OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,667
- 105,968
Haya mambo ya kuzunguka zunguka hayafai kwa sababu muda unaenda kasi sana.
Siwezi kujifanya sijashtuka Phiri kukalia bench dakika 90. Ni uongo. Kila mtu kaona kikosi cha kwanza huku majembe mengine yakiwa pale bench. Baadae wakapewa nafasi wachezaji wa kawaida na wakali kama kina Ngoma. Halafu uone ni sawa tu Phiri kukalia bench. Kuna Wachezaji walishindwa kuonyesha kiwango toka robo ya kwanza ya kikosi lakini kocha hakumuona Phiri.
Tunasemaje..Phiri ndio aliyetupeleka makundi CAFCC msimu uliopita. Usiniambie kuhusu kiwango chake cha sasa kwa sababu ile ilikuwa mechi ya kutest mitambo. Sijasema ni bora kuliko wengine lakini anao uwezo wa kushindana na kushindania timu. Mambo ya hovyo kama haya ndio yanayosababisha kocha apangiwe kikosi. Kumbania mchezaji mpaka watu wanashtuka.
Kocha afikishiwe habari. Asituone mafala, awaulize waliotangulia. Tuna uwezo wa kumkataa mpaka akashangaa.