Kuhusu hili la kutoa sadaka makanisani ni vyema kila mtu akaachwa ashinde mechi zake

Rabonn

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
5,733
10,929
Habari za mchana huu wadau.

Natumain mko salama na mnaendelea kulijenga taifa letu Tanzania kwa moyo mmoja.
Niiingie kwenye Mada.

Huu ni ushuhuda wangu binafsi kuhusu jambo ambao wana JF wengi humu hulitolea mapovu sana..KUTOA

SADAKA YA ZAKA

Declaration of interest ni kwamba, binafsi nimekua sio mtu mwaminifu kwenye eneo hili kwa muda wa miaka mingi sana na ofcourse nilikua na sababu zako kadha wa kadhaa.
Mfano
  1. watumishishi wengi kutokua na ufaham mzuri juu ya zaka hivyo kwa sisi tuliopita shule kidogo huwa hatushawishiki sana kuamini wanachofundisha maana wengi hufundisha kuhusu sadaka (zaka) not in a DIVINE perspective ut in 'PERSONAL GAIN' perspective. Hili limekua tatizo
  2. waumini wamekosa elimu na imani kwa wanaowafunza kuhusu zako kwasababu hata waiipojaribu kutoka kwa "ushawishi" wa mafundisho manyonge ya viongozi wao, wakajikuta utoaji huo wa zaka HAUNA MANUFAA YOYOTE kwaoo..sio kimwili tu bali hata kiroho.
  3. matapeli wengi wameibuka na kujificha kwenye mwamvuli wa utumishi wa kidini wakati kiuhalishia ni waganga njaa tuu na hawa ndio huwaibia sana waumini na kuwafanya wengine wakate tamaa na kuamini hili suala ni utapeli tapeli kumbe sivyo..
NB: Ni muhimu kwa viongozi wa dini kuzingatia hili, Msiwashawishi watu watoe zaka.Hapaana..Bali WAFUNDISHENI KWELI kuhusu kutoa zaka.Na hamtaweza kuwafunza watu kweli kama ninyi wenyewe hamijui kweli.

USHUHUDA WANGU
Juzi kati kanisani katika ibada ya maombi ya kufunga mchungaji aliniita nisaidie kufanya huduma ya maombi kwa watu waliokuwa na vifungo mbali mbali na wanahitaji maombezi.(ofcz kwasasa sisi kanisani tuko kwenye Maombi ya kufunga kwa siku 40).

Baada ya ile huduma kumalizika jioni kama saa 12 hiv,nikawa nafanya utaratibu wa kutoka nirudi zangu ofisini kwangu kuendelea na majukumu yangu. Ghafla nikasikia sauti ya mama mchingaji ikiniita.

mimi: Bwana Yesu asifiwe mama

Mama mchungaji : Amina mpendwa, vipi mbona jumapiili ya juzi (tar 22 Jan) sijakuona ibadani? lakini pia hata leo huonekani kama uko sawa, kuna shida gani mwanangu?

[huwa anatuita waumini woote "mwanangu" hata kama wengine wamezidi umri,,mfano mimi kanizidi ila ile kawaida tu like 8 years hivi..Na sis waumini tushazoea kumuita "mama"]

Mimi: (nikajifikiria kidogo kisha nikajishauri acha tu nimwambie).Nikaanza kwa kusema "Unajua mama angu mimi kwasasa napitia changamoto nyingi sana hususani za kifedha na uchumi. Mambo yangu mengi yamekwama, wateja wangu wangu wengi ninao wadai hawanilipi na hata pesa yangu ninyoshika kwasasa haina utulivu kabisa. Inapotea haraka sana ingawa kila niki review naona imetumika kwenye masuala ya msingi ila bado kuna hali ya utofauti nai experience. sasa hali hii mama imenifanya nijikute nimeingia kwenye madeni na nimejikuta nimekopa hapa na pale nadaiwa na kilichonishtua nimejikuta mpaka kanisani humu kuna watu naheshimiana nao sana ila wananidai na niseme ukweli hata jumapili sikuja kanisani kwakua kuna mpendwa humu niliahidi kumpa pesa yake jumamosi ila ikshindikana na kwakwel nikajiskia hata aibu kuja kanisani (japo j2 hiyo jioni niliweza pata pesa nikamlisha mdau)

Nikaendela;

"Sasa hii hali mama mchungaji kiukweli inanivuruga sana nakosa amani na utulivu wa nafsi hata kumkaribia Mungu nakosa ujasiri kabisa. NIISHIE HAPO japo nikamweleza kwa undani sana mama mchungaji kitu ambacho huwa sio kawaida yangu kujieleza eleza sana lakini kiukwel nilipata tu msukumo wa kumweleza.

Yule mama akanisikiliza sanaa kwa umakini, kuna time akawa anacheka pia nikiwa naeleza situation yangu.Ila mwisho wa siku nikaweka kitu kumpa nafasi ili kama kuna la kusema basi aseme kama kuhani wangu wa Mungu.

Mama mchungaji kiukwel japo sio msomi na pia ni wale watumishi ambao hawana uwezo sana kifedha akaniambia mambo yafuatayo

AKASEMA;
  • Ujue kwa mtu wa Mungu kuna wakati kuptia hali kama hizi ni kitu cha kawaida tuuu,,Ni suala la vipindi katika maisha,kama mtu mwingine yoyote yule hata asiyemjua Mungu, kupata au kukosa ni jambo linalompata mtu yoyote yule hivyo usijali hii hali itapita tu mwanangu usiogope, Mungu atakusaidia ila kwa kipindi hiki jitahid kuzingatia ibada, usiache. Kuna wakati Mungu huziruhusu shida kwa mtu ili yamkini afike hatua ya kuhusi kuna jambo haliko sawa hivyo amrudia Mungu kuuliza tatizo ni nini? Hivyo pia muombe Mungu akusaidie kuja kama kuna jambo lolote lisilo la kawaida linaendelea kukuhusu maana maisha haya ni vita mwanangu hasa kwa sisi tunaomcha Mungu.
  • PILI, kwasasa familia yako imeongezeka mwanangu maana umetoka kupata mtoto wa 4 hiv karibuni,Sasa haliinawezekana bado unaishi kwa mipangilio ile ile kama ulipokua hujaanza kusomesha maana watoto wa3 wako shule..Sasa jaribu kuangalia pia mipangilio yako maana inawezekana familia imeongezeka lakini kipato hakija ongeza au kimepungua.sasa kama ni hivyo hii hali itakusumbua tu.Lifanyie kazi suala hili pia
  • TATU, ni kwamba mwanangu wewe nakujua vizuri kipindi unaanza kuabudu pamoja nasi mahala hapa mwaka 2014.Ulivyokua sivyo ulivyo kwasasa kwa habari ya kumtolea Mungu. zamani ulikua ni mtoaji mzuri lakini sasa hujawa ukitoa sadaka ya ZAKA na hii kiimani ni hatari sana kwani ndio sadaka inayompa Mungu (au Miungu) kuwa na sehemu /share kwenye fedha /Mali yako. ni kanuni ya kibiblia kwamba katika 100%, Mungu anataka umpe 10% wewe ubaki na 90% ili yeye ahusike na kulinda fedha yako maana kiroho mali yoyote au kitu chochote ili kiwe na ustawi na kudumu kisha kuongezeka ni lazima Mungu au miungu ihusike. sasa wewe SIO MWAMINIFU kwenye hilo eneo pia yaweza kuwa sababu ya kuingia kwenye sintofahamu hii, Nakushauri uombe rehema kwa Mungu na kisha ujaribu kumshirikisha Mungu Baraka zako ili adui (shetani/majini yasikuonee kwa kuiba na kutapanya mali yako.
BASI baada ya mazungumzo hayo mareefu akasema "piga magoti nikuombee kwa Mungu atakusaidia maana naamini Mungu ana baraka zako nyingi sana hata hizo unazopata ni kama tone tu anakupa ili KUUPIMA UAMINIFU WAKO na sasa maadam umegundua hilo tarajia tena utapimwa uaminifu ndani ya muda mfupi tu kuona utachukua hatua gani".

Basi akaniombea pale nikaondoka.

Baada ya siku mbili nikapigiwa simu na mteja wangu mmoja anataka SOFTWARE FLANI.( proffesionally mimi ni software developer) na baada ya kufikia agreements flani, mzigo ukasoma bank kama advance payment.

aloooohhh!! sikutaka kujifanya jeuri tena, nikabebe 10% nikapeleka kwa WATUMISHI WA BWANA ahahahahahahahah baasi nikaambiwa weka sadaka yako pale kisha piga magoti.. wakuu maombi niliopigiwa pale ni balaaa.

KWAKIFUPI NIKAJIONA SINA TOFAUTI NA WALE WATU AMBAO HUWA WANAENDA KUZINDIKA MALI ZAO KWA WAGANGA..yan ile unakuta mtu hata kama unamdai vipi hachomoi hata 100 kwenye hela yake mpaka afike kwa mganga wake..Au zile stori kama ushawahi kusikia kwamba kuna watu ikifika saa 12 jioni hawatoagi pesa hata ulie shida kiasi gani bora ufe ahudumia msiba ila ukitaka hela yake njoo kabla ya saa 12.. Basi na mimi nikaona anhaa kumbe mambo ndio yako hivi. Kinacho endelea sasa aahhh ni Mungu tu anajua...ila nikajifunza pesa inahitaji sana nidhamu ya kiroho ili itulie na iongezeke mikononi mwako vinginevyo itakua inapita tuuuu kwenda kwa wanaojua kuzitega.

Mwisho.
Eyce
 
Nikuulize tu maswali mawili Madogo, je Mungu anahitaji pesa kutoka kwa binadamu?

Pili ni lini mwanamke aliwahi kuwa kuhani?
 
Je, ulikuwa na kinasa sauti ili kurekodi hayo mazungumzo yako na huyo mama mchungaji?
 
Kubali ukatae sadaka nyingi hutolewa kwa kinyongo......
Hili mkuu nakubaliana na wewe kwa 96% mimi nikiwa mmoja wapi ndio maana nilikua sitoi..Kwakifup principle yangu ni 1 sitoi sadaka isiyoninufaisha..hiyo pesa bora nile tuu
 
Nikuulize tu maswali mawili Madogo, je Mungu anahitaji pesa kutoka kwa binadamu?

Pili ni lini mwanamke aliwahi kuwa kuhani?
Dahh mkuu mimi nadhani Mungu haihitaji pesa.Anahitaji utii toka kwetu na nadhani kutoa ni moja ya maagizo ambayo tunapswa kuonyesha utii ili watu walipswe na huduma za kiroho ziendeshwe maana ni ghrama hizo.

Pili huyu yeye sio mchungaji bali ni mke wa mchungaji
 
These issues of tithing should always remain undebatable.
Nakubaliana na wewe sema tu klichonisukuma ku share ni ile hali ya kuelekezwa kuhusu utoaji katika namna ambayo sio ya kujinufaisha binafsi..plus namna ambavyo hawa watu wanapaswa kuwa na uelewa mkubwa nje ya maandiko kuhusu maisha mana huwez kushauri kila mtu kufuatana na biblia.Hayo mawili yalinifurahisha toka kwke
 
Hapana kiongozi. Nimeuliza vile kutokana na ulivyom-quote neno kwa neno kana kwamba ulikuwa ukimrekodi kwa kinasa sauti.
Kiukwel mkuu sikujua kama angeweza kuongea mambo kwenye context ya kimaisha kwa ufasaha ndio maana nikamuelewa sanaa
 
Back
Top Bottom