana anapinga Fundisho la Utatu Basi Waumini wa Madhehebu karibu yote ya Kikristo huungana na kuanza kutetea.


Ulokole si uprotestanti bali ndio umeua uprotestanti, Uprotestant si jina tu fulani la kidini bali ni movement ambayo inawaleta watu katika Ukristo wa kibiblia ambao unamfanya mtu kumwabudu Mungu kwa uhuru (Biblia na Kristo tu). Ndio maana kuna kitu kinaitwa "counter reformation" ni harakati iliyoanzishwa na shirika la Jesuit chini ya Papa Paul mnamo 1540 ili kuua uprotestanti. Ndio maana leo unaona uprotestanti hauna madhara tena dhidi ya Roma, zaidi wameipigia magoti Roma na kutaka umoja (kwamba wanarudi nyumbani) naam kumwabudu Mungu kinyume cha dhamiri yao.


Pichani ni mwaka 2014 wakati balozi wa papa Tony Palmer) ambaye ni Muanglikana alivyowakokota waprotestant wa Marekani ambao wanawakilisha 70% ya waprotestant duniani hadi Vatican na kusema Uprotestant umekwisha na kufungua mlango wa maridhiano. Ni Uprotestant ndio umebadilika na si Roma, maana Roma haibadiliki. Kuungana na upapa ni kuuza uhuru wako ambao mababa wa kiprotestant waliupigania hadi kufa.

download (1).jpeg
 

Attachments

  • download.png
    download.png
    6 KB · Views: 9
Heri wenye Moyo Safi, ndio Watakaomwona Mungu

Hakuna cha Roman Catholic , Lutheran, Moravian, Anglican, Islam, Hinduism wala Usabato

Kama unaabudu popote na huna Moyo safi ni BURE na UNAFIKI
 
Jambo jema sana,liharakishwe tupate dunia moja yenye imani moja siasa moja na fedha moja,mana kinachoendelea sasa na utengano na upuuzi wa kigaidi
 
hivi kuna watu mpaka leo mnaenda makanisani kuomba au kuombewa?.
Mi siendi church wala masjid lakini watu acha waende tu huko.

Usiwapotoshe mkuu, bila imani kuna kitu binadamu anakosa. Wanaenda huko lakini imani za kishirikina unaona zinavyopamba moto, wakiacha?
 
  • Thanks
Reactions: K11
Back
Top Bottom