Kumbe kubeba mimba si mchezo!

Mshukuru Mungu kwa kumjalia neema mke wako ya kujifungua salama kwa wakati na bila usumbufu au matatizo yoyote ki afya ila hiyo neema aliyokupa Mungu isikupe kiburi ukamkufuru.

Unataka kuniambia wanaofia leba wakijifungua nao huwa wanaigiza kufa? Au wanaoshindikana kujifungua kawaida hadi wanaamua kumfanyia upasuaji ule ni uigizaji?

Kiburi cha uzima kinakusumbua . Mshukuru Mungu kwa ajili ya neema yake maishani mwenu ila usikufuru. Hiyo ni Neema tu wala haukustahili.

Hayo maneno aliyotamka katamka kws kuwa mkewe hajawahi kupitia changamoto za ujauzito
Ila siku wkipitia atakuja hapa kuomba msamaha
 
Sawa kwa experience yako hiyo unayosema unayo, haujawahi kuona wanawake wajawazito wanalazwa hospitali kwa sababu kila wanachokula wanatapika? Haujawahi kuona?

Wewe hata experience hauna una udikteta wa kijinga kudhani kila hali ya ujauzito inayojitokeza kwa mwanamke ni maigizo. Pengine hata mke wako alikuwa akisikia kutapika anajizuia maskini asijeonekana anajiendekeza.

Kipenzi usibishane na mpumbavu ukaja kufanana nae
Ni mtu mjinga tu ambaye anadhani mwanamke akibeba mimba anaigiza kuumwa na kudeka
Halafu hajui km hilo jambo sio kila mwanamke linamtokea yeye kakomaa tu et mkewe hajawahi kuumwa amshukuru Mungu kwa hilo

Hii ni km ajali basi linapinduka wengine wanakufa wengi wanapona huwezi sema waliokufa wametaka wao
 
Jamani kwema?
Ila wanawake ni wasiri jamani, mbona hata hamsemagi kwamba hizi "morning sickness" hilo ni neno tu ila inashinda siku nzima jamani?

Natamani hata mtu angeniambia kwamba ni vichefuchefu siku nzima. Mimi nilijua kama jina lilivyo basi ikifika mchana natakiwa niwe fresh.

Week 8 sasa ila food eversion na nausea muda wote. Kila chakula ninachokifikiria nahisi kichefuchefu.

Nahisi kuumwaumwa tu nikikaa sisikii raha nikilala sisikii raha bora hata kutembea tembea nje. Hiki kichefuchefu natamani hata nitapike ila ni kichefuchefu tu bila kutapika. Khaaa hadi natamani nipige mayowe.

Acha tu jamani watu waringe na watoto wao. Sasa nimeelewa.



View: https://youtube.com/shorts/Wb-RNCSZ6Ns?feature=shared
 
Sikia miezi mitatu minne ya mwanzo yaani hakuna rangi utaacha kuona.mimi nilikuwa natamani kutapika dunia yote.yaani chakula unachagua nilikuwa najipikia mwenyewe maana mtu akipika asipopika kama navotaka na yeye namchukia vibaya mno sitaki hata kumuona tena nikija kumuona natapika tu
Ila nikuombe usiache kutumia folic japo zinachangia kuchefua ila usiache
Ukimaliza miezi ya mwanzo mwezi wa nne kati hapo hadi saba unakuwa sawa ila kuchoka sana maana mtumbo unakuwa ushaanza kujaa na unatakiw ulale kushoto sana.so unachoka na uzito unakuwa umeongezeka hata kilo 10 hivi
Miezi ya mwisho nayo ni kuchooka maana mtoto anakuwa kawa mkubwa zaidi ila hujiskii vibaya kiivo jikaze
Ila hakikisha una folic na mavitamins ili uzae katoto kazuri
Sasa hivi nimeshapita ile miezi ya tabu😍😍. Nilifungulia kutapika , nilikuwa natapika hata ninusa harufu ya pregnacare. Nilikuwa nakula ili tu nipate cha kutapika maana ukimaliza kula tu ni kutapika.

Mungu ni mwema sasa hivi nina kichefuchefu cha kawaida na nitatapika tu endapo nitajilazimisha kula chakula ambacho sikipendi.

hebu fikiria sipendi kuku eti🤨 na samaki aina yoyote ile na nyama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom