Elections 2010 Kumbe kuna wabunge kumi wa chadema hawajatoka Bungeni Rais alipokua akihutubia bunge

- Mkuu una-raise a very interesting point na mimi jana niliona kwenye mdahalo, nikashitushwa sana kwamba kumbe kuna wabunge wa Chadema ambao hawakutoka nje ile siku, ikiwa na maana kwamba hawakukubaliana na ule uamuzi ambao at the heart of it ni kwamba Rais wa sasa ni wa halali na hakuna tatizo lolote na matokeo ya NEC,

- Very interesting point mkuu!

William.

..Bill achana na kina mtu wa pwani ....you are above that....maoni yao yapo so biased ,napendaga sana michango yako kwani pamoja na kuwa upo connected na unatoka moja ya familia mashuhuri ..huwa unatoa mawazo huru ambayo si mara zote huwa yanaunga mkono kila kinachofanywa na CCM.

Nadhani tunakubaliana wote kuwa ..hoja ya katiba mpya iliyoanza mwaka 1992 pale DIAMOND JUBILEE sasa imeiva...bila kuangalia ufuasi wetu wa vyama ni bora sasa tuombe katiba mpya kwa njia za amani .....nadhani kama JK atakubali katiba mpya atakumbukwa na historia....katiba yetu tuliyoicopy lancaster ..sasa haikidhi tena mahitaji ya kizazi kipya cha watanzania.

Mwisho ,tulitegemea ungetimiza ndoto za kaka yako kumpokea mzee ubunge pale MVUMI...inawezekana ukawa hupendi active politics kutokana na gharama ambazo ni za kibinafsi ....lakini its time sasa ukafikiria kuwatumikia wananchi in a more wider role and carry your family name through the second generations..

Wasalaam

PMike.
 
icon1.png
Re: Kumbe kuna wabunge kumi wa chadema hawajatoka Bungeni Rais alipokua akihutubia

So this is an assumption and not fact, yah??! "If.... then...." nenda tena shule kaangalie principles za kustate an assumption, fact, hypothesis na opinion. Huwezi kuwaambia watu unaongea fact na wakati huna basis za hiyo fact. Ukweli ni kwamba HR aliupotosha Umma wa watanzania, na Mbowe hakuona sababu ya kujibu kitu ambacho kipo wazi; "full stop". Haya mengine ya umbea na ushabiki wa CCM yawekeni pembeni ongeeni yaliyo dhahiri, na si kuleta opinions na kutuambia hizo ni facts.
 
Facts zingine ovyo kweli kweli! Kila alichosema Mh Hamadi kimekuwa ni Kama msahafu! Ndo maana Malecela alisema go to hell wengine tulimwona alichemka!
 
Uhuru wa manyani, weka chochote, kula chochote, tupa chochote cheza cheza mpaka ucheze. Vigumu sana kuelewa hapa lengo ni nini. we all know that JK is president,sio issue kuwa alishinda kwa wizi au kwa haki. It is open secret that uchakachuaji ulifanyika kupunguza na kuongeza kura za waombea na NEC imekiri na kubadilisha matokeo ya baadhi ya sehemu. Si issue ya maana sasa, tuangalie ya muhimu yanayofuata. Sera ya ku=destabilze opposition inasaidia kuilinda CCM lakini haisaidii kuleta maendeleo
 
..Bill achana na kina mtu wa pwani ....you are above that....maoni yao yapo so biased ,napendaga sana michango yako kwani pamoja na kuwa upo connected na unatoka moja ya familia mashuhuri ..huwa unatoa mawazo huru ambayo si mara zote huwa yanaunga mkono kila kinachofanywa na CCM.

Nadhani tunakubaliana wote kuwa ..hoja ya katiba mpya iliyoanza mwaka 1992 pale DIAMOND JUBILEE sasa imeiva...bila kuangalia ufuasi wetu wa vyama ni bora sasa tuombe katiba mpya kwa njia za amani .....nadhani kama JK atakubali katiba mpya atakumbukwa na historia....katiba yetu tuliyoicopy lancaster ..sasa haikidhi tena mahitaji ya kizazi kipya cha watanzania.

Mwisho ,tulitegemea ungetimiza ndoto za kaka yako kumpokea mzee ubunge pale MVUMI...inawezekana ukawa hupendi active politics kutokana na gharama ambazo ni za kibinafsi ....lakini its time sasa ukafikiria kuwatumikia wananchi in a more wider role and carry your family name through the second generations..

Wasalaam

PMike.

Mkuu kwa ninavyofahamu hakutakuwa na katiba mpya. Katiba mpya itakuwa kiama kwa CCM, as long as CCM wanashikilia sehemu kubwa ya madaraka na dola, as long as watanzania walio wengi wataendelea kuwa usingizini, hakuna kipya kitakachotokea. At thisi moment naweza kusema we are doomed. Pamoja na mijadala yote hiyo ya kataiba, utaona issue itakavyokufa. Atatokea mtu CCM atasema kwa sasa si muhimu na si muda mwafaka au katiba inakidhi mahitaji, labda inatakiwa ifanyiwe marekebisho tu. Wait and see nchi hii inaendeshwa kiushakaji.
 
tajeni hao wabunge tuwafahamu mapema, mjue kuwa hawa ni kenge kwenye msafara wa mamba ambao siku zote wamo
 
..Bill achana na kina mtu wa pwani ....you are above that....maoni yao yapo so biased ,napendaga sana michango yako kwani pamoja na kuwa upo connected na unatoka moja ya familia mashuhuri ..huwa unatoa mawazo huru ambayo si mara zote huwa yanaunga mkono kila kinachofanywa na CCM.

- Mkuu wangu heshima sana, in my opinion ni kwamba hapa Wapenzi wa Chadema wanashindwa ku-grasp the big picture kwamba Mwenyekiti wa Chadema jana aliksoea kutojibu hii hoja, kinachotakiwa hapa ni fundisho kwamba next time awe muangalifu na hasa wasaidizi wake, maana this falls right in their hands, mmojawapo alitakiwa kufikiri haraka sana na kugundua hili na kumpasia ki-note ili aliseme hata kama muda wa debate umekwisha, that is all I could ask!

Nadhani tunakubaliana wote kuwa ..hoja ya katiba mpya iliyoanza mwaka 1992 pale DIAMOND JUBILEE sasa imeiva...bila kuangalia ufuasi wetu wa vyama ni bora sasa tuombe katiba mpya kwa njia za amani .....nadhani kama JK atakubali katiba mpya atakumbukwa na historia....katiba yetu tuliyoicopy lancaster ..sasa haikidhi tena mahitaji ya kizazi kipya cha watanzania.

- Mkuu wangu sana, mimi ni mfuatiliaji sana wa mambo ya katiba za mataifa mbali mbali, hakuna katiba ya taifa lolote Duniani, ambayo ina mwanya wa urahisi rahisi katika kurekebishwa, kule Zambia walijaribu hili la kukurupuka na kurekebisha katiba kumbe Chiluba alikuwa na mikakati yake ya siri ambayo thanks to Mwanawasa, ikaja ikamlipukia usoni akashindwa kufanya alichotaka yaani kuwahadaa wa-Zambia, ili aendele na madaraka, Kenya tumejionea wananchi walivyogoma kabisaa through their votes kwamba hawataki kina Kibaki waiguse katiba maana hawawaaamini, USA ndio kabisaa huwezi gusa katiba bila mpango maana Judicial Branch watakulima tena kiroho mbaya sana, kama walivyokataa kusikiliza kesi ya uchaguzi ya New Jersey State.

- Sawa ninaikubali hoja yako kimsingi kwamba katiba yetu ina upungufu inahitaji marekebisho, tatizo langu ni nina wasi wasi kwamba a lot is missing katika kuirekebisha hii katiba, unahitaji wananchi ambao so far sio siri hawaonyeshwi kuona tatizo na katiba yetu kuacha wananchi wachache sana wanaopiga kelele, sasa huwezi kubadili katiba bila kuwa sambamba na wananchi, tuwapeni nafasi wananchi ambao tayari wameshaanza kuonyesha kuamka usingizini, waamke vizuri ama sivyo tutakuwa tunafukuza hewa! Nimesema mara nyingi sana na ninarudia tena kwamba huwezi kuwa na political system ya Checks and Balance katika taifa ambalo uwiano wa wabunge uko kama hapa kwetu Tanzania, na huwezi kulazimisha kuongeza wabunge wa Upinzani kwa kutumia katiba, Demokrasia ina njia moja tu inayokubalika sana na ni perfect sana nayo ni votes, yaani kura za wananchi.

- As much as ninaheshimu sana mafanikio ya Chadema recently, lakini I am not going over my head na kuanza kuamini kwamba wamepata mafanikio makubwa sana ya kuwapa mandate ya wananchi wengi on kubadilisha katiba, halafu infact taifa letu bado ni changa miaka 50 sio mingi sana kwa taifa lililokuwa under chama kimoja, kwamba ukitoa miaka 15 ya vyama vingi unaweza kupata busara ya kubadili katiba na uwiano uliopo sasa, hapana hiyo katiba itaishia kupwaya tu ndugu yangu. Kwa mfano NEC, inawezaje kuwa fair under our political system ya sasa, unless imechaguliwa na kusimamiwa na Chadema, sasa how could that be possible wakati CCM ndio majority boom your stuck, I mean dead end, sasa why waste time na hoja zisizojadilika ma kutaka kulazimisha kwa nguvu?

- Chadema wajiimarishe zaidi kwenye chaguzi, wananchi wameonyesha mwamko na kuanza kuamka usingizini wapeni time, tumejionea jinsi wananchi walivyoyazingira majengo ya kutoa matokeo ya uchaguzi, itawachukua muda kuelewa kwamba wanachohitaji ni kuchagua wabunge wengi wa Upinzani inaitwa political maturity ambayo inahitaji progress, sasa ukiilazimisha hiyo utakuja kuleta matatizo makubwa sana kwa taifa mbele ya safari kwa sababu utakua unalilia short term results over long term, I mean mtoto anakuwa sasa aachiwe akue, sawa kupiga makelele inakubalika lakini yawe makelele ambayo yako samba samba na political realities on the ground!

Mwisho ,tulitegemea ungetimiza ndoto za kaka yako kumpokea mzee ubunge pale MVUMI...inawezekana ukawa hupendi active politics kutokana na gharama ambazo ni za kibinafsi ....lakini its time sasa ukafikiria kuwatumikia wananchi in a more wider role and carry your family name through the second generations..

Wasalaam

- Well, thanks for the compliment ninaamini umetoa huu ushauri kutokana na kupima uwezo wangu wa kuelewa siasa zaidi kuliko kujali jina la familia na kaka yangu au generations!

Thanks.

William.
 
icon1.png
Re: Kumbe kuna wabunge kumi wa chadema hawajatoka Bungeni Rais alipokua akihutubia

Facts zingine ovyo kweli kweli! Kila alichosema Mh Hamadi kimekuwa ni Kama msahafu! Ndo maana Malecela alisema go to hell wengine tulimwona alichemka!

- I see great thinker samahani sana umenivunja sana mbavu hapa ha! ha! ha! ha!

William.
 
Bongo bwana, mtu anajiita "mwanasiasa mkongwe" halafu anasema "niko makini sana katika statements zangu", halafu anamwaga misleading half truths kama hizi makusudi kabisa?

What is this? Sloppy thinking or plain old malicious intent ?
 
Watu wengine humu jf inaelekea hawajui maana ya demokrasia nini hata yule hamad hajui maana ya demokrasia , wabunge 10 wa chadema kupinga hoja ya kutoka bungeni walifuata utaratibu wa kidemokrasia ndani ya chadema ambapo sio kitu cha ajabu ni kawaida kabisa, ccm na cuf wamezoea udikteta kwenye maamuzi yao, prof.lipumba amegombea uraisi tangu 95 mpaka leo inamaana cuf hawana mtu mungine ila nini yeye tu? Au ni mambo ya kuburuzwa? Ukija ccm ndio kabisa mifano ni kibao ya kuendesha mambo yao kidikteta .mataifa yenye demokrasia yenye nguvu jambo la kupingana kwenye maamuzi yao ni kawaida, mfano taifa la ISRAEL likitaka kutekeleza masuala ya muhimu kama kubadilishana wafungwa na waarabu au kupigana vita waziri mkuu anaitisha kura kwenye baraza la mawaziri na hapo lazima kuna wataopinga na wataokubaliana na maamuzi ila wale wanaounga mkono maamuzi kwa maslahi ya ISRAEL huwa wanakuwa wengi na hivyo hoja yao inashinda kama ilivyotokea juzi kwa chadema ukizingatia chadema inatetea maslahi ya taifa
 
Hivi wanaJF mnakubali kweli kudanganywa kirahisi namna hiyo na Hamad Rashid-na mnadanganyika kweli jamani??????????????????? Hivi hamkumuona Hamad kwamba ni dying horse-serikali ya umoja ZBR imemtema, sasa bungeni anajaribu kujenga kisichojengeka-anadai bungeni kitu ambacho hakiwezekani ili mradi awe kiongozi!!!!!!!!!!!!! Maadam mkwere amemchenga, na kule zenji ndiyo basi ssa anajaribu kulazimisha mambo!!!! Hamkumuona alivyokuwa anatweta na jazba nyingi!!!!!!!!!; hivi alikuwa anagombana na nani pale kwenye mdahalo????????????????????? Ukisikia kufilisika kisiasa ndiko kule!!!!!!!!- kama Lyatonga naye alivyomalizika-tena CDM wasithubutu kumkaribisha katika serikali kivuli-yeye lyatonga, hamad rashid, cheyo mapesa (sasa sapesa kalas!!!!) chunga sana!!!!!
Jibu sahihi lilitoka kwa Mkiti wa CDM-mwana falsafa Mbowe!!!!!!!!!!!!!!!!!Pipooooooooooooossssssssss Pawaaaaaaaaaaaass!!!!!!!!!!!!!!!!Yaani CDM ndiyo serikali kivuli makini-bungeni kutawaka moto- we ngoja Feb 2011 ifike!!!!!!!!!!!! Mlimuona kiboko cha sisiemu Tundu Lissu-alikuwa wakati wote ametulia akimsoma hamad kupima janja yake ili kubuni mbinu za kisheria kumzuia kupata mwanya wa kujiunga na serikali ya CDM bungeni!!!!!!!! Kuna formula moja naipenda-Mbunge mmoja wa CDM=wabunge 200 wa sisiemu!!!!!!!!!!!!!!!!!!pale bungeni!!!
 
Huyu William Malecela, nae usikute wanamwandaa kuwa rais 2015. Na usomi wake wote, na uzoefu wa kuishi nje ya nchi bado tuu anataka CHADEMA ishinde ndio katiba ibadilishwe. Mwaka 1992, baada ya tume ya kuratibu maoni ya kutaka vyama vingi kuonyesha wanaotaka vyama vingi nia asilimia 20 tuu na asilimia 80 wanataka chama kimoja tuu, Nyerere akasema rukhsa vyama vingi. Je, Bill anataka mpaka Chadema iwe na zaidi ya asilimia 50 ndo katiba ibadilishwe? Nyerere alitoa hoja nzuri na kusema, asilimia 20 ya wanaotaka vyama vingi inaonyesha upo umuhimu wa vyama vingi. Kama Chadema imepata zaidi ya asilimia 20 ndio katiba ibadilishwe, Je, Bill na wenzie wanaogopa nini? Au kwa kuwa wanajua wanaandaliwa kuja kuchukua nchi. Peace no hate
 
hamna wa chadema aliyebaki bungeni wakati rais anaongea......mimi nilikuwepo siku hiyo ndani na naomba tuufunge mjadala huu............!
kama rashid hakughafilika kwenye matamshi yake basi alikuwa na nia ya kuupotosha umma!
 
Huyu William Malecela, nae usikute wanamwandaa kuwa rais 2015. Na usomi wake wote, na uzoefu wa kuishi nje ya nchi bado tuu anataka CHADEMA ishinde ndio katiba ibadilishwe. Mwaka 1992, baada ya tume ya kuratibu maoni ya kutaka vyama vingi kuonyesha wanaotaka vyama vingi nia asilimia 20 tuu na asilimia 80 wanataka chama kimoja tuu, Nyerere akasema rukhsa vyama vingi. Je, Bill anataka mpaka Chadema iwe na zaidi ya asilimia 50 ndo katiba ibadilishwe? Nyerere alitoa hoja nzuri na kusema, asilimia 20 ya wanaotaka vyama vingi inaonyesha upo umuhimu wa vyama vingi. Kama Chadema imepata zaidi ya asilimia 20 ndio katiba ibadilishwe, Je, Bill na wenzie wanaogopa nini? Au kwa kuwa wanajua wanaandaliwa kuja kuchukua nchi. Peace no hate

- Hapa sasa mkuu ndio kabisaa unakubaliana na hoja yangu kwamba mambo ya haraka haraka kabla ya wakati ndio yametufikisha hapa tulipo, ukweli ni kwamba matokeo ya uchaguzi yanaonyesha exactly wananchi walichosema then kwamba bado wanataka chama kimoja, Mwalimu alitakiwa kuwasikiliza wananchi maana ndio Demokrasia yaani wananchi kuamua wanachotaka, kuwalazimisha wasichotaka ndio matokeo yake haya ndugu yangu, wananchi bado wanachagua CCM tu!

- Maana yake ni kwamba tulifkiri kwamba vyama vingi ndio jawabu, sasa sio siri kwamba hatukuwa tayari, naona imeanza ya katiba sasa utabadili vipi katiba na majority ya CCM, ndio ninasema tusidanganyane jamani, mambo badooo kidogo tusitafute njia za mkato mkato ndio zimelifikisha hili taifa tulipo sasa, yaani kwenye dead end!

I see the glass is one quarter Full and you say it is three quarters empty. We talk about the same thing projecting different perspective.
Ni kweli kwa mtazamo wako tumefika mwisho hatusongi mbele. Ukimwuliza bwana Mdogo Masha pale Nyamagana atakwambia opposition si mchezo hata Polisi wote wawe upande wako ushindi si jambo la wazi.

Are we even trying to approach the dead end?
 
- Hapa sasa mkuu ndio kabisaa unakubaliana na hoja yangu kwamba mambo ya haraka haraka kabla ya wakati ndio yametufikisha hapa tulipo, ukweli ni kwamba matokeo ya uchaguzi yanaonyesha exactly wananchi walichosema then kwamba bado wanataka chama kimoja, Mwalimu alitakiwa kuwasikiliza wananchi maana ndio Demokrasia yaani wananchi kuamua wanachotaka, kuwalazimisha wasichotaka ndio matokeo yake haya ndugu yangu, wananchi bado wanachagua CCM tu!

- Maana yake ni kwamba tulifkiri kwamba vyama vingi ndio jawabu, sasa sio siri kwamba hatukuwa tayari, naona imeanza ya katiba sasa utabadili vipi katiba na majority ya CCM, ndio ninasema tusidanganyane jamani, mambo badooo kidogo tusitafute njia za mkato mkato ndio zimelifikisha hili taifa tulipo sasa, yaani kwenye dead end!

William.

Kuna Mfaransa mmoja anaitwa Alex Tocqueville kaandika seminal work on Democracy, kaongelea sana kuhusu haja ya kulinda matakwa hata ya minority katika Democracy, Thomas Jefferson naye kaongelea wajibu wa Demokrasia kulinda hata haki za minority, ndio maana haki za kikatiba hazijali kama watu fulani ni majority au minority.

Of course vyama vingi si jawabu, vyama vingi ni njia tu kuelekea kwenye demokrasia zaidi. Soviet Union wao mpaka Perestroika ya Gorbachev walikuwa hata hawana ndoto za vyama vingi, wao mageuzi yao walitaka chaguzi ziwe na wagombea zaidi ya mmoja tu (kama sisi tulivyokuwa tunafanya wakati wa chama kimoja) kwao hii ilikuwa ni hatua kubwa, na Gorbachev alivyoleta Perestroika na Glasnost walitaka hata kumpindua.

The point is, there is no silver bullet here, this is a gradual process, and any step in the right direction, kwa mfano vyama ving, inaendana na kuongezeka kwa demokrasia.

Ukifikiri hili jini litarudi chupani utakuwa unaota.i
 
Kiranga umenena.
Mageuzi ni kama Land Slide.
Layer za chini ya ardhi huanza ku slide kwanza hali layer ya juu ikiwa imetulia tuli. Ikifika zamu ya layer ya juu kuslide yeyote asimamaye juu ya layer ile hana awezalo kufanya zaidi ya kufuata mkondo.
Wote tumerundikana pamoja tunajadiri matokeo kwa sababu ni rahisi kuyajadiri pia yanaonekana wazi. Tukigeuka na kurudi nyuma kuangalia chanzo ambacho mara nyingi hujaa usiiri utokanao na vitisho, mjadala unaweza geuka kuwa mgumu lakini wenye mantiki.
 
Tuko ukurasa wa tatu lakini mpaka sasa hatujaona majina ya hao wabunge kumi ambao "hawakutoka wakati rais analihutubia bunge".SMH!
 
Back
Top Bottom