Kuku wa kuoka

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,772
23,162
MAHITAJI

kuku 1 mkate vipande upendavyo
swaumu(thomu)
tangawizi
vinegar
pilipili ( napendelea black papper grounded)
vijiko viwili vya curry powder (simba mbili is the best)

MAANDALIZI
- osha kuku wako kwa kutumia vinegar (hii hukata shombo ya `kuku kwa sie tusiopenda harufu), mwaga maji uliyooshea
- mkate upendavyo, mtie tena vinegar kadri uonavyo inafaa
- mweke vitunguu swaumu vilivyopondwa na tangawizi
-tia pilipili yako na curry powder
-mweke chumvi

acha kwa muda wa saa moja
washa oven ipate moto

-paka baking tin yako mafuta
-weka kuku wapo nyunyuzia mafuta kiduuuuuuuuuchu
-weka kuku wako, pika mpaka aiveeeeeee

ipua unaweza kula na vizazi, viepe, ugali chapati ......usisahau salad/kachumbari na juicy pembeni

kulaaaaaaa mpaka kitambi kitokeeeee
 
Kuku wa kuoka haleti kitambi kama wa kukaanga. Sasa hivi nimeingia msituni, ni kuoka mwanzo mwisho. Nimeambiwa kuna hadi maandazi ya kuoka, hebu nitonyemo kama unajua.

Combinenga recipe hii hapa kwa mabachela: humo kwenye baking tray ya kuku unawekelezea viazi vitamu ama mbatata vilivyokatwa size mara mbili ya chipsi.
Dakika 10 kabla ya kuiva kuku na viazi, weka carrots, brocolli, koliflower, hoho na vitunguu vilivyokatwa vikubwa kiasi na endelea kuoka. Ukitoka hapo una full meal, kachumbari na juice mambo shega.
 
Maandazi ya kuoka yapo ya aina nyingi ila mbili kati ya hayo ni

1. Ya kukatwa na kuchomwa kwenye tray (kama ulivyooka kuku)

2. Ya sufuria aka mahamri

Kwa yaliyokatwa, ponda unga wako maandazi kama unga wa maandazi ya kukaanga kwa mafuta (tafadhali tumia yeast badala ya baking powder, na fanya Unga uwe mwepesi zaidi ya maandazi ya kukaanga)

Kata katika size upendazo, funika kitambaa katika sehemu yenye joto, hadi yaumuke (unayaona yanakuwa mepesi, na ukiyabonyeza hayarudi)

Panga kwenye tray yako iliyopakwa mafuta, choma kwenye pre-heated oven (200C) hadi yatakapogeuka rangi ya kahawia.

Toa jikoni, yapake maandazi yako mafuta while hot (chovya brush yako kwenye mafuta kidogo kisha pakaa maandazi-itasaidia kuyafanya yasikakamae)

Yakipoa, tayari kwa kula

Note: unaweza kufanya ya chumvi pia badala yake ukipenda
 
Asante sana mwalimu Gaijin
sasa yanapikwa kama scones? Na kuumua ni mara moja,manake scones huwa naumua mara mbili. Baada ya kukanda naacha unga uumuke kwanza to twice the volume, nakanda na kukata na kupanga na kuacha ziumuke mara ya pili ndo nioke.
 
Last edited by a moderator:

Unaumua mara moja tu.

Ukishakukanda unga, kata, tandika sehemu yako vizuri, panga, yafunike mpaka yaumuke, choma jikoni.

*Hapa labda nikuulize, maandazi ya kuchoma kwa mafuta kawaida kwani unafanyaje?
 
Hayo huwa nayaumua mara moja na nachanganya yeast na baking powder. Nikishakanda nakata immediately, yakiumuka ndo nachoma.

Mkate ndo naumua kwanza, nakata uumuke mara ya pili ndo nichome.
Unaumua mara moja tu.

Ukishakukanda unga, kata, tandika sehemu yako vizuri, panga, yafunike mpaka yaumuke, choma jikoni.

*Hapa labda nikuulize, maandazi ya kuchoma kwa mafuta kawaida kwani unafanyaje?
 
Hayo huwa nayaumua mara moja na nachanganya yeast na baking powder. Nikishakanda nakata immediately, yakiumuka ndo nachoma.

Mkate ndo naumua kwanza, nakata uumuke mara ya pili ndo nikate.

Vitumbua navyo twaweza kuviita ubwabwa mdogo?
 
safi sana, msosi wa uhakika...

maandazi ya kuoka siyajui mie, hebu tiririka,

tena hayo ndo mazuri unaepukana na mifuta ya maandazi

Kuku wa kuoka haleti kitambi kama wa kukaanga. Sasa hivi nimeingia msituni, ni kuoka mwanzo mwisho. Nimeambiwa kuna hadi maandazi ya kuoka, hebu nitonyemo kama unajua.

Combinenga recipe hii hapa kwa mabachela: humo kwenye baking tray ya kuku unawekelezea viazi vitamu ama mbatata vilivyokatwa size mara mbili ya chipsi.
Dakika 10 kabla ya kuiva kuku na viazi, weka carrots, brocolli, koliflower, hoho na vitunguu vilivyokatwa vikubwa kiasi na endelea kuoka. Ukitoka hapo una full meal, kachumbari na juice mambo shega.
 
Maandazi ya kuoka yapo ya aina nyingi ila mbili kati ya hayo ni

1. Ya kukatwa na kuchomwa kwenye tray (kama ulivyooka kuku)

2. Ya sufuria aka mahamri

Kwa yaliyokatwa, ponda unga wako maandazi kama unga wa maandazi ya kukaanga kwa mafuta (tafadhali tumia yeast badala ya baking powder, na fanya Unga uwe mwepesi zaidi ya maandazi ya kukaanga)

Kata katika size upendazo, funika kitambaa katika sehemu yenye joto, hadi yaumuke (unayaona yanakuwa mepesi, na ukiyabonyeza hayarudi)

Panga kwenye tray yako iliyopakwa mafuta, choma kwenye pre-heated oven (200C) hadi yatakapogeuka rangi ya kahawia.

Toa jikoni, yapake maandazi yako mafuta while hot (chovya brush yako kwenye mafuta kidogo kisha pakaa maandazi-itasaidia kuyafanya yasikakamae)

Yakipoa, tayari kwa kula

Note: unaweza kufanya ya chumvi pia badala yake ukipenda

nice one mkuu nimeipenda hiyo na kuhusu mafuta unatumia yalioganda yaani tanbond au ya kawaida kama alizeti?
 
Hayo huwa nayaumua mara moja na nachanganya yeast na baking powder. Nikishakanda nakata immediately, yakiumuka ndo nachoma.

Mkate ndo naumua kwanza, nakata uumuke mara ya pili ndo nikate.

Unafanya kama ya hayo maandazi ya kuchoma tu, kuumua mara moja, sema unga uwe mwepesi zaidi kidogo

*mimi siweki baking powder kwenye maandazi ya aina yoyote.
 
nice one mkuu nimeipenda hiyo na kuhusu mafuta unatumia yalioganda yaani tanbond au ya kawaida kama alizeti?

Mafuta yoyote ni sawa, chagua kwa urahisi wako tu.

Unatakiwa kupaka layer nyembamba ya mafuta ili maandazi yasikakamae, so haijalishi mafuta ya aina gani kwa vile hata mafuta yaliyoganda yatayeyuka yakipakwa kwenye maandazi ya moto
 
Lol. Bata mie najua wa kuoka tu na anakuwa stuffed japo mie sipendi kula.
Unampaka bata mzima mafuta na viungo vyote kama chumvi, swaumu, binzari, tangawizi na ndimu. Unaweza kumlaza kwenue friji ama akae masaa kadhaa akikolea viungo.
Stuffing ni kumjaza tumboni, unaweza kuweka wali (njia bomba ya kula kiporo kwa furaha zote,lol) uliochanganywa na viazi, njegere, vitunguu na bread crumbs.
Oka kwa lisaa limoja ama endelea kuangalia abadilike rangi. Muhimu uchanje kuangalia kama bado ana damu manake.kama bata ana umri sawa na wewe ni kasheshe.
bata na bata mzinga na jamii zao sijawahi kula wala kupika....labda king'asti atusaidie kama ana utaalam eneo hilo
 
Hapo kwenye maandalizi ya bata umesahau kumtahadharisha kuhusu kufunga mdomo wkt wa kumnyonyoa. Maana akisahau hilo aweza kuta akatumia siku nzima kunyonyoa mpaka hamu ya kula iishe
 
King'asti asante kwa pishi la bata, labda nikipata mgeni mla bata nitamwandalia, mie bata noooooo....

Ila ya kujaza wali nimeipenda, ipo siku nitajaribu kwenye kuku.... Ila kwanza nitaanza na kujaza wali kwenye hoho.... Nikifuzu nitahamia kwenye kuku....

Lol. Bata mie najua wa kuoka tu na anakuwa stuffed japo mie sipendi kula.
Unampaka bata mzima mafuta na viungo vyote kama chumvi, swaumu, binzari, tangawizi na ndimu. Unaweza kumlaza kwenue friji ama akae masaa kadhaa akikolea viungo.
Stuffing ni kumjaza tumboni, unaweza kuweka wali (njia bomba ya kula kiporo kwa furaha zote,lol) uliochanganywa na viazi, njegere, vitunguu na bread crumbs.
Oka kwa lisaa limoja ama endelea kuangalia abadilike rangi. Muhimu uchanje kuangalia kama bado ana damu manake.kama bata ana umri sawa na wewe ni kasheshe.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom