Hadithi za Kusisimua9933
Member
- Apr 1, 2022
- 96
- 175
SEASON 01
TAMTHILIA: MTU ALIYETHIBITISHWA KWA MAISHA YANGU
CERTIFIED PERSON OF MY LIFE (CPL)
( 1-5 )
SEHEMU YA 01.
D ARASANI:
llikua ni muda wa kipindi cha ujasiriamali kwa wanafunzi wa kozi ya biashara. Mwalimu wa somo alikuwa mbele ya Darasa akifundisha. Kutokana na ukali wa Mwalimu huyo; darasa lilikua kimya sana. Frank akiwa kama mmoja wa wanachuo alikua makini sana kusikiliza. Ilifikia hatua alitikisa kichwa juu chini kuonyesha namna ambavyo alielewa mafunzo kutoka kwa mwalimu wake. Kabla kipindi hakijaisha Mwalimu aliuliza swali;
MWALIMU: Wanafunzi, nani anapenda kuwa mfanyabiashara? kwanini? Na mtaji utaupata wapi? (Mwanachuo wa kwanza kunyosha mkono alikuwa ni Loveness, aliambiwa ajibu swali, naye bila kupoteza muda alisimama kisha alijibu kama ifuatavyo)
LOVENESS: Mimi sipendi kuwa mfanyabiashara kwa sababu biashara zina hasara nyingi, ni ngumu kupata mtaji kwa sababu watu wengi wanaitaji fedha na fedha ni ngumu kupatikana.
(Love alimaliza kutoa jibu lake. Kabla mwalimu hajaongea chochote mara aliona mkono mwingine kutoka kwa Frank)
MWALIMU: Naona mkono mwingine pale, bila shaka uliyenyosha mkono una jibu jipya; Ebu tupe jibu lako. FRANK:
(Alisimama kisha alijibu) Mwalimu nataka nimjibu Loveness. Love unaposema kwa m ba hupendi kuwa mfanyabiashara una maana gani? Na kama hupendi tuambie kwanini unasomea kozi ya biashara?
LOVENESS: Mfanyabiashara ni sawa na mtu aliyejiajiri, sasa mimi nikijiajiri kuna faida gani za kusoma? Si nitakua nimepoteza fed ha zangu. Sasa si bora ningekaa nyumbani na hizo fedha za ada ningezitumia kama mtaji. Nasomea Biashara kwa sababu Serikali itanipa ajira zinazohusu usimamizi wa biashara za wananchi.
FRANK: Hapana, kumbe una mawazo finyu hivyo? Tena wewe mwanachuo wa elimu ya juu unawezaje kutupatia majibu kama hayo? Hata hiyo Serikali haiwezi ikakuamini kwa sababu huwezi kuongoza wafanyabiashara wakati hupendi biashara.
LOVENESS: Kwani tatizo lipo wapi? Jamani kila mtu ana ndoto zake. Humu ndani kuna watu wanawaza kujiajiri na kuna wengine akina sisi hatuna mpango huo. Mimi nachoamini ni kwamba baada ya kuhitimu chuo kinachofuata ni kuajiriwa tu, na nina imani kuwa nitaajiriwa tu. Siwezi kupoteza muda wangu na fed ha zangu bure! Eti nijiajiri, looh! hata wale wenzangu walioko mtaani si watanicheka?
FRANK: Loveness!! kwanza serikali ni nini? Unataka kusema Serikali haifanyi biashara? Hivi hujawai kusikia Serikali inanunua au kuuza vitu nje ya nchi? Tena ni juzi tu tulimaliza mada ya biashara za kimataifa (international trade), unataka kusema ile mada hukuilewa au?
SEHEMU YA 02
LOVENESS: Kwanza wewe unataka nini? Kama unaona jibu langu sio sahihi basi tupatie jibu lako. Kwa sababu naona unapinga sana mawazo yangu. (aliongea akiwa amepanick, kwa hasira aliamua kukaa chini)
FRANK: Haina haja ya kukasirika kwa sababu swali liko wazi kwa sisi wote ambao tunachukua kozi ya biashara. Mimi sijamaanisha kwamba sitaki kuajiriwa, pia sijamkataza mtu kuajiriwa, ila kutokana na swali la mwalimu; majibu ya dada yetu Love sidhani kama ni sahihi. Mwanachuo aliye kamili kifikra hawezi kutujibu majibu kama hayo, alafu....
(Frank kabla hajamaliza kuongea; Loveness alisimama akiwa amejazwa hasira na jazba)
LOVENESS: Kwahiyo mimi sina fikra? mimi sifai kuwa mwanachuo au sio? unaamua kunitu.... (Love alishindwa kuendelea kuongea, pale pale alianza kulia kwa kwikwi, ghafla alipiga hatua alitoka nje ya darasa pasipo kugeuka nyuma)
(Baada ya tukio hilo kulitokea ukimya mzito, wanachuo walikausha kimya.
Baadhi walimuonea huruma Love. Wengine waliona ni jambo la kawaida. Frank bado alisimama, alitaka kukaa lakini alisimamishwa na mwalimu, aliambiwa ajibu swali kwa faida ya wengine)
FRANK: Mimi napenda kuwa mfanyabiashara, hata kama ikitokea nikapata ajira selikalini lakini sitoacha kufanikisha ndoto zangu za kuwa mfanyabiashara. Na ndio maana niliamua kusomea kozi hii. Napenda biashara kwa sababu inapatikana kila sehemu. Biashara ipo kwenye sekta za umma hata sekta binafsi. Kuwa mfanyabiashara kuna faida nyingi kama vile uhuru wa maisha, uhuru wa maamuzi, pesa zisizo na kikomo na faida nyinginezo. Biashara inatengenezwa na bidhaa pamoja na huduma za kijamii, hivyo basi ni rahisi mtu yeyote kujikita katika sekta hiyo, na ndio maana hata serikali inatengenezwa na biashara.
Kuhusu mtaji ni rahisi tu, kuna mikopo kutoka benki na mashirika, akiba binafsi, misaada toka kwa watu wa karibu (familia na marafiki), wadhamini na kadhalika.
MWALIMU: Safi sana, nadhani hakuna
hasiyekuelewa, hii inaonyesha ni jinsi gani una upeo wa kielimu hasa katika kozi yako ya biashara.
Darasa tutaonana kipindi kijacho. (Mwalimu aliondoka darasani).
(Baada ya Mwalimu kuondoka tu; huku nyuma kulisikika minong'ono na mijadala kuhusu yaliyotokea, kuna waliosema Frank amekosea sana kwa kumdhalilisha Loveness, wengine walisema Frank ameongea sahihi. Ilikua ni kelele tu, kila mtu aliongea neno lake. Wanachuo walitawanyika walielekea hosteli. Ndani ya darasa alibaki Frank pekee. Ilikuwa ni mida ya saa sita mchana, jamaa aliona bora ajisomee akiwa anasubiri muda wa chakula cha mchana. Alitoa daftari na peni kisha alianza kupiga pindi. Hakutaka kuwaza sana kuhusu kilichotokea kwa sababu aliona ameongea vitu ambavyo mtu yeyote angeweza kuongea.
Akiwa anajisomea mara aliingia mdada flani hivi aitwaye Maria
MARIA: Frank vipi? mbona umebaki peke yako humu ndani?
FRANK: Nimeamua tu, napitia pitia vitu flani.
MARIA: Hivi una taarifa kuwa mwenzio kapelekwa hospitali?
FRANK: Mwenzangu gani?
MARIA: Loveness. Baada ya kususa kipindi alikimbilia hosteli akiwa analia. Sie tumetoka kipindi tumefika hosteli tumekuta mtu kazidiwa, ilibidi tumuwahishe hospitali ya chuo.
FRANK: (Akishangaa) Eeh! lakini si alikua poa tuü amezidiwa kwa tatizo gani?
MARIA: Hospitali wanasema alizidiwa na maumivu ya kichwa. Na inasemekana kuwa chanzo ni wewe!
(Frank alikodoa macho, alishindwa kuelewa! Balaa zitoooo!!)
ITAENDELEA
SEHEMU YA 03
FRANK: Kwahyo hata wewe Maria unaamini mimi ni chanzo?
MARIA: Sasa chanzo ni nani? Nahisi ni kutokana na yale uliyoongea Darasani.
FRANK: Kwani niliongea vibaya?
MARIA: Hapana, ulikua sahihi tena sana tu, ila ndo hivyo mtu yupo hospitali.
FRANK: Sawa, mimi naenda kula. Kwanza nishachoka, nataka nikapumzike hosteli (Aliongea akisimama kisha alipiga hatua akiondoka)
MARIA: We Frank wewe, ina maana huendi hospitali kumuona Love?...Mmh! makubwa.
Frank alipotelea nje, Maria aliganda kwa sekunde flani akiwa anashangaa kisha nae aliamua kuondoka! HOSPITALI:
Loveness akiwa hospitali alitembelewa na marafiki zake ambao ni wanachuo wenzie. Baadhi walimletea zawadi kama Juisi, Biskuti na matunda; aliwashukuru. Issa alikuwa ni mmoja wa wanachuo ambao walimtembelea Love hospitali, yeye baada ya kufika ndani ya chumba cha mgonjwa alikaa pembeni ya Godoro kisha alitoa pole zake kama ifuatavyo;
LOVENESS: Kwa sasa naendelea vizuri, dokta kasema naweza kuruhusiwa.
ISSA: Kwani tatizo lilikua nini?
LOVENESS: Ni kichwa tu ila kwa sasa niko poa.
ISSA: Kwahiyo kesho utakuja kwenye kipindi?
LOVENESS: Nitaangalia.
(Mara aliingia daktari, aliwaomba wanachuo wampishe ili aongee na mgonjwa wake. Wanachuo walitoka nje.)
DOKTA: (Akimtazama Love) Kama nilivyosema; jitahidi kupunguza mawazo. Mara nyingi mawazo ndio sababu kubwa ya maumivu ya kichwa. Pia hakikisha unakunywa maji mengi na ufanye mazoezi ili mwili upate afya bora na nguvu. Pia usipende kukaa pekeyako, njia kuu ya kuondoa fikra, stress na mawazo mabovu ni kujichanganya na watu wengine. LOVE: Sawa.
Dokta alimaliza kutoa ushauri kisha alimruhusu Love kuondoka hospitali. Love na marafiki zake waliondoka, walirudi chuoni hosteli.
HOSTELI:
Frank baada ya kula alielekea hosteli, alitulia akijisomea. Mara aliingia Rama ambaye ni mwanachuo mwenzie, wanasoma darasa moja.
RAMA: Kwa raha zote umetulia bila wasiwasi, kaka hivi hujishtukii?
FRANK: Kujishtukia kwa lipi?
RAMA: We si ndiye umempa ugonjwa wa kichwa mwenzio, au ulimpa makusudi? (Rama aliongea akiwa anacheka)
FRANK: Ah! nikaushie, sio kila mtu lazma aende akamuone, wengine tutamuombea kwa Mungu atapona.
SEHEMU YA 04
RAMA: Dah! tena unajibu utafikiri wewe sio chanzo, haya bwana.
FRANK: We kama ulienda poa. Mimi Siwezi kwenda.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa, Frank hakwenda kabisa kumuona Loveness. Watu wengi hawakupendezwa na jambo hilo, walimlaumu wakimwambia kuwa ana roho m baya. M baya zaidi kila akiulizwa kwanini hakwenda alijibu kirahisi tu.
Kama kawaida Love baada ya kurudi hosteli alijitupa kitandani akiendelea kupona taratibu. Rafiki zake waliendelea kumtembelea, akitoka mmoja aliingia mwingine, wanaume kwa wan awake, pia wengi walimuuliza wakitaka kujua kama kes ho ataingia darasani, hata hivyo Love hakuwa na jibu kuhusu swali hilo.
SIKU ILIYOFUATA:
DARASANI: llikuwa ni siku nyingine tena, mida ya asubuhi wanachuo walikusanyika kwaajili ya kipindi oha uchumi. Darasa lilijaa kweli kweli, kila kona kulitapakaa utitiri wa watu. Walikaa katika makundi makundi wakijadili mambo mbalimbali.
Hata hivyo macho ya watu wengi yalikuwa yakiwatafuta vijana wawili ambao ni Frank na Love, vijana hao hawakuonekana ndani ya darasa.
ISSA: Naona pasua kichwa hafiki leo, au naye anaumwa?
MARIA: Achaga unafki na wewe. Mwalimu tu bado hajafika, muda bado.
ISSA: Muda bado kivipi wakati yeye kila siku huwa anakua mtu wa kwanza kuingia kwenye kipindi!! tena huwa anakaa siti za mbele.
(Wakiwa bado wanamjadili Frank hatimaye Frank aliingia. Huwa anapenda kukaa mbele lakini kwakuwa siti za mbele zilijaa alitulia akitafuta sehemu nyingine ya kukaa, nyuma ya darasa aliziona siti mbili zikiwa hazina watu, alijongea taratibu alienda kukaa kwenye siti moja. Hazikupita dakika nyingi mwalimu wa uchumi aliingia darasani.)
MWALIMU: Natumaini kila mtu ameingia, hivyo basi CR (kiongozi wa darasa) naomba ukafunge milango yote.
(CR alisimama kisha alienda kufunga milango. Alifunga mlango wa mbele kisha aliufuata mlango wa nyuma, yaani ile anataka kufunga tu; Loveness alizama ndani, watu wote macho kodoo, patamu hapo mwanawane!!. Baada ya Love kuingia CR alifunga mlango. Balaa lilikuwa kwenye siti za kukaa, Love alizungusha macho akijiuliza akakae wapi, kwa mbali aliona siti moja ikiwa haina mtu, taratibu alipiga hatua hadi kwenye siti iliyobaki, baada ya kuifikia aliganda, macho yalimtoka kama popo bawa vile, sura ilimshuka akihisi kichefuchefu, alitamani kutapika!
Hakutegemea kama angemuona mtu anayemchukia kupita maelezo. Alitulia akijiuliza ataanzaje kukaa karibu na mtu hasiyetaka kumuona? Yaani aanze tu akae na huo utopolo? Akae na huo utelembwe? Hakunaga kitu kama hicho. Alihisi kinyaa, alitamani ateme mate chini ila alipotezea, kwa makusudi alipitiliza kama sio yeye vile, aliamua kwenda kujibana na marafiki zake. Kitendo hicho kilizua gumzo na minong'ono ya chini chini, bifu ndo kwanza limechanua! Atakufa mtu mwaka huu! Minong'ono ilizua kelele, ilibidi ticha aingilie kati)
SEHEMU YA 05
MWALIMU: Darasa naomba utulivu.
(Wanachuo walitulia, mwalimu aliendelea)
MWALIMU: Nafikiri hakuna hasiyejua kushuka kwa uchumi wa nchi. Uchumi wa nchi unategemea sana biashara mbalimbali za wananchi wa nchi husika.
Mfano kupitia kodi na tozo mbalimbali. Kama wananchi wasipofanya biashara na kuichangia nchi yao kupitia kodi hivyo basi ni lazima uchumi utashuka tu. Lakini pia biashara hizi za wananchi zina changamoto nyingi, changamoto hizo ndizo zinazofanya watu kukwepa kodi. Sasa kila mtu aandae karatasi moja kisha aniandikie ni changamoto zipi zinazowakabili wafanyabiashara hadi washindwe kulipa kodi? Natoa dakika 10 tu kwa zoezi hili. Hakikisha unaandika jina lako na namba ya usajili.
(Baada ya maelezo ya mwalimu wanachuo waliandaa karatasi kisha walijibu swali. Kila mtu alikuwa bize akiandika majibu ya ke, wengine walishuka tu, baadhi walitazama juu wakihesabu kenchi, hatimaye dakika 10 zilikwisha.)
MWALIMU: Natoa dakika 2 za kukusanya, kunja karatasi yako alafu mpe wa mbele yako nae ampe wa mbele yake hadi zifike kwangu.
(Karatasi zilikusanywa kisha ziliwekwa kwenye boksi. Mwalimu alishika box kisha alitangaza tena kama ifuatavyo)
MWALIMU: Sasa nitapita na hili box, kila mtu ataingiza mkono kisha atachukua karatasi moja alafu baadae atapita mbele atatusomea majibu ya kwenye karatasi ambayo ataichukua.
(Zoezi lilifanyika kwa haraka, wanachuo walizamisha mikono kwenye box kisha walichukua karatasi moja moja. Mwalimu aliendelea kutoa maelekezo
MWALIMU: Kila mtu afungue karatasi yake kisha atazame ili ajue amechukua karatasi ya nani. (Frank alifungua haraka haraka, alitazama jina la mwenzie alikuta amechukua karatasi ya LOVENESS JOHN. Jamaa alipagawa, alijiuliza abadili karatasi au afanyaje?)
"Dah hili balaa, naona kama nimechukua bomu...sasa sijui nifanyaje, na mwalimu alisema akimuona mtu anabadili karatasi atapata tabu sana!! Duh! ila itafahamika mbele kwa mbele" Frank aliteseka kwa mawazo, macho yake bado yaliganda yakitazama jina la Love.
(Wanachuo waliendelea kukagua makaratasi yao, Maria alitazama alikuta kachukua karatasi ya mtu hasiyemjua, hata Issa alikuta kachukua karatasi ya mtu hasiyemtambua. Love kabla hajafungua alichungulia karatasi za marafiki zake kisha alifungua karatasi yake kwa madoido na mbwebwe zote, alitabasam akiona raha kufungua karatasi yake, tena aliringa akiwaziba wenzie wasione. Mara ghafla tabasam lote lilikwisha, manjonjo yote yalipotea, sura ilipauka kisha ilisinyaa ilitengeneza mikunjo na minuno, alikasirika kweli kweli, alichukia kuona ameshika karatasi ya FRANK KAKOLANYA. Hapo ndo penyewe sasaa!