Kuhusu "mwanga" na "giza" sayansi inasemaje?

p { margin-bottom: 0.08in; } Kuna mwanasayansi mmoja anaitwa Einstein.Alisema kwamba mwanga kama chanzo cha nishati una uzito(E=MC^2 M=mass na C=spidi ya mwanga).Kama ni hivyo basi mwanga ni maada.Na maada mbili haziwezi kuchukua nafasi kwa wakati mmoja,lazima maada moja ireplace nyenzake mfano ukitumbukiza jiwe ndani ya ndoo iliyojaa maji,kuna kiasi cha maji yatamwagika chini,vivyo hivyo mwanga na giza haviwezi kukaa pamoja kwa sababu ni maada mbili tofauti.
Kinachosumbua hapa ni kwamba unapoziama taa mwanga unapotea!!,je unakwenda wapi?
Pointi ya chamoto inanishawishi niamini kwamba huenda mwanga unakimbia kurudi pale kwenye chanzo chake pindi unapozima taa
Na kwa mantiki hiyo kwa nini giza lisiwe maada? Na chanzo cha nishati?.Baadhi ya watu wanapinga hili..Manake kuna taa nyingine haziwaki bila giza kuingia

Baba Mahendeka umenipa shinikizo la kujibu hoja zako japo ninaliogopa hili suala la mwanga. Nitasema nikijuacho, nisichokijua ntakiacha. Ngoja nikumbuke pia physics yangu ya sekondari. Kuhusu mwanga aliyeanza kusema juu ya unachokiita uzito wa mwanga ni Newton. Yeye alielezea kwamba mwanga unaundwa na chembechembe (light corpuscles). Sayansi inaunga mkono hoja hii kwa kile kinachofahamika kama Photoelectric effect, yaani kuna kiwango fulani cha mwanga kikielekezwa katika metali (metals) husababisha metali hizo kutoa elektroni. Hii inamaana kuwa elektroni zimesukumwa (knocked off) na light corpuscles (maada moja imechukua nafasi ya nyingine kama usemavyo).

Hii habari ya E=mc^2 inazungumzia kuwa ikiwa particle yeyote (hata kama ni nyumba) itakwenda kasi ya mwanga basi nishati itakayotengenezwa itakuwa sawa na uzito wa particle hiyo zidisha na kkasi hiyo ya mwanga, hata hivyo hoja kubwa zaidi ni kuwa particle ikienda kwa kasi hiyo basi particle hiyo hubehave kama energy (nimesema hubehave kama energy na si huwa energy). Nikuchanganye kidogo, kimahesabu tukiandika Tanzania=Tanganyika+Zanzibar matamshi (fikra/hoja/mantiki) sahihi zaidi ni Tanganyika na Zanzibar zimeunda Tanzania na si Tanzania imeundwa na Tanganyika na Zanzibar. Namaanisha cha kwanza ni Tanganyika na Zanzibar ndiyo ikaja Tanzania na si Tanzania iliyoundwa na Tanganyika na Zanzibar. Kimahesabu components ni upande wa kulia wa sawasawa (=), upande wa kushoto wa sawasawa (Ilipokaa Tanzania katika equation yangu au ilipokaa E katika equation ya Einstein) ni majibu ya michakato iliyofanyika upande wa kulia wa sawasawa. Chemistry ni kinyume chake kilicho upande wa kushoto wa mshale (tuseme equal sine ) ni michakato wakati majibu yako upande wa kulia (hesabu majibu ni kushoto mwa equation). Hivyo E=mc^2, hatuzungumzii mwanga halafu tukasema una uzito na unakwenda kwa kasi ya mwanga. Tunasema particle yenye uzito m, inayokwenda kwa kasi ya mwanga c itakuwa ina behave kama energy ambayo kiwango chake ni E. Hata hivyo mahusiano ya energy na particle yenye kasi ya mwanga ni yana ukaribu kiwango cha kuthibitisha tabia ya energy (especially light) kuwa na tabia ya particle na energy interchangeably (wave-particle duality nature of light). Muendelezo ya fikra hizi unakwenda hadi kwenye mawazo ya kusababisha particles fulani (neutrons mfano) ambazo huweza kwenda kwa kasi ya mwanga zigonge nyukliasi (nucleus) ya atom na particles zitakazosababishwa na kugongwa huku zigonge nucleus zingine na zingine na zingine itengenezwe energy kubwa kupindukia E=mc^2....... bomu la nyuklia. Nadhani hatukusudii kwenda mbali hivi.

MWANGA NA GIZA

Ni kazi ya ubongo kutafsiri rangi, mwanga, giza kwa msaada wa macho. Ngoja nikupe dondoo. Mwanga wa jua au mwanga mwingine wowote mweupe (simaanishi mweupe kama maziwa) ni mchanganiko wa rangi kadhaa. Mwanga huo ukitua katika shati ya MwanaCCM itakutana na pigment/chemical ambayo huzuia rangi zingine zisiakisiwe na kuakisi (kureflect) mwanga wa kijani ambao ukifika kwenye macho na kisha ubongo hutafsiriwa kuwa "rangi ya kijani." Njano hivyo hivyo, bluu, nyekundu, pinki etc. Kama rangi zote zitamezwa maana yake ubongo hautapelekewa mionzi ya mwanga. Ubongo kwa sababu ya "uvivu wa kufikiri" unatafsiri hapo ni peusi (na wala si kuwa unapelekewa rangi/mwanga mweusi).

Hivyo giza ni tafsiri tu ya ubongo kama jicho halijapeleka taarifa ya kuwepo mwanga. Jiulize, ukiwasha au kuzima taa, watu wasiokuwa na macho wanatafsiri nini? Wao all the time wanaona giza kwa sababu ubongo umekuwa programmed kuona weusi/au giza pasipokuwa na taarifa ya kuwepo mwanga. Hivyo hata kama mwanaga upo, kama hakuna taarifa, utaona giza tu. Fanya hivi sasa hivi, funga macho yako kwa mikono kwanini unaona giza? Mwanga umeenda wapi? Umezima taa? Hapana, umezuia taarifa ya mwanga, ubongo unakudanganya kuwa ni giza!!! Hivyo mwanga ukiwepo ubongo unasema kuna mwanga. Mwanga usipokuwepo ubongo unakudanganya kuwa giza hilooooo limekuja wakati si kweli kuwa giza linakuja kuchukua nafasi ya mwanga.

Niishie hapa kwanza upime kama umenielewa.
 
Unapoingia ndani ya chumba chenye giza,kisha ukabonyeza swichi ili kuwasha taa,je giza linakwenda wapi?. Au unapokuwa ndani ya chumba chenye mwanga wakati wa usiku halafu ukabonyeza swichi kuzima taa ili ulale.Je mwanga unakwenda wapi?

[FONT=helvetica, arial][FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Light is everywhere in our world. We need it to see: it carries information from the world to our eyes and brains. Seeing colors and shapes is second nature to us, yet light is a perplexing phenomenon when we study it more closely.[/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Here are some things to think about:
  • Our brains and eyes act together to make extraordinary things happen in perception. Movies are sequences of still pictures. Magazine pictures are arrays of dots
  • Light acts like particles-little light bullets-that stream from the source. This explains how shadows work.
  • Light also acts like waves-ripples in space-instead of bullets. This explains how rainbows work. In fact, light is both. This "wave-particle duality" is one of the most confusing-and wonderful-principles of physics
[/FONT][/FONT]
 
Pointi ya chamoto inanishawishi niamini kwamba huenda mwanga unakimbia kurudi pale kwenye chanzo chake pindi unapozima taa
Na kwa mantiki hiyo kwa nini giza lisiwe maada? Na chanzo cha nishati?.Baadhi ya watu wanapinga hili..Manake kuna taa nyingine haziwaki bila giza kuingia

Mwanga haukimbii kurudi kwenye chanzo chake unapotea na kuwa absorved na matter iliyo karibu. Ukizima taa energy ya mwanga inapungua nguvu.

Washa tochi kwnye jua kali sehemu yenye uwazi bila kuta kwa nini huoni kitu? Sababu ule mwanga wa tochi unayonywa na mwanga wa jua na kuzidiwa. Mwanga unasaidia reflection na hivyo kutusaidia kutambua nakuona Kwa hiyo hata giza ni mwanga sema tu mwanga wa giza hauna reflection au reflection yake ni very poor kuwa na msaada kwa macho ya binadamu. Lakini chui au paka uwezo wao kuona na kutambua itu kwenye mwanga wa giza ni mkubwa kuliko binadamu. Teh teh teh

So giza nao ni mwanga.

thanks kwa kuchemsha ubongo
 
Labda nikusaidie hivi kijana:

Giza au dark, ndio natural presence ya kitu chochote au mahali popote, nikiwa namaanisha kwamba giza halitengenezwi kama ambavyo mwanga unaweza tengenezwa, na giza ndio ambalo lipo na litazidi kuwepo, ila mwanga ndio unaoweza kuja na kupotea.

Imagine no sun. Unadhani ingekuwaje? Kwa sababu hata mwezi unapomulika duniani ni kwamba una reflect light from the sun.

SO GIZA KAMWE HATA UKIINGIA CHUMBANI UKAWASHA TAA, SIO KWAMBA LIMEONDOKA, LA HASHA, BADO LIPO ILA MWANGA ULIOINGIA, UMECHUKUA NAFASI YAKE.

Mwanzo 1:1-3

1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.
2 Dunia ilikuwa bila umbo, na ukiwa, na giza lilikuwa juu ya uso wa kilindi cha maji; na nguvu za utendaji za Mungu zilikuwa zikienda huku na huku juu ya uso wa maji.
3 Mungu akasema: "Kuwe na nuru." Kukawa na nuru. 4 Kisha Mungu akaona ya kuwa nuru ilikuwa nzuri. Mungu akatenganisha nuru na giza. 5 Mungu akaanza kuiita nuru Mchana, lakini giza akaliita Usiku. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
 
p { margin-bottom: 0.08in; } Kuna mwanasayansi mmoja anaitwa Einstein.Alisema kwamba mwanga kama chanzo cha nishati una uzito(E=MC^2 M=mass na C=spidi ya mwanga).Kama ni hivyo basi mwanga ni maada.Na maada mbili haziwezi kuchukua nafasi kwa wakati mmoja,lazima maada moja ireplace nyenzake mfano ukitumbukiza jiwe ndani ya ndoo iliyojaa maji,kuna kiasi cha maji yatamwagika chini,vivyo hivyo mwanga na giza haviwezi kukaa pamoja kwa sababu ni maada mbili tofauti.
Kinachosumbua hapa ni kwamba unapoziama taa mwanga unapotea!!,je unakwenda wapi?
Pointi ya chamoto inanishawishi niamini kwamba huenda mwanga unakimbia kurudi pale kwenye chanzo chake pindi unapozima taa
Na kwa mantiki hiyo kwa nini giza lisiwe maada? Na chanzo cha nishati?.Baadhi ya watu wanapinga hili..Manake kuna taa nyingine haziwaki bila giza kuingia

If Rutherford or Borh could hear what you said he would have slapped you,but thanks to Heinsenberg,Plank and the Guy on ma avatar they would have agreed.lol.
Yeah light as said above has wave particle duality,ie it has both particle properties and wave properties, ila sio kama ulivyosema yes mwanga una mass but not 'rest mass'. Light being a photon has only mass as it moves(it's mass is imaginary after comparing the energy due to rest mass'E=MC^2' and energy due to its frequency'E=hf'
mc^2=hf
hence
m=hf/c2
NOTE:mass cant exist without speed ndo maana ya 'zero rest mass' hivyo huwezi sema ukakamata mwanga ukaupima kilo,photons of light are either reflected,absorbed.) back to the topic. We can see things when the 'light' is reflected from them to our eyes,if there is no light you see black(that's why black cloth are seen as black because black body absorbes the light and none is reflected to your eye)
 
Mwanzo 1:1-3

1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.
2 Dunia ilikuwa bila umbo, na ukiwa, na giza lilikuwa juu ya uso wa kilindi cha maji; na nguvu za utendaji za Mungu zilikuwa zikienda huku na huku juu ya uso wa maji.
3 Mungu akasema: “Kuwe na nuru.” Kukawa na nuru. 4 Kisha Mungu akaona ya kuwa nuru ilikuwa nzuri. Mungu akatenganisha nuru na giza. 5 Mungu akaanza kuiita nuru Mchana, lakini giza akaliita Usiku. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

Walokole bana, hapa ni sayansi tu hizo siasa zipotezee.
 
Mwanzo 1:1-3

1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.
2 Dunia ilikuwa bila umbo, na ukiwa, na giza lilikuwa juu ya uso wa kilindi cha maji; na nguvu za utendaji za Mungu zilikuwa zikienda huku na huku juu ya uso wa maji.
3 Mungu akasema: “Kuwe na nuru.” Kukawa na nuru. 4 Kisha Mungu akaona ya kuwa nuru ilikuwa nzuri. Mungu akatenganisha nuru na giza. 5 Mungu akaanza kuiita nuru Mchana, lakini giza akaliita Usiku. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

naomba tujadili hoja hii kisayansi tu, kama kichwa cha habari cha bandiko langu kinavyojieleza
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Mwanga haukimbii kurudi kwenye chanzo chake unapotea na kuwa absorved na matter iliyo karibu. Ukizima taa energy ya mwanga inapungua nguvu.

Washa tochi kwnye jua kali sehemu yenye uwazi bila kuta kwa nini huoni kitu? Sababu ule mwanga wa tochi unayonywa na mwanga wa jua na kuzidiwa. Mwanga unasaidia reflection na hivyo kutusaidia kutambua nakuona Kwa hiyo hata giza ni mwanga sema tu mwanga wa giza hauna reflection au reflection yake ni very poor kuwa na msaada kwa macho ya binadamu. Lakini chui au paka uwezo wao kuona na kutambua itu kwenye mwanga wa giza ni mkubwa kuliko binadamu. Teh teh teh

So giza nao ni mwanga.

thanks kwa kuchemsha ubongo

Ohoooo!! Unakoelekea baba siko.
 
Kwa elimu yangu ya darasa la saba 'A'
somo la sayansi, Mwalimu Mwaisaka wa Sisimba alinifundisha kuwa mwanga ni nishati inayotuwezesha kuona.
Nikamuuliza giza ni nini, nikachapwa fimbo zaidi ya sita ambazo yeye alikuwa anaziita Sendemaaa

Mkuu ahsante, yaani machozi yamenitoka kwa kicheko. Hakika ulikua mdadisi, lakini bahati yako mbaya ukakutana na mwalimu wa upe hahahaha
 
Naona nimejiweka matatani!!!

Ndiyo joto litakuwepo. Imagine hakuna kiumbe hai ila kuna karatasi na nyasi kavu. Karatasi na nyasi zitaungua. Kinachounguza karatasi ni joto. Joto na sauti zote ni nishati (energy) lakini athari ya mwisho ya sauti ni kusikika. Kusikika kunahitaji viumbe hai tu. Athari ya mwisho ya joto ni kuunguza au kuongeza joto (umoto) katika viumbe hai na visivyo hai.Ni wazi kuwa chuma hakitacomplain kuwa kinasikia joto ila kitabehave kuonesha kuna joto kama kutanuka, kupinda ama kuyeyuka kabisa

Sauti,

Mti ukianguka porini na wakati hakuna kiumbe hai, kama kuna makaratasi yatarukaruka hata kama hayajaangukiwa na mti. Sababu ni mbili. Moja, mtikisikiko wa ardhi utazirusharusha. Mbili (muhimu), mti na matawi yake yatadisturb hewa wakati yanaanguka, hewa iliyokuwa disturbed (inayomove) itakwenda kusukuma (kupuliza) karatasi na kitakachokuwa kinatikisa karatasi ni mtikisiko wa hewa na si msikiko wa mtikisiko (sound) ambao kimsingi hautakuwepo.

Thanks 3D. I like the way una defend hoja zako.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Ohoooo!! Unakoelekea baba siko.

Si ndio maana tuko hapa kuelimishan mkuu. Ebu niambie intesity ya mwanga inapimwaje. Mi nadhani giza nalo ni mwanga sema ni mwanga wenye intesity ndogooooo.

Betri iliyohsiwa charge haiwezi kuwasha tochi si kwasababu haitoi mwanga bali ni kwa sababu mwanga inatoa ni giza. ambayo intesity yake ni ndogo.

Vile vile nimabie kwa nini paka au chui ana uwezo mkubwa kuona kwenye mwanga wa giza kuliko binadamu. So utaona kuwa huwezi kuongelea mwanga bila kuongelea kuakisiwa au reflection

Au nieleweshe wapi napolekea sipo.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Wazo lako ni zuri limenisaidia kuelewa kitu,je
nikisema kuwa unapozima taa mwanga unakimbia kurudi kwenye chanzo chake nakosea?
Mwanga haurudi kwenye chanzo bali baada ya chanzo cha mwanga
kutoweka (taa kuzimwa) mwanga uliobaki hunyonywa na vitu vya
karibu na kubadilika kutoka nishati ya mwanga kwenda kwenye nishati
ya joto.
 
Na kwa mantiki hiyo kwa nini giza lisiwe maada?
Hii bado ni debatable kwasababu hata hizo MOND theories
bado hazielezei vizuri mambo ya dark matter.

Manake kuna taa nyingine haziwaki bila giza kuingia
Hii hutokana na logic circuit ya photoelectric
censor ( aina ya opposed ) ya kwenye taa kuwa
true (absence of light), na kuruhusu conduction.
 
Mwanga haukimbii kurudi kwenye chanzo chake unapotea na kuwa absorved na matter iliyo karibu. Ukizima taa energy ya mwanga inapungua nguvu.

Washa tochi kwnye jua kali sehemu yenye uwazi bila kuta kwa nini huoni kitu? Sababu ule mwanga wa tochi unayonywa na mwanga wa jua na kuzidiwa. Mwanga unasaidia reflection na hivyo kutusaidia kutambua nakuona Kwa hiyo hata giza ni mwanga sema tu mwanga wa giza hauna reflection au reflection yake ni very poor kuwa na msaada kwa macho ya binadamu. Lakini chui au paka uwezo wao kuona na kutambua itu kwenye mwanga wa giza ni mkubwa kuliko binadamu. Teh teh teh

So giza nao ni mwanga.

thanks kwa kuchemsha ubongo

Natofautiana na wewe hapo kwenye red! Hauwezi kuwa na mwanga bila chanzo, lakn giza ndy mwenyeji wa ulimwengu, ndy jinsi ulimwengu ulivyo. wengine wanaeleza mwanga ni kitu cha kuexist kinachotokana na chanzo, lakn giza halipo kwa sababu ndy haswa asili ya ulimwengu.
 
Haya ni baadhi ya maswali magumu mengine ni kama....... Mungu alitoka wapi?
Dunia ilitoka wapi?
Kwa nini mtu akitaka kufa anaanza kujua?

Maswali hayo ni tofauti kabisa na swali la mdau hapo juu!
 
Si ndio maana tuko hapa kuelimishan mkuu. Ebu niambie intesity ya mwanga inapimwaje. Mi nadhani giza nalo ni mwanga sema ni mwanga wenye intesity ndogooooo.

Betri iliyohsiwa charge haiwezi kuwasha tochi si kwasababu haitoi mwanga bali ni kwa sababu mwanga inatoa ni giza. ambayo intesity yake ni ndogo.

Vile vile nimabie kwa nini paka au chui ana uwezo mkubwa kuona kwenye mwanga wa giza kuliko binadamu. So utaona kuwa huwezi kuongelea mwanga bila kuongelea kuakisiwa au reflection

Au nieleweshe wapi napolekea sipo.

Kwa kiasi flani uko sahihi, lakn ikumbukwe kuwa kuna aina mbalimbali za mwanga, na vyanzo vyake ni tofauti; kwa mfano infrared, aina hizi za mwanga zinaweza kuonekana kuwa giza katika macho ya mwanadamu, lakini kwa baadhi ya viumbe vikaonekana kama mwanga. Unapozima taa kukawa kama "total darkness" kuna kiumbe anayeona mwanga wa aina flani.
 
intensity ya mwanga inapimwa kwa kuangalia kiasi cha mwanga kutoka kwenye chanzo.tunaongelea positive intensity yenye wavelength ambayo binadamu anaweza kuitambua.na siyo negative uliyoibatiza jina la mwanga wa giza..kweye maelezo yako kuna logic,lakini ni rahisi kuchanganya watu
 
Si ndio maana tuko hapa kuelimishan mkuu. Ebu niambie intesity ya mwanga inapimwaje. Mi nadhani giza nalo ni mwanga sema ni mwanga wenye intesity ndogooooo.

Betri iliyohsiwa charge haiwezi kuwasha tochi si kwasababu haitoi mwanga bali ni kwa sababu mwanga inatoa ni giza. ambayo intesity yake ni ndogo.

Vile vile nimabie kwa nini paka au chui ana uwezo mkubwa kuona kwenye mwanga wa giza kuliko binadamu. So utaona kuwa huwezi kuongelea mwanga bila kuongelea kuakisiwa au reflection

Au nieleweshe wapi napolekea sipo.

Mkuu Mtazamaji tuko pamoja. Nafuta kauli yangu ya kushangaa. Sasa najibu maswali yako pamoja na mifano uliyotoa:

Betri isiyowasha taa:

Mkuu, kwani kitu gani kinasababisha umeme utoke upande mmoja kwenda mwingine? Ni tofauti ya kiwango cha charge kati ya upande mmoja na mwingine. Kisayansi tofauti hii huitwa potential difference na hupimwa kama Voltage (SI Unit Volts). Naomba nifananishe na kitu hiki: Kitu gani hufanya maji ya mto kutoka upande mmoja hadi mwingine. Ni tofauti ya mwinuko. Maji ya mto hutoka upande wa juu zaidi kwenda wa chini zaidi. Hata umeme (electric current) hutiririka toka upande wenye potential kubwa (fananisha na charges nyingi) kwenda kule kwenye charge kidogo. Betri ikichajiwa maana yake inaongezewa potential (charge) ili iwe juu kuliko taa. Sasa betri ikitumika charge huisha (hata simu zinaisha charge, hili unalijua sana) maana yake potential huja chini na matokeo yake kunakuwa hakuna potential difference (tofauti ya mwinuko) toka upande mmoja (betri) na upande mwingine (taa, simu redio, jiko etc) hivyo mkondo/current (maji ktk mfano wa mto) hauwezi kupita. Hii ndiyo sababu ya betri kutowasha taa. Sijajua unatatizika nini hapa. Jikumbushe principles za Voltage, Current, Resistance. Ukijua resistance utajua pia kwanini taa za balbu nyaya zake katika bulb ni nyembamba. Utajua pia kwanini zimenyongwanyongwa kuwa coil/helix. Sababu hizi zinaapply katika pasi na majiko ya umeme. Kama kuna kinachokuchanganya hapa niulize.

Mbwa/Paka kuona katika giza kuliko binadamu

Ukitaka kujua sababu unatakiwa ujue kitu gani kinawatofautisha hao wanyama na binadamu katika mfumo wa fahamu. Mbwa na paka wanamzidi binadamu hata katika uwezo wa kunusa pia. Tuweke kiporo suala la kunusa tuzungumzie kuona. Hebu japo kidogo tujifunze sayansi ya kuona.

Ndani ya jicho la binadamu kuna eneo lenye seli nyingi linaloitwa retina. Retina kimsingi ina aina 2 za seli aina ya kwanza ni rods na ya pili ni cones. Kazi ya rods ni uonaji katika mwanga hafifu na mijongeo (movement); na cones kazi zake ni kuona mwanga mwingi (bright light) pamoja na rangi. Mbwa na wanyama wengine wengi wana rods nyingi kuliko binadamu hivyo huona vizuri zaidi katika mwanga hafifu kuliko binadamu. Hiyo ndiyo sababu. Kwa upande mwingine binadamu ana cones zaidi ya wanyama hivyo anaona rangi vizuri kuliko mbwa na wenzake. Kifupi tu ni kuwa mbwa hawaoni rangi zote kama binadamu aonavyo, wao huona kijivujivu na aina fulani ya unjano. Kwa haraka waweza sema wanaona black and white.

ZIADA KIDOGO

Katika retina kuna reactions ambazo hufanyika kutokana na mwanga kuingia. Kuna aina fulani ya kemikali iitwayo Retinene ambayo part of it inatengenezwa na Vitamin A. Ukipungukiwa Vit A uwezo wako wa kuona unapungua. Hujawahi kusikia watu wanakwambia "Dogo huoni nini, kula mchicha"?

Intensity ya Light

Sijui unauliza nini. Niseme tu kuwa light intensity ni matokeo ya kiwango cha light ukilinganisha na eneo. Yaani kiwango fulani cha mwanga kikisambazwa katika eneo dogo huwa na intensity kubwa na kiwango hicho hicho cha mwanga kikisambazwa katika eneo kubwa huwa na intensity ndogo. Waweza kufananisha na mfano huu (kama unafahamu physics na hisabati): Pressure = Force/Area hapa fananisha pressure na intensity.
Kama kuna tatizo naweza kufafanua zaidi. Sijui nimeelewa ulichoniuliza? Utanifahamisha.

Kwa kiasi flani uko sahihi, lakn ikumbukwe kuwa kuna aina mbalimbali za mwanga, na vyanzo vyake ni tofauti; kwa mfano infrared, aina hizi za mwanga zinaweza kuonekana kuwa giza katika macho ya mwanadamu, lakini kwa baadhi ya viumbe vikaonekana kama mwanga. Unapozima taa kukawa kama "total darkness" kuna kiumbe anayeona mwanga wa aina flani.

Labda niseme tu kuwa uonaji wa infrared ni matokeo ya kudetect heat inayosababishwa na mwanga huo. Hili halina uhusiano na "umaada" wa giza. Spectrum ina rangi nyingi lakini kuna range ya frequency/wavelength ambayo macho ya binadamu yana uwezo wa kudetect hii huitwa visible light. Hata katika sauti si zote ambazo binadamu husikia. Kuna frequencies ambazo popo na tembo husikia wakati binadamu atasema hasikii kitu. Hii haimaanishi ukimya ni sauti. Ni suala la uwezo tu wa binadamu kusikia. Lakini nisisitize tu kuwa hata ukizima taa bado kuna aina fulani ya mwanga ambayo huwepo (hata kama huoni) kwa sababu ya reflection ya jua kupitia mawingu. Lakini kukiwa na mawingu meusi/mvua nadhani giza lake linaongezeka. Kwa wale waliowahi kuingia mapango ya Amboni Tanga wanajua maana ya giza. Achana na giza la kuzima taa ambalo baada ya dakika chache macho yanaadapt unaanza kuona zaidi.
 
Back
Top Bottom