Kumbe kuna salamu maalumu ukikutana na mtu usiku mzito? Usiku wa leo mbio ndiyo zimeniokoa

Hiyo ni kijijini mbona, mkikutana na mtu mida hiyo yoyote atakaetangulia kumuuliza mwenzake USIKU jibu MCHANA hapo kila mtu anajua amani

Hii niliikuta moja ya mikoa ya Kanda ya Ziwa sijui ndo ilivyo kote ama lah!

Lakini huko ukiuliza usiku na mwenzako wewe jibu mchana
 
Kuna knowledge ndogo sana ila ni za muhimu sanaa,
Usiku wa Leo Mida ya saa nane hivi nilikua napita kwenye chocho flani hivi, Ilikua ni njia ndefu iliyonyooka, upande wa Juu/kulia ni ukuta mrefuu, chini/kushoto ni mto wenye vichaka chaka..., kuanzia mwanzo wa ukuta mpk mwisho ni kama 500M hivi maana ni karakana ya reli kwa ndani.

Kwa mbele kuna mtu anakuja, ni giza kali naona weupe wa shati kidogo na ile mikwaruzo ya kiatu...
Wala sikuwaza chochote..

Nikasikia Sauti Kubwa "USIKU" mimi sikuelewa anamanisha nini, akasema tena "USIKU" nikiwa sina uhakika anaongea na mimi, Maana walikua wawili.
Nikajibu kwa Sauti "USIKUU"

Khaaaa, ghafa nasikia Mvurugano ya Vichaka, "kwacha kwacha kwachaaa" na mtu kama kaingia kwenye Maji, ghafa sione ule weupe wa shati, Nikiwa sielewi nini kinaendelea, kulipita upepo unafanya kuvuma sikioni kwangu, kumbe ni jiwe, nilishtuka baada ya kutua ukutani... ,

Hapo ndio nikajua hapa hakuna usalama,nikazima simu fasta tusionane, mbele nilikokua naelekea ndio pafupi, nyuma parefu mno.

Nikatoka kwenye kale ka njia, nikajibana upande wa chini wenye kichaka, nasikia tuu mtu anatembe kwenye maji, Mara nikasiki Washa tochi....

Aaaaaaaah, hapo ndio walipoharibu, kule nyuma nilikokua naona ni mbali sijui nilifikaje, ninachokumbuka tuu kuna washakaji wawili walikua nyuma yangu, mmoja alivyoona nimempita kwa speed naye nyuma akaunga kunifuata, wa pili hakusubiri nimpite kaona/sikia mtu anakuja kwa kasi akageuza.....

Kituo changu ilikua ni huku karibu na Tazara ushapita Mchicha, maana ilibidi nirudi nyuma huku, wale washkaji sijui waliishia wapi, ila ni kama walikunja kushoto kama wanaelekea njia ya vingunguti, Anyeifahamu kiwalani vzr ashafahamu chocho ninayoizungumzia.

Kufika home naelezea naambiwa, Nilitakiwa niseme "MCHANA" , ndio nikashangaa? How comes?
Anyway mimi niliyokua najua ni mtu akikuambia "SALAMA?" unajibu "SALAMA"

Tupeane tips kama kuna ishara au salamu nyingine za siku, haya maisha ya kuishi kwa mbio, sio siku zote utashinda.
Ha ha ha!
Za vijiweni hizo , lakini ujue mtu mbaya naye ana woga!
Aliposema USIKU, ungemjibu AMA ZAKO AU ZANGU.....uone unyayo unavyopotea!
 
Sahihi.

Wakati wa usiku unapokaribia kupishana na mtu ambaye bado hujaweza kumtambua. Unatakiwa kutoa salamu hiyo "Usiku?" hii maana yake ni "Shari?"

Kama ni amani imetawala unatakiwa kumjibu "Mchana"

Kama ni shari imetawala unatakiwa kumjibu "Usiku"
 
Sahihi.

Wakati wa usiku unapokaribia kupishana na mtu ambaye bado hujaweza kumtambua. Unatakiwa kutoa salamu hiyo "Usiku?" hii maana yake ni "Shari?"

Kama ni amani imetawala unatakiwa kumjibu "Mchana"

Kama ni shari imetawala unatakiwa kumjibu "Usiku"
Kwahy jomba alijibu kam Ngwaa na iwe ngwaa 😅😅 njooni kati niwafunze adabu
 
Back
Top Bottom