Kumpa HOUSE GIRL makufuli afuwe ni UNYAMA......

mkayala

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
555
72
Mama mmoja mwenye asili ya Kondoa,ana binti msaidiz wa miaka 15,anamnyanyasa sana huyu binti,anampiga mara kwa mara,na mbaya zaidi huwa anampa mtoto afuwe had nguo zake za ndani,kwa kweli huu ni UNYAMA KABISA
 
Nakuomba sana kwa kuwa uko jirani na huyo mama, hebu jaribu kuchukua hatua ili kumsaidia huyo binti kutokana na huo unyanyasaji.Kuna watu wana roho mbaya sana.
 
Yan ananikera,najaribu kuangalia utaratibu wa kisheria,lazima nimchome tu huyu mama!

hapo utakuwa umefanya la maana kwanza anamtumikisha mtoto umri chini ya miaka 18 na serikali inapiga kelele kila kukicha suala la ajira kwa watoto! mpeleke polisi haraka huyo mama
 
Nikisema acheni nyumba ndogo somesheni watoto hamtaki unyanyasaji utaisha kwa kanuni zipi
 
Mama mmoja mwenye asili ya
Kondoa,ana binti msaidiz wa miaka 15,anamnyanyasa sana huyu
binti,anampiga mara kwa mara,na mbaya zaidi huwa anampa mtoto afuwe had
nguo zake za ndani,kwa kweli huu ni UNYAMA KABISA

Kwa kweli huo ni unyama unyamani. Huyo mama hajitambui,hajiheshimu na hajithamini. Hana marafiki jirani wakamshauri?
 
tembele TAWLA.TAMWA afisa ustawi wa jamii,hii tabia ni mbaya,but haya ni madhara ya kuwa na wababa wasifit kuwa kichwa cha familia na wamama wanaopenda kuwa vichwa katka familia zao,nasema hivi kwa sababu hadi tatzo linaonekana nje ya nyumba(jiran mleta uzi)ni waz familia inaoungozwa na mtu dhaifu,tupatie ripoti ya hatua utakazochukua tafadhal!
 
Kuna mama wa Iringa nimewahi kuishi kwenye nyumba yake kimara kwa mara ya kwanza nilishangaa kuona housegirl anafua nguo za ndani za huyu mama siku za jumapili kamba nzima inajaa chupi zake.
 
toa taarifa kwenye mamlaka zinazohusika maana bado mtoto ni mdogo kwa umri wake kufanya kazi na huo pia ni unyanyasaji wa hali ya juu sana
 
tena ni unyama wa hali ya juu...
hivi watu wengine hawajipendi eeeh...
maisha yake yote yapo mikononi mwa huyu binti kwa nini amtese?
u-hg ni kazi kama kazi nyingine kwa nini asiheshimu kazi ya mwenzie? kwa nini amfanye mtumwa?

hana adabu huyo mwanamke, arudi unyagoni, pichu haifuliwi na mtu , pichu unafua mwenyewe....
 
Kwa kweli huo ni unyama unyamani. Huyo mama hajitambui,hajiheshimu na hajithamini. Hana marafiki jirani wakamshauri?

Kwanza anajisikia sana,juz amempiga mtoto alipoulizwa eti kapika kuku mapaja mawili hayaonekan
 
toa taarifa kwenye mamlaka zinazohusika maana bado mtoto ni mdogo kwa umri wake kufanya kazi na huo pia ni unyanyasaji wa hali ya juu sana

Niliongea na binti arud nyumban anasema kwao shida sana
 
Kuna mama wa Iringa nimewahi kuishi kwenye nyumba yake kimara kwa mara ya kwanza nilishangaa kuona housegirl anafua nguo za ndani za huyu mama siku za jumapili kamba nzima inajaa chupi zake.

Ni sawa kabisa na huyu,kasoro tu yeye pia ni mpangaji!
 
tembele TAWLA.TAMWA afisa ustawi wa jamii,hii tabia ni mbaya,but haya ni madhara ya kuwa na wababa wasifit kuwa kichwa cha familia na wamama wanaopenda kuwa vichwa katka familia zao,nasema hivi kwa sababu hadi tatzo linaonekana nje ya nyumba(jiran mleta uzi)ni waz familia inaoungozwa na mtu dhaifu,tupatie ripoti ya hatua utakazochukua tafadhal!

Asante mkuu...
 
Jimama hilo lichafu sana sijui liliolewaje. Karne hii anakusanya vchupi vyake vya 500, 500, 500 afuliwe na mtoto wa mwanamke mwenzio?
 
kama vipi tafuta u.pupu then spray juu ya hayo makufuli

Na hili lilishatokea, niliwasikia wadada wakisimulina visa walivyokutana navyo wakati wakiwa mayaya, mmoja alisema alikuwa anapewa nguo za ndani afue, mama akiondoka wanazitenga ili baba azione anapokwenda kuoga, kwa aibu alikuwa anazichukua na kurudisha chumbani. Mama akirudi anakuwa mkali matusi kibao na masimango, japo mumewe alikuwa akimwonya asiwape mabinti makufuli yake.

Baada ya manyanyaso ya muda mrefu cku moja alizifua vizuri na baada ya kukauka akazianua akatia *****, akaweka chumbani kisha akachukua virago na kuishia zake.Alikuja kupata taarifa baadae namna alivyomkomo huyo mwajiri na chuki alianzia hapo kwa kuwa walitoka kijiji kimoja,
 
Back
Top Bottom