KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,603
Sikutaka kusema haya lakini ni bora niyaseme Sasa ili 2025 baada ya kampeni ndefu ninayokusudia kuifanya inayokwenda kwa jina la 2025 MPE MAMA TABASAMU kukamilika na matokeo kuonekana ,isije ikatokea watu wakapotoshwa na upotoshaji ukageuka ukweli, Kwa hiyo mada hii inabaki kuwa kumbukumbu ya rejea ya yatakayo tokea mbeleni.
Kampeni ya 2025 MPE MAMA TABASAMU ni sehemu ya mpango mkakati wa kujitolea kuufahamisha Umma juu ya kazi nzuri za Rais Samia, mara nyingine Umma unatakiwa kujulishwa ili ujue zaidi maana isipofanyika hivyo Kuna mwingine anaweza kuchukua nafasi ya kufanya hivyo.
2025 MPE MAMA TABASAMU imezingatia vigezo na sifa zifuatazo:
Kwanza, imezingatia uchapakazi wa Rais Samia, kama Rais Samia asingekuwa mchapakazi kampeni hii isingekuwa na maana na ingekosa uhalali.
Pili , imezingatia uongozi bora wa Rais Samia. Kila Kona ya dunia inatambua Rais ni kiongozi bora. Kiongozi bora ni lazima apewe TABASAMU.
Tatu, imezingatia nguvu ya ushawishi aliyonayo Rais Samia Kwa Sasa. Ni kubwa sana si tu Kwa hapa Tanzania bali Afrika na Dunia Kwa ujumla hivyo nguvu hiyo itakuwa ni msingi mkubwa wa utekelezaji wa kampeni hiyo adimu.
Kwa Leo, tuziweke kando sifa namba 1 na 2 na tujikite zaidi kwenye sifa namba 3 ambayo ni nguvu ya ushawishi.
Sitaki kujitia upofu kwamba sioni hata yanayoonekana, ninaona wala sisimuliwi. Ninaona nguvu ya ushawishi ya Rais wetu imeongezeka maradufu na inazidi kukua Kila siku na nguvu yake imekuwa ni tishio Kwa wapinzani wake wa kisiasa.
Kutokana na kuongezeka nguvu yake maradufu, Rais wetu anatazamwa kama mtu aliyeshinda 2025 kabla ya shindano kuanza. Nguvu hiyo ni tishio kweli kweli.
Ili wapinzani wake waonekane nao wamo na nguvu ya ushawishi ya Rais si lolote wameanzisha kampeni ya kuonesha Kila kinachofanywa na Rais Samia si chochote na zaidi wanatamani 2025 ASIGOMBEE.
Kwa kuwa utaratibu, utamaduni ,desturi na miiko ya CCM inajulikana kwenye suala la kugombea Kwa kiongozi anayeendelea ili kumalizia kipindi cha awamu ya pili basi 2025 MGOMBEA WA CCM NI RAIS SAMIA kama hakutakuwa na sababu yoyote itakayokuja nje ya uwezo wa kibinadamu.
Nguvu ya ushawishi wa Rais Samia inachagizwa na unyenyekevu, upole, uwezo wa kufanya maamuzi, ufuatiliaji na utendaji wake.
Kwa kuwa nguvu ya ushawishi ya Rais wetu ni kubwa sana hivyo si vema kushindana nayo maana kufanya hivyo ni sawa na jaribio la kujitoa muhanga.