Kukataliwa kwa Mkapa Burundi: Je, ni mwisho wa "ushawishi" wa TZ katika Siasa za Afrika?

Benjamin Mkapa alikuwa nje ya nchi.Bila shaka alikuwa Burundi kwa ajili ya kusuruhisha ule mgogoro wa Nkurunzinza na wenzake.Bahati mbaya safari hii Warundi wamemgomea na amerudi mikono mitupu.Hivyo kutokuwepo kwake katika sherehe za kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru si kwa sabbu "alisusia" bali alikuwa anatekeleza majukumu ya Tanzania katika siasa za Afrika Mashariki na Nchi za Maziwa Makuu.

JK hakuwepo,naye alikuwa na safari nje ya nchi,msafara wake jana jioni ulitusimamisha wengi barabarani wakati akipita kurudi nyumbani.

Kutokuwepo kwao hakumaanishi lolote baya,zaidi ya wao kama marais wastaafu kutumikia jumuiya ya kimataifa kwa kutumia uzoefu wao wa uongozi katika kutatua mizozo na migogoro pamoja na kuhudumia Afrika ktk masuala mtambuka ya kidiplomasia.

Licha ya mapungufu yetu kama Taifa,licha ya kuwa na watu kama Jecha kule Znz na Lubuva huku Bara.Bado Tanzania nje ya mipaka ya nchi tuna heshima yetu.Hata baada ya nusu karne,ushawishi wetu ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere unavuka mlima Kilimanjaro na Ziwa Tanganyika,fukwe za Tanganyika na kando ya pili ya Ziwa Nyasa.Hii si kazi ya siku moja,ni juhudi za nusu karne,na walioipigania si wote wangali hai.

Ushawishi huu ulisimikwa na Julius;huyu hata baada ya kuondoka Ikulu aliogopeka ndani na nje ya nchi.Masaa kadhaa kwenye gereza la Kemwela-Kabwe Zambia,akiwa na sharubati ya chungwa (Orange juice)na biscuit,Nyerere alimfanya Kaunda kuacha kugoma kula na kunywa na kufungua "mfungo" wake alioufanya gerezani baada ya kuswekwa rumande na Chiluba.Wakati Nyerere akipanda ndege Lusaka kurudi Butiama,huku nyuma Chiluba alimfungulia Kaunda na kumtoa gerezani na kurudi nyumbani.Huu ni ushawishi unaovuka mipaka.Tuliaminiwa Burundi na Rwanda kuwaweka pamoja baada ya mauwaji ya kimbari.

Sasa tunakoelekea,tunaweza kuzalisha viongozi ambao hata "ushawishi" wao hauvuki kisiwa cha Chumbe ktk moja ya kina cha bahari ya Hindi, ushawishi usiovuka Ziwa Tanganyika kuelekea maziwa makuu.

Tutakosa watu wenye nguvu za ushawishi kuvuka Ziwa Nyasa na Pwani ya Afrika Mashariki.Nyakati hizo tulisimika Marais ktk nchi jirani na wakawa "vibaraka" wa Ikulu ya Dsm; kuanzia Ikulu ya Nakasere Uganda mpaka Bujumbura,Ututsi mpaka Moroni,eneo la Nampula mpaka Maputo ya Msumbiji.Tuliambaambaa kuanzia Lusaka mpaka Salisbury ya Zimbabwe na Windhoek.Wote hawa walikuwa "vijana" wetu tuliowakuza na kuwalea.

Leo kuna mtu kakataliwa huko Bujumbura;sababu anakosa "moral Authority" ya kukemea yale wanayotenda wengine sbb na yeye ana harufu ya yanayotendwa na yule anayelalamikiwa.Habari ya mtu anayeitwa Jecha inaweza kuwa na matokeo hasi ya muda mrefu katika ushawishi wetu wa siasa za kimataifa ndani na nje ya mipaka ya Afrika.

Unawezaje kumkemea Museveni kwa matendo yake kwa Kiiza Besigye wakati na wewe unayabariki kama hayo kwa wapinzani ndani ya nchi yako?Utamuwekaje meza moja Nkurunzinza na wapinzani wake wakati kwako hao wapinzani unaonekana kwenye youtube ukiwaita "mal.ofa na uchwara".

Huwezi kuwa na sauti kama ktk nchi yako wapinzani wa Serikali wananyimwa nafasi ya mikutano ya kisiasa na uhuru wa kutoa habari unadhibitiwa kwa sheria zilizotungwa na bunge (A law which is not just,is a useless law) na wewe umekaa kimya.

Wakati wa msiba wa Mama Mzazi wa Nyerere,upinzani wa Tanzania ulikuwa mikononi mwa Augustine Mrema na NCCR-Mageuzi,siku ya msiba ule pale Butiama na Mrema alifika,katika watu wa kuweka mashada ya mauwa,watu wa protokoli walimkacha Mrema wakidhani watamfurahisha Mwalimu,kwa ajabu Mwalimu alichukua shada moja na kumpelekea Mrema ili kuweka katika kaburi la Mama yake.Wale wote waliomkacha Mrema wakapatwa na aibu kubwa.

Wakati wa kupeana pole,Mrema alifika alipokaa Mwalimu na kumshika mkono wa pole,na baadae akahamia kwa aliyekuwa Makamu wa Rais marehemu Dr Alli Juma,na wakati wakiongea hili na lile,marehemu Dr Alli akajisemesha;"Huyu Augustino alikuwa rafiki yangu sana wakati akiwa serikalini",na Mwalimu akamuuliza Dr Alli;kwani sasa imekuwaje?Dr akajibu "Aa toka aende upinzani sina hamu nae tena"...Basi Mwalimu akamwambi "Aaa basi huyo hakuwa rafiki yako;angekuwa rafiki hata leo ungeendelea kumuona ni rafiki tu"

Katazo la Bujumbura si ishara njema kwa sisi kama Taifa;hata kama laweza kuwa katazo la "muda" tu,lakini ni taa ya tahadhari kuwa sasa ule "ushawishi" tuliokuwa nao enzi za Mwalimu na baada ya Mwalimu unaweza kuwa ktk eneo la mwisho wa enzi...Ni wapi tulipotereza??
Du! Hiyo story ya Mrema na Nyerere imenisisimua mno!
 
Nakumbuka kifo cha mondurane wa msumbiji,
Ndio ujue wakatimwingine usuluklhishi uahitaji ubabe lakini unahakikisha muhusika hajui kama unafanya ubabe,maana kuna migogoro mingine kwa kukaa mezani tu,hamuwezi kupata muafaka,lazima mmoja anaesumbua saana afanyiwe kitu yeye mwenye bila ya kujua,lakin ukianza kuwatukana maanayake unataka waendelee kuumizana.
 
Ni mwisho wa ushawishi wa Mkapa mwenyewe. Tanzania ina wanadiplomasia mahiri kama Salim Ahmed Salim na Augustino Mahiga na wengine wengi bado watatusaidia. Mkapa na ubabe ubabe wake hakuwahi kuwa msuluhishi mzuri wanamlazimisha kipaji ambacho hana. Yule mzee wa mihasira ni sawa huyu tuliyenaye sasa hawawezi kuwa wasuluhishi
Pia tuna mzee wa kung'ata na kupuliza JK anaweza kusuluhisha vizuri tu
Hana hekima
 
Benjamin Mkapa alikuwa nje ya nchi.Bila shaka alikuwa Burundi kwa ajili ya kusuruhisha ule mgogoro wa Nkurunzinza na wenzake.Bahati mbaya safari hii Warundi wamemgomea na amerudi mikono mitupu.Hivyo kutokuwepo kwake katika sherehe za kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru si kwa sabbu "alisusia" bali alikuwa anatekeleza majukumu ya Tanzania katika siasa za Afrika Mashariki na Nchi za Maziwa Makuu.

JK hakuwepo,naye alikuwa na safari nje ya nchi,msafara wake jana jioni ulitusimamisha wengi barabarani wakati akipita kurudi nyumbani.

Kutokuwepo kwao hakumaanishi lolote baya,zaidi ya wao kama marais wastaafu kutumikia jumuiya ya kimataifa kwa kutumia uzoefu wao wa uongozi katika kutatua mizozo na migogoro pamoja na kuhudumia Afrika ktk masuala mtambuka ya kidiplomasia.

Licha ya mapungufu yetu kama Taifa,licha ya kuwa na watu kama Jecha kule Znz na Lubuva huku Bara.Bado Tanzania nje ya mipaka ya nchi tuna heshima yetu.Hata baada ya nusu karne,ushawishi wetu ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere unavuka mlima Kilimanjaro na Ziwa Tanganyika,fukwe za Tanganyika na kando ya pili ya Ziwa Nyasa.Hii si kazi ya siku moja,ni juhudi za nusu karne,na walioipigania si wote wangali hai.

Ushawishi huu ulisimikwa na Julius;huyu hata baada ya kuondoka Ikulu aliogopeka ndani na nje ya nchi.Masaa kadhaa kwenye gereza la Kemwela-Kabwe Zambia,akiwa na sharubati ya chungwa (Orange juice)na biscuit,Nyerere alimfanya Kaunda kuacha kugoma kula na kunywa na kufungua "mfungo" wake alioufanya gerezani baada ya kuswekwa rumande na Chiluba.Wakati Nyerere akipanda ndege Lusaka kurudi Butiama,huku nyuma Chiluba alimfungulia Kaunda na kumtoa gerezani na kurudi nyumbani.Huu ni ushawishi unaovuka mipaka.Tuliaminiwa Burundi na Rwanda kuwaweka pamoja baada ya mauwaji ya kimbari.

Sasa tunakoelekea,tunaweza kuzalisha viongozi ambao hata "ushawishi" wao hauvuki kisiwa cha Chumbe ktk moja ya kina cha bahari ya Hindi, ushawishi usiovuka Ziwa Tanganyika kuelekea maziwa makuu.

Tutakosa watu wenye nguvu za ushawishi kuvuka Ziwa Nyasa na Pwani ya Afrika Mashariki.Nyakati hizo tulisimika Marais ktk nchi jirani na wakawa "vibaraka" wa Ikulu ya Dsm; kuanzia Ikulu ya Nakasere Uganda mpaka Bujumbura,Ututsi mpaka Moroni,eneo la Nampula mpaka Maputo ya Msumbiji.Tuliambaambaa kuanzia Lusaka mpaka Salisbury ya Zimbabwe na Windhoek.Wote hawa walikuwa "vijana" wetu tuliowakuza na kuwalea.

Leo kuna mtu kakataliwa huko Bujumbura;sababu anakosa "moral Authority" ya kukemea yale wanayotenda wengine sbb na yeye ana harufu ya yanayotendwa na yule anayelalamikiwa.Habari ya mtu anayeitwa Jecha inaweza kuwa na matokeo hasi ya muda mrefu katika ushawishi wetu wa siasa za kimataifa ndani na nje ya mipaka ya Afrika.

Unawezaje kumkemea Museveni kwa matendo yake kwa Kiiza Besigye wakati na wewe unayabariki kama hayo kwa wapinzani ndani ya nchi yako?Utamuwekaje meza moja Nkurunzinza na wapinzani wake wakati kwako hao wapinzani unaonekana kwenye youtube ukiwaita "mal.ofa na uchwara".

Huwezi kuwa na sauti kama ktk nchi yako wapinzani wa Serikali wananyimwa nafasi ya mikutano ya kisiasa na uhuru wa kutoa habari unadhibitiwa kwa sheria zilizotungwa na bunge (A law which is not just,is a useless law) na wewe umekaa kimya.

Wakati wa msiba wa Mama Mzazi wa Nyerere,upinzani wa Tanzania ulikuwa mikononi mwa Augustine Mrema na NCCR-Mageuzi,siku ya msiba ule pale Butiama na Mrema alifika,katika watu wa kuweka mashada ya mauwa,watu wa protokoli walimkacha Mrema wakidhani watamfurahisha Mwalimu,kwa ajabu Mwalimu alichukua shada moja na kumpelekea Mrema ili kuweka katika kaburi la Mama yake.Wale wote waliomkacha Mrema wakapatwa na aibu kubwa.

Wakati wa kupeana pole,Mrema alifika alipokaa Mwalimu na kumshika mkono wa pole,na baadae akahamia kwa aliyekuwa Makamu wa Rais marehemu Dr Alli Juma,na wakati wakiongea hili na lile,marehemu Dr Alli akajisemesha;"Huyu Augustino alikuwa rafiki yangu sana wakati akiwa serikalini",na Mwalimu akamuuliza Dr Alli;kwani sasa imekuwaje?Dr akajibu "Aa toka aende upinzani sina hamu nae tena"...Basi Mwalimu akamwambi "Aaa basi huyo hakuwa rafiki yako;angekuwa rafiki hata leo ungeendelea kumuona ni rafiki tu"

Katazo la Bujumbura si ishara njema kwa sisi kama Taifa;hata kama laweza kuwa katazo la "muda" tu,lakini ni taa ya tahadhari kuwa sasa ule "ushawishi" tuliokuwa nao enzi za Mwalimu na baada ya Mwalimu unaweza kuwa ktk eneo la mwisho wa enzi...Ni wapi tulipotereza??
Naoma unauliza ndevu kwa osama
 
Kwa upeo wangu na kwa yanayoendelea tanzania tusitegemee kutoa wasuluhishi watakao kubalika tena
 
Wababaishaji tu ambao wanatoa kauli za kustaajabisha sana, "Wanaohoji uwepo wa Nkurunzinza madarakani ni wehu" kweli aliye mwehu hata kwa sekunde moja hawezi kujitambua kama yeye ni mwehu.
BWM hakuwai kuwa kiongozi mzuri bali ni mtawala aliyewai kutokea mana hana busara, hekima, wala uvumilivu yani hana uwezo binafsi wa uongozi zaidi ya kutumia nguvu na cheo.
 
Ndiyo maana nasema mara nyingi tu kwamba Nyerere pamoja na mapungufu yake lakini yule ilikuwa ni zawadi kwa Mungu toka kwa Watanzania. Siku zote alikuwa very careful kwenye kuchagua maneno yake kwenye hotuba zake na alikuwa na mapemnzi ya kweli kwa Watanzania na Tanzania hakuwahi kudokoa/kukwapua hata senti moja ya Watanzania ili kujitajirisha. Hawa wengine ni waropopokaji tu, wezi, mafisadi, wababaishaji wenye kupenda kutumia kauli zinazoudhi n.k.

BWM hakuwai kuwa kiongozi mzuri bali ni mtawala aliyewai kutokea mana hana busara, hekima, wala uvumilivu yani hana uwezo binafsi wa uongozi zaidi ya kutumia nguvu na cheo.
 
Kama kitu hujui usionyeshe kiasi cha ujinga wako! Kujua kutumia smartphone au PC isiwe kero kwa wenzio kwani hata robbot linaweza kupress button!

Sema basi wewe kitu unajua tuone kiasi cha werevu wako
 
Tanzania kwa sasa kimataifa linaonekana kama taifa la wahuni wahuni. Mkapa, Kikwete nk. ni wale wale tu. Wanaganga njaa ili kuvuta vuta siku ziende tu. Hivi issue za kuwa wasuluhishi wa migogoro ni dili zao za kuunga unga tu. Hawana Weredi wala dhamira ya dhati ya kutatua migogoro hiyo.
Msuluhishi wa Kweli alikuwa Nyerere na Mandela kwa Afrika.
 
suala la zanzibar ndio linawamaliza .sasa anachokifanya ni kukwela majukumu yake .eti anadai mabalozi wabaonekana na makaratasi
 
Sema basi wewe kitu unajua tuone kiasi cha werevu wako

Bora wamemtoa nishai maana alitaka kwenda kutafuta kick kwa jina la nchi wakati wananchi tunamju ana roho mbaya. Uhuni uliofanyika Znz kauona na kaukalia kimya, huko nje kaenda kufanya nini kama sio mzandiki?
 
Mpaka walikuwa wanamkubali mwanzo walikuwa hawamjui kwamba ni adui mkubwa wa demokrasia Tanzania na Africa kwa ujumla hamna faida ya kumkubali ili aendelee kutumbuwa fedha za umoja wa mataifa
 
Nimesikitika sana nilivyosikia BBC Focus in Africa akiwaita wanaomkataa Nkurunzinza wapumbavu!
Kiukweli wanaweza wakawa wapumbavu lakini ndio walio wengi na kura zao zilikuwa nyingi pia kabla hazijapinduliwa. Ukienda mbele zaidi ni kwamba watu hawa hawa wamekubali kukaa meza moja kuyamaliza na wewe umeaminiwa kama msuluhisi hivyo huna budi kuwasikiliza badala ya kuwakatisha tamaa na kuwatukana. Naamini Nelson Mandela kukaa gerezani miaka 27 na baadae akatolewa huku idadi kubwa ya watu ikimuunga mkono kwenda Ikulu lazima watesaji wake walijua ni 'mkorofi' na 'mpumbavu'!
Lukindo hayo unayoyataka yatakuja kawaulize waganda,wacongoman,warundi kinachowapata.Ulichokiandika hukifahamu.
 
Back
Top Bottom