Kuna mengi yaliyojificha nyuma ya uchomaji makanisa Unguja

Sioni ni kwa vipi UWT wangetumia mbinu dhaifu hivyo kuiangamiza JUMIKI. Tumewaona kwenye vyombo vya habari waandamanaji wa JUMIKI wakichoma matairi barabarani na kuziba barabara. Why should that happen?

Kuchoma matairi barabarani siyo sawasawa na kuchoma makanisa ambayo inasemekana yalichomwa usiku.
 
Sioni ni kwa vipi UWT wangetumia mbinu dhaifu hivyo kuiangamiza JUMIKI. Tumewaona kwenye vyombo vya habari waandamanaji wa JUMIKI wakichoma matairi barabarani na kuziba barabara. Why should that happen?

Mkuu hii inawezekana kweli, sababu sidhani kama wale viongozi walipanga kuchoma makanisa ila kuna uwezekano mkubwa wa mapandikizi ya UWT yaliingia kati, hance kuwaconvice vijana wa kiislam kufanya vile, mkuu lazima tufilie zaidi ya upeo wa macho yetu!
 
Yote yanawezekana ila kwa maneno yao hawa watu sio waungwana, wamesababisha wao kwani kulikuwa na ulazima gani wakujadili muungano kwa kupitia taasisi ya dini yakiislamu si wangeunda tasisi nje ya dini mimi napapenda zanzibar sana ila wamenikwaza mno.
 
JAMANI HAYA MAMBO YAKO WAZI HAWA VIJANA WAMEANDAMANA SIKU TATU ,NA KANISA WAMECHOMA SIO MARA MOJA,
  • SIKU YA KUKAMATWA KWA KIONGOZI WAO WAKIWA KWENYE MAANDAMANO KWENDA KWEREKWE WAKACHOMA KARIAKOO AU KUNA UTATA?
  • SIKU YA PILI WAMEWASHA MATAIRI BARABARANI HAO UAMSHO WANAFUKUZWA NA MABOMU WANARUDI ILI KIONGOZI WAO ATOE AU HILO LA KUCHOMA MATAIRI ROAD LINA UTATA?
  • WAKICHOMA MATAIRI MITAA YA KISONGE NAKWEREKWE MCHANA KWEUPE WAKAENDA KUCHOMA KANISA LA MPENDAE TENA WAKIWA WANATOKEA KWEREKWE AU KUNA UTATA?
  • WAKIWA KISONGE WAMEWASHA MATAIRI MAGARI HAYAPITI WANASHINIKIZA KIONGOZI WAO AACHIWE WAKACHOMA MAGARI YA WATU AU KUNA UTATA?
  • MAANDAMANO YAO WALIYOKUWA WANAFANYA KUTOKEA MSIKITINI NA KUSABABISHWA BARABARA KUFUNGWA NALO LINA UTATA KUWA PENGINE WALIOKUWA WANAFUKUZWA NA MABOMU AMBAO HATA KWENYE TV NA MAGAZETI WAMEONEKANA NAO SIO UAMSHO?
  • MIKUTANO YAO WANAYOENDELEA MSIKITINI NA WANAYOENDELEA KUITANGAZA HUKU VIONGOZI WAO WAKISEMA WATAENDELEA NA MIKUTANO NAYO WAMESINGIZIWA?

hapo kuna nini kisicho wazi ndani ya siku tatu maandamano na kuchoma makanisa kila siku yote hiyo wamesingiziwa?kama sio kikundi cha fujo hiyo kuchoma matairi na vurugu barabarani serikali imedanganya?naombeni majibu
Mkuu zipo picha nyingi zinaonyesha vijana wanawasha matairi barabarani,
Swali, je kuna picha hata moja inayoonyesha hao vijana wakiwa wanachoma moto kanisa lolote?
 
Huenda kuna ukweli wa thread hii!!! Labda ndiyo maana serkali imesema itayajenga upya makanisa yote yaliyochomwa kwa gharama zake maana inajua iko 100% responsible!!

Usicheze na UWT (TISS)!! With it, everything is possible under this sun, except kuumba mtu!!!
 
Wewe ni great thinker.

umesahau kuongeza na mkakati wa just baad ya masaa 12, kualikwa mabalozi wa canada n US na wengineo na kisha tamko kutolewa naubalozi wa US.

Kimsingi serikali wameshinda, nimemsikiliza nimesoma maelezo ya shein leo nkajua ndio basi tena.

Shein anasisitiza watu wasubiri tume ya katiba! lakini haijulikani ni kwa kiasi gani hiyo tume itayachukua hayo maoni na kuyatekeleza.

Bahati mbaya kuna baadhi ya member humu wameingia katika mtego huu kwa makusudi au kwa bahati mbaya. inasikitisha sana.
Imekula kwenu! chezea wabara wewe....we ulisikia wapi kikundi cha dini kinataka kuvunja muungano? na wanasiasa wa
fanya nini?
 
Nilishasema hilo suala la uchomaji wa makanisa ni mkakati wa serikali ya CCM. Uamsho sio wajinga kiasi hiko hata kama wana chuki na Wakristo lakini wasingeweza kutumia mbinu ya kuchoma makanisa.
Matusi,na uchafu mwingine ulokuwa unahutubiwa wakati wa mihahara ya Uamsho ilionekana kama ni ruksa kwa waumini au wafuasi.Kwani mambo yaliwekwa wazi bila kificho.Je Uhamsho walichukua hatua gani ?Au Uamsho ndio Usalama wa taifa? kama sio hivyo wao ni nani kwa ngazi ya uongozi wa serikali Zanzibar?
 
Wawe ccm wawe uamsho dhambi ya kuchoma kanisa haitawaacha salama!

Mungu wa Isaka siyo Mungu wa Ismael!.
 
Waliochom kanisa la tag ni raia, yupo ndugu amenihadithia alikuwakwenye mkesha ndio jamaa wakaja wengi na kuanza kuwafurusha kisha wakachoma
 
Hebu usiwe mvivu wa kufikiri kiasi hocho! Kwani watu wa UWT huvaa sare za utambulisho?

" UWT are capable of doing anything! naona mnasahau upesi enzi zile za siasa chafu Zanzibar, jinsi chama cha CUF kilivyokuwa kikibambikiwa ugaidi, matukio kama haya yamewahi sana kutokea huko nyuma, enzi zile ilikuwa yakiripuliwa majengo ya serikali, ilifikia hadi ofisi ya Mufty nakumbuka ilipigwa mabomu, wakaja mpaka FBI hapa Znz, bahati hakushitakiwa mtu yeyote kuhusu kadhia zile! Mimi ni mwendaji sana wa mihadhara ya Uamsho, nakumbuka si mara moja wala mbili tushaaidhiwa kuhusu tukio kama hili, tuwe waangalifu na njama tunazoandaliwa juu yetu kama uchomaji wa makanisa kisha tutupiwe lawama sisi. ila wallahi, sisi wla hatutarudi nyuma kwa dai letu, nalo ni MUUNGANO HATUUTAKII! tunataka kura ya maoni tuulizwe. kaeni na msubiri mziki wetu mtajua nani Wazenji mwaka huu!"
 
Hao uamsho bado, hata bara kuna waliokuwa inspired na uamsho na hawakupenda hata kuilaumu.So tusitafute kwa darubini nani muovu.Ii tupotoshe ukweli.
No way hawa jamaa wakwepeshwe, hata kama inauma imani yao ila tayari walishfika mbali sana, labada wanahitaji kujiuliza kwanini wamefikia hapo, kwanini wamedhalilisha imani yao kiasi cha kuitwa wahuni (wanamini UHUNI)ili kuokolewa km kikundi cha imani.Na video zinaonyesha ushirikiano mkubwa, na mabango yalikuwa yakionyesha nia yao,km hawausiki wangeyakataza, na bado kiongozi wao kashikilia msimamo wake, wamelalama wazi makanisa yapo km uyoga. Unless mnatakasema kuwa wote walikuwa U.W.T

Hizi ni theories za kuondoa embarassment, hata osama kuna watu walimtetea wakati yeye mwenyewe alijisifu kwa hilo.Hizi ni hila za politically correct useful ****** wanaopenda ku appeae uapnde mmoja na kupotosha mwigine.Just because they cant stand embarassment of the others.
 
Mnakumbuka Janja widi walipewa kazi gani wakati wa siasa za chuki na matendo gani walikuwa wanafanya? wamechoma majumba watu waliachwa na vilema hadi hii leo hakuna janja widi hata mmoja aliweza kukamatwa isitoshe mnamkumbuka Omari mahita aliyekuwa Mkuu wapolisi alivyokuwa anadangaya uma na kuonesha silaha alizokuwa akidai ni za wapinzani wanataka kuzitumia kumbe yeye binafsi alikuwa anashirikiana na majmbazi kuiba magari na mengi akiyanunuwa kwa ajili yake binafsi siamini kama hawa Uamsho wapo nyuma ya hilo isipokuwa kunauwezekano ni njia moja ya kuwazofisha kimataifa imepangwa na watu fulani kutokana na kushituka kwao na maneno yao
 
Hii issue ya maandamano ya Uamsho, vurugu zilizotokea na uchomaji wa makanisa ina mengi yaliyojificha kuliko tulivyoona na kuamini (au kuaminishwa).

Kuna wanaoona kuna mikakati ilibuniwa rasmi na kupangwa kimakusudi kwa lengo la kupindisha ajenda ya awali waliokuwa nayo Uamsho ya kuuhoji Muungano au hata kutaka uvunjwe.

Haijulikani mikakati hii ilifanywa na akina nani lakini kulikuwapo thread moja humu JF siku chache zilizopita ambayo iliondolewa iliyosema kuwa kule Visiwani wengi walikuwa wanaamini kuwa Usalama wa Taifa (UWT) ndiye walipanga mikakati hiyo kwa madhumuni hayo hayo ya kupotezesha lengo halisi la mikakati ya Uamsho.

Mikakati hii ya UWT kama kweli wao ndiyo walitekeleza itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani dhoruba kali tayari imewaangukia Uamsho kwani hatimaye wamejikuta wanabebeshwa lawama la uchomaji wa makanisa, kitu ambacho wengi katika taasisi hiyo wanaamini kuwa siyo wao waliotenda kitendo hicho, ingawa katika mazingira yalivyokuwa itakuwa vigumu kutohusishwa nayo.

Tutegemee vyombo vya dola iwapo kweli watawakamata watu wale hasa waliochoma makanisa hayo, na siyo kamata-kamata tu ya holela. Kuna usemi unaosema kwamba Uchomaji wa majengo (yaani arson) ni rahisi sana kutenda lakini ni vigumu sana kuwabaini mhusika/wahusika halisi. (It is easy to commit arson than to detect those responsible).

Kuna watu wameicheza hii kama Messi. Ni dhoruba ambayo kwa waliokusudia wanaona wamefanikiwa kuizima kabisa mikakati yote ya ajenda ya kuuhoji na/au kuuvunja Muungano kwani hakuna tena huko Unguja atakayeweza kuja na kitu hii – kwani wataambiwa ‘Nyie hamna lolote – ajenda yenu kumbe ni udini tu, na siyo Muungano!"

Ni hakika watu wa uamsho wamejinasa. Dola imepata sababu kubwa ya kupiga marufuku tena maandamano/harakati zozote kuhusu kuhojiwa Muungano kule Unguja.

Hii inatokana na ukweli kwamba suala zima la Muungano katika mchakato wa kuandika Katiba mpya limawakalia vibaya sana watawala kwani wameshasema kwamba Muungano usiguswe. Na ugumu mkubwa ulikuwa unatoka Visiwani lakini sasa inaonekana wamefanikiwa kulizima – pengine labda kwa muda tu.

Sasa hivi Tume ya Katiba inaweza kuingia Visiwani na kufanya kazi bila hofu, pamoja na kwamba kutumika kwake Zanzibar bado ni kitendawili kutokana na sheria iliyoiunda ktk Bunge la Muungano kutothibitishwa na Baraza la Wawakilishi.

Hapa mnataka kuwachezea watu akili. Kama hoja ni Muungano kwanini hao wanaopinga Muungano wasijikite kwenye kuukataa Muungano pasi ya kuzungumzia chuki dhidi ya Watanganyika na Tanganyika? Kwa mfano Scotland na Britain zina matatizo ya muungano wao kwa muda mrefu sana lakini wanahusiana vizuri na watu wa Scotland watakapoanzisha taifa lao si kwa sababu wana chuki na Waingereza. Hili ni kweli pia kati ya Quebec na Canada. Hawa nao wamekuwa na mjadala mkubwa sana wa muungano wao na Quebec wanataka kujitenga kwa muda mrefu sana.

Wanaopinga Muungano Zanzibar wanachanganya mambo mengi sana kiasi kwamba kuchomwa majengo, kutishiwa watu wa bara na hata baadaye vurugu zitakazotokea haziwezi kutenganishwa na hoja za hawa jamaa. Wanaopinga Muungano wangeweza kabisa - kama wanataka - kupinga muungano kwa kutumia hoja dhidi ya Muungano na utaifa wa Zanzibar. Hoja ya kupinga Muungano ingeweza kutolewa kwa misingi miwili:

a. Muungano haukuwashirikisha watu wa Zanzibar na hivyo hauna uhalali (msimamo wa baadhi ya wasomi wengi wa Zanzibar kama kina Prof. Sharrif na wengine.

b. Muungano ulivyo sasa hauna sababu ya kuendelea kwani Zanzibar hainufaiki na inaweza kujinufaika yenyewe bila kuwa katika Muungano.

Hoja hizi mbili zinatosha kabisa kuwaunganisha Wazanzibari wote - na sisi wengine tutawaunga mkono.

Bahati mbaya hizi siyo hoja; hoja zao zimeongezwa "anti-Tanganyikans" and "anti-Christians". Sijui kama watu wamewasikliza hawa wanaozungumzia kupinga Muungano. Wanapinga kwa sababu ni wa Watanganyika. Sasa chuki wanayopandikiza dhidi ya watu wa bara inapoota mizizi wanashangaa inapochanua maua halafu wanaruka? Umwitie mtu "mwizi mwizi" halafu watu wakaja wakamtia kiberiti uruke na kusema ulikuwa unaimba tu wala hukumaanisha?
 
Hapa mnataka kuwachezea watu akili. Kama hoja ni Muungano kwanini hao wanaopinga Muungano wasijikite kwenye kuukataa Muungano pasi ya kuzungumzia chuki dhidi ya Watanganyika na Tanganyika? Kwa mfano Scotland na Britain zina matatizo ya muungano wao kwa muda mrefu sana lakini wanahusiana vizuri na watu wa Scotland watakapoanzisha taifa lao si kwa sababu wana chuki na Waingereza. Hili ni kweli pia kati ya Quebec na Canada. Hawa nao wamekuwa na mjadala mkubwa sana wa muungano wao na Quebec wanataka kujitenga kwa muda mrefu sana.

Wanaopinga Muungano Zanzibar wanachanganya mambo mengi sana kiasi kwamba kuchomwa majengo, kutishiwa watu wa bara na hata baadaye vurugu zitakazotokea haziwezi kutenganishwa na hoja za hawa jamaa. Wanaopinga Muungano wangeweza kabisa - kama wanataka - kupinga muungano kwa kutumia hoja dhidi ya Muungano na utaifa wa Zanzibar. Hoja ya kupinga Muungano ingeweza kutolewa kwa misingi miwili:

a. Muungano haukuwashirikisha watu wa Zanzibar na hivyo hauna uhalali (msimamo wa baadhi ya wasomi wengi wa Zanzibar kama kina Prof. Sharrif na wengine.

b. Muungano ulivyo sasa hauna sababu ya kuendelea kwani Zanzibar hainufaiki na inaweza kujinufaika yenyewe bila kuwa katika Muungano.

Hoja hizi mbili zinatosha kabisa kuwaunganisha Wazanzibari wote - na sisi wengine tutawaunga mkono.

Bahati mbaya hizi siyo hoja; hoja zao zimeongezwa "anti-Tanganyikans" and "anti-Christians". Sijui kama watu wamewasikliza hawa wanaozungumzia kupinga Muungano. Wanapinga kwa sababu ni wa Watanganyika. Sasa chuki wanayopandikiza dhidi ya watu wa bara inapoota mizizi wanashangaa inapochanua maua halafu wanaruka? Umwitie mtu "mwizi mwizi" halafu watu wakaja wakamtia kiberiti uruke na kusema ulikuwa unaimba tu wala hukumaanisha?

Heshima mbele Mkuu MMKJJ:

Kielimu tu na kimaendeleo ni vigumu kuwalinganisha watu wa Scotland na Quebec na hawa Wazanzibari. Huko majuu wanafanya mambo yao kistaarabu zaidi, au tunaaminishwa wanbafanya hivyo.

Kutumia udini ktk malengo ya siasa yamefanyika mahala mengi kama historia inavyotuambia. Miaka ya karibuni ni Iran, pale udini ulitumika kumuondoa Shah mwaka 1979. Hii ni kwa sababu Iran ni Waisilamu kwa asilimia 95%.

Halafu tusisahau Ireland ya Kaskazini. Kuna udini unatumika kudai haki au kuiminya haki ya kujitenga kwa jimbo lile la uingereza (UK). Waprotestanti ambao ndiyo wengi kule wanatumia udini kutaka kubakia chini ya utawala wa London, na Wakatoliki wanataka kujiunga na Jamhuri ya Ireland (Ireland ya Kusini) ambayo ina Wakatoliki wengi.

Hali kadhalika huko Palestina ambako udini unatunmika sana kwa malengo ya kisiasa na Kashmiri, jimbo (state) pekee la India ambalo lina Waisilamu wengi (majority). Udini unatumika ktk harakati za kujitenga.

Huko Zanzibar Waisilamu ni kama 95 % hivyo kuitumia dini ktk malengo ya kisiasa yapo na yanaeleweka hasa katrika nchi zenye dini moja au dini moja kubwa. Ila swali la kujiuliza ni kwamba jee ni haki au dhambi kufanya hivyo?
 
Back
Top Bottom