Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'

Kuna baadhi ya familia ....mwanaume akishindwa baadhi ya majukumu yake hasa ya kipato ni kawaida kusikia mume akimwambia mkewe 'fanya maarifa' au ufanye maarifa basi'.......

Hivi hili hasa linaamaanisha nini?

Maarifa gani ambayo mwanaume akishindwa, mwanamke ndo ataweza?

Halafu unakuta mwanamke 'anafanya kweli maarifa' na maisha yanakwenda...

Sasa 'haya maarifa' ya wanawake ni yapi?
mfano vunja kile kisanduku chako unachoweka vi mia mia, lakini ukimwambia direct hivi kwamba vunja hicho kisanduku hupati ng'o bora useme indirect kama ambavyo umesema hapo juu!
 
we huwezi maarifa kabisa?

Nitajibu vyema kama nikijua maarifa yanayozungumzwa. ila kama ni kuwezesha familia baba anaposhindwa ninaweza fanya maarifa. kwani na mimi nina kazi inayonipa kipato na kama mama wa nyumba yanipasa kutumia busara tele pale mwenzangu anapoishiwa. tatizo lenu wanaume siku hizi mkishaona mama anaweza kutoa basi kila wakati nyinyi mmekwama na kumsukumizia mwanamke majukumu tele.

ila kwa wale wanaume wanaojua wake zao hawana kazi yoyote wanapowaambia wakafanye maarifa kwa kweli siwaelewi kabisa
 
Wanawake huwa wanabana kiasi fulani cha pesa za matumizi ya nyumbani na kuzificha. Siku mume ukikwama mwanamke anazitoa zile pesa, wengine watajifanya wamekopa kwa wenzao
 
Wanawake tuna maarifa mengi ikiwemo kuweka akiba,mkitupaga matumizi hua tuna tabia ya kuweka,siku dingi akikwama mama unaingia kwny kibubu siku Zinasonga!
 
886c23b52319a35a66259c62773dff43.jpg

6febb05c94d7ebc6c130d6283afdad90.jpg
 
Maarifa ya kujiongeza ili kuokoa jahazi...ila sasa inategemea sasa na kazi kama mwanamke anayo ama laa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom