3D.
JF-Expert Member
- Sep 7, 2010
- 1,018
- 283
p { margin-bottom: 0.08in; } Kuna mwanasayansi mmoja anaitwa Einstein.Alisema kwamba mwanga kama chanzo cha nishati una uzito(E=MC^2 M=mass na C=spidi ya mwanga).Kama ni hivyo basi mwanga ni maada.Na maada mbili haziwezi kuchukua nafasi kwa wakati mmoja,lazima maada moja ireplace nyenzake mfano ukitumbukiza jiwe ndani ya ndoo iliyojaa maji,kuna kiasi cha maji yatamwagika chini,vivyo hivyo mwanga na giza haviwezi kukaa pamoja kwa sababu ni maada mbili tofauti.
Kinachosumbua hapa ni kwamba unapoziama taa mwanga unapotea!!,je unakwenda wapi?
Pointi ya chamoto inanishawishi niamini kwamba huenda mwanga unakimbia kurudi pale kwenye chanzo chake pindi unapozima taa
Na kwa mantiki hiyo kwa nini giza lisiwe maada? Na chanzo cha nishati?.Baadhi ya watu wanapinga hili..Manake kuna taa nyingine haziwaki bila giza kuingia
Baba Mahendeka umenipa shinikizo la kujibu hoja zako japo ninaliogopa hili suala la mwanga. Nitasema nikijuacho, nisichokijua ntakiacha. Ngoja nikumbuke pia physics yangu ya sekondari. Kuhusu mwanga aliyeanza kusema juu ya unachokiita uzito wa mwanga ni Newton. Yeye alielezea kwamba mwanga unaundwa na chembechembe (light corpuscles). Sayansi inaunga mkono hoja hii kwa kile kinachofahamika kama Photoelectric effect, yaani kuna kiwango fulani cha mwanga kikielekezwa katika metali (metals) husababisha metali hizo kutoa elektroni. Hii inamaana kuwa elektroni zimesukumwa (knocked off) na light corpuscles (maada moja imechukua nafasi ya nyingine kama usemavyo).
Hii habari ya E=mc^2 inazungumzia kuwa ikiwa particle yeyote (hata kama ni nyumba) itakwenda kasi ya mwanga basi nishati itakayotengenezwa itakuwa sawa na uzito wa particle hiyo zidisha na kkasi hiyo ya mwanga, hata hivyo hoja kubwa zaidi ni kuwa particle ikienda kwa kasi hiyo basi particle hiyo hubehave kama energy (nimesema hubehave kama energy na si huwa energy). Nikuchanganye kidogo, kimahesabu tukiandika Tanzania=Tanganyika+Zanzibar matamshi (fikra/hoja/mantiki) sahihi zaidi ni Tanganyika na Zanzibar zimeunda Tanzania na si Tanzania imeundwa na Tanganyika na Zanzibar. Namaanisha cha kwanza ni Tanganyika na Zanzibar ndiyo ikaja Tanzania na si Tanzania iliyoundwa na Tanganyika na Zanzibar. Kimahesabu components ni upande wa kulia wa sawasawa (=), upande wa kushoto wa sawasawa (Ilipokaa Tanzania katika equation yangu au ilipokaa E katika equation ya Einstein) ni majibu ya michakato iliyofanyika upande wa kulia wa sawasawa. Chemistry ni kinyume chake kilicho upande wa kushoto wa mshale (tuseme equal sine ) ni michakato wakati majibu yako upande wa kulia (hesabu majibu ni kushoto mwa equation). Hivyo E=mc^2, hatuzungumzii mwanga halafu tukasema una uzito na unakwenda kwa kasi ya mwanga. Tunasema particle yenye uzito m, inayokwenda kwa kasi ya mwanga c itakuwa ina behave kama energy ambayo kiwango chake ni E. Hata hivyo mahusiano ya energy na particle yenye kasi ya mwanga ni yana ukaribu kiwango cha kuthibitisha tabia ya energy (especially light) kuwa na tabia ya particle na energy interchangeably (wave-particle duality nature of light). Muendelezo ya fikra hizi unakwenda hadi kwenye mawazo ya kusababisha particles fulani (neutrons mfano) ambazo huweza kwenda kwa kasi ya mwanga zigonge nyukliasi (nucleus) ya atom na particles zitakazosababishwa na kugongwa huku zigonge nucleus zingine na zingine na zingine itengenezwe energy kubwa kupindukia E=mc^2....... bomu la nyuklia. Nadhani hatukusudii kwenda mbali hivi.
MWANGA NA GIZA
Ni kazi ya ubongo kutafsiri rangi, mwanga, giza kwa msaada wa macho. Ngoja nikupe dondoo. Mwanga wa jua au mwanga mwingine wowote mweupe (simaanishi mweupe kama maziwa) ni mchanganiko wa rangi kadhaa. Mwanga huo ukitua katika shati ya MwanaCCM itakutana na pigment/chemical ambayo huzuia rangi zingine zisiakisiwe na kuakisi (kureflect) mwanga wa kijani ambao ukifika kwenye macho na kisha ubongo hutafsiriwa kuwa "rangi ya kijani." Njano hivyo hivyo, bluu, nyekundu, pinki etc. Kama rangi zote zitamezwa maana yake ubongo hautapelekewa mionzi ya mwanga. Ubongo kwa sababu ya "uvivu wa kufikiri" unatafsiri hapo ni peusi (na wala si kuwa unapelekewa rangi/mwanga mweusi).
Hivyo giza ni tafsiri tu ya ubongo kama jicho halijapeleka taarifa ya kuwepo mwanga. Jiulize, ukiwasha au kuzima taa, watu wasiokuwa na macho wanatafsiri nini? Wao all the time wanaona giza kwa sababu ubongo umekuwa programmed kuona weusi/au giza pasipokuwa na taarifa ya kuwepo mwanga. Hivyo hata kama mwanaga upo, kama hakuna taarifa, utaona giza tu. Fanya hivi sasa hivi, funga macho yako kwa mikono kwanini unaona giza? Mwanga umeenda wapi? Umezima taa? Hapana, umezuia taarifa ya mwanga, ubongo unakudanganya kuwa ni giza!!! Hivyo mwanga ukiwepo ubongo unasema kuna mwanga. Mwanga usipokuwepo ubongo unakudanganya kuwa giza hilooooo limekuja wakati si kweli kuwa giza linakuja kuchukua nafasi ya mwanga.
Niishie hapa kwanza upime kama umenielewa.