Kuhusu "mwanga" na "giza" sayansi inasemaje?

MAHENDEKA

JF-Expert Member
Jul 9, 2010
306
152
Unapoingia ndani ya chumba chenye giza,kisha ukabonyeza swichi ili kuwasha taa,je giza linakwenda wapi?. Au unapokuwa ndani ya chumba chenye mwanga wakati wa usiku halafu ukabonyeza swichi kuzima taa ili ulale.Je mwanga unakwenda wapi?
 
Labda nikusaidie hivi kijana:

Giza au dark, ndio natural presence ya kitu chochote au mahali popote, nikiwa namaanisha kwamba giza halitengenezwi kama ambavyo mwanga unaweza tengenezwa, na giza ndio ambalo lipo na litazidi kuwepo, ila mwanga ndio unaoweza kuja na kupotea.

Imagine no sun. Unadhani ingekuwaje? Kwa sababu hata mwezi unapomulika duniani ni kwamba una reflect light from the sun.

SO GIZA KAMWE HATA UKIINGIA CHUMBANI UKAWASHA TAA, SIO KWAMBA LIMEONDOKA, LA HASHA, BADO LIPO ILA MWANGA ULIOINGIA, UMECHUKUA NAFASI YAKE.
 
Nikwamba unapowasha taa kunakuwa na excited particles nyingi
ambazo zinatoa nishati (mwanya). Wakati unapozima, hizo excited
particles hupungua (giza) kwasababu zinarudi kwenye stationary
state.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.

Nakubaliana na Firefox lakini nataka pia kuongeza kwamba dunia hii hakuna kitu kingine kinachotembea haraka zaidi ya mwanga. Speed ya mwanga ni 300,000 km/sekunde au 1079 milioni km/hour. Nadhani hii tabia ya mwanga ndo inafanya ukiwasha tuu taa chumba chote kinajaa mwanga na ukizima mwanga unapotea na giza linajaa. kitukingine napenda kuongeza wajua jua linachukua dakika 8 na sekunde 19 kutufukia linapochomoza, najua lipo umbali wa 150millioni km kutoka duniani
 
Kwa elimu yangu ya darasa la saba 'A'
somo la sayansi, Mwalimu Mwaisaka wa Sisimba alinifundisha kuwa mwanga ni nishati inayotuwezesha kuona.
Nikamuuliza giza ni nini, nikachapwa fimbo zaidi ya sita ambazo yeye alikuwa anaziita Sendemaaa
 
Hahahahaaaa
You made my day mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Najaribu kujiuliza ikiwa aliyeuliza swali anatambua uzito (si ugumu) wake. Naamini anajua. Giza na mwanga havielezwi kwa physics pekee. Nitarudi. Lakini kwa haraka sana niseme kuhusu giza. Giza halina physical existence ila ni matokeo ya "absence" ya mwanga. Ni kama vile uondoe maji kwenye glass na uzuie hewa kuingia, kitachokuwepo ni vaccuum. Thus, giza si opposite ya mwanga bali inexistence ya mwanga.

Swali lililoulizwa ni zuri na kubwa sana. Kubwa sana. Ni sawa na swali "Mti ukianguka porini na kusiwepo kiumbe chochote kingine sauti ya kuanguka kwake itasikika?"
 
unataka kusema kuwa kwa sababu hakuna aliyesikia then haijasikika?
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
We always see things when light falls on it.
refer..physics ya V & VI soma kitabu cha NELKON utaelewa zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
p { margin-bottom: 0.08in; } Wazo lako ni zuri limenisaidia kuelewa kitu,je
nikisema kuwa unapozima taa mwanga unakimbia kurudi kwenye chanzo chake nakosea?..
 
Nikwamba unapowasha taa kunakuwa na excited particles nyingi
ambazo zinatoa nishati (mwanya). Wakati unapozima, hizo excited
particles hupungua (giza) kwasababu zinarudi kwenye stationary
state.
Wazo lako ni zuri limenisaidia kuelewa kitu,je
nikisema kuwa unapozima taa mwanga unakimbia kurudi kwenye chanzo chake nakosea?
 
unataka kusema kuwa kwa sababu hakuna aliyesikia then haijasikika?

Tuepuke kuhamisha mjadala toka kwenye mwanga hadi sauti. Tutalaumiwa kwa kuvamia thread ya wengine na kuweka mijadala yetu. Niseme tu kuwa:

Ndiyo, inaelezwa kuwa sauti haitosikika. Sababu ni kuwa hakuna sauti nje ya mfumo wa fahamu wa kiumbe hai. Binadamu husikiaje sauti? Chanzo cha sauti hudisturb hewa inayokizunguka (surrounding air). Hiyo hewa iliyokuwa disturbed haitoi sauti yoyote zaidi ya kutikisika kimyakimya. Mtikisiko huo (sound waves (not sound)) ikifika sikioni kwa binadamu inaitikisa ngoma ya sikio ambayo hupeleka taarifa kwenye ubongo kuwa kuna mtikisiko (sauti fulani). Hii inamaanisha:

  1. Bila hewa hakuna sauti (medium zingine eg solids zinaweza kupitisha vibrations)
  2. Bila mfumo wa fahamu hakuna sauti zaidi ya hewa kutikisika kimyakimya.
ZIADA:
Binadamu husikia sauti yake kupitia masikio yake na kupitia vibrations ndani ya kichwa chake. Ukiziba masikio halafu ukaongea bado utajisikia, pia utasikia sauti ya mririko wa damu. Hii inamaanisha kuwa sauti zetu tunazozisikia ni tofauti kidogo na watu wengine wanavyotusikia kwa kuwa wao hawasikii vibrations tuzisikiazo ndani ya mafuvu yetu ya vichwa. Hii inamaanisha pia sauti na mitikisiko yaweza kusikika katika sehemu za ndani ya sikio bila kupitia kwanza kwenye kiwambo cha sikio (ngoma).

Tusisahau kuchangia thread ya Mahendeka.
 
Haya ni baadhi ya maswali magumu mengine ni kama....... Mungu alitoka wapi?
Dunia ilitoka wapi?
Kwa nini mtu akitaka kufa anaanza kujua?
 
Kwa elimu yangu ya darasa la saba 'A'
somo la sayansi, Mwalimu Mwaisaka wa Sisimba alinifundisha kuwa mwanga ni nishati inayotuwezesha kuona.
Nikamuuliza giza ni nini, nikachapwa fimbo zaidi ya sita ambazo yeye alikuwa anaziita Sendemaaa

Mamaa mbavu zangu!
 
Labda nikusaidie hivi kijana:

Giza au dark, ndio natural presence ya kitu chochote au mahali popote, nikiwa namaanisha kwamba giza halitengenezwi kama ambavyo mwanga unaweza tengenezwa, na giza ndio ambalo lipo na litazidi kuwepo, ila mwanga ndio unaoweza kuja na kupotea.

Imagine no sun. Unadhani ingekuwaje? Kwa sababu hata mwezi unapomulika duniani ni kwamba una reflect light from the sun.

SO GIZA KAMWE HATA UKIINGIA CHUMBANI UKAWASHA TAA, SIO KWAMBA LIMEONDOKA, LA HASHA, BADO LIPO ILA MWANGA ULIOINGIA, UMECHUKUA NAFASI YAKE.

Umempa jibu sahìhi my dear, aulize kingine.
 
Tuepuke kuhamisha mjadala toka kwenye mwanga hadi sauti. Tutalaumiwa kwa kuvamia thread ya wengine na kuweka mijadala yetu. Niseme tu kuwa:

Ndiyo, inaelezwa kuwa sauti haitosikika. Sababu ni kuwa hakuna sauti nje ya mfumo wa fahamu wa kiumbe hai. Binadamu husikiaje sauti? Chanzo cha sauti hudisturb hewa inayokizunguka (surrounding air). Hiyo hewa iliyokuwa disturbed haitoi sauti yoyote zaidi ya kutikisika kimyakimya. Mtikisiko huo (sound waves (not sound)) ikifika sikioni kwa binadamu inaitikisa ngoma ya sikio ambayo hupeleka taarifa kwenye ubongo kuwa kuna mtikisiko (sauti fulani). Hii inamaanisha:

  1. Bila hewa hakuna sauti (medium zingine eg solids zinaweza kupitisha vibrations)
  2. Bila mfumo wa fahamu hakuna sauti zaidi ya hewa kutikisika kimyakimya.
ZIADA:
Binadamu husikia sauti yake kupitia masikio yake na kupitia vibrations ndani ya kichwa chake. Ukiziba masikio halafu ukaongea bado utajisikia, pia utasikia sauti ya mririko wa damu. Hii inamaanisha kuwa sauti zetu tunazozisikia ni tofauti kidogo na watu wengine wanavyotusikia kwa kuwa wao hawasikii vibrations tuzisikiazo ndani ya mafuvu yetu ya vichwa. Hii inamaanisha pia sauti na mitikisiko yaweza kusikika katika sehemu za ndani ya sikio bila kupitia kwanza kwenye kiwambo cha sikio (ngoma).

Tusisahau kuchangia thread ya Mahendeka.

3D majibu yako nimeyapenda yana convince, I mean they make a lot of sence, na mimi naongeza swali, kama ukiwasha moto na kusiwe na kiumbe hai karibu, je, joto litakuwepo?
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
We always see things when light falls on it.
refer..physics ya V & VI soma kitabu cha NELKON utaelewa zaidi.

Au Abbot. cha O level. teh teh teh. dah kweli tumetoka mbali. nakumbuka enzi hizo unakariri kitu bila kuelwa vizuri swali likiwa twisited kidogo kasheshe.
 
p { margin-bottom: 0.08in; } Kuna mwanasayansi mmoja anaitwa Einstein.Alisema kwamba mwanga kama chanzo cha nishati una uzito(E=MC^2 M=mass na C=spidi ya mwanga).Kama ni hivyo basi mwanga ni maada.Na maada mbili haziwezi kuchukua nafasi kwa wakati mmoja,lazima maada moja ireplace nyenzake mfano ukitumbukiza jiwe ndani ya ndoo iliyojaa maji,kuna kiasi cha maji yatamwagika chini,vivyo hivyo mwanga na giza haviwezi kukaa pamoja kwa sababu ni maada mbili tofauti.
Kinachosumbua hapa ni kwamba unapoziama taa mwanga unapotea!!,je unakwenda wapi?
Pointi ya chamoto inanishawishi niamini kwamba huenda mwanga unakimbia kurudi pale kwenye chanzo chake pindi unapozima taa
Na kwa mantiki hiyo kwa nini giza lisiwe maada? Na chanzo cha nishati?.Baadhi ya watu wanapinga hili..Manake kuna taa nyingine haziwaki bila giza kuingia
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
3D majibu yako nimeyapenda yana convince, I mean they make a lot of sence, na mimi naongeza swali, kama ukiwasha moto na kusiwe na kiumbe hai karibu, je, joto litakuwepo?

Naona nimejiweka matatani!!!

Ndiyo joto litakuwepo. Imagine hakuna kiumbe hai ila kuna karatasi na nyasi kavu. Karatasi na nyasi zitaungua. Kinachounguza karatasi ni joto. Joto na sauti zote ni nishati (energy) lakini athari ya mwisho ya sauti ni kusikika. Kusikika kunahitaji viumbe hai tu. Athari ya mwisho ya joto ni kuunguza au kuongeza joto (umoto) katika viumbe hai na visivyo hai.Ni wazi kuwa chuma hakitacomplain kuwa kinasikia joto ila kitabehave kuonesha kuna joto kama kutanuka, kupinda ama kuyeyuka kabisa

Sauti,

Mti ukianguka porini na wakati hakuna kiumbe hai, kama kuna makaratasi yatarukaruka hata kama hayajaangukiwa na mti. Sababu ni mbili. Moja, mtikisikiko wa ardhi utazirusharusha. Mbili (muhimu), mti na matawi yake yatadisturb hewa wakati yanaanguka, hewa iliyokuwa disturbed (inayomove) itakwenda kusukuma (kupuliza) karatasi na kitakachokuwa kinatikisa karatasi ni mtikisiko wa hewa na si msikiko wa mtikisiko (sound) ambao kimsingi hautakuwepo.
 
kwanza lazima ujuwe kuwa Mwanza una source lakini giza halina source! Hivyo mwanga una sababishwa na nguvu ya electrons zinavyo vibrate kutoka kwenye one orbit kwenda nyingine kwenye atom! Kwa kifupi ili kupata mwanga LAZIMA nguvu fulani itumike kuutengeneza. Lakini giza siyo energy ingawa kuna "NGUVU za Giza" ambayo ni mambo ya kishetani!
 
Back
Top Bottom