SoC02 Kiswahili kwa maendeleo ya Mtanzania

Stories of Change - 2022 Competition

GMbise1991

New Member
Aug 28, 2022
1
0
KISWAHILI NA MAENDELEO YA MTANZANIA

Kiswahili ni lugha ya Taifa letu pendwa Tanzania, lugha hii inazungumzwa maeneo mengi ulimwenguni lakini chimbuko lake likiwa ni wabantu wanaopatikana maeneo ya Afrika ya mashariki hususani Tanzania.

Ushahidi wa kihisimu(sayansi ya lugha) unathibitisha asili ya kiswahili kuwa ni kibantu Kwa kutumia vigezo vikuu vinne ambavyo ni
I. Msamiati wa msingi​
II. Nomino​
III. Vitenzi​
IV. Muundo wa sentensi​

Kwa Watanzania wengi hii imekuwa Lugha yao ya pili baada ya Lugha za makabila (Lugha Mama) na wengine kiswahili ni Lugha yao yakwanza hasa watoto wazaliwao maeneo ya mijini

Kwa Watanzania waliobahatika kwenda shule, kiswahili kimekua Lugha ya kufundishia masomo yote kuanzia ngazi ya awali Hadi darasa la Saba, isipokuwa Kwa shule za michepuo ya kiingereza (English Medium) na kwa upande wa Sekondari na vyuo vikuu kiswahili kinafundishwa kama somo

Lugha Hii yenye asili yake hapa kwetu Tanzania tumeshindwa kuitumia katika kujikwamua kiuchumi kwani tuna idadi kubwa ya vijana wengi walioko mtaani ambao ni wamilisi na mahiri wa lugha hii wakiwa na stashahada, shahada, na hata shahada ya uzamili katika kiswahili lakini wengi wako mtaani Bila kazi yoyote ya kufanya mbali na ukweli kuwa lugha Hii inakuwa Kwa Kasi sana Afrika na ulimwenguni Kwa ujumla

Tumeliona hili kwani tumeshuhudia kiswahili kikitumika katika baadhi ya mikutano ya Kimataifa, Kiswahili ni Lugha rasmi ya Umoja wa Africa (AU).

Pia rejelea mkutano wa 39 wa SADC uliofanyika August 2019 Kiswahili kilitangazwa Kuwa lugha rasmi ya nne ya umoja huo Na mwenyekiti aliyekuwa anamaliza muda wake Dr. Hage Geingob Ambaye ni rais wa Namibia, katika mikutano ya SADC Tumeshuhudia kiswahili kikitumika na wakuu mbalimbali wa nchi wanachama, mbali na SADC pia Kiswahili ni Lugha rasmi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Pia ni lugha rasmi Kwa benki ya maendeleo ya Africa (AfDB)

Pia katika kazi mbali mbali za wasanii wa ndani na nje ya Tanzania wamekuwa na utamaduni wa kuchanganya maneno ya kiswahili katika Kazi zao mfano nyimbo, tazama baadhi ya wasanii kama vile Yemi Alade kutoka Nigeria na wimbo wake uitwao-Na Gode,, Meddy ambaye ni mnyarwanda anayeishi nchini Marekani kwenye wimbo wake wa MY VOW amechanganya maneno mengi ya kiswahili, Kundi la Sauti Sol kutoka kenya na wengine wengi ambao siyo watanzania Lakini wameimba Kwa kutumia lugha ya kiswahili

Pia sanaa ya Filamu na maonyesho kiswahili bado hakijabaki nyuma katika kutanabaisha ubora wake kimatumizi tazama mfano wa tamthiliya ya SHE IS MY SISTER iliyoigizwa na marehemu Steven Kanumba na kuwashirikisha wasanii kutoka Nigeria kama akina Mercy Johnson na wengineo, katika Tamthiliya hii lugha ya kiswahili imetumika Kwa kiasi kikubwa sana, hii inaonyesha ni Kwa kiasi gani lugha hii inakua na kupendwa na watu.

Ninaandika makala Hii fupi Kwenda kwa Serikali na Baraza la kiswahili la Taifa (BAKITA) na wadau wote wa kiswahili wanaohusika wafanyie kazi jambo hili Ili kiswahili kiwe mwarobaini wa kukosekana Kwa ajira Kwa vijana wengi wa kitanzania waliobobea katika kiswahili

Serikali Kwa kushirikiana na BAKITA na wadau wote wa kiswahili wanaohusika wachukue jukumu la kutengeneza fursa za kufundisha kiswahili nje ya Tanzania Kwa nchi zote duniani zinazohitaji kujifunza lugha Hii, BAKITA watengeneze fursa hizi Kwa kwenda katika vyuo mbalimbali nje ya Tanzania Kwa kuanza na mataifa yote ya Africa kwakua kiswahili kimepata upendeleo wa kuwa miongoni mwa Lugha rasmi katika Umoja wa Afrika (AU) Basi ni dhahiri mataifa mengi yana uhitaji wa wataalamu

Pia katika yale mataifa makubwa ya Ulaya na Marekani ambayo wanahitaji huduma Hii ya kujifunza kiswahili BAKITA waingie nao ubia wa kuwapelekea wataalamu wa kufundisha kiswahili katika vyuo vyao, ikiwa BAKITA watalifanyia kazi hili sisi kama Taifa tutapanua wigo wa kiutambulisho lakini zaidi sana vijana wa Kitanzania walio wengi mtaani wataondokana na tatizo la ukosefu wa ajira na watajipatia kipato, pia sisi kama Taifa tutaongeza mapato ya nchi yetu ikiwa vijana Hawa watapata fursa hizi nje ya Tanzania kupitia Kodi na Tozo mbalimbali

BAKITA pia watajipatia kipato kutokana na ukweli kwamba wataandaa KAMUSI mbalimbali Kwa lugha ya kiswahili wakishirikiana na taasisi nyingine za ukuzaji wa kiswahili kama vile TUKI n.k, KAMUSI hizi zitauzwa katika mataifa hayo ambayo wataalamu wetu wataenda kufundisha, Mbali na KAMUSI pia wajifunzaji watahitaji vitabu mbalimbali vya kiswahili kwaajili kujifunzia

BAKITA wasiwatumie wanyonge kujipatia kipato badala yake wawatengenezee fursa wanyonge hao baadae watajipatia mapato Zaidi, Kwanini nimesema jambo hili? Kumekuwepo na programu ya kuwaandaa vijana waliosoma kiswahili Ili kuwafundisha wageni na mafunzo haya yanalipiwa, mfano kwa mkoa wa Arusha wanafunzi waliodhuria semina hii ya wiki Mbili walilipia kiasi Cha shilingi laki Moja na zaidi za Kitanzania Lakini wako tu mtaani hakuna fursa yoyote Ile iliyotengenezwa kutoka BAKITA (kama ipo Sina Data Kwani wanasemina wengi baada ya kumaliza wamerudi na vyeti vyao mtaani)

Inawezekana kufikiri kuwa ni jukumu la vijana Hawa niliowasemea mmoja mmoja kuzitafuta fursa hizi Kwa binafsi yao lakini wengi wao hawajui waanzie wapi katika kulifanya hili, umasikini na mazingira magumu ya watanzania walio wengi ni miongoni mwa vikwazo katika hili.

Mzigo huu nimewatwika BAKITA Kwakua ndiyo Taasisi Mama ya kiswahili nchini, na ni matumaini yangu kuwa Kwa andiko hili watafanya jambo Kwa maendeleo mapana ya Taifa letu.

Mwl Gerald Mbise.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom