Kuku wa kuoka

Hahaha, karibu muke ya Asprin. Usisahau limbwata.
Hiyo ya hoho mwaniwani sijajaribu manake.nawanza ntajaza hoho ngapi? Usisahau ukinunua hoho uchanganue rangi itapendeza za njano, nyekundu na kijani. Lakini kuna stuffing inauzwa kwa packet supermarket japo huwa naona ina funny artificial taste ndo maana naweka crumbs.
King'asti asante kwa pishi la bata, labda nikipata mgeni mla bata nitamwandalia, mie bata noooooo....

Ila ya kujaza wali nimeipenda, ipo siku nitajaribu kwenye kuku.... Ila kwanza nitaanza na kujaza wali kwenye hoho.... Nikifuzu nitahamia kwenye kuku....
 
Last edited by a moderator:
Lol. Bata mie najua wa kuoka tu na anakuwa stuffed japo mie sipendi kula.
Unampaka bata mzima mafuta na viungo vyote kama chumvi, swaumu, binzari, tangawizi na ndimu. Unaweza kumlaza kwenue friji ama akae masaa kadhaa akikolea viungo.
Stuffing ni kumjaza tumboni, unaweza kuweka wali (njia bomba ya kula kiporo kwa furaha zote,lol) uliochanganywa na viazi, njegere, vitunguu na bread crumbs.
Oka kwa lisaa limoja ama endelea kuangalia abadilike rangi. Muhimu uchanje kuangalia kama bado ana damu manake.kama bata ana umri sawa na wewe ni kasheshe.

bata wa kubanika ni bomba sana .... samosa na ndizi za kubanika .... ukipata ndizi aina ya Jamaica au myenyele
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom