Kumbe kiswahili ni Kiarabu kitupu!

article

Senior Member
Sep 10, 2016
174
326
Katika harakati zangu za kujiongezea ufahamu wa lugha ngeni niliamua kuanza kujifunza lugha ya Kiarabu kwa miezi kadhaa sasa.

Jambo ambalo limenishangaza ni kukutana na maneno mengi ya kiarabu ambayo yana maana sawa na maneno ya kishwahili ila mengine yana utofauti kidogo kwenye uhandishi kwa mfano saba=sab'a, bakia=baqiya, shaka= shakka, sababu=sabbaba, hamsini=khamsuun, sitini=sittuun, mia = mi'a, elfu = alf kwa kutaja machache.

Wataalamu wa lugha ya kiswahili naomba mnipe uhusiano kati ya lugha hizi mbili kwa kifupi, historia zao na chochote muhimu kwenye lugha hizi mbili zinazohusiana kwa karibu sana kwa jinsi nilivyoona kwa kutumia elimu yangu ya msingi kwenye hizi lugha.

Ahsante sana,

Article.
 
Ni kweli kabisa Kiswahili kina msamiati wa kiarabu ambao unakadiriwa kuwa ni asimilia 30 ya msamiati wote wa Kiswahili.. Ambapo kibantu ni asilimia 60 na lugha nyingine Kama kijerumani, kireno, kiyunani,kingereza na lugha nyingine zikichukua asilimia kumi ya msamiati wote wa Kiswahili..
Mwingiliano wa kibiashra kati Ya waarabu na watu wa pwani.. Ndiyo iliyosababisha kuingia kwa msamiati wa kiarabu katka lugha ya Kiswahili..
Ambayo kiujumla ni tabia ya Lugha kuathiri au kuathiriwa inapotokea kwa lugha mbili zenye Utamuduni tofauti kuingiliana....
 
Shule Ulienda kusoma nini kama hujui hata historia ya lugha yako?

Kukopa maneno ni tabia ya kawaida ya lugha yeyote ile ila hiyo haimaanishi kiswahili ni kiarabu. Kwa kuhakikisha hilo sikiliza habari ya kiarabu uone kama utaelewa kama hujui kiarabu au mwambie muarabu asikilize kiswahili uone kama ataelewa, msipende kulazimisha mambo na unasaba na waarabu. Kiswahili ni kibantu
 
Yaaap upo uhusiano lakini usiludie kusema ni kiarabu kitupu kwani ni asilimia chache tuu ya misamiati ndo huunda lugha inakadiliwa kuwa na asilimia 30 ya maneno yaliyomo kwenye lugha ya kiswahil yanaasili ya kiarabu kwa mfano vitenzi vyote vya lugha ya kiswahil huishia na a kwenye umoja na ni kwenye wingi tofauti na vitenzi vya kiarabu
 
Shule Ulienda kusoma nini kama hujui hata historia ya lugha yako?

Kukopa maneno ni tabia ya kawaida ya lugha yeyote ile ila hiyo haimaanishi kiswahili ni kiarabu. Kwa kuhakikisha hilo sikiliza habari ya kiarabu uone kama utaelewa kama hujui kiarabu au mwambie muarabu asikilize kiswahili uone kama ataelewa, msipende kulazimisha mambo na unasaba na waarabu. Kiswahili ni kibantu
Huyu kasharukia ktk udini tayari...

Ukweli ni kwamba 35% ya misamiati ya kiswahili imetoka ktk lugha ya kiarabu,sasa ukitoka huko umekurupuka useme eti mwarabu aongee hlf tuone msaahil atamuelewa unaonyesha jinsi gani ulivyo na uelewa mdogo hata kutojua maana ya msamiati.

(Swahili translated from arabic word Saahil)
 
Huyu kasharukia ktk udini tayari...

Ukweli ni kwamba 35% ya misamiati ya kiswahili imetoka ktk lugha ya kiarabu,sasa ukitoka huko umekurupuka useme eti mwarabu aongee hlf tuone msaahil atamuelewa unaonyesha jinsi gani ulivyo na uelewa mdogo hata kutojua maana ya msamiati.

(Swahili translated from arabic word Saahil)

Kwahiyo 35% inafanya kiswahili kuwa kiarabu kamili? Hisabati hujui wala hesabu. Huoni kwamba hata katika utohoaji tulifanyia marekebisho ili kiwe kiswahili hivyo kutofautisha na kiarabu? Shule ulienda kusomea ujinga!
 
Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye msamiati mkubwa kutoka Kiarabu. Sarufi na muundo wake ni karibu yote Kibantu. Lakini kuna zile asimilia 30-40 kutoka Kiarabu. Hapo inafanana sana na Kiingereza ambayo ni lugha ya Kigermanik iliyopokea msamiati wa 40-45% kutoka Kifaransa/Kilatini. Au Kiajemi ambacho ni lugha ya Kihindi-Ulaya iliyopokea karibu nusu ya msamiati kutoka Kiarabu.

Nadhani ni sawa na ng'ombe: chotara kiasi si kosa, inaongeza nguvu!
 
Historia uliyofichwa kusomeshwa na badala yake kujazwa ujinga ni kuwa Waarabu walikuja Afrika.

Ukweli ni kwamba Waarabu Afrika ni kwao na lugha ya Kiarabu ndiyo lugha kuu ya kwanza Afrika licha ya lugha zingine kama Kiswahili kutokana na Kiarabu kwa asili na fasili.

Wabantu Afrika ya Mashariki ni wakuja tu na walipohamia walikuta wenyeji wapo tayari, na hususan walikuta pwani yote ya Afrika Mashariki kuna wastaarabu.

Jee hao wenyeji wa pwani ya Afrika Mashariki wastaarabu ni akina nani? Na walizungumza lugha gani?

Nnauhakika kwa historia ya kujazwa ujinga maswali hayo mawili hautakuwa na majibu na utaanza kutokwa povu.

Usifadhaike kwa huo ukweli wala usighadhibike.

Kama utapenda kujuwa pitia uzi wa Faidika na darsa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa ili upate majibu.
 
Mkuu, umesoma mpaka level gani? Maana hilo linafundishwa katika historia na hata kiswahili chenyewe. Kiswahili ni zao la mahusiano ya kibiashara baina ya Waarabu waliokuwa wakija katika pwani ya bahari ya Afrika mashariki na makabila ya kibantu. Katika kutafuta maelewano na kujichanganya, ikatokea lugha iliyounganisha maneno kutoka pande zote mbili pamoja na nyongeza ya maneno ya Kiingereza, Kireno na Kijerumani.
Upo?
 
Maneno mengi nafikiri tumeyapata kutoka katika Kiarabu. Hivi karibuni niliwasiliana na ndugu anaishi huko na kumueleza kuwa cancer kwa Kiswahili ni saratani, akasema na wao wanatumia neno hilo hilo.
 
Baada ya miaka 100 asilimia 70 ya maneno ya kiswahili yatakuwa na asili ya Kiarabu.
1.Wataalamu wa kiswahili wengi wanapendelea kiarabu ndiyo sababu wanaondoa maneno yenye asili ya kiingereza na kupachika ya kiarabu.Mfano: kompyuta,kalkuleta,televisheni nk.
 
Katika harakati zangu za kujiongezea ufahamu wa lugha ngeni niliamua kuanza kujifunza lugha ya kiarabu kwa miezi kadhaa sasa.

Jambo ambalo limenishangaza ni kukutana na maneno mengi ya kiarabu ambayo yana maana sawa na maneno ya kishwahili ila mengine yana utofauti kidogo kwenye uhandishi kwa mfano saba=sab'a,bakia=baqiya,shaka= shakka,sababu=sabbaba ,hamsini=khamsuun,sitini=sittuun,mia = mi'a, elfu = alf kwa kutaja machache.

Wataalamu wa lugha ya kiswahili naomba mnipe uhusiano kati ya lugha hizi mbili kwa kifupi ,historia zao na chochote muhimu kwenye lugha hizi mbili zinazohusiana kwa karibu sana kwa jinsi nilivyoona kwa kutumia elimu yangu ya msingi kwenye hizi lugha.

Ahsante sana,

Article.
Kaka in makosa kusema kiswahili no kiarabu.Sahihi no useme lugha ya kiswahili ina msamiati mwingi wenye asili ya kiarabu.
 
Yaaap upo uhusiano lakini usiludie kusema ni kiarabu kitupu kwani ni asilimia chache tuu ya misamiati ndo huunda lugha inakadiliwa kuwa na asilimia 30 ya maneno yaliyomo kwenye lugha ya kiswahil yanaasili ya kiarabu kwa mfano vitenzi vyote vya lugha ya kiswahil huishia na a kwenye umoja na ni kwenye wingi tofauti na vitenzi vya kiarabu
To a mifano kurrthibitisha kauli yako.
 
Back
Top Bottom