Kumpa HOUSE GIRL makufuli afuwe ni UNYAMA......

Na hili lilishatokea, niliwasikia wadada wakisimulina visa walivyokutana navyo wakati wakiwa mayaya, mmoja alisema alikuwa anapewa nguo za ndani afue, mama akiondoka wanazitenga ili baba azione anapokwenda kuoga, kwa aibu alikuwa anazichukua na kurudisha chumbani. Mama akirudi anakuwa mkali matusi kibao na masimango, japo mumewe alikuwa akimwonya asiwape mabinti makufuli yake.

Baada ya manyanyaso ya muda mrefu cku moja alizifua vizuri na baada ya kukauka akazianua akatia *****, akaweka chumbani kisha akachukua virago na kuishia zake.Alikuja kupata taarifa baadae namna alivyomkomo huyo mwajiri na chuki alianzia hapo kwa kuwa walitoka kijiji kimoja,

Ndio dawa yao!
 
hapo utakuwa umefanya la maana kwanza anamtumikisha mtoto umri chini ya miaka 18 na serikali inapiga kelele kila kukicha suala la ajira kwa watoto! mpeleke polisi haraka huyo mama

Sheria za Tanzania zinaruhusu mtoto wa miaka 14 kufanya kazi ambazo hazitamzuilia haki yake ya kusoma.
 
Mama mmoja mwenye asili ya Kondoa,ana binti msaidiz wa miaka 15,anamnyanyasa sana huyu binti,anampiga mara kwa mara,na mbaya zaidi huwa anampa mtoto afuwe had nguo zake za ndani,kwa kweli huu ni UNYAMA KABISA

Nguo ni nguo tu, iwe ya ndani iwe ya nje, sijui hili la mfanya kazi asifuwe chupi mmelitoa wapi? na wale wasiovaa chupi jee? wasiwape suruali zao kufua?
 
Kuna mama wa Iringa nimewahi kuishi kwenye nyumba yake kimara kwa mara ya kwanza nilishangaa kuona housegirl anafua nguo za ndani za huyu mama siku za jumapili kamba nzima inajaa chupi zake.

Asilimia kubwa ya wanawake wanaojiita wa kisasa, unakuta yuko peke yake anafanya kazi ana housegirl, huwapa mpaka chupi zao kufua.. yeye ni kuja , kula kulala na weekends kuleta mabwana, huyu hata akija kuolewa ataona hilo sio tatizo. Ni kawaida yao kabisa.Ushahidi ninao na ninajua hata humu wapo ila kwa hapa watajidai wana piga vita, ila wanafanya hivyo. Mimi nikiona upuzi kama huu lazima ni kutose!!!
 
Kuna wamama wazembe mno! Wakivua nguo hawachambui, kwa mfano, mmama anavua suruali skini tight na chupi wa pamoja, kisha anapeleka kwenye dishi la nguo chafu ili HOUSEBOY afue.
 
Kuna wamama wazembe mno! Wakivua nguo hawachambui, kwa mfano, mmama anavua suruali skini tight na chupi wa pamoja, kisha anapeleka kwenye dishi la nguo chafu ili HOUSEBOY afue.

Ni udhalilishaji wa hali ya juu,tena kama n mm lazima nikukomeshe tu!
 
Asilimia kubwa ya wanawake wanaojiita wa kisasa, unakuta yuko peke yake anafanya kazi ana housegirl, huwapa mpaka chupi zao kufua.. yeye ni kuja , kula kulala na weekends kuleta mabwana, huyu hata akija kuolewa ataona hilo sio tatizo. Ni kawaida yao kabisa.Ushahidi ninao na ninajua hata humu wapo ila kwa hapa watajidai wana piga vita, ila wanafanya hivyo. Mimi nikiona upuzi kama huu lazima ni kutose!!!

Tena unakuta jimama lenyewe nene kama kabati na bonge la kitambi,linakapa katoto kafue ch**i yake,aaahggh!
 
kama ni binti mzuri mlete kwangu tusaidiane..aishi maisha comfortable, alipwe vizuri na anisaidie kazi za ndani na kulea mtoto. kama yuko tayari niPM nikutafute..
 
kama ni binti mzuri mlete kwangu tusaidiane..aishi maisha comfortable, alipwe vizuri na anisaidie kazi za ndani na kulea mtoto. kama yuko tayari niPM nikutafute..

Mkuu una maanisha mzuri wa kazi au?cjaelewa kidogo hapo!
 
yes kama ni mzuri wa kazi, tabia yani ana heshima n.k. mcha mungu itakuwa vizuri pia..otherwise familia yetu yani mimi na mume wangu ni watu wastaarabu na waelewa.
 
Mtoto: Dada hizo chupi ni za nani
Hg (dada): Ni za mama
Mtoto: Mbona sijawahi ona amevaa
Hg(dada): Huwa ana vaa ndani kule
Mtoto: Oh ina maana mama naye anavaa chupi
Hg(dada): ebu toka, niache nizifue......
Mtoto: ???????
 
Hii habari imekaa ki unafik unafik. Huyu mleta mada alijuwaje? labda kupigwa anaona, jee na la kufuwa mpaka kufuli kajuwaje? anaambiwa na huyu hg? kama jibu ni ndio, mtaelewaa kwanini nasema huyu mleta mada ni mnaa. Ana special interest na huyo hg na kusema humu hawezi.
 
yes kama ni mzuri wa kazi, tabia yani ana heshima n.k. mcha mungu itakuwa vizuri pia..otherwise familia yetu yani mimi na mume wangu ni watu wastaarabu na waelewa.

Asante sana dada kwa moyo safi,ila kuhusu tabia yake cna uhakika sana,ngoja nilifanyie kazi!
 
Mtoto: Dada hizo chupi ni za nani
Hg (dada): Ni za mama
Mtoto: Mbona sijawahi ona amevaa
Hg(dada): Huwa ana vaa ndani kule
Mtoto: Oh ina maana mama naye anavaa chupi
Hg(dada): ebu toka, niache nizifue......
Mtoto: ???????

Ndio madhara yake hayo!
 
jamani wanawake wengine lol, sijui hawakufundwa mweeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hii habari imekaa ki unafik unafik. Huyu mleta mada alijuwaje? labda kupigwa anaona, jee na la kufuwa mpaka kufuli kajuwaje? anaambiwa na huyu hg? kama jibu ni ndio, mtaelewaa kwanini nasema huyu mleta mada ni mnaa. Ana special interest na huyo hg na kusema humu hawezi.

Wewe inaonekana ndio walewale,mim nna mke wangu,mtoto wa miaka 15 ni kama mdogo wangu na hawez kamwe kuwa na mvuto kwangu!CHUPI ZINAFULIWA NA ANAANIKA KWENYE KAMBA ukiangalia sio size zake.Lazima tujiheshimu huwez kumpa mtoto uchafu wako afuwe bwana,kisa nin?BINADAM WOTE NI SAWA!
 
Back
Top Bottom