Kumbe kuna salamu maalumu ukikutana na mtu usiku mzito? Usiku wa leo mbio ndiyo zimeniokoa

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Kuna knowledge ndogo sana ila ni za muhimu sana,

Usiku wa leo Mida ya saa nane hivi nilikua napita kwenye chocho fulani hivi, Ilikua ni njia ndefu iliyonyooka, upande wa Juu/ kulia ni ukuta mrefuu, chini/ kushoto ni mfereji wenye vichaka chaka.

Kuanzia mwanzo wa ukuta mpaka mwisho ni kama 500M hivi maana ni karakana ya reli kwa ndani.

Kwa mbele kuna mtu anakuja, ni giza kali naona weupe wa shati kidogo na ile mikwaruzo ya kiatu. Wala sikuwaza chochote..

Nikasikia Sauti Kubwa "USIKU" mimi sikuelewa anamanisha nini, akasema tena "USIKU" nikiwa sina uhakika anaongea na mimi, Maana walikua wawili.
Nikajibu kwa Sauti "USIKUU"

Khaaaa, ghafa nasikia Mvurugano ya Vichaka, "kwacha kwacha kwachaaa" na mtu kama kaingia kwenye Maji, ghafa sione ule weupe wa shati, Nikiwa sielewi nini kinaendelea, kulipita upepo unafanya kuvuma sikioni kwangu, kumbe ni jiwe, nilishtuka baada ya kutua ukutani.

Hapo ndio nikajua hapa hakuna usalama, nikazima simu fasta tusionane, mbele nilikokua naelekea ndio pafupi, nyuma parefu mno.

Nikatoka kwenye kale ka njia, nikajibana upande wa chini wenye kichaka, nasikia tu mtu anatembe kwenye maji, Mara nikasikia Washa tochi.

Aaaaaaaah, hapo ndio walipoharibu, kule nyuma nilikokua naona ni mbali sijui nilifikaje, ninachokumbuka tuu kuna washakaji wawili walikua nyuma yangu, mmoja alivyoona nimempita kwa speed naye nyuma akaunga kunifuata, wa pili hakusubiri tumpite kaona/sikia mtu anakuja kwa kasi akageuza, pamoja na kutojua kinachoendelea, ila speed yake hata mimi ninayejua nini kinaendelea ilinishangaza.

Kituo changu ilikua ni huku karibu na Tazara ushapita Mchicha, maana ilibidi nirudi nyuma huku, wale washkaji sijui waliishia wapi, ila ni kama walikunja kushoto kama wanaelekea njia ya vingunguti, Anyeifahamu kiwalani vizuri ashafahamu chocho ninayoizungumzia.

Kufika home naelezea naambiwa, Nilitakiwa niseme "MCHANA" , ndio nikashangaa? How comes?

Anyway mimi niliyokua najua ni mtu akikuambia "SALAMA?" unajibu "SALAMA"

Tupeane tips kama kuna ishara au salamu nyingine za siku, haya maisha ya kuishi kwa mbio, sio siku zote utashinda.
 
"Huwa najibu nilikotoka ni amani vipi huko mlikotoka/mlipotoka"

Huwa sirudii tena kuongea wala kuuliza huku mkononi nimeshika jiwe lililojaa kwenye kiganja vizuri na kama mpo wawili huwa napita katikati yenu bila kuonesha kama nawaogopa sasa jichanganye ukione cha mtemakuni.
 
Back
Top Bottom