Mkasa wa treni ya usiku wa manane na mauaji ya watu wanaoipanda

SteveMollel

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
8,494
23,893
Huu ni mkasa unaoenda mwanzo mpaka mwisho wake. Enjoy.

Leon ana talanta ya kupiga picha lakini bado haijamlipa kama vile yeye anavyotamani.

Anaamini anastahili kupata zaidi na zaidi na jambo hili linamfanya akose kabisa furaha.

Screenshot_20240427-213258.png

Siku moja mpenzi wake (Maya) anampasha habari kuhusu bi. Susan Hoff, mwanamama anayefanya kazi ya kukusanya picha na kuzifanyia maonyesho makubwa yenye fedha kichele. Anamshauri akaonane na mwanamke huyo kwani huenda akapata kitu.

Kama mnavyojua mtafutaji hachoki, akichoka basi jua kapata.

Leon anashikana na mwenzake (Jurgis) njia na njia mpaka mezani kwa Susan. Anajitambulisha mimi ni mpiga picha mkali wa jiji la New York.

Anamwonyesha kazi ya mikono yake, zile kazi anazoziamini, lakini Susan anapozitazama, anaishia kutikisa kichwa.

Kazi zimepoa mno.

Kazi hazina msisimko.
Screenshot_20240427-213343.png

Anamshauri Leon kama kweli anataka kazi zake zitambulike na apige pesa ya maana basi avuke mipaka. Achakarike kuleta kazi zenye mikasa ya jiji la New York na matukio yake.

Hivyo Leon anaondoka na hili kichwani. Inapowadia usiku mzito, anazama subway (njia za chini za treni) kwenda kusaka content kali na huko anakumbana na kisa cha mwanamke alozingirwa na wahuni watatu wanaomshikashika maungo yake bila kutaka.

Leon anapiga picha za kutosha kisha anamsaidia mwanamke huyo ambaye anamshukuru kwa kumpa busu zito alafu anaaga na kwenda zake kupanda treni.

Ajabu kesho yake, Leon akiwa katika shughuli zingine, anastaajabu kukutana na sura ya mwanamke huyo kwenye uso wa gazeti na habari ya kuwa amepotea.
Screenshot_20240427-213455.png

Mara ya mwisho kuonekana kwake ni stendi ya treni za chini.

Imekuaje tena?

Anaenda polisi kutoa taarifa akiwa ameambatana na picha zake. Huko anakutana na mpelelezi Hadley, anamweleza lile tukio la jana na anamwonyesha picha za wale wanaume wahuni, anamwambia wanaume hawa watakuwa wanahusika na tukio, awafuatilie.

Mpelelezi anamvunja moyo kwa kumpuuzia.
Screenshot_20240427-213558.png

Leon anatoka hapo na kupeleka picha zake bi. Susan. Huko zinapokelewa kwa mikono ya furaha bi. Susan akimwambia hizi ndo' zenyewe. Anamtaka akapige picha zaidi na amletee kwaajili ya kazi.

Basi Leon anatoka hapa akifurahia.

Anampasha habari mpenzi wake na jamaa yake, Jurgis. Wanapata mbili tatu kujipongeza.

Lakini asipoteze majira, Leon anazama tena chimbo, wapi? Kulekule subway kwenda kutafuta picha kali.
Screenshot_20240427-213258.png

Anaketi kwenye viti akiangaza huku na kule kusaka tukio la kudaka macho. Kitambo kidogo anamwona bwana mmoja alovalia suti akiwa anapandishwa na ngazi ya umeme.

Bwana huyu ni jitu la miraba minne. Sura yake ni kavu. Haina hisia. Mkononi mwake amebebelea mkoba mweusi na amesimama hatikisiki kama vile mstimu.

Leon anavutiwa naye, hivyo anampiga picha kadhaa, na haishii hapo anamfuatilia kwa siri akiwa amebebelea kamera yake mkononi.

Hatua kwa hatua.

Mguu kwa mguu.

Hawafiki mbali, jibaba hili linamkamata Leon kwa mkono wake mmoja na kumtaka aache kumfuatilia kama kweli anajipenda.

Baadae nyumbani, Leon anapokagua picha alizopiga, anabaini jibaba lile limo kwenye picha ya yule mdada alopotea. Ni yeye ndo aliushikilia mlango wakati binti huyo akiwa anaingia kwenye treni.

Anaishia kujiuliza jibaba hili ni nani?

Kwasababu ya tetesi zinazozagaa mtaani juu ya watu kupotea kwenye treni nyakati za usiku, Leon anapata hamu ya kumfuatilia zaidi huyu mtu asijue anauingia mkenge.

Kwani huyu bwana ni balaa.

Mchana anafanya kazi ya bucha la wanyama na usiku anafanya kazi ya bucha la binadamu.

Treni ile ya mwisho, ya usiku wa manane, ndiyo sehemu yake ya kazi. Ukipanda humo basi badala ya kwenda nyumbani, unapelekwa akhera.
36a84386e6adf1f3a051a5d336bb7d6e.png

Kitambo kidogo utaona treni inahama njia na unapokuja kutahamaki, ushapigwa nyundo ya kichwa na shughuli yako inaishia hapo.

Unakatwakatwa na kisha unaning'inizwa kwenye vyuma vya kubebea nyama. Ndio. Vile vyuma unavyovionaga buchani vimeshikilia paja la ng'ombe.

Ndo' hivyohivyo.

Sasa treni inaelekea wapi na hizi nyama za binadamu zina kazi gani?

Calm down ... turudi kwa mpiga picha.

Leon anamfuatilia jibaba hili na anabaini huwa anakaa kituoni kwa masaa mengi. Treni zinakuja na hapandi. Ana kazi ya kutazama huku na kule, kule na huku, watu wanakatiza na kuishia.

Anasubiri hapo mpaka usiku wa manane inapokuja treni ya mwisho kabisa. Sasa watu ni wachache sana kituoni na ni wachache sana wanaopanda.

Anaingia humo na kutulia akitazama mawindo yake vema.

Leo treni hii inaposimama kwenye majira yake ya kila siku, Leon anaipanda akimfuata jibaba hili kwa usiri.

Baada ya treni kuondoka tu, jibaba linaamka, linachomoa kitendea kazi kwenye mkoba, nyundo mshindo, kisha linaanza kutekeleza kazi yake kwa ustadi.

Alooh.

Unaijua ile nyimbo ya Marioo anaimba, nipo nyuma naiokota, dondosha mmmh aaah dondosha ... basi mwana ndo' anapita humohumo.

Mmoja mmoja.

Sema na nyundo.

Leon ananyanyua kamera yake kunasa tukio hili la ajabu. Anapiga picha kadiri anavyoweza. Jibaba linamwona na wala halina papara naye, atakimbilia wapi ndani ya treni hii?

Anapomaliza amamfuata Leon na kumdhibiti. Anambamiza bwana huyo kwenye kioo na Leon anazirai papo hapo!

Kuja kuamka yupo machinjioni kule buchani. Anatazama kando na kando, hamna mtu. Anajikokota na kutoka sehemu hii akiugulia maumivu ya kichwa.

Lakini kwanini hakuuawa kama wale wengine ndani ya treni?

Relax ...

Leon anafika nyumbani, anapokelewa na mpenzi wake, Maya. Kwenda kutazama kwenye kioo anagundua amechorwa chapa kubwa kifuani, chapa iliyochimba kifuani.

Anamweleza mpenzi wake kila kitu kilichotokea. Anamwambia wakienda polisi hawataaminika maana ushahidi wote umebebwa kwenye kamera.

Kwa kumsaidia mpenzi wake, Maya pamoja na Jurgis wanatumia data za Leon kutafuta na hatimaye kupata makazi ya jibaba la treni.

Humo ndani wanapekua kusaka kamera ya kazi lakini pia kamera yenye ushahidi.

Kabla hawajamaliza, mwenye nyumba huyu hapa!

Jurgis hana hili wala lile, jibaba anamkandika nyundo ya kichwa, ubongo unaitika abeeh. Analamba mchanga.

Jibaba linamsogelea Maya lakini bahati nzuri mwanamke huyo anajinusuru na kutoroka zake.

Hajaondoka mikono mitupu. Amefanikiwa kubeba nyaraka zenye rekodi ya watu walouawa kwenye treni kwa takribani miaka mia moja mfululizo. Rekodi hii aliikuta chumbani mwa jibaba lile.

Anaenda moja kwa moja polisi kutoa taarifa. Huko anakutana na mpelelezi Hadley. Anamwambia afande sikiliza, Jurgis katekwa kwenye ile nyumba na pia yule bwana anaua watu kwenye treni, tazama rekodi zake hizi hapa.
Screenshot_20240427-213558.png

Mpelelezi anamwambia tuliza munkari. Kwanza kunywa maji, alafu pili hamna kitu kama hicho. Baada ya Maya kusihi sana mpelelezi anasema ametuma watu kwenye eneo la tukio, hawajaona kitu.

Ni kweli haya?

Maya anaona huu ni utani. Na kweli ni utani. Anamnyooshea bunduki mpelelezi aseme kweli, hatimaye mpelelezi anafunguka akautazame mwili wa Jurgis kwenye treni.

Kumbe anayafahamu haya!

Maya anaenda kituoni na anaipanda ile treni ya usiku wa manane. Leon naye anatokea hapo kituoni akitokea kuonana na bi. Susan. Anaiwahi na kuidandia treni hiyo.
d37aad8018cac522bb9932f2f6fbcf9e.png

Kwahiyo humu ndani sasa wanakuwa watu watatu.

Pambano kali linazuka.

Kwa mbinde wanamzima jitu la miraba minne lakini si punde treni inasimama. Safari imefika ukomo. Taa zinazima ndani ya treni na dereva anakuja kuwaambia waende nje.

Kumbe kuna viumbe vinavyoletewa nyama hizi za binadamu. Viumbe hivyo vinaingia ndani na kuanza kujichana mapande kwa mapande.

Kula bila kuvimbiwa.
32f8e132f029b340a4d758d8daf5d4ad.png

Leon na Maya wanatoka nje ya treni na huko wanakabiliana tena na jitu la miraba minne ambalo limetoka kuamka.

Katika mapambano haya, Maya anauawa na pia Leon anadhibitiwa na Dereva wa treni ambaye anakuja kumsaidia jitu.

Humu ndo' Leon anapata kuujua ukweli. Ukweli ya kwamba hii oparesheni ya watu kuuawa ndani ya treni inafahamika na kufadhiliwa na serikali.

Lengo la watu hawa kuuawa ni kuwalisha viumbe hatari, reptilians, kwa lengo la kuufanya jiji kuwa salama kwani wasipofanya hivyo watakuja kulivamia jiji na kusababisha maafa makubwa.

Leon anashangaa.

Na zaidi tunakuja kushangaa kumbe ile alama alopachikwa Leon kifuani ni chapa ya mchinjaji. Leon ndiye atarithi nafasi ya jitu la miraba. Kumbe ndo' maana hakuuawa muda ule.
Screenshot_20240427-213832.png

Na kwa kawaida mtu anayemuua 'the butcher' yeye ndo' anakuwa mrithi moja kwa moja.

Hivyo mpelelezi Hadley, yule tulokuwa tunamwona hapo mwanzo, anamkabidhi Leon vitendea kazi na anamwambia:

"Karibu kwenye secret society."

Kesho yake tunamwona mtu akiwa anakwea treni ya usiku wa manane huku amevalia suti na kubebelea mkoba mkononi.

Mtu huyo anaketi kwenye kiti. Na punde anapogeuza uso wake, dah, ni Leon!

Tayari ashaanza kazi.

Kazi ya kumaliza watu waliomo ndani ya hii treni.
.
.
.
Mzigo unaitwa "The Midnight Meat Train"

Screenshot_20240427-214133.png
 
Huu ni mkasa unaoenda mwanzo mpaka mwisho wake. Enjoy.

Leon ana talanta ya kupiga picha lakini bado haijamlipa kama vile yeye anavyotamani.

Anaamini anastahili kupata zaidi na zaidi na jambo hili linamfanya akose kabisa furaha.

View attachment 2975566
Siku moja mpenzi wake (Maya) anampasha habari kuhusu bi. Susan Hoff, mwanamama anayefanya kazi ya kukusanya picha na kuzifanyia maonyesho makubwa yenye fedha kichele. Anamshauri akaonane na mwanamke huyo kwani huenda akapata kitu.

Kama mnavyojua mtafutaji hachoki, akichoka basi jua kapata.

Leon anashikana na mwenzake (Jurgis) njia na njia mpaka mezani kwa Susan. Anajitambulisha mimi ni mpiga picha mkali wa jiji la New York.

Anamwonyesha kazi ya mikono yake, zile kazi anazoziamini, lakini Susan anapozitazama, anaishia kutikisa kichwa.

Kazi zimepoa mno.

Kazi hazina msisimko.
View attachment 2975567
Anamshauri Leon kama kweli anataka kazi zake zitambulike na apige pesa ya maana basi avuke mipaka. Achakarike kuleta kazi zenye mikasa ya jiji la New York na matukio yake.

Hivyo Leon anaondoka na hili kichwani. Inapowadia usiku mzito, anazama subway (njia za chini za treni) kwenda kusaka content kali na huko anakumbana na kisa cha mwanamke alozingirwa na wahuni watatu wanaomshikashika maungo yake bila kutaka.

Leon anapiga picha za kutosha kisha anamsaidia mwanamke huyo ambaye anamshukuru kwa kumpa busu zito alafu anaaga na kwenda zake kupanda treni.

Ajabu kesho yake, Leon akiwa katika shughuli zingine, anastaajabu kukutana na sura ya mwanamke huyo kwenye uso wa gazeti na habari ya kuwa amepotea.
View attachment 2975568
Mara ya mwisho kuonekana kwake ni stendi ya treni za chini.

Imekuaje tena?

Anaenda polisi kutoa taarifa akiwa ameambatana na picha zake. Huko anakutana na mpelelezi Hadley, anamweleza lile tukio la jana na anamwonyesha picha za wale wanaume wahuni, anamwambia wanaume hawa watakuwa wanahusika na tukio, awafuatilie.

Mpelelezi anamvunja moyo kwa kumpuuzia.
View attachment 2975569
Leon anatoka hapo na kupeleka picha zake bi. Susan. Huko zinapokelewa kwa mikono ya furaha bi. Susan akimwambia hizi ndo' zenyewe. Anamtaka akapige picha zaidi na amletee kwaajili ya kazi.

Basi Leon anatoka hapa akifurahia.

Anampasha habari mpenzi wake na jamaa yake, Jurgis. Wanapata mbili tatu kujipongeza.

Lakini asipoteze majira, Leon anazama tena chimbo, wapi? Kulekule subway kwenda kutafuta picha kali.
View attachment 2975570
Anaketi kwenye viti akiangaza huku na kule kusaka tukio la kudaka macho. Kitambo kidogo anamwona bwana mmoja alovalia suti akiwa anapandishwa na ngazi ya umeme.

Bwana huyu ni jitu la miraba minne. Sura yake ni kavu. Haina hisia. Mkononi mwake amebebelea mkoba mweusi na amesimama hatikisiki kama vile mstimu.

Leon anavutiwa naye, hivyo anampiga picha kadhaa, na haishii hapo anamfuatilia kwa siri akiwa amebebelea kamera yake mkononi.

Hatua kwa hatua.

Mguu kwa mguu.

Hawafiki mbali, jibaba hili linamkamata Leon kwa mkono wake mmoja na kumtaka aache kumfuatilia kama kweli anajipenda.

Baadae nyumbani, Leon anapokagua picha alizopiga, anabaini jibaba lile limo kwenye picha ya yule mdada alopotea. Ni yeye ndo aliushikilia mlango wakati binti huyo akiwa anaingia kwenye treni.

Anaishia kujiuliza jibaba hili ni nani?

Kwasababu ya tetesi zinazozagaa mtaani juu ya watu kupotea kwenye treni nyakati za usiku, Leon anapata hamu ya kumfuatilia zaidi huyu mtu asijue anauingia mkenge.

Kwani huyu bwana ni balaa.

Mchana anafanya kazi ya bucha la wanyama na usiku anafanya kazi ya bucha la binadamu.

Treni ile ya mwisho, ya usiku wa manane, ndiyo sehemu yake ya kazi. Ukipanda humo basi badala ya kwenda nyumbani, unapelekwa akhera.
View attachment 2975571
Kitambo kidogo utaona treni inahama njia na unapokuja kutahamaki, ushapigwa nyundo ya kichwa na shughuli yako inaishia hapo.

Unakatwakatwa na kisha unaning'inizwa kwenye vyuma vya kubebea nyama. Ndio. Vile vyuma unavyovionaga buchani vimeshikilia paja la ng'ombe.

Ndo' hivyohivyo.

Sasa treni inaelekea wapi na hizi nyama za binadamu zina kazi gani?

Calm down ... turudi kwa mpiga picha.

Leon anamfuatilia jibaba hili na anabaini huwa anakaa kituoni kwa masaa mengi. Treni zinakuja na hapandi. Ana kazi ya kutazama huku na kule, kule na huku, watu wanakatiza na kuishia.

Anasubiri hapo mpaka usiku wa manane inapokuja treni ya mwisho kabisa. Sasa watu ni wachache sana kituoni na ni wachache sana wanaopanda.

Anaingia humo na kutulia akitazama mawindo yake vema.

Leo treni hii inaposimama kwenye majira yake ya kila siku, Leon anaipanda akimfuata jibaba hili kwa usiri.

Baada ya treni kuondoka tu, jibaba linaamka, linachomoa kitendea kazi kwenye mkoba, nyundo mshindo, kisha linaanza kutekeleza kazi yake kwa ustadi.

Alooh.

Unaijua ile nyimbo ya Marioo anaimba, nipo nyuma naiokota, dondosha mmmh aaah dondosha ... basi mwana ndo' anapita humohumo.

Mmoja mmoja.

Sema na nyundo.

Leon ananyanyua kamera yake kunasa tukio hili la ajabu. Anapiga picha kadiri anavyoweza. Jibaba linamwona na wala halina papara naye, atakimbilia wapi ndani ya treni hii?

Anapomaliza amamfuata Leon na kumdhibiti. Anambamiza bwana huyo kwenye kioo na Leon anazirai papo hapo!

Kuja kuamka yupo machinjioni kule buchani. Anatazama kando na kando, hamna mtu. Anajikokota na kutoka sehemu hii akiugulia maumivu ya kichwa.

Lakini kwanini hakuuawa kama wale wengine ndani ya treni?

Relax ...

Leon anafika nyumbani, anapokelewa na mpenzi wake, Maya. Kwenda kutazama kwenye kioo anagundua amechorwa chapa kubwa kifuani, chapa iliyochimba kifuani.

Anamweleza mpenzi wake kila kitu kilichotokea. Anamwambia wakienda polisi hawataaminika maana ushahidi wote umebebwa kwenye kamera.

Kwa kumsaidia mpenzi wake, Maya pamoja na Jurgis wanatumia data za Leon kutafuta na hatimaye kupata makazi ya jibaba la treni.

Humo ndani wanapekua kusaka kamera ya kazi lakini pia kamera yenye ushahidi.

Kabla hawajamaliza, mwenye nyumba huyu hapa!

Jurgis hana hili wala lile, jibaba anamkandika nyundo ya kichwa, ubongo unaitika abeeh. Analamba mchanga.

Jibaba linamsogelea Maya lakini bahati nzuri mwanamke huyo anajinusuru na kutoroka zake.

Hajaondoka mikono mitupu. Amefanikiwa kubeba nyaraka zenye rekodi ya watu walouawa kwenye treni kwa takribani miaka mia moja mfululizo. Rekodi hii aliikuta chumbani mwa jibaba lile.

Anaenda moja kwa moja polisi kutoa taarifa. Huko anakutana na mpelelezi Hadley. Anamwambia afande sikiliza, Jurgis katekwa kwenye ile nyumba na pia yule bwana anaua watu kwenye treni, tazama rekodi zake hizi hapa.
View attachment 2975573
Mpelelezi anamwambia tuliza munkari. Kwanza kunywa maji, alafu pili hamna kitu kama hicho. Baada ya Maya kusihi sana mpelelezi anasema ametuma watu kwenye eneo la tukio, hawajaona kitu.

Ni kweli haya?

Maya anaona huu ni utani. Na kweli ni utani. Anamnyooshea bunduki mpelelezi aseme kweli, hatimaye mpelelezi anafunguka akautazame mwili wa Jurgis kwenye treni.

Kumbe anayafahamu haya!

Maya anaenda kituoni na anaipanda ile treni ya usiku wa manane. Leon naye anatokea hapo kituoni akitokea kuonana na bi. Susan. Anaiwahi na kuidandia treni hiyo.
View attachment 2975574

Kwahiyo humu ndani sasa wanakuwa watu watatu.

Pambano kali linazuka.

Kwa mbinde wanamzima jitu la miraba minne lakini si punde treni inasimama. Safari imefika ukomo. Taa zinazima ndani ya treni na dereva anakuja kuwaambia waende nje.

Kumbe kuna viumbe vinavyoletewa nyama hizi za binadamu. Viumbe hivyo vinaingia ndani na kuanza kujichana mapande kwa mapande.

Kula bila kuvimbiwa.
View attachment 2975575
Leon na Maya wanatoka nje ya treni na huko wanakabiliana tena na jitu la miraba minne ambalo limetoka kuamka.

Katika mapambano haya, Maya anauawa na pia Leon anadhibitiwa na Dereva wa treni ambaye anakuja kumsaidia jitu.

Humu ndo' Leon anapata kuujua ukweli. Ukweli ya kwamba hii oparesheni ya watu kuuawa ndani ya treni inafahamika na kufadhiliwa na serikali.

Lengo la watu hawa kuuawa ni kuwalisha viumbe hatari, reptilians, kwa lengo la kuufanya jiji kuwa salama kwani wasipofanya hivyo watakuja kulivamia jiji na kusababisha maafa makubwa.

Leon anashangaa.

Na zaidi tunakuja kushangaa kumbe ile alama alopachikwa Leon kifuani ni chapa ya mchinjaji. Leon ndiye atarithi nafasi ya jitu la miraba. Kumbe ndo' maana hakuuawa muda ule.
View attachment 2975576
Na kwa kawaida mtu anayemuua 'the butcher' yeye ndo' anakuwa mrithi moja kwa moja.

Hivyo mpelelezi Hadley, yule tulokuwa tunamwona hapo mwanzo, anamkabidhi Leon vitendea kazi na anamwambia:

"Karibu kwenye secret society."

Kesho yake tunamwona mtu akiwa anakwea treni ya usiku wa manane huku amevalia suti na kubebelea mkoba mkononi.

Mtu huyo anaketi kwenye kiti. Na punde anapogeuza uso wake, dah, ni Leon!

Tayari ashaanza kazi.

Kazi ya kumaliza watu waliomo ndani ya hii treni.
.
.
.
Mzigo unaitwa "The Midnight Meat Train"

View attachment 2975577
Umepiga mulemule haya mambo ya secret society yapo sana basi ni vile tuko mbele ya pazio sio Nyuma
 
Back
Top Bottom