Kukataliwa kwa Mkapa Burundi: Je, ni mwisho wa "ushawishi" wa TZ katika Siasa za Afrika?

Acheni kukuza mambo, waliomkataa ni hao waliojificha Rwanda waliotaka kupindua serikali, sababu amewaita wehu na hawataruhusiwa kushiriki kwenye meza ya mazungumzo, na ni kweli Nkurunzinza alishinda kwa kura nyingi zaidi.
Juzi juzi hapa walitaka kumuua msemaji wa Nkurunzinza, wakaua bodyguard wake, watu kama hao ndio wawekwe kwenye mazungumzo, wa kazi gani, wabongo mnapenda complain nonsense sana lately, tuacheni siasa kwenye kila kitu
 
Kwa sasa Ni Africa nzima tunakosa viongozi wenye Legitimacy ya usuluhishi.

Inaonekana kwamba viongozi wengi wa Africa wanaunga mkono uhuni wa viongozi wao kupindua matokeo ya kura au kung'ang'ania madaraka kwa nguvu.
 
Huwezi kwenda kumwogesha mwenzako wakati wewe unanuka,

Huwezi kuwapatanisha wapinzani wa Burundi wakati Malimu Seif anazurura UN kudai haki yake.

Hao wapinzani wangekuwa wehu kamili kama wangekubali kusuluhishwa na Beni.

Mzee anapobariki dhulma badala ya kuikemea, heshima yake inashuka hadi himaya za jirani.

Hali ikiendelea hivi, tutabakiza marafiki madikteta tu.
 
Mara 1000 angeenda Diamond au King Kiba,wangepewa burudani wakasahau machungu kwa muda!
 
Ni mwisho wa ushawishi wa Mkapa mwenyewe. Tanzania ina wanadiplomasia mahiri kama Salim Ahmed Salim na Augustino Mahiga na wengine wengi bado watatusaidia. Mkapa na ubabe ubabe wake hakuwahi kuwa msuluhishi mzuri wanamlazimisha kipaji ambacho hana. Yule mzee wa mihasira ni sawa huyu tuliyenaye sasa hawawezi kuwa wasuluhishi
Pia tuna mzee wa kung'ata na kupuliza JK anaweza kusuluhisha vizuri tu
 
Acha wamkate huyu mzee. Hawatakagi ujinga kule. Ni huku tu ndio tuna "amani na utulivu" ambapo hata ukitukanwa kuwa wewe ni juha, lofa na mpumbavu, bado utakenua tu na kupiga makofi.
 
Basi Mwalimu akamwambi "Aaa basi huyo hakuwa rafiki yako;angekuwa rafiki hata leo ungeendelea kumuona ni rafiki tu"

Mwalimu angekuwepo leo upuuzi mwingi unaofanywa sasa usingefanywa kabisa

Mungu amlaze mahala pema peponi
 
Ni mwisho wa ushawishi wa Mkapa mwenyewe. Tanzania ina wanadiplomasia mahiri kama Salim Ahmed Salim na Augustino Mahiga na wengine wengi bado watatusaidia. Mkapa na ubabe ubabe wake hakuwahi kuwa msuluhishi mzuri wanamlazimisha kipaji ambacho hana. Yule mzee wa mihasira ni sawa huyu tuliyenaye sasa hawawezi kuwa wasuluhishi
Pia tuna mzee wa kung'ata na kupuliza JK anaweza kusuluhisha vizuri tu

Jk ni noma wewe...Hakuna mwanasiasa anamfikia ukanda wa afrika mashariki kati na kusini...He is exceptional
 
Unapoitwa kwenye usuluhishi hutakiwi kuwa na upande lakini pia kuepuka kufunika kombe mwanaharamu apite...! Dalili zozote za kuonyesha kuwa kuna mmoja unamkubali mwingine humkubali hukuondolea mandate ya cheo husika
Na mzee alishaanza kuonyesha upande,hilo ndilo lililowauzi wapinzani
 
Upinzani WA afrika huwa hawataki kusuruhishwa wanataka kubembelezwa kwa kupewa vyeo..
Naomba nikumbushwe ni wap Tanzania tumesuluhisha tukakubarika ukiachana na kupigania Uhuru WA nchi nyingine kipindi Kile cha ukombozi...!?
Kipindi cha mauaji Ya haraiki Rwanda walimkataa Nyerere kusuluhisha
Mwaka 2007 pale Kenya kikwete alishindwa kusuruhisha hadi akaja koffi Anan.
Kwahiyo tusitake kusema suala la Zanzibar Ndo limetuharibia wala magufuri kuzuia siasa.
Ni utiari tu wawasuluhishwa hawajataka....!!
 
Back
Top Bottom