Kumewaka Songea: Leo CHADEMA kufanya maandamano kupinga mgao wa umeme.

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
690
350
Leo kuanzia muda wa saa 5 asubuhi, chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) mkoa wa Ruvuma kitafanya maandamano ya amani yatakayoanzia kuanzia Mfaranyaki, wakipitia barabara ya Mbinga/Sokoine road na kuzunguka hadi maeneo ya benk ya NBC na NMB na pale kituo kikuu cha polisi na kumalizia soko la samaki. Dhamira ya maandamano hayo ni kushinikiza serikali kutoa tamko la ufumbuzi juu ya mgao wa umeme unaoendelea kwa takribani miaka minne mfululizo. Katibu wa CHADEMA jimbo la Songea bwana Masumbuko Geoge jana alikuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani hapa. Tatizo la umeme mjini Songea limekuwa sugu kwani umeme unaweza kuuona nyumbani kwa saa 2-3 kati ya masaa 24. SOURCE: Radio one NIPASHE at 6:30, 05th, may,2012
 
Ni kweli Songea tatizo hilo lipo kwa muda mrefu. Hebu ishitueni serikali yenu labda mtakumbukwa 2015.

Kigoma ilikuwa hivyo hivyo lakini walipoikataa CCM saizi wapo mbele sana wale jamaa!!!! Na nyie kataeni CCM, haiwezekani tokea uhuru bado mnatumia majenereta ambayo yamechoka mara mafuta hakuna yaani uozo mtupu.

Ushauri mpigeni chini Nchimbi 2015 ndiyo watashituka!!!!!
 
Nishati ya Umeme inategemewa kwa mambo mengi sana hasa kwa wajasiriamali ambao ni wengi.Mungu awabariki makamanda katika maandamano yenu ya kuifikishia Serikali ujumbe,kwa sisi huku Arusha leo 5/5/2012 tutawashuhudia wale wanaotudisha kadi za ccm na kuchukua za Chadema katika uwanja Wa NMC unga ltd.
 
Pamoja tutafika. Wapeni moto, msisahau 2015 kumng'oa Nchimbi. Na mwambieni MWAMBUNGU na mwenzio MAIKO KAMHANDA wale vijana waliowaua wanawasubiri, ipo siku bwana atalipa vivyo hivyo walivyofanya.
 
Leo kuanzia muda wa saa 5 asubuhi, chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) mkoa wa Ruvuma kitafanya maandamano ya amani yatakayoanzia kuanzia Mfaranyaki, wakipitia barabara ya Mbinga/Sokoine road na kuzunguka hadi maeneo ya benk ya NBC na NMB na pale kituo kikuu cha polisi na kumalizia soko la samaki. Dhamira ya maandamano hayo ni kushinikiza serikali kutoa tamko la ufumbuzi juu ya mgao wa umeme unaoendelea kwa takribani miaka minne mfululizo. Katibu wa CHADEMA jimbo la Songea bwana Masumbuko Geoge jana alikuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani hapa. Tatizo la umeme mjini Songea limekuwa sugu kwani umeme unaweza kuuona nyumbani kwa saa 2-3 kati ya masaa 24. SOURCE: Radio one NIPASHE at 6:30, 05th, may,2012

Mlio Songea mbona hamtuambii matokeo ya maandamano haya???
 
Mi nilifikiri wananchi ndo wanayakiwa kuandamana na si chadema
 
Back
Top Bottom