Kulikuwa na Sababu ya Watoto wa Kikwete kuhudhuria sherehe za kuapishwa Mawaziri?

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Marais toka awamu ya kwanza hadi ya Tatu hatuwaona watoto wao kwenye hizo sherehe za Mawaziri kuapishwa

Ni Miaka Miwili na Nusu imebaki wataichukua ikulu hapo 2015?

A4.jpg

Ridhiwan Kikwete akizungumza na aliyekuwa rais wa Yanga Jamal Malinzi wakati wa hafla hiyo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo.

A5.jpg

Miraji Kikwete akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo
 
Mh! Tusije fanya tena makosa 2015, huyu miraji si ndiyo alikuwa IT wa uchaguzi wa 2010 na inasemekana ali-master mind lile zoezi la wizi wa kura. Mimi ningekuwa mtoto nisingekuja hapo ikulu.
 
nawewe naye huna dogo!, ulitaka wakauzie wp sura? Kwao ndo kule,na jana brassband ndo hiyo kiwanja cha nyumbani, juice ya kumwaga, sasa ulitaka miraj na riz1 waje tupigane nao vkumbo uswaz? Kwa taarifu tu na mwana**** naye alikuwepo!
 
Kwa ufalme tulio nao sasa si kosa. Iwapo wanaweza kuwasukia watu dili hadi wakateuliwa uwaziri watashindwa uapishaji ambao ni matokeo ya dili zao? Nani mara hii kasahau tuhuma kuwa Lau Masha aliteuliwaje tokana na konnekisheni na RizOne? Wapo wanaokwenda mbali kudai eti wengine waliteuliwa kutokana na ukaribu na Bi Mkubwa rais wa WAMA. Ajabu wahusika hawakanushi tuhuma hizi. Waulize akina Mwanaidi Majaar waliulaje.
 
- Mkuu mleta mada kwani katiba ya Jamhuri inasemaje kuhusu Watoto wa The sitting President na Sherehe za Ikulu?

- Halafu pia uweke wazi Katiba hiyo hiyo inasema nini kuusu hao wananchi wengine wa kwaida waliohudhuria huko jana, infact na mimi nilikuwepo pia, I mean ndio njia pekee ya kukata mzizi wa fitina, otherwise isije ikawa wivu na chuki binafsi bila hoja za msingi! au?

William.
 
inabidi walio aapishwa wawajue kuwa wale ndiyo wadau wakubwa wa ikulu, ili watakapotaka michongo ya biashara wasijesema hawawajui
 
Mfalme asipowashirikisha warithi wake katika day to day activities za ufalme watajifunzaje kazi wanazotakiwa kurithi? Haya ni mafunzo kwa vitendo jamani!
 
2015 watasononeka sana. Hawaoni Mubarack na wanae? Hata hivyo ndiyo wadau na ndiyo wapanga timu zote za uwaziri au ubalozi na kila kitu cha big house.
 
Eee ee jamani, mwanadamu hatosheki, hata ukimpa nini, milele hataridhika...

Nyerere kawabana watoto wake mpaka leo kina Ganesh wamechanganyikiwa na maisha, tumemsema sana Nyerere. Mzee wa watu wanawe alikuwa hata haonani nao mpaka hela za madaftari wanapewa na Butiku. Tumemsema Nyerere mnoko.

Kikwete katokea rais social, anawapa good time watoto, naye tunamsema.

Tunataka nini hasa?
 
- Mkuu mleta mada kwani katiba ya Jamhuri inasemaje kuhusu Watoto wa The sitting President na Sherehe za Ikulu?

- Halafu pia uweke wazi Katiba hiyo hiyo inasema nini kuusu hao wananchi wengine wa kwaida waliohudhuria huko jana, infact na mimi nilikuwepo pia, I mean ndio njia pekee ya kukata mzizi wa fitina, otherwise isije ikawa wivu na chuki binafsi bila hoja za msingi! au?

William.

-Tunaongelea Facts wewe ni mtoto wa Mkubwa na Unamjua Makongoro Nyerere Wakati J.K. Nyerere alipokuwa anawaapisha Mawaziri Baba yako akiwa Mmoja wao sidhani ilikuwa faragha pia ya watoto kuvaranda Ikulu bila sababu yoyote ile na kuongea na Wageni Wakuu Waalikwa.

Ni Sherehe Ngapi Umehudhuria za Mawaziri kuapishwa?

- Katiba sio pana kiasi cha kusema kuhusu wageni watakao hudhuria kuapishwa kwa Mawaziri, Hakuna Fitina ni kuwa logistically kuna umaana gani ya hao watoto kwenda?

- Kuhudhuria kwako sio kubaya ni vizuri na ni njia ya kujionyesha ili mbeleni ufanikiwe kugombea Ubunge, kwahiyo kuwepo kwako kulikuwa sio bila maana yoyote, ilikuwa baadaye itakulinda na kukujengea chakula kwa kuupata Ubunge au Ujumbe wa NEC.

Tunampenda Rais wa nchi yetu, kwanini tuwe na chuki na amebakiza Miaka Miwili na Nusu kutawala nchi?
 
Mimi naona haina tabu kwani ndio wakati wao kwani si muda mrefu watakuwa hawna access tena na hilo jumba waaaacheni jamani
 
Watakuwa walikuja home kwao mara moja, they ar too old kujifungia jamani. Wakianza kumsindikiza baba yao kwenye misiba ya kitaifa kama ule wa Kanumba, basi hapo ndo mseme.
 
- Mkuu mleta mada kwani katiba ya Jamhuri inasemaje kuhusu Watoto wa The sitting President na Sherehe za Ikulu?

- Halafu pia uweke wazi Katiba hiyo hiyo inasema nini kuusu hao wananchi wengine wa kwaida waliohudhuria huko jana, infact na mimi nilikuwepo pia, I mean ndio njia pekee ya kukata mzizi wa fitina, otherwise isije ikawa wivu na chuki binafsi bila hoja za msingi! au?

William.

W. J. Malecela, naamini kuwepo kwao kusingeleta gumzo kama hayo mengine yaliyo nyuma ya pazia yasingekuwepo. Mengi yamezungumzwa kuhusu Riz1 na Miraji. Kwa kifupi kuwapo kwao ni news!
 
Back
Top Bottom