Elections 2010 Kumbe saa ya ukombozi iliwekwa betri za kichina!!!!

Ninasema kwa idadi ya majimbo tuliyopata HAKI ni zaidi ya uraisi mnaouota. Cha moto mtakiona 2015. Hapo ndipo mtakapolia na kusaga meno.
Baada ya JK mna mtaji gani kama sio garasha?
 
Inawezekana wametumwa kuja kuharibu hali ya hewa! Hao ni ma - houseboy wa mafisadi wanafurahia hizo keep change wakitumwa sokoni
 
Hatimae imefahamika kwamba kumbe ile tuliyokuwa tunaambiwa ni saa ya ukombozi ama ni ya kichina au iliwekwa betri za kichina baada ya kuonekana mwendo wake kusuasua kiasi cha kutishia ule mtiririko wa kwamba siku moja ni saa 24!!! Hadi inafika saa 10 jioni, saa ya ukombozi ndo kwanza ilikuwa inaonesha saa 6 mchana jambo lililotia shaka kwamba huenda betri za saa hiyo zimeishiwa nguvu na hivyo kuufanya mshale wake wa sekunde kutembea kwa mwendo wa mdebwedo mithili ya ule mshale wa saa!!! Hofu ya wale waliokuwa wanaiamini saa ya ukombozi ni kwamba huenda kuna mjanja mmoja ambae badala ya kununua betri kutoka kwa authorised dealers; mjanja huyo akaenda kununua kwa wamachinga wa pale mchikichini!!

Alamsiki, lakini nasikia Dr. Slaa is badly defeated pale Dom na wilaya zake huku wakielekea kugalagazwa kule Kahama!!!!Hata hivyo, don' mind abt hayo matokeo kwani my thread here was just abt saa ya ukombozi ambayo iliwekwa betri za kichina!

Wakikosekana watu kama hawa, JF inapoa. NasDaz, endeleeni kuandika ili tujue athari ni kubwa kiasi gani.
 
Hatutaki betri ya kijapan au ya kijerumani inayomulika sehemu tusiyohitaji kuona. Bora tupate ya kichina au Nationa ya kitanzania imulike hata kwa masaa sita kwenye EPA, RICHMOND, RADA, KAGODA, MEREMETA

Sasa hii betri ya kijerumani (Kikwete kwa mtazamo wako usio sahihi)
-Pale BOT imemmulika Liyumba.. Huyu sio muhusika hata ya kichina inaweza kumulika muhusika kwa dk 1ja.
-Imemmulika kidogo Chenge na mramba alafu kwa mlango wa nyuma inawaruhusu wagombee ubunge???

Betri Hii haifai kabisa bora za kichina tuuuuuuuu
 
Hainiingii akilini! Ni kweli watanzania wanakubaliana na haya?

1.Rais wa kwanza duniani kudanganywa vibaya mno na wasaidizi wake
2.Rais wa kwanza kuwa na rekodi ya kuanguka anguka mbele ya kadamnasi
3.Rais wa kwanza duniani kufanya safari nyingi za nje ya nchi ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakaini
4.Rais wa kwanza duniani kutamka hadharani kwamba hajui umaskini wa watu wake unatokana na nini.
5. Rais wa kwanza duniani kuchakachuliwa mafuta kwenye gari yake ikazima barabarani
6. Rais wa kwanza anaechukulia wingi wa magari kama kipimo cha maisha bora!

7. Rais wa kwanza duniani anaepata ulinzi wa nguvu za Giza.(mnajimu)
8. Rais wa kwanza aliyesema watoto wadogo wa shule kupata mimba ni kiherehere chao....
9. Rais wa kwanza anayeogopa mafisadi.
10.Rais wa kwanza duniani aliyetumia mabango yote ya biashara nchini kwake kujinadi wakati wa kampeni mpaka picha zake

11. Rais wa kwanza duniani kutamka hadharani kwamba hahitaji kura za wafanyakazi
12. Rais wa kwanza kutamka hadharani kwamaba atatembeza kopo kuombaomba ili kulisha wananchi wake
13. Rais wa kwanza duniani kunyang'anyana wanawake na raia wake kisha kuwabambikizia kesi

14. Rais anayefanya kila namna kuiba kura ili ashinde

15. Rais wa kwanza kufanya mchezo wa kubembea.

 
Moto wake utaujua Bungeni. Hapo ndo utajua ni betri za mchina au???? Kikosi cha wapinzani kinachoingia bungeni nguvu na effect yao ni sawa na
( ) X 100 ya wabunge wa CCM walioingia kwa ajili ya kupata Posho na Kulinda biashara Zao.
 
Mkuu Nas Daz saa yenyewe ya ukombozi ni ya kichina,,, betri za kichina mbaya zaidi aliyepewa hizo betri kuweka mikono yake ina kitetemeshi na macho yana makengeza,,,amebadilisha sehemu ya (plus) + ameweka - (minus)
 
NasDaz inawezekana saa hiyo imewekwa betri za kichina sawa, lakini mbona unasahau kuwa mbaya zaidi ni uwa huyo mnaemtegemea arudi pale ikulu ni Puppet ( mwanasesere) hachezi mpaka achezeshwe na walioshika kamba! ni bora hii saa iliyowekewa betri za mchina inatembea yenyewe bila kusukumwa!
 
Jambo la kufurahisha kwenye uchaguzi huu ni namna kura zilivyoongea. Kwa ubungwe wa na CCM wengi walitaka baadhi ya viti viende upinzani hivyo wakawapigia baadhi ya wapinzani kama adhabu kwa uongozi wa juu wa CCM ili ufaNYE MABADILIKO NDANI YA ccm.

LAKINI KWA slaa NAWATHIBITISHIENI kuwa ataburuzwa kweli kweli. Slaa anawez akaambulia chini ya asilimia 20 kama ambavyo nimekuwa nikisema na pengine anaweza akazzidiwa hata na Lipumba.
 
Moto wake utaujua Bungeni. Hapo ndo utajua ni betri za mchina au???? Kikosi cha wapinzani kinachoingia bungeni nguvu na effect yao ni sawa na
( ) X 100 ya wabunge wa CCM walioingia kwa ajili ya kupata Posho na Kulinda biashara Zao. (QUOTE).



Bunge lina kanuni zake. Wakiongea ovyo ovyo tu bungeni kwa kutamka maneno ya ovyo wakidhani kuwa wako kwenye jukwaa la kampeni, watashuihulikiwa kwa mujibu wa kanuni. Hivyo ni lazima watabwabwaja bungeni kwa tahadhari kubwa.
 
Saa ya ukombozi!!!!!!. Kwani kuna mtu alitegemea SLAA atashinda? Kwa tume ya Makame? Alichofanya slaa ni kuwafungua macho watanzania waliokuwa wamelala na kuuanika uovu wa serikali ya dakta . But he wasnt expecting to become the president .Hivi ni daktari wa mifugo au nini?
 
Back
Top Bottom